Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 13 Julai 2018

MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa mradi wa Tuwatumie ambao unawaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika vijiji vyote vya halmashauri hiyo chini ya ufadhili wa AMREF

Wadau mbalimbali wa sekta ya afya walifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichani) aliyekaa kushoto ni Niall Morris Mkuu wa Arish Aid,Dar.Aisa Muya -Kaimu Mkurugenzi Mkazi Amref Tanzania(katikati) na kulia ni Dkt.Helen Senkoro Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation

Wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa mradi huo ambapo watoa huduma hao watakua kiungo kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma.

Waziri Ummy Mwalimu akifungua mradi huo


MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA. 

NA WAMJW-SIMIYU. 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepiga marufuku kuajiri watoa huduma wa afya ngazi za jamii kutoka nje ya Halmashauri husika. 

Katazo hilo limetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE uliofanyika mkoani Simiyu wilaya ya Itilima. 

"Nataka kuwaambia viongozi wa Mkoa na Wilaya nchi nzima pamoja na taasisi zisizo za kiserikali ni marufuku kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii (CHW) kutoka nje ya  makazi yao ili kusiwe na  kutotofautiana kimazingira,kwani wenyeji wanajua tamaduni na mila za wakazi wanapotoka" alisema Waziri Ummy. 

Waziri Ummy amesema kuwa watoa huduma ngazi ya jamii wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kukinga kuliko kutoa tiba ili kupunguza idadi ya wagonjwa na kuokoa fedha. 

"Nataka kuwaambia wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanatakiwa kuweka kipaumbele kinga kuliko tiba kwani mimi ni Waziri wa Afya na sio Waziri wa wagonjwa,siwezi kusubiri watu wale ,nitawatumia CHW kuwakinga ama kuwazuia wanaoumwa kupata matibabu" alisema Waziri Ummy. 

Alisema nchi ipo kwenye mikakati ya kufikia malengo endelevu ya millennia ya kumfikia kila mtanzania kwa wakati na popote,hivyo kwa kuanza CHW wanaanza eneo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania Dkt. Aisa Muya amesema kuwa asilimia 50 ya miradi yao wanatumia watoa huduma za afya ngazi ya jamii . 

Aidha, Dkt. Muya amesema kuwa wametoa mafunzo kwa watoa huduma  2,265 na mradi huo utawaajiri watoa huduma 2,015 mbapo Wilaya ya Itilima watakuwa 102 na Misungwi 113 ambao wataenda kwenye vijiji vyote vya wilaya hizo. 

Dkt. Muya amesema kuwa matarajio ya mradi huo ni kuwatumia watoa huduma hao kama kiungo kati ya jamii na vituo vya kutolea huduma za afya. 

0 on: "MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA."