MWISHO
Jumatano, 19 Agosti 2020

HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO ZIMEENDELEA KUIMARIKA NCHINI
Jumamosi, 8 Agosti 2020
WAZIRI UMMY APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUPEWA VIDONGE VYA FOLIC ACID MASHULENI
NA EMMANUEL MALEGI-MOROGORO
“Mbali na kuanzishwa kwa
bustani shuleni lakini pia fedha hizo zinaweza kupelekwa kwa vijana ili
waanzishe miradi ya bustani za mboga kwa ajili ya kuzalisha mazao yanayozalisha
asidi hiyo yakiwemo maboga, matunda na hata karoti badala ya kutoa vidonge kwa
wanafunzi”. Amesema Ummy.
Kuhusu unywaji wa maziwa mashuleni, Waziri Ummy amesema kuwa atamwandikia
barua ya pendekezo Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ili kuanzia
Septemba mosi mwaka huu kila shule iwe na kibanda cha maziwa kwa ajili ya
wanafunzi kununua.
Jumatatu, 3 Agosti 2020
WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUTUMIA UTAALAMU WAO KWA AJILI YA USTAWI WA TAIFA
Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Wauguzi na Wakunga nchini wametakiwa kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo iliyopo wakati wakitoa huduma kwa weledi ili kufikia malengo na matumaini ya wateja kwa ajili ya ustawi wa Taifa.
Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Idara Kuu ya Afya Bw. Edward Mbanga wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi wauguzi wakuu wa wilaya kinachofanyika jijini Dodoma.
Bw. Mbanga amesema kuwa wauguzi na wakunga ndio watendaji wakuu katika vituo vya afya kwenye ngazi ya jamii hadi Taifa hivyo uwajibikaji mzuri na utawala bora utaboresha utendaji hali itayosaidia kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea katika ngazi zote.
"Viongozi mnatakiwa kuwa wabunifu, wachapa kazi, wenye nidhamu na mfano bora wa kuigwa katika utekelezaji wa majukumu yenu,kwahiyo ni lazima msimamie utoaji wa huduma uliyo mzuri na wenye heshima na utu.”Alisema
Aidha, Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwakumbusha washiriki hao kuwa, suala la huduma za uuguzi na ukunga ni suala la ubinadamu zaidi na kuvaa viatu vya wagonjwa wao.
“Hakuna aliyegongwa muhuri wa kuugua au kuwa mgonjwa akalazwa ,sisi sote ni wagonjwa watarajiwa kwahiyo kama ambavyo sisi tungependa kuuguzwa vizuri, kijibiwa kwa kauli nzuri basi tuhakikishe tunasimamia maadaili ya kazi”.Alisisitiza Mbanga.
Hatahivyo alisema kuwa, Serikali inawahakikishia itaendelea kufanya kazi pamoja na waauguzi kwa kutoa miongozo thabiti na kuhakikisha upatikanaji wa nyenzo muhimu katika hospitali na vituo vya kutolea huduma ya afya na kuboresha mazingira ya kazi yaliyo bora na salama.
Aliendelea kusema kuwa, hivi karibuni kumekuwa na malalamko mbalimbali ya kiutendaji na kitaaluma kutoka kwa wateja wanaofika kupata huduma za afya na hivyo kuleta taswira mbaya kwa taaluma yao na kuonyesha hakuna usimamizi mzuri wa utoaji huduma za uuguzi na ukunga.
“Tungependa wateja wetu watoe sifa badala ya malalamiko hivyo kikao hiki mje na mipango ya kuondokana na malalamiko kwani taaluma yenu ni zaidi taaluma." alisema.
Hata hivyo, amewakumbusha viongozi hao kuwa mstari wa mbele kupambana dhidi ya rushwa na kuhakikisha inatokomezwa katika maeneo yao ya kazi kwani rushwa imekuwa ikilalamikiwa na kuripotiwa katika kada ya afya nchini.
