Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 7 Januari 2019

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WAKANDARASI UTEKELEZAJI MIRADI KATIKA SEKTA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII NCHINI.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Afya Afisa tabibu COTC Bw. Geoffrey Mdede wakati wakiwa katika chumba cha darasa chuoni hapo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua vyoo vya wanafunzi wa Chuo cha Afya Afisa tabibu COTC Songea wakati akiwa katika  ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Ruvuma

Wanafunzi wa Chuo cha Afya Afisa tabibu COTC Songea wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea taarifa ya hali ya utendaji katika chuo cha Afisa tabibu COTC Songea wakati akiwa katika  ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Ruvuma.


Kaimu Mkuu wa chuo cha Afisa tabibu COTC Songea akisoma taarifa ya utendaji wa chuo hicho mbele ya Naibu Waziri wa Afya, Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha) wakati  wa  ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Ruvuma.


Mkuu wa Wilaya ya Songea mhe. Pololeti Mgema akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile (hayupo kwenye picha) ili aweze kuzungumza na wanafunzi na uongozi wa chuo cha Afisa tabibu COTC Songea,


Na WAMJW - RUVUMA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Halmshauri zote nchini kutotumia wakandarasi katika kujenga miradi inayohusu Sekta ya Afya na Maendeleo  ya Jamii nchini, bali kutumia mtindo wa 'Forced Account' (kuwahusisha mafundi wa kawaida katika kujenga miradi hiyo)

Agizo hilo limetolewa mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na  kujionea ukarabati na ujenzi katika Chuo cha Wauguzi Songea na Chuo cha Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya  ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani hapo.

Dkt. Ndugulile amefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa baadhi ya majengo na ukuta wa Chuo cha Afisa tabibu (COTC - Songea) mkoani humo ambao unagharimu  zaidi ya Shilingi millioni 900 ambazo fedha hizo zingetumia mtindo wa 'Forced Account' zingejenga majengo mengi zaidi na ukuta.

Aidha, Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa katika zama hizi,  Serikali ya Awamu ya Tano itazingatia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya Maendeleo na Wizara itasimamia kwa karibu Miradi hiyo.

"Niseme tu ni marufuku kutumia wakandarasi katika kutekeleza miradi inayohusu Wizara hii niliyopo labda muyafanye haya wakati mimi sipo" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.Pololeti Mgema amemuahidi Naibu Waziri huyo kusimamia uendeshaji wa vyuo vyote  vilivyopo katika Wilaya yake kwa ukaribu.

Akitoa taarifa ya ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Wauguzi Songea Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Geoffrey  Mdede amesema Chuo kinakabiliwa na changamoto za miundombinu pamoja na  upungufu wa wakufunzi ambapo mpaka sasa kuna wakufunzi saba wanaofundisha jumla ya wanafunzi 105.

MWISHO.

0 on: "SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WAKANDARASI UTEKELEZAJI MIRADI KATIKA SEKTA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII NCHINI."