Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Picha. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Picha. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 22 Agosti 2019

CHUPA 51819 ZAIDI ZA DAMU SALAMA ZAKUSANYWA KWA MWAKA 2018/2019

- Hakuna maoni
Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt.Magdalena Lyimo akiwasilisha mada ya hali ya upatikanaji damu kwenye kikao cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaoendelea jijini Dodoma

Wadau wa sekta ya afya ambao ni wastaafu Dkt.Deo Mtasiwa ambaye alikua ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI  na Bi.Jane Ndyetabula ambaye alikua kamishna wa ustawi wa jamii wakifuatilia uwasilishaji wa mada wakati wa kikao kazi hicho.

Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho akiuliza swali


CHUPA 51819 ZAIDI ZA DAMU SALAMA ZAKUSANYWA KWA MWAKA 2018/2019

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

 Mpango wa damu salama umefanikiwa kukusanya chupa  51819 sawa  na asilimia ishirini zaidi ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka 2018/2019.

Hayo yameelezwa leo na meneja mpango wa taifa wa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo wakati akiwasilisha mada ya upatikanaji wa damu kwenye kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri  kinachoendelea jijini hapa.

Dkt. Lyimo amesema kwamba kwa mwaka 2018/2019
wizara ya afya kupitia mpango huo uliweka malengo ya kukusanya kiasi cha chupa 309376 nchi nzima ikilinganishwa na chupa 257557 zilizokusanywa mwaka 2017/2018.

Hata hivyo Dkt. Lyimo alisema kuwa wameweza kukusanya chupa 309,376 sawa na,asilimia sitini ya mahitaji ya nchi kulingana na idadi ya wananchi waliopo “tumeweza kufanikiwa kuvuka lengo la kukusanya chupa za damu zaidi na hii ni kutokana na uelewa mkubwa wa wananchi wa kuelewa umuhimu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha hususani akina mama wajawazito na wahitaji wengine wa damu".Alisema.

Aidha, Dkt. Lyimo alitaja makundi ya wachangia damu kuwa wanawake  ni asilimia 14 pekee huku idadi ya wanaume ikiwa ni asilimia 86 hapa nchini.

Hata hivyo alisema hali ya maambukizi  ya magonjwa kwa damu zinazobainika katika ukusanyaji huo  ameeleza kuwa ugonjwa wa homa ya Ini ndio inayoongoza kwa asilimia 5.9 ikifuatiwa HIV kwa asilimia 2.8.

Dkt. Lyimo amewashukuru wananchi  wanaoendelea kuchangia damu ikiwemo vijana watumishi wa umma, taasisi na mashirika mbalimbali  kwa moyo wa kutekeleza zoezi hilo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

Jumatano, 21 Agosti 2019

PONGEZI KWAKO MHE. RAIS; DKT. CHAULA

- Hakuna maoni
Katibu Mkuu Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula


Na.Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula  amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwekezaji mkubwa aliouweka katika sekta ya afya nchini.

Dkt. Chaula ameyasema hayo jana wakati wa mahojiano na kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) wakati wa taarifa ya habari baada ya Mhe. Rais kutembelea Mamlaka ya Maabara  ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo jijini Dar es Salaam.

Katika mahojiano hayo Dkt. Chaula alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano sio kwamba imewekeza tu kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali bali katika sekta yote ya afya  kwa kuboresha huduma za afya kwa upande wa   miundombinu, dawa, vifaa na vifaa tiba katika hospitali pamoja na taasisi zake.

Kwa upande kwa mamlaka ya maabara  ya mkemia mkuu  wa serikali alisema kuwa serikali kupitia wizara ya afya  imefanya jitihada kubwa za kusogeza huduma  za mamlaka hiyo katika kanda zote nchini na hivi karibuni inatarajia kuwa na kanda nyingine  jijini Dodoma.

“Sisi hapa kwa afrika mashariki, Tanzania tunaongoza kwa kuwa na mitambo ya uchunguzi ya  kisasa vya kufanya utambuzi wa miili na tuna imani tutapokea hata vinasaba kutoka nchi za jirani pale panapotokea mkanganyiko hususani kwenye kesi za jinai,ajali,sumu,madawa ya kulevya pamoja na kemikali.

Dkt. Chaula alisema mitambo hiyo ya kisasa inatoa majibu ndani ya  siku saba tofauti na zamani ambapo sampuli thelathini na tano zilichukua  mwezi kuthibitisha ila kwa sasa wanachukua sampuli hadi mia mbili.

Hata hivyo katibu Mkuu huyo amewashauri watanzania kupenda na  kujenga mazoea ya kutumia taasisi za serikali zilizopo nchini hususani mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali pale panapotokea mkanganyiko kwa kisheria au utambuzi wa vinasaba mbalimbali.

Jumanne, 20 Agosti 2019

WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA.HALMASHAURI IMARISHENI LISHE

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma.

Picha ya pamoja  wakati wa kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma.


WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA.HALMASHAURI IMARISHENI LISHE

Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kuweka mikakati ya kuimarisha hali ya lishe katika ngazi ya jamii ili kupunguza   hali ya udumavu kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwenye  kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini hapo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwe na taifa lisilo na  kiwango cha chini cha hali ya lishe waganga wakuu hao lazima wapange mikakati ambayo itaanzia ngazi ya jamii ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa lishe bora  na inayostahili kwa familia hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili mikakati hiyo ifanikiwe.

Hata hivyo alisisitiza  watoa huduma  kutoa huduma bora kwa wananchi kwa  kuimarisha huduma za afya katika maeneo yao ili wananchi wanaoenda kupata huduma wapate huduma hizo kwa haki na usawa" na katika hili ni vyema mwananchi anayekuja  kupata huduna ni vyema  aridhike na huduma anayopata katika vituo vyetu  vyote nchini”.Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliwataka waganga wakuu hao kusimamia utendaji wa kazi katika maeneo yao ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii“inasikitisha  kuona mama mjamzito  anafariki kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uzembe  au kutokupata huduma sahii jambo hili halikubariki”.

Kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri  mwaka huu kinafanyika jijini hapa ambapo kilifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na kauli mbiu ya kikao hicho ni “Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati na utakua wa siku tano.

Jumatatu, 19 Agosti 2019

CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

- Hakuna maoni
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Chrisogone Justine German akitoa mafunzo kwa Watoa huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa  wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata  taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC sstandard)

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya, kwa kufuata kanuni za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC standard ).

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akielekeza umuhimu wakufuata taratibu kwa mgonjwa wakati wa kumuudumia (IPC Standard) kwa Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza.


Baadhi ya Watoa  huduma za Afya kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza wakifuatilia Mafunzo kwa makini ya jinsi yakujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata kanuni na taratibu (IPC Standard) wakati wa kumuudumia mgonjwa.

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali jijini Mwanza wakifuatilia kwa makini  Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard)

Picha ya pamoja ikiongozwa na Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa na Watoa huduma kutoka Halmashauri mbali mbali za Mwanza baada ya kumaliza mafunzo ya namna ya kujikinga na kudhibiti  magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa Mkoani hapo.



CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- MWANZA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Mwanza zimeelekezwa kusimamia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi (Magonjwa) wakati wanatoa huduma za Afya kwa Wagonjwa.  

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti  magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande mwingine mafunzo hayo yametumika kama njia ya kusambaza muongozo mpya wa namna ya kujikinga na kudhibiti  maambukizo (IPC Guidline), ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za Afya nchini. 

Katika mafunzo hayo imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Inakadiriwa kuwa watu Bilioni 2.5 Duniani wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, huku kati yao 60% ikiwa ni watu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku nchi za Sudan, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiripoti kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao ulisnza tangu 1976.

Kulingana na Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 1790 wapoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018 Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania tayari imekwisha kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Katika mafunzo hayo, Watoa huduma wameaswa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote wa kutoa huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Akitoa mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo amesema kuwa Watoa Huduma za Afya wapo katika hatari kubwa za kupata maambukizi ya ugonjwa huu, endapo hawatofuata miongozo na taratibu za utoaji huduma kwa kadri ya muongozo huu

“Mara kwa mara ni muhimu kuwa na tahadhari wakati unahudumia Wagonjwa, hususan kunawa mikono kabla na baada ya kutoa huduma kwa wagonjwa na wasio wagonjwa kwani Watoa huduma mpo kwenye hatari kubwa sana yakupata maambukizo” alisema Dkt. Joseph Hokororo.

Ameendelea kusema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Pia alisisitiza kuwa Dunia imekumbwa na tatizo la Usugu wa vimelea vya magonjwa ambukizi dhidi ya dawa (antimicrobial resistance), hivyo amesisitiza juu ya umuhimu mkubwa wa kufuata taratibu za kutoa huduma (IPC Standard) ili kusaidia kutokomeza vimelea hivyo.   

Akitoa mafunzo kwa Watoa Huduma za Afya, juu ya namna ya kukinga maambukizi wakati wa kujifungua, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogone German amesema kuwa ni muhimu kwa Watoa huduma kufuata viwango vya kukinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard) ili kudhibiti ya ugonjwa wakati wa kutoa huduma ikiwemo kuhakikisha kunawa mikono kabla ya kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa.

Aliendelea kusisitiza kuwa, si jambo zuri kwa Watoa huduma za Afya, kufanya mambo kwa mazoea, hali inayopelekea kufanya kazi kwa mazoea na kujikuta kunasambaa maambukizi kutoka kwa mtu anaepokea huduma za Afya au kinyume chake 

Mwisho.

Jumanne, 13 Agosti 2019

WATOA HUDUMA ZA AFYA MWANZA WAFUNDWA

- Hakuna maoni
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akieleza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza.

Afisa Afya ya Mazingira kutoka Taasisi ya JBHN Said Chibwana akitoa Elimu kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya  Watumishi wa Sekta ya Afya  wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akijibu hoja kutoka kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya  Watumishi wa Sekta ya Afya  wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana akisisitiza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Semina hiyo inaendelea Jijini Mwanza.

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Seketoure wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini  Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), mafunzo yanaendelea Jijini Mwanza.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya baada ya kumaliza Wiki ya kwanza ya Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Jijini Mwanza.



WATOA HUDUMA ZA AFYA MWANZA WAFUNDWA

Na Rayson Mwaisemba WAMJW-MWANZA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yawafunda Watoa Huduma za Afya Jijini Mwanza  kuwakumbusha namna ya utoaji huduma kwa kufuata misingi na taratibu za utoaji huduma kwa Wagonjwa ili kupunguza maambukizi mapya na vifo visivyo na ulazima.

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na Wizara ya Afya imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Kwa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Aidha, Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Afisa Mkuu Uhakiki Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokololo amesema kuwa zaidi ya watu milioni 1.4 Duniani wanaugua magonjwa yanayosababishwa na kupata maambukizi mapya wakati wakupata huduma ya afya, hii hutokana na Watoa huduma za Afya kutofuata taratibu za namna ya kutoa huduma.

Aliendelea kusema kuwa Asilimia 15 ya Wagonjwa hupata maambukizi ya magonjwa mapya pindi waendapo kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya, kutokana na kutofuatwa kwa taratibu, kanuni za miongozo ya kutoa huduma za Afya (IPC Guideline, SOP).

Kwa Upande wake Afisa kutoka Kitengo Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogane Justine amesema kuwa kufuata taratibu za utoaji huduma kama kanuni za uoshaji sahihi wa mikono kutamsaidia Mtoa huduma kuzuia kusambaza maambukizi ndani ya Kituo cha kutolea huduma za Afya na nje.

Licha ya changamoto za upatikanaji wa huduma za maji safi kwa baadhi ya Vituo vya Afya, Dkt. Chrisogone Justine German amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Mtoa huduma za Afya kuhakikisha ananawa mikono yake vizuri kwa sabuni na maji safi ili kuepuka kusambaza maambukizi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Akitoa Elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi mapya yanayotokea wakati wa matibabu kutokana na baadhi ya Watoa huduma kutofuata taratibu na miongozo Dkt. Radenta Bahegwa amesema kuwa asilimia 40 ya magonjwa yanayopatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya nayosababishwa na kutofuata kwa taratibu za miongozo ya utoaji huduma.