-MWISHO-
Ijumaa, 12 Juni 2020
DKT. MOLLEL ATETA NA MADEREVA WA MALORI, NAMANGA
Ijumaa, 14 Februari 2020

HOSPITALI YA WILAYA MWANGA YAPEWA WIKI MBILI KUJA NA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA VIPIMO MUHIMU VYA AFYA
Na WAMJW - Mwanga, Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kuandaa mkakati madhubuti utakaowawezesha kuwa na vipimo muhimu vya afya.
Dkt Ndugulile ametoa agizo hilo leo alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kujionea hali ya utoaji huduma na kubaini kuwa hospitali hiyo haina vipimo vya damu, vipimo vya kemia pamoja vipimo vya CD4.
”Kwa miaka miwili sasa hakuna vipimo vya msingi katika hospitali hii, tunawakosesha huduma wananchi” amesema Dkt. Ndugulile
”Haiwezekani Hospitali kubwa ndani ya Wilaya kukosa vipimo vya msingi, haiwezekani mtu hapa sasa hivi anahitaji kipimo cha damu atoke hapa aende Hospitali ya Mawenzi Moshi kwa ajili ya vipimo” amesema Naibu Waziri Ndugulile.
Katika hatua za kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Waziri Ndugulile ameushauri uongozi wa afya ndani ya Wilaya kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua vifaatiba hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za vipimo ndani ya Wilaya ya Mwanga.
Aliendelea kushauri kuwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wao wanatoa mkopo wa majengo na vifaa kwa taasisi za umma na binafsi, mnaweza kuwafikia NHIF na kujadili kuhusu suala hili.
”Huko kwingine wanazitumia hizo fursa, kaeni na watu wa NHIF, Meneja wa NHIF kaa na viongozi wa Hospitali hii ikiwezekana mkubaliane hivyo vitu vipatikane kwa haraka” ameshauri Dkt. Ndugulile.
”Naamini mna wadau wa maendeleo ambao mnashirikiana nao katika mambo mbalimbali, timu ya afya ndani ya mkoa, wilaya pamoja na hospitali nawaombeni sana tuwe tunaomba vitu ambavyo vina manufaa kwa wananchi” amesisitiza Dkt. Ndugulile.
Awali akitoa salamu za wananchi wa Wilaya ya Mwanga, Mbunge wa Jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa changamoto ya kijiografia ndani ya Wilaya hiyo inachangia wananchi kukimbilia hospitali za Wilaya jirani ili kuweza kupata huduma.
”Wilaya yetu hii ina upande wa mlimani na huku tambarare, wananchi wengi walio huku tambarare wanaona ni bora kwenda Moshi kwa ajili ya matibabu kuliko kwenda juu mlimani iliko Hospitali” amesema Prof. Maghembe.
Hata hivyo Prof. Maghembe amesema kuwa tayari ndani ya Wilaya wameshaanza taratibu za kujenga Hospitali nyingine eneo la chini (tambarare) ili wananchi wanaoishi maeneo hayo waweze kupata huduma za afya ndani ya Wilaya ya Mwanga.
-Mwisho-
Jumatano, 5 Februari 2020

MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 27
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akisikiliza maoni ya washiriki, wakati kikao na umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance).
Na WAMJW - Dodoma.
Maambukizi mapya ya ugonjwa wa malaria yamepungua nchini kwa asilimia 27 na hiyo ni kutokana na kuboreka kwa utoaji huduma za mapambano ya ugonjwa huo ukilinganisha na waginjwa 164 kati ya watu 1000 mwaka 2015 hadi wagonjwa 119 kati ya watu 1000 mwaka 2018.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wakati akitoa taarifa kwa umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance) waliofika wizara ya afya kufanya uraghibishaji wa kadi ya tathimini ya malaria kwa ajili ya uwajibikaji na utendaji kwa viongozi wa wizara jijini hapa.
Dkt. Subi amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na jitahada za viongozi wa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na muhimili wa Bunge katika ushirikiano mzuri na wadau pamoja ma wananchi katika kupambana na ugonjwa huo.
Amesema kuwa viongozi wa nchi za afrika wanawajibika kwa afya za wananchi na hivyo kwa Tanzania vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua kwa asilimia 63 kutoka vifo 6,737 mwaka 2015 hadi 2,540 mwaka 2018.
“Ingawa hivi sasa tupo kwenye kudhibiti ila tunalengo la kutokomeza,hivyo tuna imani kwamba tanzania tunao uwezo mkubwa wa kufikia huko kwani kuaniza Mh. Rais Wetu hadi muhimbili kama Bunge nao wako mstari wa mbele kuondosha malaria nchini”.
Aidha, amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kupungua kwa wagonjwa wanaougua malaria kupungua pia hata kwa watoto chini ya miaka mitano vifo vimepungua.
“Tanzania tumeamua kupambana na wadudu dhurifu kuanzia ngazi ya viluilui hadi mbu wapevu waenezao maradhi, hivyo kila mwananchi anawajibu wa kuchukua hatua, hivyo ni vyema tukaungana ili kuiondosha Malaria nchini”.Amesema Dkt. Subi
Naye Katibu wa TAPAMA Mhe. Raphael Chegeni amesema kuwa msingi wa taifa ni kuwa na afya ,hivyo wanafarijika na afua zinazochukuliwa na wizara ya afya katika kupambana na malaria nchini “Malaria inaua hivyo tunajivunia kuona tanzania inazidi kupambana kutokomeza ugonjwa huu.
Kadi ya tathimini ya malaria ni kitendea kazi cha usimamizi kilichotolewa na wizara ya afya kinachoonyesha takwimu za utendaji wa viashiria vya malaria vilivyopewa kipaumbele katika ngazi ya mikoa na wilaya ambayo inaleta urahisi katika kutambua wapi kuna tatizo ili hatua za kuokoa maisha ziweze kuchukuliwa.
Jumapili, 26 Januari 2020
KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI
Bibi Catherine Mushi akiendesha kinu cha kuzalisha hewa safi (Oxygen plant) katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC.
Mtaalam wa kutengeneza baskeli za magurudumu matatu(wheelchair) Bw. Samson Shirima akiwa katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Grace Manyika akiweka alama za ukomo wa matumizi ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika kiwanda hicho kilichopo hospitali ya KCMC, Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu, KILIMANJARO.
IMEELEZWA kuwa uwepo wa kinu kipya na cha kisasa chenye uwezo wa kufua hewa ikiwemo hewa safi ya Oxygen na ile ya Naitrojeni kitakuwa msaada kwa wenye tatizo la uzazi nchini.
Akizungumzia hospitalini hapo ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya yenye lengo la kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uwamu ya tano ndani ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Kaimu Mkurugenzi wa KCMC Dkt. Sarah Urasa alisema:
"Uhifadhi wa mbegu za kiume na kike upo mbioni kuanza hapo baadae. Hatua hiyo kwani tayari tumeanzisha klininiki maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya uzazi ambayo tunaonana na wagonjwa kwa wiki mara moja ambapo huwahudumia watu 10 mpaka 12." Alisema.
Mbali na kazi hiyo kinu hicho kinauwezo wa kufua hewa ya Oksijeni ambayo kwa kiwango kikubwa hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupumua ambapo kwa siku mitungi 400 hufuliwa katika kinu hicho.
Dkt. Sarah Urasa aliongeza kuwa: "Hii ni hospitali ya kwanza kuwa na kinu ya kufua hewa ya oksijeni na Nitrogen hapa nchini.
Hewa ya Oksijeni pia inatumika kwa wale wagonjwa wanaopewa dawa za usingizi kwaajili ya upasuaji, hewa ya nitrogen inatumika kuhifadhi sampuli kutoka kwa wagonjwa,tiba kwa magonjwa ya ngozi vile vile hutumika kukata matokeo kwenye ngozi au kwenye viungo vya uzazi" alisema.
Huduma hiyo ambayo imeanza mwaka huu Dkt. Sarah alisema ununuzi wa mitungi ya gesi ya oksijeni pekee ulikuwa ukiwagharimu takribani milioni tatu kwa wiki huku gharama za usafirishaji ikiwa haijajumuishwa hatua ambayo imeokoa gaharama za uendeshaji hospitalini hapo.
Dkt.Sarah alieleza kuwa kwa kadiri uzalishaji unavyoongezeka katika kinu hicho wataanza kutumia mfumo wa kuunganisha gesi moja kwa moja hadi katika kitanda cha mgonjwa.
"Tumeona uharibifu mkubwa unaotokana namitungi hii ya gesi sakafu yetu imekuwa ikiharibika kutokana na uzito wa mitungi yenyewe kwahiyo mfumo tutakapkuja kuutumia utakuwa bora zaidi tofauti na sasa "alisema.
Mafanikio mengine aliyoyataja Dk.Sarah alisema katika utawala wa Rais Dk.John Magufuli wamefanikiwa kuanza kutengeneza maji tiba 'dripu' kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa ndani na nje ya hospitali.
"Hii inetusaidia kwa kiwango kikubwa hata hospitali zingine zimekuwa zikifika hapa kwaajili ua kujifunza namna ya kutengeneza maji tiba "alisema.
Pia alisema KCMC ndio kituo pekee inayotambulika kimaitafa kutoa mafunzo ya magonjwa ya ngozi na zinaa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.
"Kituo hiki ndio kinachozalisha mafuta ya ngozi kwaajili ya watu wenye ualbino na tayari tumeingia makubaliano na Bohari kuu ya Dawa MSD kwaajili ya kusambaza dawa na tayari tumefikia mikoa 25 kwa kutumia mfumo wetu wa usambazaji na sasa MSD watatuongezea nguvu ili kusambazwa nchi mzima "alisema
Kwa upabde wake, Mhandisi KCMC Dustan Kanza alisema mgonjwa mmoja hutumia mtungi mmoja lengo kuepukana na maambukizi.
Alisema katika kinu hicho kwa saa 24 inauwezo wa kuzalisha mitungi 400 na mpaka sasa tayari zaidi ya mitungi 600 imezalishwa tangu kuanza kufanya kazi kwa kinu hicho januari mwaka huu.
Mwisho.
Jumatatu, 16 Desemba 2019
MAOFISA AFYA WATAKIWA KUWAKINGA WANANCHI DHIDI YA MAGONJWA-DKT. SUBI
Na Catherine Sungura, WAMJW - Dodoma
Maofisa afya wa mikoa na halmashauri wametakiwa kusimamia afya ya jamii kwenye maeneo yao ili wananchi wajikinge dhidi ya magonjwa yakuambukiza na yele yasiyoambukiza.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kinga Dkt. Leonard Subi wakati akiongea na maofisa hao ambao wanakutana jijini hapa kwa kikao kazi cha siku tatu wakijadili utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa kwanza mwaka jana na Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
“Mkutano huu ni wa pili mwaka huu,ni mkutano muhimu kwa maofisa afya kwani ndio wasimamizi wa shughuli za afya katika ngazi za jamii kwa kuhakikisha wananchi wanajikinga na maradhi, kula chakula bora kuishi makazi bora,usafi wa mazingira pamoja na kuwa vyoo bora”.Amesema Dkt. Subi
Aidha, amesema katika mkutano huu mambo mbali mbali yatajadiliwa ikiwemo afya mazingira,usafi na uchafuzi wa mazingira na kila kinachotumiwa na kumzunguka mwananchi ,pia wataangalia mabadiliko ya tabia nchi na kupata taarifa kutoka ngazi za mikoa ni jinsi gani walivyotekeleza majukumu yao.
“Maafisa afya muendelee kuishauri wizara kwa kutumia takwimu kwani tunatarajia mkutano huu mtabadilishana uzoefu kutoka sehemu zenu za kazi,kama wizara tumekua tukitengeneza sera na miongozo mbali mbali ya kudhibiti maradhi yote yanayoweza kuathiri afya za binadamu hivyo kazi ya wizara ni kukusanya taarifa,kuchakata na kuzitolea miongozo na maelekezo”. Aliongeza Dkt. Subi.
