Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 3 Julai 2018

KIWANDA CHA DAWA KIKUBWA KUJENGWA NCHINI.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na masuala ya Afya wakati akiwa katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Picha ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na Masuala ya Afya, ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimuaga Rais wa Kampuni ya Fosun Pharma inayotarajia kufungua kiwanda cha uzalishaji wa Dawa hapa nchini hivi karibuni baada ya majadiliano yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Kituo cha uwekezaji yaliyomuhusisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

KIWANDA kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa  kuagiza dawa nje ya Tanzania. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha dawa hapa nchini leo jijini Dar es salaam. 

"Leo tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini", alisema Waziri  Ummy . 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na kujengwa kwa kiwanda hiko kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya manunuzi ya dawa kwani mpaka sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda kununua dawa nje na asilimia 6 ndiyo inannua dawa nchini. 

Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kutapelekea kupunguza muda wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi 9 mpaka miezi 11 kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania. 

"Tunatumia mda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora" alisema Waziri Ummy. 

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kampuni hiyo inayotengeza sindano za kutibu Maralia kali ya ATESUNAT itaweza kutengeneza sindano nyingi zaidi na kuweza kuwahudumia nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda na Burundi. 

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa hakuna kikwazo kwa Kampuni hiyo kuanzisha ujenzi wa kiwanda cha dawa hapa nchini kwani kitasaidia upatikanaji wa dawa kwa urahisi na kukua kwa uchumi kupitia viwanda. 

"Tumejadili na kuwakubalia bila ya kuweka kikwazo kwani tumeridhishwa na ubora wao katika utengenezaji wa dawa na mafuta nchini kwao hivyo tunawakaribisha kuja kufanya uwekezaji huo" alisema Waziri Mwijage. 

Naye Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Nchini Bw. Geofrey Mwambe amesema kuwa wameupokea uwekezaji huo na wanaufanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuipeleka Tanzania kuelekea uchumi wa Viwanda. 

"Kutokana na ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda na kutokomeza kabisa tatizo la uhaba wa dawa hatuna budi kushirikiana na wawekezaji hao kutimiza lengo hilo" alisema Bw. Mwambe. 

Kika hiko cha kujadili uwekezaji wa kiwanda hiko cha kutengeneza dawa kimeudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu,  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Bohari kuu ya Dawa MSD,  Kituo cha Uwekezaji nchini TIC na wadau mbalimbali.

0 on: "KIWANDA CHA DAWA KIKUBWA KUJENGWA NCHINI. "