Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 29 Novemba 2018

TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA NJIA YA SIMU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiangalia mashine ya mionzi ya CT SCAN katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipoitembea ili kujionea hali ya utoaji wa huduma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa Huduma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohamed Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo.


Picha mbalimbali zikionesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wananchi waliofika kupata huduma za uchunguzi na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kujionea hali ya utoaji huduma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya mifupa (MOI) Dkt. Samuel Swai kuhusiana na kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wakati alipoitembelea Taasisi hiyo Leo Jijini Dar Es Salaam.



TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA KWA NJIA YA SIMU

Na.WAMJW,Dar es Salaam

Taasisi ya mifupa (MOI) imetakiwa kuanzia leo kuwasiliana na wateja wao kwa njia ya simu pale panapotokea mabadiliko ya watoa huduma kutokuwepo mahali pa kazi ilikuepusha usumbufu wa kukaa hospitalini muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukuta wagonjwa wakisubiri kwa muda mrefu kupata matibabu pamoja na vipimo.

Dkt. Mpoki alisema alichokiona kwenye taasisi hiyo ni mawasiliano ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutokupata taarifa za kutokuwepo kwa madaktari wao hivyo kufanya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.

“kuanzia leo taasisi hii itawasiliana nanyi kila inapotokea changamoto inayofanya mabadiliko ya mida yenu na madaktari, mtapigiwa simu sasa wewe utafanya maamuzi yakuja au kusubiri hadi muda ulioambiwa ili uonane na daktari wako muda utakaombiwa”. Alisema Dkt. Mpoki.

Aidha, aliwataka madaktari na wauguzi wawe wanawajulisha wagonjwa mapema wao kwa wale wenye simu kwani kwenye kila jarida la mgonjwa huwa wanaandika namba za simu za wateja wao.

Hata hivyo Dkt. Mpoki alisema hii ni kutokana na mkakati wa Serikali wakutatua changamoto za wananchi wanaofika kupata matibabu kwenye taasisi zake na hivyo kuboresha huduma kwa wahitaji kadri ya uwezo unavyopatikana.

Katibu Mkuu huyo alifanya ziara katika taasisi hiyo kwa kutembelea idara ya Mionzi, wagonjwa wa nje pamoja na kuongea na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali hiyo.

-Mwisho-


0 on: "TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA NJIA YA SIMU"