Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 10 Agosti 2018

IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI.

Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe.  Penny Mordaunt (katikati) akimsalimia mtoto mchanga aliyebebwa na baba yake katika jengo la Kliniki ya Baba, Mama Na Mtoto. Kulia ni Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.





Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisoma mbao ya matangazo katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam pindi alipofika kupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza.

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa Elimu juu ya umuhimu wa kukata Bima ya Áfya kwa mtoto (Toto Afya Card) kwa mmoja kati ya wazazi  waliofika katika Zahanati ya Tabata kupata huduma za matibabu ya mtoto.

Mshauri wa masuala Ya Afya kutoka ubalozi wa Uingereza DKt. Gloria Ngaiza (wapili Kushoto) akimtafasiria Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt kilichokuwa kikisemwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tabata (Wakwanza Kushoto).Wa mwisho Kulia ni Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu.
IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI 

Na WAMJW - DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto imesema kuwa idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Afya za Kisasa za uzazi wa mpango zimeongezeka nchini mpaka kufikia Asilimia 32.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo wakati alipoupokea ugeni  wa Waziri wa Maendeleo kutoka nchini Uingereza katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kutatua changamoto za Sekta ya Áfya hususani katika huduma za Afya ya mama na mtoto.

"Kupitia Msaada wao tumeweza kuongeza idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Kisasa za uzazi wa mpango, hatupo vizuri,  tupo Asilimia 32, tumeweka lengo itapofika 2020 tufikie Asilimia 45 ya wanawake walioolewa wanatumia njia hizi" Alisema Waziri Ummy Mwalimu. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini, takribani wanawake 556,000 katika kila vizazi hai laki moja wanafariki na kwa mujibu wa Wataalam uzazi wa mpango utaweza kuchangia Mpaka Asilimia 30 katika Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

Pia Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kwa kutenga fedha za ndani katika kupambana na changamoto za sekta ya Áfya ikiwemo kuajiri watumishi wa sekta ya Áfya jambo linalosaidia Kupunguza changamoto hizo za vifo vya akina mama wajawazito na mtoto wachanga. 

"Sisi kama Serikali tumejiongeza, tumechukua hatua na kutenga rasilimali fedha za ndani ikiwemo kuajili watoa huduma za afya, kuhakikisha Kwamba tunatatua changoamoto hiyo " alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy aliishukuru Serikali ya Uingereza kupitia kwa Waziri wa Maendeleo Mhe. Penny Mordaunt kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya hasa katika huduma za mama na mtoto. 

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo kutoka Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameshukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Áfya kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi wa Tanzania na kuahidi kupeleka salamu za Tanzania nchini Uingereza.

0 on: "IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI."