Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Bugando. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Bugando. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 26 Januari 2020

KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) Dkt. Sarah Urasa akizungumza katika Mkutano wa Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake katika kampeni ya "TumeboreshaAfya".

Bibi Catherine Mushi akiendesha  kinu cha kuzalisha hewa safi (Oxygen plant) katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC.

 Mtaalam wa kutengeneza baskeli za magurudumu matatu(wheelchair) Bw. Samson Shirima akiwa katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

Madaktari pamoja na wauguzi wakiwahudumia watoto  njiti katika wodi maalum ya watoto hao   KCMC.

Mtaalam kutoka Idara ya ngozi Bw. Maghembe Juma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kilimanjaro KCMC akitengeneza dawa na mafuta maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika Hospitali hiyo.

Grace Manyika akiweka alama za ukomo wa matumizi ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika kiwanda hicho  kilichopo hospitali ya KCMC, Kilimanjaro.

Mtambo wa kinu cha kisasa cha kuzalisha hewa safi (oxygen plant)wenye uwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa siku ambao upo katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kaskazini KCMC.

KCMC



KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI

Na Mwandishi wetu, KILIMANJARO.

IMEELEZWA kuwa uwepo wa kinu kipya na cha kisasa chenye uwezo wa kufua hewa ikiwemo hewa safi ya Oxygen na ile ya  Naitrojeni kitakuwa msaada kwa wenye tatizo la uzazi nchini.

Akizungumzia hospitalini hapo ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya yenye lengo la kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uwamu ya tano ndani ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Kaimu Mkurugenzi wa KCMC Dkt. Sarah Urasa alisema:

"Uhifadhi wa mbegu za kiume  na kike upo mbioni kuanza hapo baadae. Hatua hiyo kwani tayari tumeanzisha klininiki maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya uzazi ambayo tunaonana na wagonjwa kwa wiki mara moja  ambapo huwahudumia watu 10 mpaka 12." Alisema.

Mbali na kazi hiyo  kinu hicho kinauwezo wa kufua hewa ya Oksijeni ambayo kwa kiwango kikubwa hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupumua ambapo kwa siku mitungi 400 hufuliwa katika kinu hicho.

Dkt. Sarah Urasa aliongeza kuwa: "Hii ni hospitali ya kwanza kuwa na kinu ya kufua hewa ya oksijeni na Nitrogen  hapa nchini.

Hewa ya Oksijeni pia inatumika kwa wale wagonjwa wanaopewa dawa za usingizi kwaajili ya upasuaji, hewa ya nitrogen inatumika kuhifadhi sampuli kutoka kwa wagonjwa,tiba kwa magonjwa ya ngozi vile vile hutumika kukata matokeo kwenye ngozi au kwenye viungo vya uzazi" alisema.
 
Huduma hiyo ambayo imeanza mwaka huu Dkt. Sarah alisema ununuzi wa mitungi ya gesi ya oksijeni pekee ulikuwa ukiwagharimu takribani milioni tatu kwa wiki huku gharama za usafirishaji ikiwa haijajumuishwa hatua ambayo imeokoa gaharama za uendeshaji hospitalini hapo.

Dkt.Sarah alieleza kuwa kwa kadiri uzalishaji unavyoongezeka katika kinu hicho wataanza kutumia mfumo wa kuunganisha gesi moja kwa moja hadi katika kitanda cha mgonjwa.

"Tumeona uharibifu mkubwa unaotokana namitungi hii ya gesi sakafu yetu imekuwa ikiharibika kutokana na uzito wa mitungi yenyewe kwahiyo mfumo tutakapkuja kuutumia utakuwa bora zaidi tofauti na sasa "alisema.

Mafanikio mengine aliyoyataja Dk.Sarah alisema katika utawala wa Rais Dk.John Magufuli wamefanikiwa kuanza kutengeneza maji tiba 'dripu' kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa ndani na nje ya hospitali.

"Hii inetusaidia kwa kiwango kikubwa hata hospitali zingine zimekuwa zikifika hapa kwaajili ua kujifunza namna ya kutengeneza maji tiba "alisema.

