Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 26 Novemba 2018

VITUO VYA DAMU SALAMA VYATAKIWA KUBORESHA HUDUMA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ameketi kwenye kiti maamul kinachotumika wakati wa kutoa damu alipitembelea kituo cha damu salama kanda ya kaskazini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua taarifa zilitunzwa kwenye kompyuta  katika Kituo cha Damu Salama Kanda ya Kaskazini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikaguanjofoku linatotunza damu salama katika Kituo cha Damu Salama Kanda ya Kaskazini.

Kaimu Meneja Kituo cha Damu Salama Bw. Richard Komanga akiwasilisha taarifa ya kituo kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani)

Moshi, Kilimanjaro

Vituo vya ukusanyaji damu salama nchini vyatakiwa kuboresha huduma zaidi katika ukusanyaji wa damu na kuwa na benki ya damu itakayowasaidia wenye uhitaji muda wote bila kutegemea ndugu au jamaa wa mgonjwa kuchangia damu.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile alipotembelea kituo cha ukusanyaji damu salama kanda ya kaskazini kinachohudumia mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.

“Tangia tumeanzisha mpango huu wa ukusanyaji wa damu salama mwaka 2004 ukuaji wake umekuwa ni wa kusuasua naona bado hatujapiga hatua sana” alisema  Dkt Ndugulile  na kuendela “Zipo changamoto katika upimaji wa damu, huku idadi ya damu salama inayokusanywa ikiwa ni ndogo kulinganisha na uhitaji uliopo”

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imetenga bajeti ya kununua vitendea kazi vya kisasa vitakavyosaidia vituo vya ukusanyaji wa damu salama kukusanya kiasi kingi cha damu ndani ya muda mfupi na kuitaka bohari ya dawa kushughulikia suala hilo haraka ili vituo hivyo vipate vifaa hivyo haraka.

Aidha Dkt. Ndugulile amekiri kuwa kazi ya ukusanyaji wa damu salama hugharimu muda mrefu na fedha nyingi huku damu salama inayokusanywa ikiwa ni kidogo kulishanginsha na muda na gharama zinazotumika na kuwtaka watendaji toka Vituo vya ukusanyaji wa damu salama kuja ma mifumo itakayowawezesha kutumia muda na rasilimali fedha kidogo katika ukusanyaji wa damu salama huku kiwango cha ukusanyaji kikiongezeka.

“Hiki ni kituo cha kanda, ni lazima tuongeze kasi ya ukusanyaji wa damu. Haiwezekani kwa kituo hiki kuwa na damu uniti 70, kiwango hiki bado ni kidogo huku gharama za ukusanyaji bado zipo juu” alisema DKt. Ndugulile
Aidha Dkt. Ndugulile amevitaka vituo vyote vya upimaji wa damu salama nchini kutoa majibu ya vipimo kwa haraka na kuacha mara moja urasimu wa kuchelewesha matokeo ya vipimo vya damu. “tuhakikishe sasa tunaweka mifumo mizuri kuhakikisha damu zinazokusanywa katika vituo vyetu vinatoa majibu kwa haraka ili damu hizo ziweze kutumika kwa walengwa waliokusudiwa.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa zipo changamoto katika uhifadhi wa damu salama na Serikali katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2018/19 imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo 10 vya uhifadhi wa damu salama katika hospitali za rufaa za mikoa huku huku upimaji ukiwa bado unafnayika kwa ngazi ya kanda na kuvitaka vituo vinayohusika na upimaji na uhifadhi wa damu salama kuboresha mifumo ya usafirishaji wa damu salama ili damu ziweze kupimwa kwa haraka na kurejeshwa haraka kwa ajili ya matumizi.

Awali akiwasilisha taarifa yake, Kaimu Meneja Kituo cha Ukusanyaji wa Damu Salama Kanda ya Kaskazini Bw. Richard Komanga, amesema kuwa Kituo hicho cha ukusanyaji wa damu salama huhusisha timu 36 zilizojengwa uwezo wa ukusanyaji wa damu katika ngazi za Halmashauri na Mikoa 4 iliyopo katika Kanda ya kaskazini ambapo wananchi huchangia damu bila malipo. Kituo hicho pia hupima damu zenye maambukizi ambapo damu hupimwa magonjwa ya homa ya ini (b), (c) kasendwe na Virusi Vya Ukimwi.

0 on: "VITUO VYA DAMU SALAMA VYATAKIWA KUBORESHA HUDUMA"