Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo EBOLA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo EBOLA. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 14 Februari 2020

HOSPITALI YA WILAYA MWANGA YAPEWA WIKI MBILI KUJA NA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA VIPIMO MUHIMU VYA AFYA

- Hakuna maoni
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kadi ya bima ya afya ngazi ya jamii iliyoboreshwa kutoka kwa mgonjwa aliyefika hospitali ya Wilaya ya Mwanga kupata huduma za afya.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akifafanua jambo kwa watumishi  wa Wilaya ya Mwanga (hawapo pichani) kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Thomas Apson.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto)  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Thomas Apson (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.



HOSPITALI YA WILAYA MWANGA YAPEWA WIKI MBILI KUJA NA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA VIPIMO MUHIMU VYA AFYA

Na WAMJW - Mwanga, Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kuandaa mkakati madhubuti utakaowawezesha kuwa na vipimo muhimu vya afya.

Dkt Ndugulile ametoa agizo hilo leo alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kujionea hali ya utoaji huduma na kubaini kuwa hospitali hiyo haina vipimo vya damu, vipimo vya kemia pamoja vipimo vya CD4.

”Kwa miaka miwili sasa hakuna vipimo vya msingi katika hospitali hii, tunawakosesha huduma wananchi” amesema Dkt. Ndugulile

”Haiwezekani Hospitali kubwa ndani ya Wilaya kukosa vipimo vya msingi, haiwezekani mtu hapa sasa hivi anahitaji kipimo cha damu atoke hapa aende Hospitali ya Mawenzi Moshi kwa ajili ya vipimo” amesema Naibu Waziri Ndugulile.

Katika hatua za kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Waziri Ndugulile ameushauri uongozi wa afya ndani ya Wilaya kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua vifaatiba hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za vipimo ndani ya Wilaya ya Mwanga.

Aliendelea kushauri kuwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wao wanatoa mkopo wa majengo na vifaa kwa taasisi za umma na binafsi, mnaweza kuwafikia NHIF na kujadili kuhusu suala hili.

”Huko kwingine wanazitumia hizo fursa, kaeni na watu wa NHIF, Meneja wa NHIF kaa na viongozi wa Hospitali hii ikiwezekana mkubaliane hivyo vitu vipatikane kwa haraka” ameshauri Dkt. Ndugulile.

”Naamini mna wadau wa maendeleo ambao mnashirikiana nao katika mambo mbalimbali, timu ya afya ndani ya mkoa, wilaya pamoja na hospitali nawaombeni sana tuwe tunaomba vitu ambavyo vina manufaa kwa wananchi” amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Awali akitoa salamu za wananchi wa Wilaya ya Mwanga, Mbunge wa Jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa changamoto ya kijiografia ndani ya Wilaya hiyo inachangia wananchi kukimbilia hospitali za Wilaya jirani ili kuweza kupata huduma.

”Wilaya yetu hii ina upande wa mlimani na huku tambarare, wananchi wengi walio huku tambarare wanaona ni bora kwenda Moshi kwa ajili ya matibabu kuliko kwenda juu mlimani iliko Hospitali” amesema Prof. Maghembe.

Hata hivyo Prof. Maghembe amesema kuwa tayari ndani ya Wilaya wameshaanza taratibu za kujenga Hospitali nyingine eneo la chini (tambarare) ili wananchi wanaoishi maeneo hayo waweze kupata huduma za afya ndani ya Wilaya ya Mwanga.

-Mwisho-

Jumanne, 15 Oktoba 2019

MAAMBUKIZI YA VVU YAZIDI KUPUNGUA NCHINI

- Hakuna maoni

Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akielezea jambo mbele ya kamati ya bunge ya kudumu ya masuala ya UKIMWI wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango ya taifa wa kudhibiti UKIMWI katika kipindi cha mwaka 2018/2019 katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.


Baadhi ya Wabunge walio katika kamati ya bunge ya kudumu ya masuala ya UKIMWI wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango ya taifa wa kudhibiti UKIMWI katika kipindi cha mwaka 2018/2019 katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI Mhe. Oscar Mukasa (kulia) akifafanua jambo wakati taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango ya taifa wa kudhibiti UKIMWI katika kipindi cha mwaka 2018/2019 iliyowasilishwa na Wizara na Afya katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.


