Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Taarifa kwa Vyombo vya Habari. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Taarifa kwa Vyombo vya Habari. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 13 Februari 2019

SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua idadi ya Wananchi waliofika kupata huduma wakati alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua jokofu la kuhifadhia sampuli ya Damu pindi alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mashine yakupima Sampuli za Damu, Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akiongea na Watumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu katika taasisi hiyo.

Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo, akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha)  wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kumaliza ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.


SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU


Na WAMJW - DSM

Mpango wa Taifa wa Damu salama imetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huyo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu yake.

"Ni lazima kupunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali kwa kuanzisha mfumo wa uchangiaji gharama za huduma za Afya wakati Sera inaelekea kukamilika, Mpango unapendekeza kurudisha gharama kutoka Hospitali binafsi kupitia njia ya Bima" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile alisema kuwa Idadi kubwa ya wanaokuja kuchukua Damu katika Taasisi hiyo ni Hospitali Binafsi ukilinganisha na Hospitali za Umma, ambapo mfumo wake ni wakutoza huduma kwa Wananchi (Biashara)

"Wanaokuja kuchukua Damu nyingi hapa, wengi ni Hospitali Binafsi, kuliko hata za kwetu za umma, Damu nyingi tunawapa, lakini hawa tukiwapa Damu hizi, wao wanaenda wanatoza pesa, kwahiyo sisi tunawatengenezea bidhaa bure halafu wao wanaenda kutoza pesa, hata senti tano sisi hatupati, sio sahihi" alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amewaagiza viongozi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuangalia ni namna gani Damu iwe ni moja ya vitu vitakavyo gharamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

"Muwahusishe Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kuangalia jinsi gani damu itakuwa inagharamiwa na Bima ya Afya, mtuletee mapendekezo na sisi tutafanya maamuzi" Alisema Dkt. Ndugulile.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameagiza kufanya maboresho ya mfumo wa Takwimu kuanzia kwenye ukusanyaji wa mapato  mpaka hatua ambayo mgonjwa anapata damu hiyo jambo litakalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameagiza  kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawabakishia wachangiaji Damu ambao wanakuja kuchangia, hii inatokana na takwimu kuonesha Wachangiaji wa Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63%  mwaka 2017-2018.

"Taarifa yenu ya Mwaka 2017-2018 inaonesha kwamba, wachangiaji Damu wa hiari wanapungua kutoka  67% mpaka 63% , maana yake bado kuna changamoto, na kuna kazi tunatakiwa kufanya ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaowapata Mara ya kwanza kuendelea kuwa nao" Alisema Dkt. Ndugulile

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo amesema kuwa Mpango una mkakati wa kuboresha mfumo wa ukusanyaji taarifa na Takwimu za kielektroniki unaunganishwa nchi nzima ili kuleta tija na ubora wa huduma za damu salama nchini.

Kwa upande mwingine Dkt. Lyimo amesema kuwa Mpango umefanikiwa katika kipindi cha Mwaka 2018  kwa kushirikiana na timu za Mikoa na Halmashauri ulikusanya jumla ya chupa 307,835 ambayo ni sawa na Chupa 6 kwa kila watu 1000, huku Shirika la Afya Duniani linapendekeza kukusanya chupa 10 kwa kila watu 1000, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la chupa 73,882 sawa na 32% ikilinganishwa na Takwimu za 2017.

Dkt. Magdalena Lyimo aliendelea kusema kuwa kwa Mwaka 2018, Wastani wa chupa 25,653 zilikusanywa kila mwezi na damu zote zilipimwa magonjwa ya HIV,Kaswende pamoja na makundi ya damu, huku matarajio ni kuongeza damu hadi kufikia chupa 375,000 kwa Mwaka 2019.

Mwisho.


Alhamisi, 17 Januari 2019

JUMLA YA WAGONJWA 19 WAPANDIKIZWA FIGO NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati akiwasilisha  taarifa ya Wizara ya Afya, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya, uliofanywa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya, uliofanywa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Laurence Museru akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, na baadhi kutoka Taasisi za Wizara wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya, uliofanywa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Wajumbe wa ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, Wakurugenzi wa Wizara, na  baadhi ya Taasisi zake,  wakijadili taarifa ya utendaji ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

JUMLA YA WAGONJWA 19 WAPANDIKIZWA FIGO NDANI YA MIEZI 5

Na WAMJW - DODOMA
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi Desemba 2018 jumla ya wagonjwa 19 walipata huduma ya upandikizwaji wa figo, hivyo  kufikisha jumla ya wagonjwa 28 waliopata huduma hii toka Hospitali ilivyoanza kutoa huduma za kupandikiza figo mwezi Novemba 2017. 

Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Wizara ya Afya mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 2.24, ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa 28 nje ya nchi kupata matibabu yakupandikizwa figo.

"Gharama ya huduma hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kati ya shilingi milioni 20 mpaka 30 kwa mgonjwa mmoja wakati nje ya nchi gharama hii ni kati ya shilingi milioni 100 mpaka 120. Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 2.24 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu hayo nje ya nchi" Alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili iliona jumla ya wagonjwa 30,189, Idara ya Utengamano ilihudumia wagonjwa 22,379, huku Idara ya Madawa ilihudumia maombi ya dawa 519,216 na  Kitengo cha Figo kilitoa huduma za kusafisha damu kwa mizunguko 13,248, huku Jumla ya wagonjwa mahututi 960 walihudumiwa katika ICU za Hospitali. 

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Katika kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi Disemba 2018 Hospitali imetoa huduma za kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 11 na kufikisha jumla ya watoto 21 waliopata huduma hii toka ilipoanza mwezi Juni, 2017, jambo lililosaidia kuokoa  zaidi ya shilingi milioni  840 ambazo zingetibu watoto 21.

"Kabla ya hapo huduma hii ilikuwa inapatikana nje ya nchi kwa gharama kati ya shilingi milioni 80 mpaka 100 kwa mtoto mmoja, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili gharama nishilingi milioni 35 mpaka 40" alisema Waziri Ummy.

Wakati akijibu maswali ya Wabunge wa kamati hiyo  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Taasisi ya Moyo (JKCI) imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 211, kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watu wazima walikuwa 89 na watoto walikuwa 60, huku watu wazima 62 wenye matatizo kwenye mishipa ya damu walifanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu.

Aidha, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa, wagonjwa 521 walipatiwa matibabu ya upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa upande wa mtambo maalum (catheterization laboratory).

Mwisho.

Jumatano, 14 Novemba 2018

TAARIFA KWA UMMA - TAMKO LA WIZARA KUHUSU SIKU YA KISUKARI DUNIANI TAREHE 14 NOVEMBA, 2018.






Jumatatu, 29 Oktoba 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - TAMKO LA SIKU YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UGONJWA WA KIHARUSI (STROKE) DUNIANI, TAREHE 29/10/2018

- Hakuna maoni