Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 20 Novemba 2017

MOI YAOKOA BILIONI 5 KWA KUPUNGUZA RUFAA ZA NJE YA NCHI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akimjulia hali Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji Mkubwa wa Mgongo , kulia kwake ni Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo Dkt Nicephorus Rutabansibwa akitoa maelekezo  juu ya maendeleo ya mgonjwa huyo, wa mwisho ni Mganga mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Kambi.
.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua mashine mojawapo katika benki ya damua ya MOI.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Maabara Bwana Mbuta Jackson ya namna benki  mpya ya damu inavyfanya kazi kwa kushirikiana na damu salama.

  Katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo mbele ya menejimenti ya MOI wakati akikagua miundombinu, mapema leo wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza na menejimenti ya MOI katika ukumbi wa Mikutano MOI
 
 
 Menejimenti ya MOI wakifuatilia hotuba ya katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya katika ukumbi wa Mikutano MOI

Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi wakiwa na menejimenti ya MOI wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo mapema leo.



Na WAMJWW-DSM

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje nchi kufuataia kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt Mpoki Ulisubisya alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukagua hali ya utoaji wa huduma, miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa.
Akizungumza na menejimenti ya MOI Dkt Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.
“Mnafanya kazi nzuri sana , jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu, naomba muongeze ubunifu zaidi. Hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda huu wa Afrika pekee bali duniani. Hii ni changamoto kwetu sote kuifikisha hapo”. Dkt Ulisubisya
Aidha, Dkt Ulisubisya amebaini kuwa MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 95% na inaweza kulimaliza kabisa tatizo hilo ili pasiwepo mgonjwa wa kwenda nje.
Pia, amewaelekeza viongozi wa MOI kwa kushirikiana na Wizara mama kutafuta namna ya kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri kwa wizara
“Azma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh .Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha huduma zote za Afya zinapatikana hapa nchini na vyema sote tukamuunga mkono” Dkt Ulisubisya
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuwa na maono ya mbali ya kuifanya MOI kuwa Taasisi bora barani Afrika na duniani:
“Nimefurahi kwamba MOI mna maono ya mbali , mnafikiria kuitoa Taasisi hii hapa ilipo na kuifikisha sehemu ya juu zaidi, dira yenu ni kuwa Taasisi bora Afrika kufikia 2022 fanyeni kazi kwa bidii kufikia lengo hilo .” Prof Muhamad Kambi
Awali akiwasilisha taarifa ya Utendaji, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious Boniface amesema toka Taasisi hiyo ianzishwe, imefanikiwa kuanzisha huduma za kibingwa za Upasuaji wa Nyonga, Magoti, Ubongo, Mgongo, Vibiongo, Usingizi ambazo zimesaidia kupunguza rufaa za nje ya nchi.
“Mh Katibu Mkuu ,baada ya kuanzisha huduma hizi za Kibingwa tumefanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi, tumepunguza rufaa kwa asilimia  kubwa naomba nikuhakikishie hata hizi asilimia 5% zilizobaki tutashirikiana na Serikali na naamini zitakwisha kabisa” Dkt Respicious Boniface.

0 on: "MOI YAOKOA BILIONI 5 KWA KUPUNGUZA RUFAA ZA NJE YA NCHI."