Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 25 Julai 2019

SERIKALI YA CHINA NA TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Afya kutoka China Mhe. Lin Bin wakiwa wameshikilia dawa ambazo hutengenezwa nchini China mapema leo wakiwa Ikwiriri-Rufiji Mkoani Pwani kuzindua Mradi wa Ushirikiano baina na China na Tanzania katika Kupambana na Ugonjwa wa Malaria Wilayani Rufiji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiangalia kinga za ugonjwa wa malaria pamoja na Naibu Waziri wa Afya kutoka China Mhe. Lin Bin leo Ikwiriri-Rufiji Mkoa wa Pwani kabla ya uzinduzi wa mradi wa  ushirikiano wa pamoja kati ya China na Tanzania kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipima ugonjwa wa Malaria leo Ikwiriir Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani alipoenda kuzindua Mradi wa Ushirikiano wa pamoja baina ya Tanzania na China wa kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Afya China wakisalimia mtoto katika Kituo cha Afya Ikwiriri- Rufiji Mkoa wa Pwani leo kabla ya kuzindua Mradi wa Ushirikiano baina ya Tanzania na China wa kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea hundi kutoka Taasisi ya Fosun Pharma ya china kwa ajili ya dawa za malaria katika Wilaya ya Rufiji.
Picha ya pamoja Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa kati kati mstari wa chini)  akiwa na Naibu Waziri wa Afya China Mhe. Lin Bin aliyeongozana na wataalam wake kutoka China pamoja na wataalam na wadau wa  sekta ya afya nchini


Na WAMJW - Rufiji, Pwani.

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi salama isiyo ya maambukizi ya Ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya kutoka Uchina Mhe. Lin Bin alipotembelea Ikwiriri, Rufiji Mkoa wa Pwani katika mradi wa ushirikiano wa pamoja baina ya China na Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa malaria huku akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

“China kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimatafa tutaendelea kushirikiana kwa pamoja katika kusaidia Tanzania inafikia malengo ya kutokomeza ugonjwa wa malaria” amesema Mhe. Lin Bin na kuendelea kusema Ugonjwa wa malaria unatibika na kuzuilika

Waziri Lin Bin amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na China umeleta manufaa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo Wilayani Rufiji kutoka asilimia 25 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 4.9 mwaka 2019.

“Kwa muda wa miaka 60 tumekuwa tukipambana dhidi ya ugonjwa wa malaria ambao umeathiri zaidi ya watu milioni 30, na tangia mwaka 2017 hakuna taarifa zilizolipotiwa kuhusu ugonjwa wa malaria nchini China” amesema Mhe. Lin Bin huku akiipongeza Tanzania kwa mikakati mizuri yenye lengo la kuhakikisha inatokomeza ugonjwa wa malaria.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu ameishuruku Serikali ya China inayoongozwa na Rais Xi Jinping kwa kuendeleza ushirikiano wa enzi uliopo wa baina ya nchi hizo.

Waziri Ummy amesema kuwa ugonjwa wa malaria bado ni tatizo kubwa sana nchini Tanzania, huku takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zikionyesha kuwa asilimia 55 ya vifo vitokanavyo na malaria vinatoka katika nchini saba za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tumechukua hatu ambali mbali kwa kushirikiana na wadau wakiwemo China kupambana na malaria na yapo mafanikio makubwa ambayo tumeyapata” Amesema Waziri Ummy Mwalimu na kuendelea “Tumeweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 14.7 mwaka 2015 hadi 7.3 mwaka 2018”

Amesema kuwa wagonjwa wapya wa malaria wamepungua kwa asilimia 26 kutoka watu 161 katika kila watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia 119 katika kila watu 1000 mwaka 2018 huku vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kwa asilimia 55, kutoka vifo 20 katika watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia vifo 9 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

“Serikali ya Tanzania itaendela kuchukua hatua kwa kushirikiana na wadau wetu wakiwemo Serikali ya China kuhakikisha tunapunguza kiwango cha maambukizi ya maralia hadi kufikia asilimia 1 ifikapo mwaka 2020” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

MWISHO.

0 on: "SERIKALI YA CHINA NA TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA."