Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 24 Oktoba 2018

IDADI YA WANACHAMA WACHANGIAJI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA NCHINI YAONGEZEKA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.



Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakipokea taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto


Na.WAMJW,Bungeni, Dodoma

Idadi ya wanachama wachangiaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708 waliokuwa wameandikishwa  mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi Septemba 2018.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.

“Ongezeko hili limetokana na kanuni na misingi  inayotumika katika kuendesha utaratibu wa mfuko huu ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia viwango vya mshahara,usawa katika kupata huduma na ushiriki wa Serikali katika usimamizi kwa faida ya wanachama” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa kwa upande wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), jumla ya kaya zilizojiunga hadi Septemba mwaka huu ni 2,220,953 ikiwa ni sawa na wanufaika wapatao 13,506,330 sawa na asilimia 25 ya watanzania wote’ kwa hiyo mifuko hii yote inatoa huduma kwa watu 17,656,697 sawa na asilimia 33 ya watanzania wote kwa mujibu  wa idadi ya makadirio ya watanzania kwa sasa.

Idadi ya wanufaika imeongezeka  kutoka 691,774  mwaka 2001/2002 hadi wanufaika 4,150,367 sawa na asilimia 8 ya watanzania wote” alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka sasa idadi ya wanachama wengi waliojiunga  asilimia 67 ni watumishi wa umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa sharia.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema mfuko unaendelea kutoa elimu na kubuni vifurushi mbalimbali vitakavyovutia wananchi wengi kujiunga na kufaidika  na mfuko ambapo utawawezesha wanachama wengi zaidi kujiunga hasa wale wa sekta isiyo rasmi na kujiwekea malengo ya kuwafikia watanzia asilimia 50 mwaka 2020.

“Mfuko umekamilisha uandaaji wa vifurushi vya michango na mafao kulingana na uwezo wa wananchi kulipia bima  ya afya,suala hili lipo katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kwa utekelezaji”. Alisisitiza Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa mpango huo utamwezesha mwananchi kuchagua vifurushi vya aina mbalimbaliu vya huduma  anayoitaka  kwa utaratibu utakaojulikana kama ‘JIPIMIE’ na wanachama watalipa kidogo kidogo kwa utaratibu ujulikanao kama ‘DUNDULIZA’ ambao tayari umeshakamilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa NHIF wanatakiwa kuweka mfumo wa kutoa huduma za bima ya afya kwa mashirika makubwa ya hapa nchi na yale ya nje kwa kuwauliza  huduma zipi wangependa kuhudumiwa katika hospitali za hapa nchini  hususan zile za binafsi na hivyo kuweza kuongeza idadi kubwa ya wateja watakaohudumiwa na NHIF.

Naye Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernad Konga akijibu maswali ya wajumbe wa kamati hiyo alisema kwamba NHIF imekubali kuboresha huduma zao na hivyo wapo tayari kuanza huduma za vifurushi za  ‘JIPIMIE’ mara moja  ili wananchi waweze kupata huduma za afya kulingana na vipato vyao.

Aidha, alisema hivi sasa wameajiri madaktari wapatao kumi na nane  na kuwaweka kwenye hospitali kubwa za Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutatua changamototo za wateja wa huduma za bima hiyo zikiwemo za kunyanyapaliwa  pamoja na kukagua fomu zinazojazwa na wataalam wa hospitali hizo ili kupunguza malalamiko ya wateja wa huduma za bima ya NHIF na kuahidi wataongeza hospitali zingine awamu inayofuata


0 on: "IDADI YA WANACHAMA WACHANGIAJI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA NCHINI YAONGEZEKA."