Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 15 Novemba 2017

SERIKALI YAPIGA HATUA KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE.


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi akisisitiza jambo wakati wa Semina ya uhamasishaji wa wahariri na wakuu wa Idara ya Afya juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ilofanyika mapema leo katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam, pembeni yake ni  Dkt. Janeth Mgamba.


Mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko Dkt. Janeth Mgamba akitoa taarifa fupi mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya katika semina ya uhamasishaji kuhusu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
 

Watumishi wa Idara ya Afya wakifuatilia kwa makini Semina ya uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi mapema leo katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Blog ya Full Shangwe wa Bahati Bukuku akitoa mchango katika Semina ya uhamasishaji juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya.
 

Meneja mpango wa kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira akiwasilisha mada mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya katika semina ya uhamasishaji wa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele.




Na WAMJWW
 
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto  imefanikiwa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa asilimia 90 kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa hayo hapa nchini NTD.
Hayo yamezungumzwa na Mganga Mkuu wa Serikali  Prof. Bakari Kambi wakati alipofungua semina ya uhamasishaji wa kupambana na magonjwa hayo kwa wahariri wa vyombo vya habari na Wakuu wa idara mbalimbali wa Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam.
“Tumepata mafanikio kwani mpaka kufikia Oktoba  2017  huu  tumefanikiwa kupunguza  ugonjwa wa matende na mabusha katika wilaya 95 sawa na asilimia 77 kati ya wilaya 120 na hivyo tumesitisha kutoa dawa katika wilaya hizo” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa katika mafanikio hayo pia Serikali imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Vikope (Trakoma) katika wilaya 58 sawa na asilimia 82 kati ya wilaya 71 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa kwa maeneo ya nyanda za juu hususan katika maeneo  ya Rungwe,Kyela,ileje na Busekeleo wamefanikiwa kupima wananchi na kuonyesha kuwa maambukizi yamepungua na hivyo kuendelea katika wilaya zilizobaki.
Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa  wa Mpango wa kupambana na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo mwingira amesema kuwa wanajamii wanatakiwa wajitokeze katika kupata dawa za kujikinga na magonjwa hayo  kwani muitikio ni mdogo na inaweza kusababisha madhara makubwa siku za usoni.
Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa Semina hiyo imelenga kuwaelimisha wahariri wa vyombo vya habari ili watoe kipaumbele katika kuhamasisha wananchi juu ya matumizi ya dawa za kukinga magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambayo ni Matende na Mabusha, Usubi,Minyoo na Trakoma ili kuweza kutokomeza kabisa ugonjwa huo hapa nchini.

0 on: "SERIKALI YAPIGA HATUA KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE."