Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 16 Machi 2019

WAGONJWA WATANO WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA

- Hakuna maoni
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Charles Shija

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza kushoto) akiwa katika kikao na Madaktari bingwa kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan baada yakufanikisha upandikizaji wa figo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Kikao cha Madaktari bingwa kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan na kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile baada yakufanikisha upandikizaji wa figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa na Madaktari bingwa kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan na Wataalamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma baada yakujionea upandikizaji wa figo wenye mafanikio.

Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma


WAGONJWA WATANO WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA

Na WAMJW - DOM

Hospitali ya  Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la Tokushukai lilopo nchi ya Japan.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Dkt.  Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa

"Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama, yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii" alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji  wa kibingwa ili waweze kuwahudumia Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.

"lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya upasuaji huu" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka  wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa.  80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza,  kwa sababu badala ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana " alisema Dkt. Ndugulile.

Mwisho.

WATUMISHI TUISHI KWA UPENDO

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akiongea na Watumishi wa Sekta ya Afya, katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea na Watumishi wa Sekta ya Afya (Hawapo kwenye picha) wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa Eng. Amani Msuya akiwasilisha hoja za Wafanyakazi mbele ya Mgeni rasmi wa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula

Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (Watatu kutoka kushoto) wakati wakiimba wimbo wa kuhamasisha umoja na mshikamano wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Sekta ya Afya ambao pia ni Wanachama wa TUGHE Taifa wakishikana mikono huku wakiimba wimbo wa kuhamasisha umoja na mshikamano, wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma.


Baadhi ya Watumishi wa Sekta ya Afya ambao pia ni Wanachama wa TUGHE wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Mgeni rasmi ambae ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile(Hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambae pia ni mgeni rasmi wa Mkutano huo Dkt Faustine Ndugulile akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma

Picha ya pamoja ikiongozwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakiwa na baadhi ya Wajumbe wa TUGHE Taifa akati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kujadili bajeti ya Wizara ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Mipango Jijini Dodoma.


WATUMISHI TUISHI KWA UPENDO

Na WAMJW – Dodoma.
Watumishi watakiwa kudumisha upendo, umoja na mshikamano katika mahala pa kazi na kufanya kazi kwa bidii ili kutoa huduma iliyo bora.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na watumishi wa Sekta ya afya wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika jijini hapa

Dkt. Ndugulile amesema anaamini kuwa Wizara ya Afya itafika mbali zaidi ikiwa watumishi watafanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kuheshimiana bila kujali utofauti wa vyeo baina ya watumishi.

“Kila mmoja amuheshimu mwenzake kwa sababu ana mchango katika haya yote tunayoyafanya na tunategemeana sana kwenye kazi zetu za kila siku” amesema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amewataka watumishi kuziheshimu nafasi za uongozi walizonazo sasa kwa kuzienzi na kuhakikisha wanafanya kazi ili kuthibitisha kuwa kweli wanastahili kuwa kwenye nafasi hizo.

“Bado kuna watumishi wengine hawajajitafakari katika nafasi zao, lugha tunazozitoa, kutojituma, tuache kufanya kazi kwa mazoea” alisema Dkt. Ndugulile.

Awali akizungumza na wajumbe wa mkutano, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa umoja na kujitolea ili wote kwa pamoja kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Katika Mkutano huo wajumbe walipitia na kujadili masuala kadha wa kadha kuhusiana na Wizara ya Afya ikiwemo bajeti ya Wizara, mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii, Sera ya Afya, Bima ya Afya pamoja na masuala ya utendaji ndani na nje ya Wizara.

Mwisho




Ijumaa, 15 Machi 2019

SERIKALI YAOKOA BILION 4.2 KWENYE MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe na wamwisho ni Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Figo nchini Dkt. Kisanga




Waandishi wa Habari waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.



SERIKALI YAOKOA BILION 3.4 KWENYE MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO

Na WAMJW-DOM.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa kiasi cha Shilingi Bilion 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu kwa Wagonjwa wa Figo nje ya Nchi.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ikiwa ni Siku ya Figo Duniani ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya ya figo kwa kila mmoja kila.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka  wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa.  80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” Alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt, Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia magonjwa ya figo ni pamoja na uzito wa kupindukia (obesity), matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara,kutokufanya mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa dawa za kupunguza maumivu.

Aliendelea kusema kuwa, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha matatizo ya figo, magonjwa haya yakitambuliwa mapema yanaweza kudhibitiwa kwa matibabu na kuepusha madhara kwenye figo.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Kufikia Desemba mwaka 2018, jumla ya vituo 28 vyenye jumla ya wagonjwa 1050 vilikuwa vikitoa huduma ya usafishaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.

Alhamisi, 14 Machi 2019

TAMKO LA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, DKT. FAUSTINE NDUGULILE (MB) KWENYE MAADHIMISHO YA WIKI YA KUONGEZA UELEWA KUHUSU UGONJWA WA SHINIKIZO LA MACHO “GLAUCOMA”


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB)

 

TAMKO LA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, DKT. FAUSTINE NDUGULILE (MB) KWENYE MAADHIMISHO YA WIKI YA KUONGEZA UELEWA KUHUSU UGONJWA WA SHINIKIZO LA MACHO “GLAUCOMA”

TAREHE 10-16 MARCH 2019
Ndugu wananchi,
Maadhimisho ya wiki ya elimu juu ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho huadhimishwa duniani kote ikiwa ni Mpango ulioanzishwa na Chama cha Wagonjwa wa Shinikizo la Macho na Chama cha Wataalamu wa Afya wa Shinikizo la Macho kwa lengo kuu la kuongeza uelewa na kujenga ufahamu wa wananchi juu ya ugonjwa huu hatari wa Shinikizo la Macho, ujulikanao kwa kitaalam “Glaucoma” au Presha ya Macho, katika azma nzima ya kuzuia ulemavu wa kutokuona.  Tanzania, inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha wiki hii muhimu kwa Afya ya Macho.
Maadhimisho haya yaliyoungwa mkono na wadau wa Afya ya Macho duniani, kwa mwaka huu, yanafanyika wiki ya tarehe 11 mpaka 17 mwezi wa Machi.
Ndugu wananchi,
Asilimia 2.8 ya watu wote wenye upungufu wa kutokuona vizuri, sawa na watu milioni 7 duniani wana Ugonjwa wa Shinikizo la Macho, kati yao, milioni 4.5 hawaoni kabisa.
Shinikizo la Macho ni kati ya vyanzo vinayoongoza kwa idadi ya watu wasioona duniani. Kwa Afrika, ugonjwa wa Shinikizo la Macho unachangia asilimia 15 ya watu wasioona. Ugonjwa wa Shinikizo la macho unaathiri zaidi watu wenye umri kuanzia miaka 40. Kwa Tanzania, inakadiriwa kuwa asilimia 4.2 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 40 wana ugonjwa huu, sawa na watu 440,000. Kwa bahati mbaya, 70-90% ya watu wenye ugonjwa huu hawajijui iwapo wanao ugonjwa huu. Hii inatokana na watu kutokuwa na tabia ya kuchunguzwa Afya ya Macho kama inavyoshauriwa na wataalamu. Kwa kuwa ugonjwa huu huleta ulemavu wa kutokuona katika umri mdogo, Taifa hupoteza nguvu kazi.
Kwa mwaka 2018, ni watu 18,000 tu waliohudhuria kwenye vituo vyetu vya tiba wakiwa na tatizo la Shinikizo la Macho kulingana na vituo vilivyowasilisha taarifa zao. Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na watu walio kwenye hatari ya kuwa na ugonjwa huu ambao wapo kwenye jamii yetu na hawajagunduliwa.
Ndugu wananchi,
Ugonjwa huu wa Shinikizo la Macho ni moja kati ya kundi la Magonjwa ya Macho yanayoshambuliwa mshipa wa fahamu unaopeleka mawasiliano ya uoni kwenye ubongo (Neva ya Optiki) ili kuweza kutafsiri kile unachokiona. Ugonjwa huu husababisha upofu kwa taratibu sana kwa siku hadi siku bila dalili yoyote katika hatua ya awali na hivyo umepewa jina la Mwizi wa kimya kimya wa uwezo wa Macho kuona. Ili kugungua iwapo mtu ana ugonjwa huu, kuna umuhimu sana wa kupima macho angalau mara moja kila mwaka haswa kwa makundi yaliyo hatarini hata kama mtu haoni tatizo lolote kwenye macho.

Ndugu wananchi,
Maadhimisho ya Wiki ya Shinikizo la Macho kwa mwaka 2019 yamebeba kauli mbiu isemayo:
OKOA UONI WA MACHO YAKO
Sambamba na kauli mbiu hii, ujumbe mahususi kwa jamii na wadau wa huduma za macho na afya kwa ujumla ni:
“TAA YA KIJANI, NENDA KAPIME IWAPO UNA SHINIKIZO LA MACHO!”
Kauli mbiu hii inatuhimiza wana jamii kwenda kwenye Vituo vya Tiba kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi iwapo una tatizo la Shinikizo la Macho. Kila mwana jamii anapaswa kupimwa Afya ya Macho yake angalao mara moja kwa mwaka.
Ndugu wananchi,
Aina ya Shinikizo la Macho linalopatikana zaidi kwa Waafrika ikiwemo Tanzania huwa na tabia zifuatazo; haina dalili kama maumivu katika hatua za mwanzo za ugonjwa, huwapata zaidi watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea, huambatana na tatizo la kutokuona mbali (myopia) na kuna uwezekano wa hadi asilimia 20 kuwepo katika familia. Ugonjwa huu husababisha upofu katika muda mfupi kutokana na kuanza kujitokeza katika umri mdogo na wagonjwa huwa na viwango vya juu sana vya presha ya maji ya macho.  Pamoja na kuwa ugonjwa huu mara nyingi hujitokeza kuanzia umri wa miaka 40, watu wengi zaidi hudhurika kadri umri wa kuishi unapokuwa mkubwa.
Ndugu wananchi,
Matibabu ya ugonjwa huu wa Shinikizo la Macho yanapatikana hapa nchini katika vituo vyetu vya tiba vyenye wataalamu wa Macho. Kuna Tiba ya dawa za kushusha Presha ya jicho lakini pia tiba kwa njia ya Upasuaji kwa wale ambao tiba ya dawa haitashusha presha kufikia kiwango cha presha kilicho salama. Iwapo Ugonjwa wa Shinikizo la Macho utagundulika mapema kabla ya mtu amepoteza uwezo wa kuona, tiba ya mapema itawezesha kuzuia hali ya upofu kwa asilimia kubwa.
Ndugu wananchi,
Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuboresha miundombinu pamoja na kuongeza wataalamu wa afya ya macho, Vifaa na Vifaa Tiba ili kusogeza huduma za uchunguzi na Tiba kwa Matatizo ya Macho ikiwemo Shinikizo la Macho karibu zaidi na wananchi. Aidha, kwa kupitia Mwongozo wa Tiba na Orodha ya Dawa Muhimu, Serikali itasimamia na kuhakikisha hali ya upatikanaji wa Dawa za Macho katika vituo vyetu vya tiba inazidi kuimarika.

Ndugu wananchi,
Kama sehemu ya Maadhimisho ya Juma hili, kutakuwa na shughuli za Elimu ya Afya ya Macho pamoja na upimaji wa Afya ya Macho kwenye hospitali mbalimbali hapa nchini kwa wiki nzima ya kuanzia tarehe 10 hadi 16 Machi kwa wale wote watakaojitokeza kwenye kliniki za macho. Iwapo wewe au mmoja kwenye familia yako ana umri wa miaka 40 na kuendelea au kuna ndugu mwenye tatizo hili, mnahimizwa kufika katika hospitali iliyo karibu na wewe ili uweze kupimwa presha ya macho na vipimo vingine vya kuchunguza hali ya mshipa fahamu wa ndani ya jicho.  Aidha, pamoja na elimu kwa wagonjwa wote watakaojitokeza kwenye kliniki za macho, elimu kuhusu Shinikizo la Macho itaendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya kuelimisha jamii.

