Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 10 Novemba 2017

DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI.



Na WAMJWW
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto amewataka watoa huduma na mafunzo kuhusu lishe bora yaanzie ngazi za shule ya msingi ili kuwajenga watoto kuzingatia mlo bora katika kukuza afya za watanzania.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini  inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
“Walimu wawe sehemu ya afua za kufundishia wanafunzi juu ya lishe bora hasa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili kuwajengea mazoea watoto kupenda kula mlo ulio bora hata wanapokuwa majumbani mwao” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa baadhi ya watoto walio vijini na mijini wana utapia mlo kwa kukosa chakula kilicho bora hivyo jamii inatakiwa izingatie lishe bora ili kuimarisha afya za watoto nchini.
Mbali na hayo Dkt. Mpoki amesema kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawe kipaumbele katika kutoa elimu ya lishe bora ili kuweza kujikinga na Unyafuzi, Kwashakoo na magonjwa yasiombukiza kama vile Kisukari,shinikizo la damu ,magonjwa ya moyo yanayotokana na ulaji kupita kiasi.
Kwa upande wake Meneja wa  Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe ECSA Bi. Rosemary Mwaisaka amesema kuwa wameamua kuandaa  vitini na vitita vya kufundishia lishe bora ili kuweza kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kufikisha elimu hiyo kwa walengwa.
“Tumeamua kuandaa vitini hivi ili viweze kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kuweza kuwafundisha wanajamii juu ya umuhimu wa kula mlo bora na vitatumika Kenya,Uganda na Tanzania” alisema Bi. Mwaisaka.
Mbali na hayo Mshiriki wa Mafunzo ya Lishe bora kutoka ECSA  ambae pia ni Mtoa huduma Bi. Evelyne Minja amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutoa huduma katika jamii kuhusu mlo bora hasa kwa watoto vijijini na mijini.
“Mafunzo haya yametufanya tujue jinsi ya kuwahudumia na kutoa ushauri juu ya mlo bora hasa kwa watoto wenye viashiria vya utapia mlo kwa kuwapima na kuwapangia vyakula vinavyostahili” alisema Bi. Minja.

0 on: "DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI."