Like us on Facebook

Powered by Blogger.

Search This Blog

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Tuesday, July 16, 2019

RAIS MAGUFULI AMWAGIZA WAZIRI UMMY KUFUATILIA MALIPO YOTE YA SERIKALI KWA WAGONJWA WA NJE YA NCHI

- No comments
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuonesha ishara ya uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando. Kulia kwake ni Baba Askofu Mhashamu Askofu Renatus Nkwande huku kushoto kwake ni Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu akifuatiwa na Waziri wa Nishati Medard Kalemani na mwisho ni Naibu  Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpa mkono Baba Askofu Mhashamu Askofu Renatus Nkwande baada ya kuzindua mradi wa NHIF ikiwa ni moja kati ya miradi 7 iliyozinduliwa yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akieleza jambo wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo kwenye picha) wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Baadhi ya viongozi wa Serikali wakifuatilia Maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo kwenye picha) wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wwakati wa uzinduzi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.


Na WAMJW-MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kufuatilia malipo yote ya Wagonjwa wanoenda kutibiwa nje ya nchi ili kubaini ubadilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.

Rais Magufuli ameagiza hilo leo wakati akizindua miradi Saba ya huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando yenye thamani ya shilingi Bilion15, jambo litalosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa ukaribu pamoja na kuokoa kiasi cha fedha miongoni mwa wanaohitaji huduma. 

"Na kwasababu Waziri wa Afya yupo hapa, akafuatilie malipo yote ambayo tunatakiwa kulipa, kule nje , akikuta kunamalipo yakulipa mtu ambae hakuwa mgonjwa aliyejihifadhi huko, akazilipe mwenyewe " alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 

Rais Magufuli amesema kuwa baadhiya Watendaji waliona kupeleka Wagonjwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu ni fursa yakujipatia kipato, jambo lililokuwa linapelekea hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na malipo kwa baadhiya watu wasiostaholi.

" Hata kupeleka kwa wagonjwa nje kwa Watanzania ilikuwa ni dili, ilikuwa ni fursa kwa Watendaji, wapo watu waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafia, ilikusudi apate safari na msindikizaji, bill zote zinaletwa kwa Serikali " alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 

Dkt. Magufuli aliendelea kusema kuwa ni lazima tujenge nidhamu katika nchi, huku akisisitiza kuwa Serikali haijakataza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wanaostahili kupelekwa kwa matibabu nje ya nchi ni wale walioshindikana ndani ya nchi.

Aidha, Waziri Ummy ameagiza kuboresha uzalishaji wa oksijeni ili kuhakikisha zinazalishwa kwa wingi jambo litalosaidia kuokoa kiwango kikubwa cha mapato kinachopotea kwa kuagiza nje ya nchi, pia itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania. 

"Ninawaomba ndugu zangu, tengenezeni oksijeni nyingi, panueni uzalishaji ili Wizara ya Afya iagize hapa hapa Bugando ili vijana wanaomaliza famasi hapa hapa Bugando wapate ajira hapa yakutengeneza Oksijeni " alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 

Nae, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa hadi kufikia juni 30, 2019 Serikali ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vya umma 5756 (71%),Taasisi za Dini 923 (11%) na vituo vya watu binafsi ni 1440 (18%). 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, pia Serikali, ina Jumla ya Vituo vya Afya vya Mashirika ya Dini ikiwemo Hospitali Teule za Wilaya vipatavyo 43, ambazo zinapata ruzuku (OC) kiasi cha shilingi 30,704,000/= kwa mwezi na mishahara kiasi cha Tshs.1.8 bilioni kwa mwezi kwa ajili ya watumishi 2600. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imepunguza malalamiko ya upatikanaji wa dawa kwa Wananchi na katika hospitali ya rufaa ya Bugando hii ni kufuatia ongezeko la bajeti ya dawa hadi kufikia Tshs.270 bilioni, huku Serikali ikitoa kiasi cha Tshs. milioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kununulia dawa, huku Mwaka 2015/16 walikuwa wanapata Tshs.534 milioni na Mwaka 2018/19 wanapata Tshs.1.5 bilioni.

