Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 29 Oktoba 2018

WAGANGA WAFAWIDHI NCHINI WATAKIWA KUWEKA VIKAO KUJADILI VIFO VYA UZAZI

Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali kutoka Wizara ya Afya wakifuatilia kwa makini mawasilisho kutoka kwa wawezeshaji wa mkutano wa Waganga wafawidhi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma.





Baadhi ya Waganga Wafawidhi kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia kwa makini mawasilisho kutoka kwa wawezeshaji wa mkutano wa Waganga wafawidhi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma.


Baadhi ya Wawasilishaji wa mada mbalimbali wakiwasilisha mada kwa waganga wafawidhi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Waganga afawidhi uliofanyika jijini Dodoma.
 
WAGANGA WAFAWIDHI NCHINI WATAKIWA KUWEKA VIKAO KUJADILI VIFO VYA UZAZI
 
Na WAMJW- DODOMA
 
WAGANGA Wafawidhi nchini wametakiwa kukaa vikao kila baada mara kwa mara ili kujadili sababu ya vifo vinavyotokea kwenye hospitali zao ili kuzifanyia kazi changamoto hizo na kurudisha taarifa Wizara ya Afya.
 
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waganga Wafawidhi nchini uliofanyika leo jijini Dodoma
 
“Waganga Wafaidhi mnatakiwa kukaa vikao vya kitabibu kujadili tiba pamoja na kujadili kifo cha kila mgonjwa ili kujua changamoto iliyotokea na kuipatia ufumbuzi na kuandikia taarifa ili kuondokana na vifo hasa vitokanavyo na Uzazi” alisema Dkt. Gowelle.
 
Aidha, Dkt. Gowelle amewataka wataalam wa tiba kuzingatia vikao vya tiba na kufanyia kazi changamoto au maboresho ili kuzitolea taarifa na kuzitatua pamoja na kushirikisha wadau wengine.
Dkt. Gowelle amewataka pia Waganga wafawidhi kuweka mifumo ya ufuatiliaji wagonjwa pamoja na kupokea malalamiko  katika hospitali zao ili kufanya maboresho ya huduma za afya wanazozitoa na kuchukua hatua zinazostahili.
 
“Kupitia kikao hiki, nawataka mkae kama timu na kuandaa Mipango kazi ya kuanza kushughulikia kikamilifu yale yote yaliyobainika katika taarifa hiyo ili kuondokana na kero wanazokabiliana nazo wananchi wanapokuja kupata huduma katika hospitali zenu” alisema Dkt. Gowelle.
 
Aidha, Dkt. Gowelle amewasihi Waganga Wafawidhi waliohudhulia kikao hiko kuhakikisha  kwamba wanatumia  timu zao za Uendeshaji za Hospitali za Rufaa za Mikoa kubaini changamoto zilizopo katika maeneo yenu ya kazi ikiwa ni pamoja na watumishi, majengo na vifaa vya kuzifanyia kazi ili kuboresha huduma mnazotoa kwa wananchi.
 
Mbali na hayo Dkt. Gowelle ametoa pongezi kwa timu yote ya inayoratibu utekelezaji wa Mradi wa RRHMP pamoja na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo JICA kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za Afya nchini.

0 on: "WAGANGA WAFAWIDHI NCHINI WATAKIWA KUWEKA VIKAO KUJADILI VIFO VYA UZAZI"