Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.



DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA  MAMA MJAMZITO NA MTOTO.
NA WAMJW-MWANZA
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa wadau wa sekta ya afya na watoa huduma za afya hasa wauguzi na wakunga wanatakiwa kujikita zaidi kwenye kuokoa na kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama (More and Better Midwives) uliofanyika leo katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi kilichopo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
“Sisi sote tunafahamu umuhimu wa wauguzi na wakunga katika kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo Serikali ya awamu ya tano tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inafahamu kuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada mbalimbali za afya pamoja na nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwa kutoa kipaumbele cha ajira za wauguzi na wakunga.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewaonya wakunga na wauguzi wenye  tabia ya kutumia lugha chafu kwa wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo inaendeshwa kwa taaluma na maadili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa gharama nyingi pindi wanapopata maradhi na mpaka hivi sasa wananchi wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga Salama nchini Dkt. Julius Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa kuwalipia ada pamoja na mahitaji mengine.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Uuguzi na Ukunga  katika Chuo cha Bukumbi ambaye anafadhiliwa na mradi huo Rose Julius amesema kuwa anawasihi wanafunzi wafanye bidii kwenye masomo ya sayansi na hatimae wachukue fani ya uuguzi na ukunga katika kukabiliana na changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali na ufunguzi huo wa mradi wa Ukunga salama unaojulikana kama “More and Better Midwives”  ambao umeshirikisha  taasisi isiyo ya Kiserikali JHPIEGO ,wawakilishi kutoka Chama cha wakungwa  Canada(CMA) na Chama cha wakungwa  Tanzania TAMA pia alitembelea Zahanati ya Kambi ya wazee Bukumbi,Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure ili kujua hali ya upatikanaji wa dawa .

0 on: "DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO."