Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 30 Aprili 2018

WIZARA YA AFYA YAZINDUA MFUMO WA TEHAMA KWA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma za Afya katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma, Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akimkabidhi cheti cha shukrani kwa aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za watu  binafsi Dkt.Mohamed Ally Mohamed katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.


 

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizindua kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizindua Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma za Afya katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.

 

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akimkabidhi cheti cha shukrani kwa aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za watu  binafsi Dkt.Mohamed Ally Mohamed katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.



Na WAMJW-DODOMA

Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imezindua mfumo mpya wa TEHAMA wa kusajili vituo vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali ikiwa na lengo la kuboresha mfumo wa kujisajili ambapo waombaji wapya watafanya maombi yao kupitia mfumo huo popote walipo na kufuatilia maombi hayo popote walipo kupitia mfumo huo. 

Hii ni tofauti na hapo awali ambapo muombaji alilazimika kusafiri kufika wilayani, mkoani na hata kufika  Taifa yaani kwa msajili wa hospitali nchini.

Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo, Jijini Dodoma ambapo pia alizindua kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi, mwongozo wa viwango vya msingi kwa vituo vya kutolea huduma za afya nchini pamoja uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali za watu binafsi.

*“Nina uhakika maombi ya usajili wa vituo vya afya sasa yataenda kwa haraka. Waombaji watajaza fomu na kulipia hukohuko walipo bila kufika ofisini  na vile vile watakuwa na uwezo wa kutumia mfumo kwa kutumia simu zao,” alisema Dkt. Ndugulile.*

Amesema Sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta muhimu katika Serikali ya Awamu ya Tano ambapo sekta hiyo ni ya tatu kwa kupata  bajeti kubwa. 

Aidha ,kwa mwaka huu wa  fedha jumla ya vituo vya afya 208 vimeboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya dharura ya mama na mtoto.

Dkt. Ndugulile amesema ndani ya bajeti hii Hospital za wilaya 67 zitajengwa nchini pamoja na hospitali za rufaa kwa mikoa ambayo haina hospitali ya rufaa ya mkoa.

Wakati huo huo, Waziri Ndugulile ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIF) kufanya majukumu iliyopewa ikiwa ni pamoja kusajili vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma kutokana na vigezo vilivyowekwa na mfuko huo na kuziachia mamlaka  nyingine majukumu yake ya kukagua vituo hivyo kama vile mikataba ya kazi ya wafanyakazi wa vituo husika.

Aidha, ameutaka mfuko huo kutafakari juu ya masharti yaliyowekwa katika kusajili vituo ambapo kituo hakiwezi kusajiliwa mpaka kiwe katika uangalizi na mfuko huo kwa miaka isiyopungua mitatu.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Otilia Gowele amesema kanuni mpya za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi zitasaidia kusogeza huduma kwa wananchi pia hospitali hizo kutoa huduma kulingana na mahitaji ya sasa

0 on: "WIZARA YA AFYA YAZINDUA MFUMO WA TEHAMA KWA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI."