Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wizara ya Afya na Taasisi zake. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wizara ya Afya na Taasisi zake. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 26 Machi 2020

HADI SASA TUMEWEZA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA NDANI KWA NDANI YA CORONA-WAZIRI UMMY

- Hakuna maoni
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akieleza jambo, wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na Naibu Katibu Mkuu wake wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakifuatilia neno kutoka kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha, wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.



HADI SASA TUMEWEZA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA NDANI KWA NDANI YA CORONA-WAZIRI UMMY
Na WAMJW-DOM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, amebainisha kuwa, hadi sasa Tanzania imeweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani ya ugonjwa (COVID-19) na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga.
 
Amesema, wasafiri 245 walioingia Tanzania Bara na Zanzibar tangu Machi 23, mwaka huu, wametengwa kwenye hoteli na maeneo yaliyoandaliwa na Serikali kwa gharama zao.
 
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Corona nchini.
 
Amesema hadi sasa hakuna maambukizi ya ndani (Local transmission) na wagonjwa 13 waliothibitika kuwa na virusi vya ugonjwa huo wanaendelea vizuri.
 
“Hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa lengo lakutimiza dhamira nzuri ya serikali ya kupunguza hatari ya kusambaa kwa haraka maradhi haya nchini, tunashukuru Mungu bado hatuna ‘Local transmission,”amesema.
 
Aidha, amesema mgonjwa wa kwanza wa Arusha, amepona Corona na taratibu za kumruhusu kurudi nyumbani zinaendelea.
 
“Mgonjwa wetu amepona COVID19 na amepimwa mara tatu hana, tumeanza utaratibu wa kumrudisha nyumbani, kazi ambayo nimemuelekeza Katibu Mkuu aifanye sasa hivi suala la kutoa elimu ili kuondoa unyanyapaa, kulaumiana na kunyoshewa vidole Isabela,” amesema.
 
Kadhalika, amesema wasafiri hao 245 wamewekwa karantini kwa siku 14 kwenye maeneo maalum ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Dkt.John Pombe Magufuli.
 
“Tangu agizo la Rais wasafiri 111 kwa Tanzania barana 134 kwa Zanzibar wametengwa kwenye hayo maeneo, na tunasisitiza mikoa yote nchini kuendelea na zoezi la kubainisha sehemu zitakazo tumika kuweka wasafiri bila kuleta usumbufu usio wa lazima,”amesema. 
 
Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar imeendelea kufanya ukaguzi kwa kupima joto lamwili kwa wasafiri wote wanaoingia nchini.
 
“Kuanzia Januari mosi mwaka huu hadi sasa wasafiri 1,890,532 wamefanyiwa ukaguzi wa kupimwa joto kwenye vituo 27 vya mipakani ikiwemo viwanja vya ndege na bandarini na kwa saa 24 zilizopita jumla yawasafiri 3,471 wamefanyiwa ‘screening’,”amesema.
 
Amefafanua kuwa watu 273 wamepimwa sampuli za kupima virusi vya Corona katika Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii hadi Machi 26,2020.
 
“Kati ya sampuli hizo zilizopimwa 260 hazikuonesha uwepo wa virusi hivyo na sampuli 13 zilithibitika kuwa na virusi, wagonjwa hawa ni kutoka Mkoa wa Arusha (2), Dar es salaam(8), Zanzibar (2) na Kagera (1),”amesema.
 
Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameshukuru msaada wa vifaa mbali mbali ikiwemo vya kupima virusi haraka (Rapid test kits) kutoka kwa Taasisi zilizopo Jamhuri ya watu wa China za Jack Ma na Alibaba na vitasambazwa kwenye hospitali zilizotengwa maalum kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hao.
 
Waziri Ummy amesema maabara iliyopo haijazidiwa na utaratibu mzuri umeandaliwa wa upimaji wa sampuli kutoka mikoani.
 
Aidha, amesema serikali inatarajia kuongeza maabara sita na Zanzibar moja.
 
“Tumeona pia kuna haja ya kuongeza maabara, tayari maabara ya Chuo Kikuu Sokoine (Sua) inaweza kupima sampuli, pia maabara za NIMR Mbeya, Tanga, Mwanza na Arusha ile maabara ya St.Nelson Mandela, hili tumeliona lakini tumeona kuna haja ya kuwa na ‘rapid test’, tupo vizuri hatujazidiwa na sampuli zinafika kwa wakati kwenye maabara yetu,”amesema.
 
Waziri huyo amesema vipimo vya kupima virusi kwa haraka vitawekwa kwenye Hospitali za Mikoa, Kanda na kwenye mipaka.
 
“Jumuia ya ya Afrika Mashariki pia jana tumepata msaada wa maabara zinazotembea, na tuta pata mbili kwa Tanzania ambazo zitapelekwa Arusha na Zanzibar,”amesema.
 
Naye, Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad RashidMohammed, amewataka Watanzania kujikinga na ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa Serikali haina nia ya kumuweka mtu kambini kumtesa.
 
Mwisho.

Jumatano, 25 Machi 2020

TAASISI YA BENJAMIN MKAPA YAMWAGA AJIRA 307 ZA WATUMISHI WA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza jambo wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akifafanua jambo wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt. Ellen Mkondya akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano ulioongozwa na Waziri wa Afya leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza jambo wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma. katikati ni naibu waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula (wakwanza kushoto).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Waandishi wa habari.


TAASISI  YA BENJAMIN MKAPA YAMWAGA AJIRA 307 ZA WATUMISHI WA AFYA.

Na Rayson, Mwaisemba, WAMJW-DOM

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa inayotekeleza mradi wa Uimarishaji mifumo endelevu na stahimivu ya Afya kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu, imeajiri jumla ya watumishi 307 ikiwa ni muendelezo wa kuimarisha huduma za Afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma.

“Tunapenda kuwataarifu mwendelezo wa kazi nzuri inayotekelezwa kupitia mradi huu na kwamba taratibu za ajira kwa wataalam wa afya wengine 307 zimekamilika. Lengo kuu la zoezi hili ni kuongeza nguvu katika utoaji huduma katika sekta ya afya”, alisema Waziri Ummy.

Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na Naibu Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula, Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Mkapa, kuanzia mwaka 2018 hadi February 2020, imeweza kuajiri jumla ya watumishi wa afya 461 ambao wanatoa huduma za afya sehemu mbalimbali nchini.

Aliendelea kusema kuwa, Watumishi hawa watahudumu kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizopo katika mikoa 12 ya Kagera, Mwanza, Geita, Simiyu, Mara, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Katavi, Dodoma, Songwe na Kilimanjaro.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa, wataalamu hao 307 wameshapangiwa kufanya kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 68 zilizopo katika Mikoa 11, huku akibainisha kuwa Mikoa iliyonufaika ni Mwanza (34), Shinyanga (33), Mara (43), Simiyu (51), Geita (30), Kagera (34), Katavi (41), Tabora (43), Dodoma (27), Arusha (10) na Kigoma (42).

Alisema kuwa, Kupitia mchakato huu wa ajira, Kada sita za wataalamu wa Afya zimenufaika na kibali hiki kwa mgawanyo ufuatao; Kada ya Wauguzi wenye cheti (59), Wauguzi wenye Diploma (30), Maafisa Tabibu (73), Maafisa Tabibu Wasaidizi (100), Wataalamu wa maabara ngazi ya cheti (25) na ngazi ya Diploma (20).

Mbali na hayo, Waziri Ummy ameendelea kuwahimiza wataalamu wote waliopangiwa maeneo ya kufanyia kazi kuripoti mara moja kuanzia tarehe 23 hadi 27 Machi 2020, na kuanza kutekeleza majukumu yao katika vituo watakavyopangiwa.

“Napenda kuwahimiza wataalamu wote waliopangiwa maeneo ya kufanyia kazi kuripoti mara moja kuanzia tarehe 23 hadi 27 Machi 2020, ili kuanza kutekeleza majukumu yao katika vituo watakavyopangiwa” alisema

Nae, Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa, Serikali imeendelea kuimarisha mfumo wa upataji taarifa (mawasiliano), huku akiwataka waombaji kufanya maombi ndani ya muda ulioelekezwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt. Ellen Mkondya amesema kuwa, taasisi ya Benjamin Mkapa kwa miaka 14 imetoa ajira za wataalam wa afya 2181 ambao wamekuwa wakitoa huduma katika Hospitali na Vituo vya tiba nchini kote, hususan vituo vya serikali na baadhi kwenye vituo vya kidini.

“Taasisi ya BMF kwa miaka 14 yote tokea mwaka 2006 hadi Desemba 2019, tumeshaweza kutoa ajira za wataalam wa afya 2181 ambao wamekuwa wakitoa huduma katika Hospitali na Vituo vya tiba nchini kote, hususan vituo vya serikali na baadhi kwenye vituo vya kidini” alisema.

Mwisho.

Ijumaa, 29 Novemba 2019

VIONGOZI WA DINI WASAINI MAAZIMIO YA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU

- Hakuna maoni
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea viongozi wa dini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa viongozi wa dini wa Taifa na wa kanda ya ziwa ambapo viongozi hao walitia saini maazimio ya mapambano dhidi ya kifua kikuu jijini Mwanza

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea wakati wa mkutano wa viongozi wa dini ambapo alisema wanayo imani na viongozi wa dini kwani wanawafikia wananchi wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwakaribisha viongozi mbali mbali wa Serikali Wakitaifa, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi zisizo Zakiserikali na wageni wengine katika Mkoa wa Mwanza.

 Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu (TB) na Ukoma nchini Dkt. Beatrice Mutayoba.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Josephat Kandege kwenye mkutano wa viongozi wa dini katika vita dhidi ya Kifua Kikuu.

 Viongozi mbalimbali wa dini wakifuatilia mkutano huo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

 Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa mkutano huo.

Picha ikionesha kuendelea kwa Mkutano wa viongozi wa dini wa Taifa na wa kanda ya ziwa ambapo viongozi hao walitia saini maazimio ya mapambano dhidi ya kifua kikuu jijini Mwanza.

Viongozi wa dini wakisaini maazimio ya kushiriki  mapambano ya kutokomeza  kifua kikuu.Mkutano huo umeandaliwa na Bunge kupitia mtandao wa wabunge wa kupambana na kifua kikuu.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, akiambatana na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda pamoja na Viongozi wengine Wakitaifa na Viongozi wa Dini.


VIONGOZI WA DINI WASAINI MAAZIMIO YA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU

Na. Catherine Sungura, wamjw - MWANZA

Serikali ya Tanzania inatenga mabilioni mengi katika kushughulikia masuala ya afya nchini hususani kwenye upande wa tiba ambapo gharama za matibabu zinakuwa kubwa sana.

Hayo yamesemwa leo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakati kusaini tamko la maazimio ya viongozi wa dini lililobeba ajenda ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) nchini  jijini hapa .

“Wananchi wanadhani kuwa wizara ya afya inasimamia tu tiba, hapana tusisahau kinga ni muhimu sana  dhidi ya magonjwa nchini, tutakaposimamia kinga  serikali itakua inaokoa gharama kubwa kwenye matibabu na pia kupunguza mzigo mkubwa wa kugharamia matibabu kama nchi”Alisisitiza Mhe. Ndugai

Aidha, amewashuru viongozi hao wa dini kwa ahadi pamoja na kusaini azimio  la kusimamia na kusemea kwa waumini  wao suala zima la TB hivyo anayo Imani watalibeba na kulitekeleza na kuwafanya wananchi wengi kupata uelewa juu ya ugonjwa huo na kujitokeza  mapema kwenda kupima afya zao na hivyo kuanza dawa  na  kutoambukiza watu wengine.

Awali akiongea na viongozi hao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  amesema kuwa Wizara yake  inaendelea kubuni mikakati ya kutokomeza  Tb nchini kama  mikakati Madhubuti yaliyowekwa   kwa mara ya kwanza na baraza kuu la umoja wa mataifa lililokutana Septemba mwaka 2018 na kuweka maazimio na malengo ya  kuongeza kasi ya  kutokomeza TB  ifikapo mwaka 2030.

“Maambukizi mapya ya Tb nchini yamepungua kwa asilimia 18 kulinganisha  na hali ya mwaka 2015 na hivyo kufanya Tanzania  kuwa miongoni  mwa nchi saba  Duniani ambazo zipo katika mwelekeo sahihi wa kufikia malengo ya mpango mkakati wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kutokomeza TB kwa hatua ya kwanza ya mwaka 2020.

Aidha, Waziri Ummy amesema  kuwa vifo vitokanavyo na Tb peke yake vimepungua kutoka 30,000 mwaka 2015 hadi 22,000 mwaka 2018 na hii ni sawa na punguzo la asilimia 27,“licha ya mafanikio, nchi bado ina vifo vingi vinavyosababishwa na Tb ambapo kwa sasa takribani watu sitini  hufariki   kila siku hapa nchini”, alisema .

Hata hivyo Waziri huyo wa afya amesema kuwa hadi kufikia mwaka huu serikali ina vituo 103 vinavyotoa huduma za wagonjwa wenye Tb sugu ukilinganishwa na kituo kimoja mwaka 2015  pamoja na uboreshaji wa mifumo ya  uchunguzi  na ugunduzi wa TB kwenye vituo vya  huduma za afya,upanuzi wa matumizi ya hadumini za kisasa za LED na kuongezeka kwa mashine za kisasa zinazopima vimelea vya TB kwa njia ya vina saba za GenXpert zipatazo 238 ambazo kwa sasa zinapatikana kwenye mikoa yote nchini.

MWISHO

Jumatatu, 2 Septemba 2019

HABARI PICHA: WATAALAM WA MAWASILIANO WAJIDHATITI KUTANGAZA MAFANIKIO YA SEKTA YA AFYA NCHINI.

Na Englibert Kayombo, WAMJW - Mwanza

Habari Picha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu AFYA) Bw. Gerard Chami akisema jambo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake katika Kikao kazi Jijini Mwanza kupanga mkakati wa mawalisiano wa mafanikio ya Sekta ya Afya.

"Ni lazima tufanye kazi kwa umoja na ushirikiano kuhakikisha kwamba tunatangaza vyema mafanikio ya Sekta ya Afya nchini" Bi. Anjela Mziray Meneja Mawasiliano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

"Mikakati yote ya kuboresha Sekta ya Afya imewekwa kwenye Ilani ya Chama Tawala (Chama Cha Mapinduzi CCM), ni vyema kuielewa vizuri ili kujua dira ya Serikali ya Awamu ya Tano kwenye Sekta ya Afya nchini" Bw. Aminiel Aligaesha Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Afisa Mawasiliano kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Bw. Hamza Mwangomale akiteta jambo na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Bi. Neema Mwangomo (kushoto) kwenye kikao kazi cha  Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake Jijini Mwanza.

Afisa Habari na Uhusiano kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Bw. Karimu Meshack (wa katikati) akisema jambo wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake Jijini Mwanza.

Afisa Uhusiano kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi. Grace Michael akirejea kusoma Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kufahamu zaidi malengo ya Chama Tawala kwenye Sekta ya Afya nchini.
_________________________________________________________________________________

Picha Mbalimbali za Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake wakiwa kwenye kikao kazi Jijini Mwanza wakijadili mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa mawasiliano ya Sekta ya Afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.