Hata hivyo amesema maofisa hao wana majukumu ya kusimamia na kulinda afya mipakani ili kusiingie magonjwa ya milipuko kutoka nje hususan nchi za jirani pamoja na utoaji wa chanjo ambapo Tanzania ipo vizuri.
Mkutano huo ambao utafunguliwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu umebeba Kauli mbiu isemayo “Huduma bora za afya mazingira na usafi ni kichocheo muhimu cha uchumi endelevu.
Alhamisi, 12 Desemba 2019
SERIKALI YAAGIZA HOSPITALI ZOTE NCHINI KUANZISHA MFUKO WA FEDHA ZA DAWA.
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- MWANZA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeagiza Waganga Wakuu wa Vituo vya Afya na Hospitali zote nchini kuanzisha mfuko wa fedha za Dawa kupitia makusanyo ya fedha za ndani, ili kuweza kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa dawa nchini endapo itatokea.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza.
"Kuanzia Vituo vya Afya, Hospitali zote za Halmashauri, za Mikoa , kuanzisha mfuko wa fedha za dawa, na vyanzo vikuu vya mifuko hii ni mapato yatokanayo na mauzo ya dawa, huduma za Maabara, huduma za mionzi" alisema Waziri @umwalimu.
Amesema, Bodi hiyo ya ushauri lengo lake kubwa ni kuhakikisha inaboresha huduma za kinga na tiba katika Hospitali, huku ikihakikisha huduma hizo zinaifikia wananchi kwa ubora na gharama nafua.
Aliendelea kusema, Sera ya Afya nchini inawataka Wananchi kuchangia huduma kwa gharama nafuu isipokuwa kwa makundi yote ya msamaha, wakiwemo Wazee, Watoto walio chini ya miaka mitano na mama wajawazito, hivyo kuwataka kuweka mifumo mizuri ili kurahisisha utoaji huduma.
Mbali na hayo, Waziri Ummy ameiagiza Bodi hiyo kuhakikisha inaboresha huduma za dharura na ajali, ili kuokoa vifo vitokanavyo weza kuepukika kupitia huduma za dharura, keisha kuwashauri kujenga jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) ili kuboresha huduma kwa wananchi.
"Watu wengi wanakufa wakiwa getini Mwa Hospitali, wakati utaalamu upo, kwamba mkiboresha huduma za dharura na ajari, tunaweza kuokoa maisha ya watu wengi " alisema Waziri @umwalimu.
Aidha, Waziri Ummy ameeleza majukumu ya Bodi hiyo ni kushauri, kutengeneza, kusimamia na kupitisha miongozo, malengo na mipango mikakati ya Hospitali kulingana na Sera na miongozo ya Serikali.
Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou-Toure Dkt. Dkt. Graham Mtui ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwa kuleta mashine ya uchunguzi wa figo na ini, mashine ya kusafisha figo ambazo zinatarajia kuanza kutoa huduma Januari 2020.
Kwa upande mwingine amesema, Hospitali inatarajia kupokea mashine sita ikiwemo CT Scan, X- ray yakidigitali, vifaa vya mifupa na mashine zinazosaidia kupumulia kutoka MSD.
Hata hivyo, amesema kuwa, idadi ya Wagonjwa wanaofika kupata huduma, kutoka wastani wa wagonjwa 350 kwa siku kwa mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa kati ya 500 mpaka 700 kwa Mwaka huu 2019, huku akiweka wazi kupunguza Rufaa za kwenda Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Bugando kwa asilimia 50.
"Kutokana na mafanikio hayo, idadi ya wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali imeongezeka, kutoka wastani wa wagonjwa 350 kwa siku ambayo ilikuwa mwaka 2015, na kufikia wastani wa wagonjwa kati ya 500 hadi 700 kwa mwaka huu 2019", alisema Dkt. Graham Mtui.
Mwisho.







