Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 17 Oktoba 2017

HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA YA MBEYA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KISASA VYA KUTOLEA HUDUMA YA DHARURA NA AJALI.

- Hakuna maoni





 Makamu wa Raisi wa Abbot Fund Andy Wilson akihutubia mbele ya mgeni rasmi  ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Hayupo kwenye picha) wakati
tukio la kupokea vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Dharura na ajali.










 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wafanyakazi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa  Mbeya(Hawapo kwenye picha) katika tukio la kupokea msaada wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Dharura na ajali. Kushoto ni Makamu wa Raisi wa Abbot Fund Andy Wilson na kulia kwa Katibu Mkuu ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na ajali Dkt. Prosper Bashaka.



 Wafanyakazi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa  Mbeya wakimsikiliza Mgeni rasmi ambae ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Hayupo kwenye picha) katika tukio la kupokea msaada wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Dharura na ajali.





 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea msaada wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Dharura na ajali kutoka kwa Makamu wa Raisi wa Abbot Fund Andy Wilson.






Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya pamoja na wageni waalikwa katika tukio la kupokea vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Dharura na ajali.









NAIBU WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA MSD

- Hakuna maoni

Picha yapamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) mapema leo ili kujionea shughuli mbali mbali za utendaji zinazoendelea katika eneo hilo.






Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo pindi alipokuwa akisomewa taarifa ya utendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, tukio lililojiri mapema leo katika viunga vya Bohari Kuu ya Dawa jijini Dar es salaam.





 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari  Laurean Bwanakunu akisoma taarifa fupi kuhusu utendaji wa taasisi hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara katika viunga vya Bohari mapema leo jijini Dar es salaam.

DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa  MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Mwananyamala Bw. Marco Sallingu kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.







Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za  wa Hospitali ya Mwananyamala wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.








 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa  MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Sinza Palestina Bi. Doris Messanga kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.









Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza  kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za Zahanati ya Mwenge wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.








Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa katikati waliosimama akiongea na wagonjwa wakati wa ziara yake Hospitalini  Sinza Palestina alipotembelea vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.

Jumatatu, 16 Oktoba 2017

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. FAUSTINE NDUNGULILE AKUTANA NA BAADHI YA WATUMISHI WA WIZARA YA AFYA LEO OFISI NDOGO ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM

- Hakuna maoni
Baadhi watumishii waliohudhuria kikao  wakimsikiliza kwa makini Mh.Naibu Waziri wa Afya Dr.Faustine E. Ndugulile


Mkurugenzi wa Uhakiki na Ubora akifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Mh. Naibu Waziri


         
             Mh. Naibu Waziri akisikiliza baadhi ya michango ya wajumbe

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MAGARI 58 KUSAIDIA AKINA MAMA WAJAWAZITO KANDA YA ZIWA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amepokea magari hamsini ya kubebea wagonjwa  pamoja na magari 8 ya kuratibu shughuli za huduma za afya ya mama na mtoto yenye thamani ya shilingi   bilioni 5.9 ambayo yamekabidhiwa kwa Wabunge wa  Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kigoma

Waziri Ummy amelishukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) na UNFPA kwa kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania, ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.


Alizitaja changamoto zilizoonekana katika mikoa hiyo ni huduma hafifu ya rufaa kwa wanawake wajawazito kwa kukosa magari ya kubebea wagonjwa, ukosefu wa damu salama, ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya mama ikiwemo kutotambua dalili hatari za wakati wa ujauzito pamoja na baadhi ya watumishi wasiokuwa na stadi za kuokoa maisha ambayo yanachangia wingi wa vifo vitokanavyo na uzazi

Tafiti zilizofanyika mwaka 2010 na tathmini iliyofanyika mwaka 2015 wakati wa kuandaa mpango kazi wa matokeo makubwa sasa, Mikoa ya Kanda ya Ziwa  ikiwemo Kigoma ilionekana kuwa na viashiria hafifu vya afya ya mama na mtoto kwa mfano; utumiaji mdogo wa uzazi wa mpango, wanawake wachache wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya pamoja na vifo vingi vitokanavyo na uzazi.

Wizara ya Afya imekua ikifanya  jitihada mbalimbali katika kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa awamu hii ya tano  tumetengeneza mpango mmoja utakaohusika na masuala ya uzazi wa afya ya mama na watoto na vijana ambapo ndani ya miaka minne hadi kufikia mwaka 2020 tuwe tumepunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 432 hadi 292 kutoka kila kizazi hai laki moja na kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano Tanzania imefanikiwa kufikia lengo namba nne la malengo ya maendeleo ya milenia kwa  kupunguza vifo kutoka 50 hadi 40 katika vizazi hai 1,000.

Aidha Waziri Ummy amewataka Wabunge, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Wilaya kuyatumia magari hayo ipasavyo yaani, kwa shughuli iliyokusudiwa, vilevile kuyakatia bima ya ajali pamoja na kuiomba jamii, Taasisi zisizo za kiserikali kuunganisha nguvu kwani vifo vitokananyo na uzazi vinazuilika.

Soma zaidi










MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VIPYA VYA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA BIL.1.5

- Hakuna maoni


MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VIPYA VYA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA BIL.1.5

WIZARA YA AFYA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUFIKIA 2020

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali  hawapo pichani wa Wizara ya afya kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini  leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Wakati wa kikao chake na wakuu hao.



Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo  Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.


Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakimpongeza Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani mara baada ya kuwapa maelezo wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es salaam





Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo  Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.



Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akiteta jambo na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile kushoto mara baada ya kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.


DKT.NDUGULILE AANZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KASI

- Hakuna maoni

Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile aliyesimama akiongea na watumishi wa Taasisi ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) hawapo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.





Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile katikati akiingia katika ofisi za  Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea ofisi hizo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC Dkt. Joyceline Kaganda.



Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC)  Dkt. Joyceline Kaganda kulia wakati alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es salaam.



Baadhi ya watendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani wakati alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es salaam.




Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Taasisi  ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam,  , wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIMR Dkt. Yunus Mgaya.

Balozi wa Cuba mhe. Jorge Luis amuaga waziri Ummy

- Hakuna maoni
Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Jorge Luis amuga Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na watoto Ummy mwalimu leo ofisini kwake,Balozi Luis amemaliza muda wake na hivyo kurejea nchini Cuba Waziri Ummy mwalimu amesema anaishukuru nchi ya Cuba kwa ushirikiano wao wa kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya afya hususani kwenye mafunzo na kuleta madaktari kufanya kazi nchini Tanzania(picha na Wizara ya Afya)