Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 6 Agosti 2018

SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA.

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa Serikali na wanafunzi wa Kada ya uuguzi leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwasamia wanafunzi wa Kada ya uuguzi wakati alipomkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu katika hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.

 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo cha uuguzi Tanga  Felister Bulali  akitoa maelekezo ya namna ya kumuudumia Mtoto aliyetoka kuzaliwa , mbele ya Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili Kushoto),  Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi. Leah Makala na watatu ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela.

Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu akiteta jambo juu ya kifaa cha kujifunzia chenye umbo la Mtoto,  wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga. Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi Leah Makala.

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisakata ngoma na kikundi cha ngoma cha kinamama leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga

Bweni la ghorofa nne la wanafunzi lenye uwezo wakulaza wanafunzi 380 kwa wakati mmoja likiwa ni baadhi ya majengo yaliyogharimu kiasi cha shilingi Bilion 3.5.

Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela wakiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali wakati wa Hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.


SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA KATIKA CHUO CHA UUGUZI TANGA.

Na WAMJW - TANGA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatarajia kufanya udahili wa wanafunzi kwa asilimia 100 kutoka wanafunzi Mia moja na Hamsini (150) hadi Mia tatu themanini wa kada za Afya nchini katika chuo cha Uuguzi Bombo Tanga.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga, yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na MALARIA (Global fund).

Waziri ummy aliendelea kusema kuwa  majengo yaliyokabidhiwa ni juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha wanazalisha wataalamu wa kada za Afya, hususani Wauguzi na Wakunga jambo litalowawezesha kuwa Wataalamu bora.

“Udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka 190 hadi 260, Huwa tunapata shida sana, wanafunzi wengi wanafaulu na tunakuwa hatuna nafasi ya wapi  pakuwapeleka, kwahiyo tunawashukuru Global fund , tunaweza kudahili hadi wanafunzi 368” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu  kutoka Wizara ya Afya kushirikiana na NACTE  kuwachukua wanafunzi wote waliosoma na kufaulu vizuri masomo nya Sayansi na wenye vigezo na wenye vigezo katika kada ya Afya.

Waziri Ummy aliongeza kuwa, kutokana na jitihada hizo kumekuwepo na ongezeko la wahitimu ngazi ya astashahada na Stashahada kwa mafunzo kutoka wahitimu 4473 mwaka 2012/2013 hadi 7561 kwa mwaka 2016/2017 , ongezeko hili ni sawa na Asilimia 69.

Wakati huo huo Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle amesema kwa mwaka huu wa fedha , Wizara imetenga shilingi Bilion 8 kwaajili ya ukarabati wa majengo chakavu katika chuo hicho.

Aliendelea kuwa Wakufunzi 143 wamepangiwa kufanya kazi katika vyuo vya Afya nchini, vikiwemo vyuo vya Wauguzi na Wakunga ambao ndio msingi wa kupunguza athari ya uzazi pamoja na vifo vya wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Nae Mwakilishi wa Global Fund Dkt. Hiltruda Temba amesema kuwa, Global fund  imeboresha miundombinu yakufundishia katika vyuo 14 na kuwezesha kufadhili zaidi ya wanafunzi 1500 wa kada za Uuguzi na Ukunga wa Technolojia dawa, Technolojia maabara na Tabibu katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018, pamoja na kutenga shilingi Billion 1.1 kwaajili yakuboresha mifumo ya Afya.

MWISHO.

0 on: "SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA."