Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 16 Mei 2018

MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI ASEMA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia akimkabidhi mguu wa bandia mzazi wa mtoto Daniela kwa ajili ya mwanae Daniela Palangyo (8) mkazi wa Kinyerezi wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji MOI leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na watatu kulia ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kwanza kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua chumba cha upasuaji katika Taasisi ya Mifupa Moi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na katikati ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia akipata maelezo juu ya vifaa vya upasuaji wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji MOI leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na aliyevaa kiremba ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wazazi weneye watoto wao katika Taasisi ya Mifupa MOI alipotembelea wagonjwa ha oleo jijini Dar es salaam, katikati ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Mifupa nchini MOI sasa itafanya upasuaji wa mifupa kwa wagonjwa wapatao 1000 kwa mwezi kutoka wagonjwa 500 mpaka 700 baada ya kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake kutoka kwa Serikali ya Kuwait .

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake vyenye thamani ya shilinigi milioni 186 leo katika Taasisi ya mifupa MOI leo jijini Dar es salaam.
“Hii ni faraja kubwa sana kwa Serikali kwani uboreshwaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kubwa kama MOI itaweza kuhudumia wagonjwa wengi Zaidi kutoka wagonjwa 700 kwa mwezi mpaka kufikia 1000 kwa mwezi” alisema Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Balozi wake Jasem Al Najem kwa msaada huo kwani utaisaidia kwa kiasi kikubwa MOI katika kuboresha utoaji huduma hasa katika fani ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi hapa nchini.
Kwa uapnde wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa  kukamilika kwa vyumba hivi viwili vya upasuaji, kutaiwezesha Taasisi ya MOI kuwa na jumla ya vyumba vya upasuaji 8 kutoka 6 vilivyopo sasa na miongoni mwa vyumba hivi vya upasuaji kimoja kitakuwa maalumu kwa ajili ya  watoto tu.
“MOI imeshatoa matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa 1,670 ikiwemo upasuaji mifupa (wagonjwa 1,228), kubadilisha nyonga (wagonjwa 84), kubadilisha goti (wagonjwa 72), upasuaji wa uti wa mgongo (wagonjwa 109), ubongo (wagonjwa 64), na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (wagonjwa 113” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuimarisha na kuboresha afya za Watanzania jengo hilo pia litakuwa na vitanda 16 vya ICU (Intensive Care Unit) na 16 vya HDU (High Dependency Unit), hivyo kuimarisha huduma za tiba kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Naye Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem amesema kuwa Nchi ya Kuwait ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha Hospitali na Vituo vya afya  nchini Tanzania vinatoa huduma bora za Afya kwa kutumia Taaluma na ujuzi wa kisasa ikiwemo vifaa na vifaa tiba .
“Serikali ya Kuwait itakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha afya za wananchi kwa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa,vifaa tiba na wataalamu wa afya na kutochoka katika hilo” alisema Balozi Najem.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Bi. Zakia Mejhi amesema kuwa Taasisi yake imeokoa Bilioni 3 za kufanyia upasuaji kwani kwa sasa huduma hizo za kibingwa zinafanyika nchini kwa Shilingi Bilioni 12 kutoka Bilioni 15 za rufaa ya kwenda kutibiwa nje.

 

0 on: "MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI ASEMA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN."