Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 7 Agosti 2018

JAMII YA TANZANIA INATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA ILI KUEPUKA KIPINDUPINDU.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akiongea na Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Afisa wa kudhibiti na kukinga magonjwa kutoka Shirika la Afya Duniani WHO nchini Tanzania Dkt. Grace Saguti akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa Sekta ya afya wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na kipindupindu kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wa kwanza  akifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa mwezeshaji hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na kipindupindu kilichofanyika jijini Dodoma.


Wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakimsikiliza  kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na kipindupindu kilichofanyika jijini Dodoma.


NA WAMJW-DODOMA


SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza jamii ya Tanzania juu ya utumiaji wa maji safi na salama ili kuweza kupambana na ugonjwa wa kipindupindu kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Afya) Dkt.  Mpoki Ulisubisya wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku tatu cha kujadili mikakati ya kukabiliana na ugonjwa kipindupindu nchini kinachoendelea jijini Dodoma.

"Ili kupambana na ugonjwa huu Watanzania  wanatakiwa kutunza mazingira hasa kutumia vyoo bora pamoja na kutumia maji safi na salama katika jamii inayotuzunguka" alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa hadi sasa kwa takwimu iliyopo inaonesha kuwa watu elfu 32 wameugua na watu 600 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu hapa nchini.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo mpaka kufikia 2030 wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya maji, TAMISEMI,  na wadau wengine wa afya wanatakiwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaweka pamoja wataalam mbalimbali kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa kipindupindu nchini Tanzania.

Aidha Prof. Kamuzora amesema kuwa tayari wameshaandaa madawati mbalimbali ya wataalamu katika ofisi yake ili kuwexa kuweka mifumo ya  kushughulikia kwa uharaka magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.

Naye Afisa wa kudhibiti na kukinga Magonjwa kutoka Shirika la Afya Duniani hapa  nchini Dkt. Grace Saguti amesema kuwa kutokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali Serikali ya Tanzania imeweza kufanikiwa  kutokomeza ugonjwa wa Kipindupindu kwa sehemu kubwa ya Tanzania.

 "Mpaka hivi sasa mikoa inayokabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu  katika maeneo yake ni Rukwa, Songwe na Arusha lakini maeneo yote yaliyobaki tumefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo" alisema Dkt. Saguti.


0 on: "JAMII YA TANZANIA INATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA ILI KUEPUKA KIPINDUPINDU. "