Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 2 Novemba 2017

SHIRIKA LA KIMATAIFA LA HELPAGE LAAHIDI KUWASAIDIA WAZEE WA TANZANIA





Na WAMJWW
Bodi ya Shirika la kimataifa la HelpAge yaahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wazee wa Tanzania ikiwemo ukatili dhidi ya vikongwe.
Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mh. Arun Maira wakati alipokutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Mh.  Arun Maira ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt. John Magufuli kwa jitihada kubwa anayofanya  katika kusimamia ustawi na maendeleo ya Wazee hususani katika masuala ya huduma ya Afya.
Aidha Mh. Arun Maira aliahidi kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto  kwa kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa wazee kupitia utekelezaji wa mkakati wa kutokomeza mauaji ya Wazee mara tu utakapokamilika.
Mh. Arun Maira aliendelea kusisitiza kwamba changamoto hizi za Wazee ikiwemo suala la ukatili wataliweka kama moja ya vipaumbele katika mpango kazi wao  ili kuwezesha utekelezaji  huo.
Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu aliwashukuru wajumbe hao wa bodi ya Shirika la kimataifa la HelpAge kwa kutatua changamoto mbali mbali zinazowahusu wazee  wa Tanzania  hususani katika kusaidia kampeni ya “Mzee kwanza”.
Mwisho Mh. Ummy aliiomba bodi hiyo kuweka nguvu zaidi katika suala la ulinzi wa wazee hususani  katika utekelezaji wa mkakati wa kuzuia mauaji na ukatili wa vikongwe kupitia mkakati wa kutokomeza mauaji ya wazee.

0 on: "SHIRIKA LA KIMATAIFA LA HELPAGE LAAHIDI KUWASAIDIA WAZEE WA TANZANIA"