Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 4 Novemba 2017

SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANAOTAKA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA AFYA,





Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi  kwa wadau wa maendeleo nchini wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya Afya.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga katika viwanja vya Green ground jijini  Dar es salaam.
Mh. Samia Suluhu amesema Serikali imekwisha weka mikakati thabiti ikiwemo kuongeza viwanda vya kutengeneza Dawa na Vifaa tiba ili kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma muhimu za Afya kwa binadamu. 
“Waziri wa Afya muongeze jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kina mama, mfanye tafiti na mchunguze kifo chochote cha mama na mtoto wakati wa kujifungua” 
Aidha, Makamu wa Rais alitaka kila kifo cha mama wakati wakujifungua lazima kijadiliwe vizuri na ikionekana kama kulikuwa na uzembe hatua zichukuliwe kama itakavyostahili.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema katika kuimarisha uzazi salama kwa kina mama, upatikanaji wa dawa zote za uzazi salama umeimarika na zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali.
“Hivi sasa ukipita katika vituo vyetu vya Afya  vya Serikali angalau  utakuta dawa zote muhimu  tunashukuru kwa kazi kubwa unayofanya ya kuzungumzia umuhimu wa kuboresha huduma za Afya nchini. 
Katika matembezi  yaliyofanyika mwaka jana shilingi Bilioni 290 zilikusanywa na kuwekwa kwenye fungu la kusomesha  wakunga 75 kwa ngazi ya cheti.

0 on: "SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANAOTAKA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA AFYA,"