Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 17 Oktoba 2018

MARUFUKU MGONJWA KWENDA KUNUNUA DAWA NJE IKIWA DAWA ZIPO

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi msanifu wa wilaya ya Mafia Ramadhan Madenge kuhusiana na mchoro wa kituo cha afya cha Kilongwe.
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kifinge Hamis Omary   (kushoto) wakati alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akionesha moja ya dawa za serikali wakati alipofanya ziara kuona hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya wilaya ya Mafia kuona.
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Mafia Dkt. Zuberi Mzige kuhusiana na mchoro wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa bima ya afya wakati wa ziara katika Hospitali ya Wilaya hiyo.

MARUFUKU MGONJWA KWENDA KUNUNUA DAWA NJE IKIWA DAWA ZIPO. 

Na WAMJW-MAFIA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepiga marufuku kwa watoa dawa kuwaandikia wagonjwa kwenda kununua kwenye maduka binafsi ikiwa kwenye kituo kuna dawa na vifaa tiba vya kutosha. 

Hayo yamezemwa na Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea Hospitali ili kuangalia hali ya utoaji huduma Wikayani Mafia . 

"Nauagiza uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani kuwarudishia wagonjwa wote gharama za vifaa tiba na dawa walizonunua katika maduka binafsi ambazo zinapatikana Hospitalini hapo" alisema Dkt.  Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa  amebaini baadhi ya wagonjwa walioandikiwa kwenda kununua dawa na vifaa tiba katika maduka binafsi huku baadhi ya dawa hizo zikiwepo katika stoo ya kuhifadhia dawa.

Dkt. Ndugulile amemuagiza  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Mganga Mkuu wa Wilaya ahakikishe wanawarudishia wagonjwa wote gharama walizotumia kununua dawa nje ya Hospitali hiyo.  

Pia Dkt. Ndugulile alishangazwa na Hospitali hiyo kutokuwa na dawa na vifaa tiba muhimu huku serikali ikiwa imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 270 kuanzia mwaka 2015/16 kutoka bilioni 31 za hapo awali, ikiwa na lengo la kuhakikisha dawa zote zinapatikana katika Hospitali na vituo vyote vya afya nchini.

Vikevike Dkt. Ndugulile  ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mafia kuhakikisha bajeti ya dawa inapitiwa yakinifu na kutekelezwa ili kuepuka changamoto ambazo zinaweza kuepukika za ukosefu wa dawa na vifaa tiba muhimu na kuleta usumbufu kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Amebaini upungufu huo wa dawa na vifaa tiba baada ya kutembelea wodi za watoto na akina mama waliojifungua na kuelezwa na baadhi ya wagonjwa hao kununua dawa na vifaa tiba vya kusaidia kujifungua nje ya Hopitali hali ambayo imekua kero kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika Hospitali hiyo.

Wakati huo huo Dkt. Ndugulile amesitisha ukarabati wa jengo la wagonjwa wa bima baada ya kuona kuna ubadhirifu wa fedha ambao hauendani na mazingira halisi ya ukarabati huo.

Pamoja na hayo Dkt. Ndugulile amefanya  ziara katika kituo cha afya cha Kilongwe na zahanati ya kifinge na kutoridhishwa na  maendeleo ya vituo hivyo huku akibaini utaratibu usiofaa wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi na kuamuru Halmashauri hiyo ifuate utaratibu wa manunuzi wa Force Account. 

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisitisha   mara moja ukarabati wa jengo katika zahanati hiyo  huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikishirikiana na kamati ya ujenzi kufuatilia uhalisia wa gharama hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma amemshukuru Naibu waziri huyo kufanya ziara kisiwani humo huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizobainika ili kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Naye   Fundi msanifu wa Wilaya ya Mafia Ramadhan Madenge alisema kuwa kuna  ukarabati wa jengo hilo unagharimu takribani Tsh. Milioni 94. 

 

0 on: "MARUFUKU MGONJWA KWENDA KUNUNUA DAWA NJE IKIWA DAWA ZIPO"