Pia alisema KCMC ndio kituo pekee inayotambulika kimaitafa kutoa mafunzo ya magonjwa ya ngozi na zinaa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.

"Kituo hiki ndio kinachozalisha mafuta ya ngozi kwaajili ya watu wenye ualbino na tayari tumeingia makubaliano na Bohari kuu ya Dawa MSD kwaajili ya kusambaza dawa na tayari tumefikia mikoa 25 kwa kutumia mfumo wetu wa usambazaji na sasa MSD watatuongezea nguvu ili kusambazwa nchi mzima "alisema

Kwa upabde wake,  Mhandisi KCMC Dustan Kanza alisema mgonjwa mmoja hutumia mtungi mmoja lengo kuepukana na maambukizi.

Alisema katika kinu hicho kwa saa 24 inauwezo wa kuzalisha mitungi 400 na mpaka sasa tayari zaidi ya mitungi 600 imezalishwa tangu kuanza kufanya kazi kwa kinu hicho januari mwaka huu.

Mwisho.




Jumatatu, 9 Septemba 2019

HOSPITALI YA BUGANDO YAFUFUA VIWANDA VYA OKSIJENI NA MAJI TIBA

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando Prof. Abel Makubi akifafanua jambo kwa Maofisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake (hawapo pichani) walipotembelea Hospitali hiyo.

Mfamasia Fransisco Chibunda akiweka majitiba kwenye chupa maalum tayari kwa matumizi.

Majitiba ambayo tayari yameshatengenezwa katika Kitengo cha Kuzalisha Majitiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, Bugando tayari kwa matumizi.


Na.Catherine Sungura-Mwanza

Katika kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda,hospitali ya rufaa ya kanda Bugando (BMC) imefanikiwa kufufua viwanda viwili kwa ajili ya mahitaji ya hospitali za kanda ya ziwa

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Prof. Abel Makubi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando(BMC) mwishoni mwa wiki jijini hapa.

Prof. Makubi alisema kuwa katika kutimiza hayo wamefanikiwa kufufua viwanda ambavyo vilikua vinaelekea kufa.

Alitaja viwanda hivyo ni pamoja na kiwanda cha kuzalisha oksijeni na kingine ni cha kuzalisha maji tiba ya wagonjwa katika chupa mchanganyiko.

"Mahitaji ya oksijeni kwa  hospitali yetu ni mitungi 4000 ila hivi sasa tunazalisha zaidi ya mitungi 2000 na lengo letu ni kuzalisha mitungi 5100.

Aidha, Prof. Makubi alisema kuwa wamepanga kuzalisha mitungi mingi zaidi ili kuweza kuhudumia  hospitali nyingine za kanda ya ziwa kwa bei nafuu na ya nusu bei.

Kwa upande wa kiwanda cha kuzalisha maji tiba ya wagonjwa mkurugenzi huyo alisema "tumefanikiwa kuzalisha maji tiba ya wagonjwa katika chupa mchanganyiko na za kutosha kwa wastani tunazalisha chupa 6000 kwa mwezi na hivyo kuokoa pesa ambazo zingetumika kununua nje".

Hata hivyo Prof. Makubi alisema wanahitaji kiasi cha shilingi bilioni tano ili waweze kuzalisha maji tiba hayo ya kutosheleza kanda yote ya ziwa  na hivyo kusaidia hospitali zingine kutonunua maji ya wagonjwa kutoka nchi za jirani.

Naye Mkuu wa kitengo cha kuzalisha maji tiba Mfamasia Fransisco Chibunda alisema  kwa sasa upatikanaji wa dawa hospitalini hapo ni asilimia 96 ukilinganisha na asilimia 60 ya nyuma.

"Katika kiwanda cha maji tiba tunazalisha aina 17 za dawa,kati ya hizo aina tisa hazipatikani kabisa kwenye soko letu".Alisema Chibunda

Chibunda alisema katika kuwahudumia wagonjwa kwa wakati wamepanua  vituo nane vya kutolea dawa kutoka vituo vinne na kituo kimoja kinahudumia kwa masaa 24.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inayo wafamasia wabobezi katika kuzalisha madawa ya aina mbalimbali.