Ndugu wananchi,
Napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa kila mmoja wetu kutumua Maadhimisho haya kwa kupima Macho. Ikumbukwe uwezo wa kuona uliopotea kutokana na Shinikizo la Macho hauwezi kurejeshwa tena hata baada ya tiba. Lengo kuu la matibabu ni kuzuia uharibifu usiendelee kutokea kwa kupunguza presha ya macho tu. Hivyo kupima mapema ni bora zaidi kuliko kusubiri ugundulike wakati madhara ya ugonjwa yameshajitokeza. Endapo utashindwa kupima kwa kipindi cha Juma hili la Maadhimisho, unaaswa kufika kwa ajili ya huduma ya upimaji katika hospitali zetu zote hapa nchini mara upatapo fursa hiyo.

“Tushirikiane kutokomeza ulemavu wa kutokuona”


ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

Jumatano, 13 Machi 2019

WATOA HUDUMA ZA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFUATA UTARATIBU WA KUTOA HUDUMA HIYO

- Hakuna maoni
Mtaalamu kutoka Sekretarieti ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Marko Hingi akikagua vyeti vya kuruhusu huduma za Tiba Asili kutoka kwa mmoja wa wauzaji wa dawa hizo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtaa wa Kariakoo.




Picha mbalimbali zikionesha wataalamu kutoka Sekretarieti ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala walipofanya ziara ya ukaguzi wa vibali vinavyoruhusu kufanyika biashara kwenye maduka na wauzaji ya Tiba Asili na Tiba Mbadala katika maeneo tofauti Jijini Dar Es Salaam.

Moja ya maduka yaliyofungwa na wataalam kutoka Sekretarieti ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala baada ya kukaguliwa na kubainika kukosa vigezo vya kuendesha biashara hiyo.



Na WAMJW-DSM

Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kulinda afya ya watumiaji wa dawa na huduma hizo.

Hayo yamebainika baada ya timu ya wataalam kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala lililo chini ya Wizara ya Afya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka yanayouza dawa za asili na kutoa huduma za tiba mbadala katika maeneo mbalimbali jijini Dar Es Salaam.

Katika ukaguzi huo imebainika baadhi ya maduka kufanya shughuli hiyo bila ya kuwa na vibali vikiwemo kibali cha mtoa huduma, Kibali cha duka pamoja na kibali cha usajili wa dawa, ambapo vibali hivyo vinatolewa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

Dkt. Ruth Suza msajili wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala amewataka watoa huduma hizo kufuata taratibu zilizowekwa na Wizara ili kuepuka usumbufu wa kufungiwa na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

“Ninawataka watoa huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini kote kuhakikisha wanafuata taratibu zilizowekwa na Baraza ili kuweza kuendesha biashara zao, vinginevyo tukipita kukagua na tukikuta duka lina kasoro kwa kukosa vibali basi tutapiga faini na ikishindikana kulipa faini  tutalifunga duka hilo mpaka muhusika afuate utaratibu unaotakiwa wa kufanya biashara hiyo”. Amesema Dkt. Ruth.

Katika ukaguzi huo uliochukua takribani wiki mbili katika wilaya zote za Jiji la Dar Es Salaam, jumla ya maduka 70 yamekaguliwa, maduka 10 yamefungwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maduka na wauzaji wa dawa kutokua na vibali kutoka baraza la tiba asili na tiba mbadala.
Zoezi hili lenye lengo la kulinda afya ya watumiaji wa dawa za asili na tiba mbadala ni endelevu ambapo linategemea kuendelea katika mikoa yote nchini kukagua uhalali wa usajili wa dawa za asili, vibali vya maduka na watoa huduma pamoja kuhakikisha ubora wa dawa zinazotolewa.











DKT. NDUGULILE AKUTANA NA UGENI KUTOKA SHIRIKA LA NISHATI YA ATOMIKI

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya ugeni kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ulioongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirika wa Kiufundi Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Prof. Abdulrazak Shaukat (Wakwanza kulia)

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya ugeni kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ulioongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirika wa Kiufundi Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Prof. Abdulrazak Shaukat (Wakwanza kulia)

Kikao cha kujadili misaada ya miradi wanayoipata kutoka IAEA, kikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na ugeni kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ulioongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirika wa Kiufundi Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Prof. Abdulrazak Shaukat.





Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kikao na Wadau kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya leo jijini Dodoma.


Na WAMJW - DOM

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo Machi 13, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirika wa Kiufundi Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Prof. Abdulrazak Shaukat juu ya  misaada ya miradi wanayoipata kutoka IAEA, kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Wizara ya Afya Jijini Dodoma.