Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 17 Novemba 2017

TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC

Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC) kwa kauli moja wamepitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (Pooled Procurement Services (SPPS).

Uteuzi huo wa nchi ya Tanzania umepita bila kipingamizi mwishoni mwa wiki kwenye Mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC uliowakutanisha Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaohusika  na masuala ya UKIMWI uliofanyika mjini Polokwane, Limpopo – Afrika Kusini.

Hatua ya uteuzi wa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara umetokana na juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa MSD ambapo sasa inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa .

Aidha,umahiri na uzoefu wa Bohari ya Dawa (MSD) katika masuala ya ununuzi, utunzaji na usambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara (yaani mnyororo wa ugavi) unaeleweka na kuaminika vizuri hata na nchi nyingine zilizowahi kututembelea kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Kwa hatua hiyo MSD itakuwa na dhamana na majukumu yafuatayo:
·          Kununua Dawa na Vifaa Tiba kwa ajili ya nchi za SADC

·           Usimamizi wa taarifa na takwimu za Dawa na Vifaa Tiba vitakavyohitajika

·          Usimamizi wa kanzidata (Database) ya dawa za nchi wananchama wa SADC na usimamizi wa bei elekezi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara

·           Kusimamia manunuzi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Ukanda wa SADC na kusimamia mnyororo wa ugavi

·          Kutoa huduma za kitaalamu na kupanga bei elekezi na

·          Kutoa huduma za ushauri wa kitaalam katika masuala ya dawa na vifaa tiba.

Hatua hii itapunguza kwa kiasi kikubwa bei ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya nchi wananchama wa SADC. Jambo ambalo limeipatia heshima na sifa kubwa Tanzania, kwani imeaminiwa kufanya ununuzi wa dawa kwa niaba ya nchi nyingine kumi na tano (15) ambazo ni wanachama wa SADC.

Tanzania kupewa jukumu hilo ni jambo la kujivunia sana tena inaonyesha dhahiri tumetambulika tuko vizuri kwenye masuala mazima ya mnyororo wa ugavi kwa nchi wanachama wa SADC.

Faida zitakazopatikana kwa Tanzania kuwa Mwenyeji wa huduma hii ni kama zifuatazo:

·          Heshima kwa nchi yetu kwa kuaminiwa na nchi wanachama wa SADC baada ya kukidhi vigezo vya kitaalam

·          Viwanda vyetu vya ndani vitaweza kuuza dawa zao kwa nchi za SADC, kwani wajumbe wa mkutano tumekubaliana kuwa na kituo kimoja kitakachoshughulikia udhibiti ubora na ukaguzi

·           Bei ya dawa itapungua zaidi maana sasa tutaweza kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji sio kama nchi (Tanzania), lakini kama Ukanda unaoshughulikia nchi 15

·          Itaongeza ajira na kuijengea uwezo Bohari ya dawa(MSD)

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya

16/11/2017

0 on: "TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC"