Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 26 Novemba 2018

HOSPITALI YA KIBONG’OTO KUWA KITUO CHA TAFITI, TIBA NA MAFUNZO YA MAGONJWA AMBUKIZI


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akipata maelekezo namna wanavyopima wagonjwa wa kifua kikuu toka kwa Mganga Mfawidhi Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dkt. Riziki Kisonga (kulia)

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikagua maabara katika Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) akikagua vyumba vya wagonjwa katika Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua stoo ya dawa zilizopo katika Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua ramani ya jengo la maabara litakalojengwa katika Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo  kwa watumishi (hawapo pichani) wa Hospitali Maalum ya magonjwa ambukizi ya Kibong’oto.

Watumishi toka Hospitali Maalum ya Kibong’oto wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani)

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akitoa cheti kwa Dkt. Stellah Mpagama (kulia) mara baada ya kuzindua mpango wa Remodel. 

Na WAMJW - SIHA, KILIMANJARO

Serikali kuifanya Hospitali ya Kibong’oto kuwa kitovu cha utafiti, tiba na mafuzo ya magonja yakuambukiza na magonjwa yanayopatikana maeneo ya kazini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Hospitali hiyo ya magonjwa yakuambukiza iliyopo Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro jana Novemba 25, 2018.

“Nataka kuona hospitali hii inakuwa kitovu cha mafunzo katika ugonjwa huu wa kifua kikuu, magonjwa yanayopatikana maeneo ya kazi pamoja na magonjwa mengine yakuambukiza” alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa “Wapo watu wanaougua maeneo ya kazini na hufika hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho kabisa za ugonjwa, hivyo kundi hilo nalo inabidi tulifikie kwa wakati”

Pia, Dkt. Ndugulime amesema kuwa takribani watu 150,000 huugua ugonjwa wa kifua kikuu kwa mwaka, huku idadi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu ikiwa ni 63,000 sawa na asilimia 42 huku tafiti zikionyesha kuwa mgonjwa mmoja wa kifua kikuu ndani ya mwaka mmoja anaweza kuwaambukiza watu 20 ugonjwa huo, hivyo kuwataka watendaji kuja na mkakati wa kutoka ofisini kwenda kuwatafuta wagonjwa wa Kifua Kikuu katika maeneo ya makazi.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile Dkt. Ndugulile, amezindua Mpango wa Remodel unaolenga kuongeza uwezo katika tafiti za tiba ili kuweza kudhibiti magonjwa yakuambukiza, kutoa mafunzo ya sayansi  kwa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamiri pamoja na kuandaa miongozo ya namna ya kudhibiti magonjwa yakuambukiza  yaliyopo na ambayo hayategewi kutufikia.

Mpango huo unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya unawaunganisha madaktari wazalendo kutoka hapa nchini ukiongozwa na Dkt. Stellah Mpagama pamoja na madaktari wenza kutoka katika hospitali ya KCMC.

Dkt. Mpagama anasema kuwa wamekuja na mpango huo baada ya kubaini mataifa yaliyopo kusini wa jangwa la sahara yanakabiliwa na idadi kubwa ya magonjwa yakuambukiza  huku miongoni mwa magonjwa hayo kuwa ni Ebola, Homa ya manjano, Homa ya Bonde la Ufa pamoja na ugonjwa wa Kipindupindu.

Dkt. Mpagama amesema kuwa jamii nyingi za nchi za afrika zipo katika mazingira magumu ambayo hupelekea magonjwa yakuambukiza  kusambaa kimzunguko huku idadi ya madaktari waliopo ni ndogo.

“Takwimu toka shirika la afya duniani zinaonyesha katika nchi za afrika kuna daktari mmoja kwa wagonjwa 100,000. Kupitia mpango huu, tunaamini magonjwa haya yakuambukiza tunaenda kuyadhibiti” alisema Dkt Mpagama.

Hospitali Maalum ya magonjwa yakuambukiza  Kibong’oto ilianzishwa mwaka 1925 na Dkt. Noman Davis (raia wa Uingereza) ikiwa ni kituo cha kutibu watu waliokuwa wanaugua ugonjwa wa Kifua Kikuu na mnamo mwaka 2006 Wizara ya Afya iliipa jukumu Hospitali hiyo kutibu ugonjwa sugu wa Kifua Kikuu hadi sasa hospitali hiyo inatoa huduma ya tiba na uchunguzi kwa wagonjwa wa nje na ndani wa Kifua Kikuu huku wastani wagonjwa 120 wa nje na 110 wa ndani hupatiwa huduma za matibabu kila siku.

Mwisho.

0 on: "HOSPITALI YA KIBONG’OTO KUWA KITUO CHA TAFITI, TIBA NA MAFUNZO YA MAGONJWA AMBUKIZI"