Naye, Mkurugenzi wa Hospitali ya kanda ya Bugando Prof. Abel Makubi akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, amesema  kwa  kipindi cha miaka minne wamefanikiwa kuboresha huduma za afya na kukamilisha miradi saba ambayo ni  kitengo cha  saratani, mahututi, upasuaji, oksijeni na viwanda vidogo ambavyo vitakuwa vinazalisha dawa kwa ajili ya wagonjwa.

Ameongeza kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ambao walikuwa wanakwenda katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam walikuwa wanatoka Kanda ya Ziwa, hivyo imewapunguzia gharama na usumbufu wa kusafiri kutafuta huduma hiyo.

#tunaboreshaafya

Sunday, July 14, 2019

ZIARA YA MAFUNZO 5S-KAIZEN KWA WAGENI KUTOKA WIZARA YA AFYA NA WATUMISHI YA BANGLADESH

- No comments
Muuguzi Mkuu - Hospital ya Rufaa ya Mkoa- Amana,Beauty Mwambebule akitoa maelezo kwa wageni kutoka nchi ya  Bangladesh namna mfumo wa KAIZEN  unavyofanya kazi katika Hospital hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa kutoka Wizara ya Afya -Idara ya Tiba -Kitengo cha Uratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa,Dkt. Angelina Clarisa Sijaona (kushoto) akiwa na wageni kutoka nchi ya Bangladesh akiwaonesha mambo mbalimbali yanayo tumika kwenye  mfumo wa KAIZEN  katika Hospital Amana  jijini Dar es Salaam.

Wangeni kutoka Bangladesh wakiwa katika Hospital ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam

Picha ya pamoja ya maofisa kutoka wizara ya afya,hospitali ya rufaa ya mkoa Amana pamoja na wageni kutoka Bangladesh baada ya kutembelea hospitali ya Amana

Na.WAMJW,Dsm
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mradi wa Kuimarisha Hospitali za Rufaa za Mikoa (RRHMP) katika kuendelea kuziwezesha Hospitali za Rufaa za Mikoa  ilipanga kukaribisha wageni kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika ili kubadilishana uwezo katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Kulingana na mpango kazi wa mwaka huu, Mradi ukishirikiana na Wizara ya Afya ulitarajia kupokea wageni kutoka Wizara ya Afya na watumishi wa sekta hiyo kutoka nchini Ghana  (7) na Bangladesh (7) kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM pamoja na wawakilishi wa JICA wawili kutoka kila nchi.  Pamoja na hao, tulitegemea kupokea watumishi wa Afya 14 kutoka nchi za kiafrika zikiwemo Uganda, Kenya, Malawi, Liberia, Siera Leoni, Sudan, Zambia, Zimbabwe na Benin.

Tayari wageni wote hawa waliishafika na kupata mafunzo kutoka haya.

Wiki hii, tumewapokea wageni kutoka Katika Wizara ya Afya na watumishi 7 wa sekta na wawakilishi wawili wa JICA-Bangladesh. Wageni hawa watakuwepo hapa nchini kwa wiki moja  Katika kipindi hicho watapata mafunzo ya KAIZEN na leo wametembelea Hospitali za Rufaa ya Mkoa Amana na kesho wanategemewa kutembelea Hospitali za Taifa Muhimbili.

Lengo la ziara hii ni kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN-TQM katika hospitali zetu kwa ajili ya kujifunza na kuiga mazuri ya kujifunza watakaporejea nchini kwao. Aidha, Timu zetu zinategemewa kupata nafasi ya kupata uzoefu kutoka kwa nchi zinazotutembelea.

Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inalenga kuboresha mazingira ya kutoa huduma za afya  na kukidhi mahitaji ya wateja wetu, wale wa ndani na wa nje.

Kwa ujumla wake, falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inarahisha kazi, inahakikisha usalama kwa wateja wa ndani na nje na inapunguza upotevu wa rasilimali, napunguza makosa na inapunguza gharama za uendeshaji.

Kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa ambayo wanaitimia falsafa hii wameweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora, kuongeza katika mapato na wafanyakazi kufurahia mazingira yao ya kazi.

Ni falsafa inayoweza kutumika katika maeneo mbalimbali pamoja na viwandani.

Thursday, July 11, 2019

DKT. NDUGULILE AONEKANA KUTORIDHISHWA NA UTAYARI WA MKOA WA KIGOMA KATIKA KUKABILIANA NA EBOLA

- No comments

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akipimwa joto la mwili na mhudumu wa uwanja wa ndege mara baada ya kufika katika mkoa wa Kigoma ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akioneshwa vifaa vya kujikinga na Ebola kutoka kwa mhudumu wa afya wa bandari ndogo ya Kibirizi Mkoani Kigoma wakati wa ziara yake mkoani humo kuangalia utayari wa mkoa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Mkuu wa Wilaya Samson Anga (kulia kwake) na viongozi wengine wakiwa wanatembelea maeneo mbalimbali katika Bandari ya Mkoa wa Kigoma mapema leo katika ziara yake ya kukagua utayari wa kukabiliana na Ebola mkoani humo.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (Kulia) akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Paul Chaote jinsi ya kuweka vifaa na kupangiliana hema (Isolation centre) kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga

Hema lilotengwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Ebola katika bandari ndogo ya Kibirizi ikiyoko mkoani Kigoma.

Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dawa na vifaa vinavyotumika katika kutibu mgonjwa wa Ebola, kulia ni Dkt. Praygod Swai wa Zahanati ya Bangwe iliyotengwa maalum kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa Ebola akimuonesha vifaa hivyo. 

Na WAJMW-Kigoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo ametembelea baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kigoma kuona utayari wa mkoa huo katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

Dkt. Ndugulile ametembelea maeneo ya Bandari kuu ya Mkoa, Uwanja wa ndege, bandari ndogo ya Kibirizi na Zahanati ya Bangwe ambayo imetengwa maalumu kwa ajili ya kutoa matibabu kwa mtu atakayebainika kuwa na virusi vya Ebola.

Naibu Waziri ameonekana kutoridhishwa na utayari wa Mkoa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini huku akiitaka timu iliyoandaliwa chini ya Mkuu wa Wilaya Samson Anga na Mganga Mkuu wa Mkoa Paul Chaote kuendelea kutoa mafunzo kwa timu iliyoandaliwa jinsi ya kujikinga na kutoa huduma kwa mgonjwa atakayebainika.

“Hatuna mgonjwa wa Ebola ndani ya nchi, lakini kutokana na hali ya ugonjwa huu katika nchi jirani kuna umuhimu wa sisi kama nchi kuendelea kujipanga na kuhakikisha kwamba mifumo yetu yote imekaa vizuri kipindi mgonjwa atakapojitokeza, hivyo nakuomba Mkuu wa Wilaya na Mganga Mkuu wa mkoa kuendelea kusimamia hili”. Amesema Dkt. Ndugulile.

Mapungufu aliyobaini Dkt. Ndugulile ni pamoja na wahudumu kutozingatia kanuni walizofunzwa juu ya kujikinga na maambukizi pindi watakapokua wakihudumia mgonjwa, kutokua na vifaa vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola kama vitanda kwenye vituo vya Isolation na watumishi kutokua na uelewa na utayari wa kutosha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu.

Dkt. Ndugulile yupo Mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na maeneo mengine atatembelea mpaka wa Manyovu ili kuona hali ya utayari ya mpaka huo kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola na kisha atatembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma. 


Mwisho

SERIKALI YATOA BILION 7 UJENZI WA JENGO LA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA

- No comments
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia ramani ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza msafara wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongozana na Mkurugenzi  wa Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200.

Ujenzi wa mradi wa ghorofa sita wenye gharama ya shilingi Bilion 7, katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200 ukiendelea katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mkurugenzi  wa Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji baada ya  ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya


SERIKALI YATOA BILION 7 UJENZI WA JENGO LA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA.