“Asilimia 40 ya ya magonjwa yanayopatikana katika Vituo vya kutolea huduma za Afya husababishwa na kutofuata miongozo (IPC Guidline), ndiomaana asilimia 80 ya UTI zinazoibuka katika Vituo vya Afya zinatokana na kukosea kuweka kifaa cha kupitisha haja ndogo” alisema Dkt. Radenta.

Mtaalamu kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Dkt. Alex Sanga amesema kuwa katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo ametoa wito kwa Watoa huduma kuhakikisha wanafuata miongozo na taratibu wakati wa kutoa huduma ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi mapya katika jamii.

“Tafiti za Shirika la Afya Duniani zinonesha kuwa ndani ya miaka 3 (2015-2018) kati ya watu 33,421, watu 542 walipoteza maisha, huku katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa” alisema Dkt. Sanga.

Naye Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu. 

Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Francisco Chibunda ametoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kufuata miiko na taratibu na miongozo inavyoelekeza jambo litalosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata taratibu na miongozo wakati wakutibu ugonjwa.

“Tunapoteza nguvu kubwa, tunapoteza rasilimali nyingi kwenye dawa na matibabu, mwisho wa siku tunasababisha maambukizi mapya, nah ii hupelekea usugu wa magonjwa , kwa hiyo tubadilike” Alisema Chibunda.

Mwisho.

Jumatatu, 5 Agosti 2019

PREPARING THE HEALTH WORKFORCE TO MAKE THE MOST OF DATA

- Hakuna maoni
DataUseForHealth


Health workers exchange learnings about Tanzania's electronic immunization registry. Photo: PATH/Trevor Snapp. For nearly thirty years as a health worker in Tanzania, Salome has used pen and paper to record patient data. A digital transformation promises to streamline her work and improve patient care. 

Digital health solutions increase data quality and accessibility, but to be effective and improve patient outcomes, health workers must know how to make the most of the information. For many like Salome, Tanzania’s digital transformation will require retraining and developing new digital literacy skills. 



Building the workforce of the future 
The Data Use Partnership—a collaboration between the Government of Tanzania and PATH—aims to equip Tanzania’s health sector and workforce with skills for the country’s changing digital landscape. This includes training existing and future generations of health workers to make better use of digital platforms and data. 

To facilitate trainings, the Data Use Partnership established the Capacity Building Consortium (CBC). Made up of three universities, two health research and training institutes, and zonal health training centers around the country, the CBC fosters a culture of data use and builds the capacity of health workers to identify and solve problems, measure performance, allocate resources, track patients, support clinical decisions, and streamline service delivery. 



Making the most of data 
“In the health sector, a lot of data are collected, but aren’t necessarily put into efficient use when making crucial decisions,” explains Professor Flora Lucas Kessy, Secretariat Chairperson of the CBC and instructor at the Tanzania Training Center for International Health. “The consortium was formed to build the capacity of health workers through both in-service and pre-service training.” 

The consortium is building the health workforce’s capacity by: 
• Developing trainings and innovative platforms: The Data Use Partnership is developing a new series of short-term trainings, using costeffective and innovative platforms. Trainings will be offered in person through zonal health resource centers to ensure greater accessibility, and through eLearning modules that the CBC aims to integrate under a single government-owned National Health eLearning platform.



 • Establishing new delivery methods: eLearning platforms can help deliver trainings to rural health providers, where long distances, limited resources, and poor transportation may otherwise be a barrier to education. “There are lots of current innovations in this country in terms of mobile phone and smartphone use,” explains Professor Kessy. “We can use digital platforms to deliver critical courses even to health providers that are very far away.” 

• Increasing focus on data use and analytics: The CBC will review, develop, and standardize curricula for data analytics training, so that the workforce is operating from a place of common experience. With more than 136 institutions offering certificates and diplomas in health and allied sciences programs, it’s critical that students graduate with a shared skillset, understanding, and appreciation for data use. 



• Fostering government ownership and peer learning: The CBC also recognizes the importance of ensuring that trainings are delivered by their own peers and experts, instead of an outside institution or implementing partner. “Health workers have to feel that they’re being trained by one of their own,” explains Mr. Tumaini Macha, Assistant Director, Monitoring & Evaluation from the Ministry of Health. “This mentorship model is even more efficient and ensures that trainers understand the need in different areas.” 

Achieving digital transformation 
"Having a curriculum that’s strong in data use ensures that whoever graduates from universities and other academic institutions, goes home with knowledge on how to deliver on data use,” explains Professor Kessy. “We've been able to bring together five different prime institutions that have their own different ways of operating. It’s so unique that we can work together, forget our own university boundaries, and build an open consortium that’s focused on data use.” 


The CBC is critical to Tanzania achieving digital transformation. By educating and training the existing workforce and preparing a pipeline of future talent, the health workforce will be able to make optimal use of digital tools, ultimately leading to better patient care and more equitable access to health services.

Alhamisi, 1 Agosti 2019

TANZANIA YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

- Hakuna maoni
Mgeni rasmi wa mkutano huo wa NTD ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Elias Kwesi akifungua mkutano huo ambao unawakilishwa na waratibu wa mpango huo kutoka mikoa mbalimbali,wadau wa ndani na nje ya nchi

Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka wizara ya afya Dkt.Leonard Subi akiongea na vyombo vya habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira akifanya utambulisho wa wageni walioshiriki mkutano wa mwaka wa mapitio na kutengeneza mpango kazi wa mwaka unaofanyika jijini Dar es Salaam

Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt. Christine Musanhu akipeana mkono na Mgeni rasmi wa mkutano huo mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt.Elias Kwesi

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za kitaifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

Kaimu Mwakilishi mkazi wa shirika la afya duniani(WHO)Dkt. Christine Musanhu akiongea kwenye mkutano huo.

Mratibu wa NTD Dkt.Upendo Mwingira akisalimiana na mgeni rasmi Dkt.Elias Kwesi

 Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa mkutano huo.


TANZANIA  YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia wizara ya afya imepiga  hatua katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa wa Wizara hiyo, Dk. Elius Kwesi wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya shuguli wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na mpango kazi wa mwaka.

Dkt.Kwesi alisema mkutano huo ni muhimu kwani watajadiliana na wadau hao kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara hiyo kwa upande wa rasilimali fedha.

"Tuna pengo la rasilimali  mbalimbali  na tumewaita hapa Wadau kujadiliana nao Mpango kazi wetu  na kuangalia namna gani watatusaidia kuziba pengo na kutakavyosaidiana kutekeleza," alisema Dkt.Kwesi

Alisema tangu utekelezaji wa Mpango huo ulipoanza nchini umefanikiwa kupunguza magonjwa hayo kwa kiwango cha asilimia 80.

Awali Mkurugenzi wa huduma za Kinga wizarani hapo Dkt.Leonard Subi alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yasipodhibitiwa yatapelekea watu wengi kuugua siku zijazo kwani yana athari kubwa na kusababisha upofu na ulemavu kwa jamii.

“mfano ugonjwa wa kichocho kwa watoto huathiri ukuaji na wengine wanaweza kupata saratani katika maisha yao".Alisema Dkt.Subi

Alisema wizara kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya jitihada kubwa na hivyo kufanikiwa kudhibiti magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa

"Wilaya ambazo zilikua zimeathirika sana na matende na mabusha miaka kumi iliyopita zilikua takribani 120 lakini hivi sasa zimebaki wilaya 24 ambazo bado tunaendelea na ugawaji kingatiba na trakoma kulikuwa na wilaya 71 na sasa zimebaki wilaya sita tu".

Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira amesema kwa upande wa kichocho na minyoo ya tumbo bado inahitajika   kuendelea kuwakinga watoto na baadhi ya wilaya wanaendelea kugawa kingatiba za matende na mabusha pamoja na usubi.

Mwisho

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAAJIRI WANAOWANYIMA HAKI WANAWAKE LIKIZO YA UZAZI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Sekta ya Afya(hawapo kwenye picha), wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akieleza jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Sekta ya Afya (hawapo kwenye picha), wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna, na wa mwisho kulia ni Kaimu Katibu mkuu Wizara ya Afya, ambae pia ni Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice Mutayoba.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Sekta ya Afya   yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna wa mwisho Kulia ni Mwakilishi kutoka UNICEF James Gitau.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia maelezo kuhusu huduma ya unyonyeshaji katika maeneo ya kazi kutoka Afisa kutoka Wizara  ya Afya Bi Tufingene Malambugi wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma.


SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAAJIRI WANAOWANYIMA HAKI  WANAWAKE  LIKIZO YA UZAZI. 

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetangaza kuanza kuwachukulia hatua Waajiri wote ambao wanavunja Sheria kwa kugandamiza haki ya kupata likizo ya uzazi kwa wanawake pindi anapojifungua. 

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu ya “Wawezeshe wazazi kufanikisha unyonyeshaji”.

"Haki ya Mwanamke Kuzaa na kupata likizo ya uzazi ni haki yake ya asili, haitakiwi kuwekewa vikwazo au changamoto yoyote, kwahiyo nitoe wito kwa wanawake ambao wanafanya kazi, ni haki yako kupata likizo, asije mtu anakwambia anaijaza kazi yako kwakuwa umetoka likizo ya kujifungua, tuambie sisi, tutachukua hatua, na huyo Mwajiri  tutamtangaza kuwa ni adui wa Wanawake na Watoto wa Tanzania ".Amesema Waziri Ummy. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuanzisha dawati la kutoa malalamiko litaloshughulikia kupigania na kutetea haki za wanawake kupata likizo ya uzazi, jambo litalosaidia kudhibiti tabia za baadhi ya Waajiri kukandamiza haki za wanawake baada ya kujifungua.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wananyonyeshwa maziwa ya mama, hii inaonesha kuwa hali ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama imepungua ikilinganishwa na takwimu ya mwaka 2015/2016 ambayo ilikuwa ni asilimia 98.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi (ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa) ni asilimia 53 ikilinganishwa na asilimia 51 ya mwaka 2015/2016

Aliendelea kusema kuwa, idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58 ikilinganishwa na asilimia 59 ya mwaka 2015/2016.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni 35%, huku kiwango kikionekana kuongezeka ikilinganishwa na asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, takwimu za utafiti wa hali ya lishe nchini za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa asilimia 31 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa ikilinganishwa na asilimia 34 ya mwaka 2015/2016, huku sababu kubwa ya ikiwa ni ulishaji usio sahihi ambao huchangiwa na majukumu mengi yanayomkabili mama na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto.

Naye Mwakilishi kutoka UNICEF Bw. James Gitau amesema kuwa, unyonyeshaji ni moja ya njia muhimu kuhakikisha Afya Bora kwa maisha ya mtoto, hivyo kutoa wito kwa wanahabari kuhakikisha wanapeleka Elimu kwa wananchi hususan wanawake kuhakikisha wanafahamu umuhimu wa kunyonyesha Watoto mfululizo miezi sita ya mwanzo,

Pia, Bw. James Gitau ametoa wito kwa Serikali kuongeza nguvu katika uhamasishaji juu ya umuhimu na haki ya Watoto kunyonyeshwa, amesema jambo hili litasaidia kuokoa watoto kupata magonjwa yanayotokana na kukosa virutubisho kutoka kwa maziwa ya mama.

Mwisho.

Jumatano, 31 Julai 2019

SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

- Hakuna maoni
Mkuu wa kitengo cha afya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere George Ndaki akimuonesha ufanyaji kazi wa  mashine za kupima joto(thermo scanner) Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipotembelea eneo la wasafiri wanaoenda nje ya nchi  zilizofungwa kwenye uwanja mpya wa ndege terminal three

Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akionesha kadi za homa ya manjano"Yelow Fever" ambazo zinatolewa na wizara ambapo wizara imefunga kifaa maalum cha kubaini kadi feki ambazo wasafiri huzinunua bila kuchanjwa chanjo hiyo

Dkt.Ndugulile akioneshwa utofauti wa kadi halisi na kadi feki za homa ya manjano.Dkt.Ndugulile amewasihi wananchi wanaotarajia kusafiri nje ya nchi kuacha kununua kadi feki bali kuhakikisha wanapata chanjo hiyo kwenye vituo rasmi vilivyoelekezwa na wizara  ya Afya

