Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 14 Novemba 2017

WATANZANIA WATAKIWA KUPATA VIPIMO VYA KITAALAM KABLA YA KUTUMIA DAWA.

 
Mratibu wa Taifa wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea katika Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) Dkt. Bachana Rubegwa (aliesimama) akieleza maudhui ya semina hiyo niliyofanyika mapema leo katika ofisi za FAO.

 Mwakilishi Mkuu wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea (FAO) Dkt. Raphael Sallu akiwasilisha mchango wake wakati wa seminar na Waandishi wa habari kuhusu matumizi bora ya antibiotic, ilofanyika katika ofisi za FAO jijini Dar es salaam.

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya ugonjwa Bi Rose Shija akiwasilisha mchango mbele ya wadau wa habari, pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Afya Catherine Sungura.

 Mmoja ya wadau wa Habari ambae pia ni mmiliki wa Blog ya Full Shangwe akitoa mchango mbele ya wadau wenzie wa habari na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa  katika Semina ya kuhamasisha matumizi bora ya antibiotic.


NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

WATANZANIA wanatakiwa kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kupata vipimo kutoka kwa wataalam kabla ya kutumia dawa kwa mazoea ili kuepuka usugu wa vimelea vya wagonjwa kwenye miili yao na kusababisha vifo vya mara kwa mara.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mradi wa kupambana na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) Dkt. Raphael Sallu wakati wa semina na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tatizo la kutumia vijiuasumu(Antibiotics) bila ya kupata vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya limekua kubwa ambalo linasababisha madhara ya kiuchumi na uhai kutokana na kuzidiwa na vimelea vya ugonjwa ambavyo vinakua sugu kutokana na  matumizi mabaya ya dawa hapa nchini” alisema Dkt. Sallu.

Aidha, Dkt. Sallu amesema kuwa elimu ya kutumia dawa bila ya kupata ushauri na vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya ianze kutolewa kuanzia ngazi za shule ya msingi na ngazi ya jamii kwa ujumla.

Mbali na hayo Dkt. Sallu amesisitiza kuwa wanahabari wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha umma umuhimu wa kutumia dawa kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam kuhusu ugonjwa unaomsumbua pamoja na matibabu yake.

Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa  Mradi wa kupambana na na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula (FAO) nchini Tanzania Dkt. Bachana Rubegwa amesema kuwa katika kupambana na tatizo hili kunapaswa kuwepo na matumizi ya hali ya juu ya chanjo ili kuweza kuepuka utumiaji hovyo wa dawa bila ya vipimo.

“Katika kupambana na utumiaji wa madawa bila ya utaratibu mzuri ambao hauhusishi vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ni lazima maabara ya kutambua magonjwa sugu ijengwe nchini kwetu” alisema Dkt. Bachana.

Hata hivyo Dkt. Bachana amesema kuwa wazilashaji wa chakula na mifugo wanatakiwa kutumia dawa zinazostahili na sio kutumia antibiotics katika mifugo yao pamoja na shughuli zao za kilimo ili kuepusha watanzania walio wengi kutumia vyakula hivyo vyenye usugu wa vimelea vya magonjwa.

Mbali na hayo Dkt. Bachana ametoa rai kwa watoa huduma za afya nchini kuacha kutoa dawa ambazo ni feki,zilizokwisha muda na kuwashauri wananchi kuepuka matumizi ya dawa yasiyo ya lazima ili kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa kwenye miili ya watanzania.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa Dkt. Rose Shija amesema kuwa watanzania wanatakiwa kutumia dawa sahihi na kwa wakati kadri alivyoelekezwa na mtaalam wa afya ili kuepuka matatizo hayo na kujijengea afya bora.

“Tubadili tabia katika kupunguza maambukizi kupitia chanjo,kuosha mikono kwa maji safi yanayotiririka,kuepuka ngono zembe na utunzaji salama wa chakula na sio kutumia dawa bila ya ushauri kutoka kwa wataalam wa afya ili kuepuka usugu wa vimelea vya magonjwa mwilini” amesema Dkt. Shija.

0 on: "WATANZANIA WATAKIWA KUPATA VIPIMO VYA KITAALAM KABLA YA KUTUMIA DAWA."