Baadhi ya Wakurugenzi kutoka idara mbalimbali za Wizara ya Afya wakifuatilia uwasilishwaji wa  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango ya taifa wa kudhibiti UKIMWI katika kipindi cha mwaka 2018/2019 katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.

Jumatano, 31 Julai 2019

WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA EBOLA USIINGIE NCHINI

- Hakuna maoni
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora akisema jambo wakati akifungua zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola kwa Watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana ana Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

Washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa wa Ebola kutoka Mkoa wa Kagera wakiwa kwenye majadiliano kuweka mikakati ya ugonjwa huo usiingie nchini.

Wataalam wa Afya katika Mkoa wa Kagera wakiwa katika zoezi la utayari wanajadiliana mikakati ya kudhibiti Ugonjwa wa Ebola usiingie nchini.

Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. Refeya Ndyamuba (aliyesamama) akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola nchini kwa watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma jana Mjini Bukoba.


Picha ya Pamoja washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola na Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora (aliyeketi katikati).


Na WAMJW – Bukoba, KAGERA

Watoa huduma za afya nchini wametakiwa kuweka juhudi madhubuti kuhakikisha Ugonjwa wa Ebola hauingii nchini Tanzania.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustinely Kamuzora alipokuwa akifungua zoezi la utayari jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa wataalam wa afya mkoani humo.

Akifungua zoezi la utayari, Profesa Kamuzora amesema “Tukifanya juhudi zetu za kukabiliana na ugonjwa wa ebola basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” na kuendelea “Juhudi hizi zina matunda makubwa kuliko tukaruhusu ugonjwa huo kuingia nchini”

“Mpaka sasa hivi Mwenyezi Mungu ametujaalia hakuna mtu aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini, tukifanya yale ambayo tunaelekezwa na wataalam wetu basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” amesema Profesa Kamuzora.

Prof Kamuzola amewataka watoa huduma za afya kufuata taratibu zote zilizowekwa ili endapo ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo, basi aweze kupatiwa huduma na wakati huo huo mtoa huduma akawa salama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu amesema kuwa zoezi ya utayari lina lengo la kuzuia maafa yasitokee kwa kuwaweka tayari watalaam wa sekta ya afya kukabiliana na tishio la ugonjwa wa ebola kuingia nchini.

“Tuhakikishe tunazuia ugonjwa wa ebola usiingie nchini, na endapo ikitokea umeingia basi tuhakikishe tunapunguza athari zitokanazo na ugonjwa huo” amesema Bw. Taratibu.

Naye Mtaalam wa Afya ya Jamii na Masuala ya Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Faraja Msemwa amesema kuwa kupitia mazoezi hayo ya utayari wanapata fursa ya kubaini fursa  na changamoto zilizopo katika kudhibiti ugonjwa huo wa ebola usiingie nchini.
“Katika zoezi hili tunaangalia hawa watumishi wetu wa afya tuliowandaa wana uwezo wa kiasi cha kuweza kufuata miongozo iliyoandaliwa” amesema Dkt. Msemwa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) toka kuripitiwa kuibuka kwa ugonjwa wa ebola nchini Uganda mnamo mwezi Agosti mwaka 2018 jumla ya kesi 2612 za watu kuathiriwa na ugonjwa huo zimeripotiwa huku ukisababisha vifo 1756 (sawa na asilimia 67). Zoezi la utayari limepangwa kufanyika kuanzia leo JULAI 30 mpaka AGOSTI 8 mwaka 2019 ambapo vituo vya kutolea huduma za afya katika Mikoa ya Kagera na Kigoma vitapimwa utayari wao katika kukabiliana na Ugonjwa huo hatari.

Kupitia mazoezi ya utayari, watoa huduma za afya kuanzia ngazi ya jamii wanapata fursa ya kushiriki kwa vitendo namna ya kutambua, kutoa huduma kwa mtu anayehisiwa au kuwa na ugonjwa wa ebola na kuwaondolea woga pindi ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo.

MWISHO.