Na WAMJW- MBEYA 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya inajenga jengo la Wazazi lenye thamani ya shilingi Bilioni 7 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na ujenzi wa miradi katika Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya. 

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya nchini ikiwemo huduma za kibingwa ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi wanaohitaji huduma hizo kwa kusafiri umbali mrefu i jambo linalopelekea gharama kubwa na usumbufu kwa wananchi. 

"Tunajenga jengo la wazazi na watoto wachanga la ghorofa sita, ambalo litakuwa na jumla ya vitanda 200, vyumba vitatu  vya upasuaji kwa ajili ya wanawake wajawazito ,vyumba sita kwa ajili ya uangalizi maalum (ICU) kwa wanawake wajawazito, pia vyumba  maalum vinne kwa ajili ya vitoto vichanga (NICU)" alisema Waziri Ummy. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa majengo hayo kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa majengo hayo ili wananchi waanze kupata huduma mapema jambo litalosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto  nchini. 

Aidha, Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kurahisisha gharama za matibabu.

"Nitoe Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini ili waweze kufurahia huduma nzuri lazima wajiunge na huduma za Bima ya Afya, Kuna NHIF Toto Afya kadi kwa mtu yoyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 ni shilingi 50,400 huduma mwaka mzima ndani ya Mbeya na Tanzania kwa ujumla" alisema Mhe. Ummy Mwalimu 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wanawake 100, wanawake 85 wanajifungua bila matatizo yoyote, huku akisisitiza kukamilika kwa ujenzi huu kutasaidia kukokoa wanawake 15 waliobaki kutokana na huduma Bora zakibingwa zitakuwa zikitolewa.

Naye, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kukubali kutenga fedha ili kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200 jambo litalosaidia kutatua changamoto ya ufinyu wa nafasi.

"Tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano, kwa kukubali kutenga fedha kupitia Wizara unayoiongoza ili kuweza kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta, ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200." Alisema Waziri Ummy 

Mwisho.

SERIKALI YASHUSHA NEEMA KWA WANANJOMBE

- No comments
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wakiongea na Wazee waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe wakati alipofanya uzinduzi wa huduma  za Afya katika Hospitali hiyo.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe  wakati alipotenbelea kukagua chumba cha kuhifadhia Dawa katika Hospitali hiyo, wakatikati (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua kadi inayoonesha kiasi cha dawa kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe pindi alipofanya ziara ya kuzindua Huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza juu ya umuhimu wa kuwepo kwa mabango yanayohamasisha haki ya mgonjwa kupata  huduma  za Afya zilozo Bora wakati wa  uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, kushoto kwake (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali moja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu kwa mara ya kwanza katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, ni baada ya kufanya  uzinduzi wa  huduma za Afya katika Hospitali hiyo, Kulia kwake (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wakati wa uzinduzi wa Huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipanda mti wa matunda (mpalachichi) ikiwa ni ishara ya kuhifadhi mazingira, shughuli iliyofanyika baada ya uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akipanda mti wa matunda (mpalachichi) ikiwa ni ishara ya kuhifadhi mazingira, shughuli iliyofanyika baada ya uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ulioongozwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi ramani ya ujenzi wa majengo mengine mapya saba  kwa Mkandarasi, shughuli iliyofuata baada ya uzinduzi  wa huduma katika Hospitali hiyo ya Rufaa  ya Mkoa wa Njombe.

Moja kati ya vyumba vya Wagonjwa kilicho na vitanda pamoja na mashine zakutambua hali ya Mgonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, iliyoanza kutoa huduma rasmi Julai 10, baada ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kufanya uzinduzi huo

Wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ulioongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka (Hawapo kwenye picha)

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka baada ya uzinduzi  wa huduma katika Hospitali hiyo ya Rufaa  ya Mkoa wa Njombe.Na WAMJW-NJOMBE

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeshusha neema kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kutoa kiasi cha shilingi Bilion 7.6 kwaajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kuboresha huduma kwa Wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa huduma za Afya na lililoongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika uzinduzi huo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya katika Mkoa wa Njombe ikiwemo kujenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, jengo la maabara, jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, wodi za wagonjwa gorofa tatu, nyumba za Watumishi tano, pamoja na kichomea taka.

" Tunajenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, tunajenga jengo la jengo la maabara, tunajenga jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, tunajenga wodi za wagonjwa gorofa tatu, tunajenga jengo la kufulia, tunajenga kichomea taka na tunajenga nyumba za watumishi tano" alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa Hospitali hiyo kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa majengo hayo hayo ndani ya miezi kumi ili wananchi wa Mkoa wa Njombe waanze kufaidika na huduma za Afya katika Hospitali hiyo, huku akiwatoa hofu wananchi kuwa pesa zote zipo tayari.

Mbali na hayo, Waziri Ummy mewaasa Wananchi kupambana dhidi ya magonjwa yasiyo yakuambukiza kama Kisukari, shinikizo la damu, Saratani na magonjwa ya Moyo kwa kubadilisha mtindo wa maisha ikiwamo ulaji mlo sahihi , kuacha uvutaji wa sigara na tumbaku, kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na kutofanya mazoezi mara kwa mara.

Aidha, Waziri Ummy ametoa with kwa vijana kujiepusha na mambo ambayo yatapelekea kipata maambukizi ya VVU, huku akiweka wazi kuwa maambukizi mapya ya VVU ni 82,000 kila mwaka nchini Tanzania, huku katika kila watu 100, watu 40 ni vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 umri ambao ni nguvu kazi ya taifa.

"Tunatambua kwamba kuna maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe,lazima tuzingatie kanuni za kujikinga na maambukizi ya VVU, kujizuia kufanya mapenzi kwa vijana hasa kwa wasichana ambao muda wao haijafika, pili kuwa mwaminifu kwa mwenza wako au mpenzi wako na tatu kutumia kinga" alisema Waziri Ummy

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuweka wazi kuwa huduma za Afya katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe haitoathiri utoaji huduma katika Hospitali ya Kibena iliyokuwa Hospitali ya Mkoa, ambayo kwa sasa imerudishwa chini ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.

"Na mimi ntahakikisha wale Watumishi ambao tilikubaliana waje kwenye Hospitali hii, waje na nguo zao , vifaa vyote waviache Kibena na huduma ya Kibena iendelee, na kazi ya Hospitali hii Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wataweka vifaa vyote vitakavyohitajika na huduma zitaendelea" alisema Mhe. Olesendeka

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mhe. Edwirn Mwanzinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya kwa kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba jambo linalosaidia kuokoa kwa kiasi kikubwa maisha ya Wananjombe.

Mwisho.

Wednesday, July 10, 2019

ASILIMIA 90 YA WAGONJWA WA MOYO WANATIBIWA TANZANIA

- No comments
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi kizimia moto kilichotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya vizimia moto 12 vya kisasa vimefungwa katika maeneo mbalimbali ya taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo Asha Luhomo wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Kampuni ya SUKOS KOVA Foundation Suleiman Kova akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile moja kati ya vizimia moto 12 vilivyotolewa na kampuni yake kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution kwa ajili ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi

Na.WAMJW,Dsm

Asilimia tisini ya wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo ya moyo waliokuwa wanatibiwa nje ya nchi, hivi sasa wanatibiwa ndani ya nchi kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI).
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, alipofanya ziara kwenye hospitali hiyo ambapo alitembelea  jengo la watoto lililofanyiwa ukarabati hivi karibuni.

Dkt.Ndugulile alisema Serikali inaendelea kufanya maboresho ya sekta ya afya kuanzia huduma za msingi hadi za kibingwa kwa kuwezesha vituo zaidi ya 352 kutoa huduma za upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni.

