Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 1 Agosti 2019

TANZANIA YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Mgeni rasmi wa mkutano huo wa NTD ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Elias Kwesi akifungua mkutano huo ambao unawakilishwa na waratibu wa mpango huo kutoka mikoa mbalimbali,wadau wa ndani na nje ya nchi

Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka wizara ya afya Dkt.Leonard Subi akiongea na vyombo vya habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira akifanya utambulisho wa wageni walioshiriki mkutano wa mwaka wa mapitio na kutengeneza mpango kazi wa mwaka unaofanyika jijini Dar es Salaam

Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt. Christine Musanhu akipeana mkono na Mgeni rasmi wa mkutano huo mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt.Elias Kwesi

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za kitaifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

Kaimu Mwakilishi mkazi wa shirika la afya duniani(WHO)Dkt. Christine Musanhu akiongea kwenye mkutano huo.

Mratibu wa NTD Dkt.Upendo Mwingira akisalimiana na mgeni rasmi Dkt.Elias Kwesi

 Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa mkutano huo.


TANZANIA  YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia wizara ya afya imepiga  hatua katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa wa Wizara hiyo, Dk. Elius Kwesi wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya shuguli wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na mpango kazi wa mwaka.

Dkt.Kwesi alisema mkutano huo ni muhimu kwani watajadiliana na wadau hao kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara hiyo kwa upande wa rasilimali fedha.

"Tuna pengo la rasilimali  mbalimbali  na tumewaita hapa Wadau kujadiliana nao Mpango kazi wetu  na kuangalia namna gani watatusaidia kuziba pengo na kutakavyosaidiana kutekeleza," alisema Dkt.Kwesi

Alisema tangu utekelezaji wa Mpango huo ulipoanza nchini umefanikiwa kupunguza magonjwa hayo kwa kiwango cha asilimia 80.

Awali Mkurugenzi wa huduma za Kinga wizarani hapo Dkt.Leonard Subi alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yasipodhibitiwa yatapelekea watu wengi kuugua siku zijazo kwani yana athari kubwa na kusababisha upofu na ulemavu kwa jamii.

“mfano ugonjwa wa kichocho kwa watoto huathiri ukuaji na wengine wanaweza kupata saratani katika maisha yao".Alisema Dkt.Subi

Alisema wizara kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya jitihada kubwa na hivyo kufanikiwa kudhibiti magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa

"Wilaya ambazo zilikua zimeathirika sana na matende na mabusha miaka kumi iliyopita zilikua takribani 120 lakini hivi sasa zimebaki wilaya 24 ambazo bado tunaendelea na ugawaji kingatiba na trakoma kulikuwa na wilaya 71 na sasa zimebaki wilaya sita tu".

Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira amesema kwa upande wa kichocho na minyoo ya tumbo bado inahitajika   kuendelea kuwakinga watoto na baadhi ya wilaya wanaendelea kugawa kingatiba za matende na mabusha pamoja na usubi.

Mwisho

1 on: "TANZANIA YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE"
  1. This is my first visit to this website, you have shared useful content which i like reading. I have bookmarked the website to read more similar content !

    NBA농구분석
    NBA라운드티
    NBA라이브스코어

    JibuFuta