Naibu Waziri akikagua vifaa vingine vilivyofungwa terminal three kwa ajili ya kubaini wahisiwa wa Ebola

Katika kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa SADC wizara ya afya imejipanga kukabiliana na dharura kwa wageni watakaoshiriki mkutano huo.Pichani.Dkt.Ndugulile akikagua magari ya wagonjwa wa dharura yaliyopo ofisi za Toyota

 Naibu Waziri akikagua kifaa cha huduma ya dharura kilichopo kwenye magari hayo

Naibu Waziri akikagua moja ya chumba cha dharura kilichoandaliwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya washiriki wa mkutano wa SADC

Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.Juma Mfinanga (kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wakati alipotembelea kujionea hali ya utayari ya kuwahudumia washiriki wa mkutano wa SADC ambao watapata dharura na hivyo kupatiwa huduma za afya kwenye hospitali hiyo



SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

NA.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini hapa.

Dkt.Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa  zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.

"Magari na Mabasi hayo yatatumika kwenye mkutano wa SADC na baadae yatasambazwa katika vituo vya dharura nje ya hospitali ambapo yatatumika kusafirishia majeruhi pindi ajali inapokuwa imetoka.

"Tutayatumia katika mkutano wa SADC, pamoja na ambulance hizo 12 kuna mabasi makubwa mawili ambayo yana huduma zote za msingi ndani ambapo watu wapatao 20 wanaweza kubebwa na kupatiwa msaada wa ajali," alisema.

Alisema serikali imejipanga  pia katika njia ya anga kwa kutumia  ndege  pindi mtu anapohitaji huduma ya dharura kupelekwa haraka katika eneo jingine hususani hospitali ya Taifa Muhimbili.

"Ni utaratibu ambao Serikali inauweka kuhakikisha waathirika wa ajali wanapata huduma za dharura na ajali, mapema iwezekano na tunasema ndani ya masaa yaliyowekwa ya kuwahudumia majeruhi," alisema Dkt.Ndugulile

Naibu Waziri huyo alisema wameagiza magari ya zimamoto na uokozi kwamba si tu liwe na uwezo wa kuzima moto bali linakuwa na vifaa vya kisasa, kwa mfano ikiwa gari limepata ajali, milango inashindwa kufunguka, iweze kukatwa ili kuokoa majeruhi, iwezekane.

"Haya ni maendeleo makubwa kwa Serikali katika kuhakikisha majeruhi wanapata huduma za dharura za awali mapema inavyowezekana, kwani wengi hufariki dunia kwa sababu hukosa zile huduma za awali za dharura katika lile li-saa limoja la kwanza," alisema.

Dk. Ndugulile aliongeza "Inawezekana anavuja damu, anashindwa kupumua vizuri, tuna imani magari, mabasi na mafunzo tuliyowapa wataalamu huduma hizi zitaimarika.

"Natoa rai kwa wananchi, kwani nao wamekuwa wakichangia madhara kwa majeruhi, wanawamalizia wale majeruhi, wakiamini wanawasaidia kuokoa maisha.

"Wahakikishe tu wanamtoa majeruhi na kumuweka pahala pengine mbali na tukio la ajali, kama gari litaweza kulipuka moto ule usimfikie, tunapowabeba 'mzobe mzobe' tunawasababishia madhara zaidi.

"Muhimu tuhakikishe huduma za msingi zinapatikana pale pale, kikubwa ni kuhakikisha yule Mgonjwa anapumua, havuji Damu kwa wingi na njia yake ya Hewa IPO salama.

"Jambo la msingi si kumkimbiza majeruhi hospitalini kwanza bali 'kum-stablize' pale pale eneo la tukio, kama mfupa umevunjika afunge vizuri usining'ingine, abebwe vizuri kama mshipa wa shingo umevunjika usimalizike, kwani wengi kutokana na ule ubebaji huishia kupooza mwili na hata kufa," alisema.

Sambamba na hilo, mapema asubuhi, Dk. Ndugulile alifanya ziara kwenye kitengo cha afya ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA- terminal III), kujionea hali ya utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola.

MWISHO