Alisema hivi sasa ujenzi wa hospitali 67 za wilaya unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba tangu Uhuru kumekuwako na hospitali 70 za Wilaya pekee, hivyo idadi itaongezeka.
“Nawapongeza sana JKCI kwa maboresho makubwa mliyofanya katika jengo ya watoto ni ya kiwango kikubwa sana, hongereni sana, hivyo hatutarajii hospitali kama hii iwe inatibu magonjwa madogo madogo ambayo yanaweza kutibiwa kwenye hospitali za rufaa za wilaya au mikoa,” alisema.
Aliongeza kusema kuwa, katika miaka minne ya uongozi, serikali imeweza kupiga hatua kubwa kwani ikiwamo kupunguza idadi ya wagonjwa wengi walikua wanatibiwa nje ya nchi.

“Kwa hatua hii, tumeweza kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi tulikuwa tunaweza kuhudumia watu wachache lakini kwa kuwa yanapatikana ndani wananufaika watu wengi, kwa gharama ile ile nje ya nchi angetibiwa mtu mmoja, ndani wanatibiwa watu wapatao watatu,” alibainisha.

Alisema mafanikio hayo ni matokeo ya hatua za kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo madaktari wa ndani (wazalendo) ambapo sasa wanaweza kufanya upasuaji mkubwa wao wenyewe.
“Hivyo, Serikali itaendelea kuwapatia mafunzo wataalam wa afya na kuwapatia vibali kwenda kujifunza ama kusoma nje ya nchi ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini na kuweza kuwatibia wananchi.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile alipokea vifaa vya kuzima moto vipatavyo kumi na mbili vya hospitali hiyo kutoka kampuni ya SUKOS Kova Foundation inayomilikiwa na Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution ya hapa nchini.

Dkt. Ndugulile alisema Watanzania wengi wanafariki wakati wa uokoaji kwani watu wengi hawana elimu ya uokoaji kwani zipo kanuni zinazotumika wakati wa  kumuokoa mtu anayepata ajali.
MWISHO

Monday, July 8, 2019

TANZANIA IMEFANIKIWA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VIKOPE

- No comments
Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira akifungua mafunzo ya Kimataifa ya uchukuaji wa Takwimu za  ugonjwa wa Vikope(Trakoma) yanayofanyika jijini Arusha

Wataalam wa Macho kutoka mataifa mbalimbali wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo

Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya afya,wadau mbalimbali wa macho nchini pamoja na nchi mbalimbali Duniani zikiwemo Afrika Mashariki,Magharibi na Kati


Na.WAMJW,Arusha

Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Trakoma kutoka wilaya 71 hadi
sita ambazo zitaendelea na umezaji kingatiba

Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Dkt.Upendo Mwingira wakati wa mafunzo ya Kimataifa ya uchukuaji wa takwimu za ugonjwa wa vikope(Trakoma) yanayofanyika jijini hapa.

Dkt.Mwingira amesema kuwa kama nchi inajivunia kwa mafanikio makubwa kwani hivi sasa wilaya 65 hazihitaji tena kingatiba kulingana na vigezo vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

"Lengo la WHO hadi ifikapo mwaka 2020 tuwe tumeweza kutokomeza ugonjwa wa Trakoma kama tatizo la kijamii,kwamba hatutaki maambukizi mapya"Alisisitiza Dkt.Mwingira.

Aidha,alisema mwaka 2010 katika tathimini Tanzania kulikua na makadirio ya wagonjwa wa vikope  takribani 160,000,lakini kutokana na jitihada za Wizara ya Afya  hadi Julai 2018 inakadiriwa wagonjwa hao wamepungua mpaka kufikia 17,000.

Hata hivyo Dkt.Mwingira alisema zoezi la kusawazisha vikope hapa nchini linaendelea zaidi ya mikoa kumi sasa hivi katika halmashauri zenye maambukizi.

Mafunzo haya yanahusisha wataalam wa macho kutoka mataifa mbalimbali Duniani na kwa nchi za Afrika yanahudhuriwa na nchi za afrika Mashariki,Magharibi na Kati.

Friday, July 5, 2019

DKT. NDUGULILE ATAKA UONGOZI BORA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.

- No comments

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa wakati akifunga Kikao kazi kilichofanyika kwa siku tano na kupitisha maazimio ya kuimarisha huduma Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa tiba toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Maghembe akiongea wakati wa kilele cha kikao kazi cha Waganga Wafawidhi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi cheti cha pongezi kwa uongozi bora na usimamizi kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt. Yustina Tizeba wakati akifunga kikao cha waganga wafawidhi kilichofanyika Jijini Dodoma.


Picha mbalimbali zikimuonesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi vyeti kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt. Meshack Shimwela wakati akifunga kikao cha waganga wafawidhi kilichofanyika Jijini Dodoma. Hospitali ya Rufaa ya Amana imeongoza na kupata vyeti vitatu ikiwa ni pamoja na kuongoza kupunguza vifo vya mama na mtoto, uongozi bora na mikakati endelevu ya kukusanya mapato.


Picha za pamoja za Viongozi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile, Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula na Wakurugenzi wa Idara Mbalimbali wakati wa kufunga kikao cha Waganga Wafawidhi kilichofanyika katika ukumbu wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Na WAJMW-DOM

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka Waganga wafawidhi kutekeleza maazimio waliyopitisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa siku tano Jijini Dodoma.

Dkt. Ndugulile amesema hayo wakati akifunga kikao hicho kilichohusisha Waganga Wafawidhi, Makatibu Tawala wa Halmashauri na Manispaa pamoja na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya nchini waliohudhuria kikao hicho.

“Ninatambua kuwa katika kikao hiki tumepitia mwongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa za Mikoa na kuweka mipango na mikakati endelevu kwa timu za uendeshaji wa Hospitali hizi, ninaomba sana muende mkatekeleze ili kuimarisha Hospitali zetu za Rufaa za Mikoa. Amesema Dkt. Ndugulile.

Katika kikao hicho Waganga Wafawidhi wameweka maazimio ambayo yataratibiwa katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kukusanya mapato na kuondoa mianya ya upotevu wa mapato, kuimarisha na kuendelea kuzijengea uwezo timu za uendeshaji za Hospitali za rufaa za Mikoa katika kusimamia rasilimali watu, fedha, miundombinu n.k. Kuweka mikakati endelevu ya kupunguza vifo vya mama na mtoto, kila Hospitali kuandaa mkakati wa kununua vifaa na vifaa tiba vitakavyowezesha huduma za kibingwa kutolewa wakati wote, pamoja na kila Hospitali kuja na ubunifu/mikakati ya kukabiliana na upungufu wa watumishi katika maeneo yao kwa kushirikiana na wadau wa mikoa yao.

Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maagizo kwa Waganga Wafawidhi kutekeleza mambo muhimu katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwa na mfumo wa uongozi na utawala, upatikanaji wa watumishi wenye sifa stahiki katika kada zote, uimarishaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma zilizokusudiwa, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba na vitendanishi pamoja na uimarishaji wa matumizi ya teknolojia, taarifa za afya na mawasiliano.

Pamoja na hayo Naibu Waziri amewapongeza Waganga Wafawidhi kwa kushiriki kikao hicho na kuwataka kwenda kutekeleza maazimio waliyopitisha ili kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa katika maeneo tofauti yaliyokusudiwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kabla ya kufunga kikao Dkt. Ndugulile alitoa vyeti vya ubora wa huduma na pongezi, ambapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Katavi Dkt. Yustina Tizeba alipata cheti cha pongezi kwa muongozo wa maono, uongozi bora na usimamizi huku Hospitali ya Rufaa ya Amana ikipata vyeti vitatu vya ubora ikiwa ni pamoja na kuongoza katika kupunguza vifo vya mama na mtoto, uongozi bora na mikakati endelevu ya kukusanya mapato na kuwepo kwa vifaa na vifaa tiba vinavyotumika katika huduma za kibingwa.

MWISHO