Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

MH. UMMY MWALIMU (MB) AFUNGUA MATEMBEZI YA HISANI YAKUHAMASISHA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI.

- Hakuna maoni
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu watatu kutoka kushoto wakati alipofungua matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, kulia kwa Mh. Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage na kushoto  ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Grace Maghembe.




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi cheti moja ya wadau waliofanikisha matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti iliofanyika mapema leo katika viunga vya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakirusha Maputo juu kuashiria ufunguzi rasmi wa matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, iliofanyika katika viunga vya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.





Wadau kutoka taasisi mbali mbali walioungana na Mh. Ummy Mwalimu na watumishi wa Hospitali ya Ocean Road katika matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti yaliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
 
 
 
 
 
 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiambatana na Binti yake katika matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti yaliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
 
 
 
 
 
 
 

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

AFYA YANGU, MTAJI WANGU

- Hakuna maoni

"Hakikisha unamkinga mwanao dhidi ya ugonjwa wa Polio kwa kukamilisha Dozi 4 za Polio"

AFYA YANGU,MTAJI WANGU

- Hakuna maoni



Zuia Mtoto Kuzaliwa na Mgongo Wazi au Kichwa Kikubwa kwa kutumia Vyakula vilivyowekwa Virutubishi zaidi kwa Afya Bora.

MH. UMMY AWAJIA JUU VIONGOZI WANAOWAKAMATA MADAKTARI BILA KUFUATA UTARATIBU

- Hakuna maoni

Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 49 la Afya na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Madaktari yaliofanyika jijini Dar es salaam, huku likihudhuliwa na Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu.

MH. UMMY AHIMIZA UTARATIBU UFUATWE ILI KUWACHUKULIA HATUA MADAKTARI.

- Hakuna maoni





Na WAMJWW  
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ahimiza weledi na kukemea vitendo vya baadhi ya Viongozi  kuwachukulia hatua madaktari na badala yake kuwataka wafuate utaratibu uliowekwa.
Mhe. Ummy aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 49 la Afya na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Madaktari.
Nae Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameliagiza Baraza la Mitihani kufanya uhakiki haraka ili wataalamu wa Sekta za Afya wapangiwe vituo.
“Tangu tuingie madarakani  serikali imeweza kutoa vibali vya ajira mpya vipatavyo 3,410 kwa awamu mbili, awamu ya kwanza vibali vya madaktari 258 na awamu ya pili vibali 3,150 kwa wataalamu wa kada ya afya na taratibu za ajira kwa wataalamu hawa 3150 zimekamilika na imebakia hatua ya uhakiki wa vyeti katika Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)” alisema Mh. Samia Suluhu.
Makamu wa Rais aliwapongeza Chama cha Madaktari kwa kuweza kuandaa Kongamano la 49 na kuweka historia ya kuandaa Makongamano tangu mwaka 1965.
Kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “ Malengo ya Maendeleo Endelevu: Uweledi wa Kitaaluma na Utoaji Bora wa Huduma za Afya Nchini Tanzania.” Mada hii ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza kwa vitendo wajibu wake wa kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa huduma za afya zenye viwango na zinazokidhi mahitaji.

Jumatano, 25 Oktoba 2017

Mh. UMMY MWALIMU(MB) AGAWA MASHINE ZA KUCHUNGUZA SARATANI

- Hakuna maoni


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu agawa mashine 100 za tiba mgando (Cryotherapy) na mashine 9 za upasuaji mdogo (LEEP) ambazo zitatumika kwaajili ya matibabu ya awali ya Saratani kwa Wanawake. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viunga vya ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam. Pia makabidhiano hayo yalihudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile, Baadhi ya Watumishi wa Wizara hiyo na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali.

Jumanne, 24 Oktoba 2017

BALOZI WA IRANI MH. MOUSA FARHANG ATETA NA WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU KATIKA OFISI NDOGO ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM.

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu watatu kutoka kushoto akimsikiliza Balozi wa Irani nchini Tanzania Mh. Mousa Farhang mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam huku lengo la ugeni huo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo hususani katika sekta ya Afya. Kulia mwa Barozi Mousa ni Dkt. Mahmoud.




Na WAMJWW
Balozi wa Irani nchini Tanzania Mh.Mousa Farhang mapema leo amemtembelea Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili hususani katika nyanja za teknolojia na matibabu ya kibingwa.
Aidha Balozi Mousa amemtoa hofu Mh. Ummy na kumuahidi Irani itaendelea kushirikiana na Tanzania bega kwa bega katika kuhakikisha kwamba wanasukuma gurudumu la maendeleo hasa katika nyanja ya Afya kwa kuimarisha huduma za kibingwa.
Kwa upande mwingine Balozi Mousa ameishukuru Serikali yake ya Misri kwa kuisaidia Tanzania ikiwemo uchimbaji wa visima maeneo ya vijijini jambo lililosaidia kupunguza hadha ya maji kwa jamii hususani wanawake.
Hata hivyo Balozi Mousa Farhang ameahidi kuendeleza ushirikiano huo na Serikali ya Tanzania huku akiwataka wawekezaji kutoka Irani kuja kufanya uwekezaji mkubwa nchini hapa hususani katika viwanda vya dawa.
Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameshukuru ugeni huo kutoka Irani ulio na tija kwa taifa la Tanzania huku akisisitiza na kuweka  mkazo wa ushirikiano huo katika uwekezaji wa chanjo, kutoa madawa,vifaa na vifaa tiba, ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa watoa huduma wa Tanzania na kujenga uwezo wa Ushirikiano katika maeneo ya utafiti wa tiba.

Jumatatu, 23 Oktoba 2017

PICHA ZA BAADHI YA MATUKIO YAKUKABIDHI MASHINE ZA KUCHUNGUZA SARATANI.

- Hakuna maoni





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 23 Oktoba, 2017 amekabidhi mashine 100 za tiba mgando (cryotherapy) na mashine  9 za upasuaji mdogo (LEEP) ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake watakaofanyiwa uchunguzi na kukutwa na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Waziri Ummy amesema katika kuhakikisha tunaongeza upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ya Saratani ya Mlango wa Kizazi, Wizara ya Afya imekuja na mkakati wa kuboresha huduma hizi kwa kununua mashine na vifaa hivyo ambavyo vimegharimu kiasi cha shilingi bilioni moja na vitasambazwa katika mikoa 10 ikijumlisha halmashauri 31 ambazo tumebaini zina vituo vichache vya kutolea huduma  hizi ukilinganisha na Mikoa mingine.

SERIKALI YAONGEZA VITUO 100 KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA AWALI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NCHINI

- Hakuna maoni



Ndugu wanahabari,
Tanzania ni mojawapo ya nchi za kusini mwa Afrika zinazokadiriwa kuwa na  idadi kubwa ya wagonjwa na vifo vingi vitokanavyo na Saratani.  Takribani wagonjwa wapya 50,000 kila mwaka wanagundulika kuwa na Saratani, na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia hamsini (50%) ifikapo mwaka 2020.

Taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2015 zinaonyesha kwamba aina za Saratani zinazoongoza hapa nchini ni kama ifuatavyo; Saratani ya mlango wa kizazi (34%),Saratani ya Ngozi (kaporsis Sarcoma)(13%), Saratani ya matiti (12%), Saratani ya mfumo wa njia ya chakula (10%), Saratani ya Kichwa na shingo (7%), Saratani ya Matezi (6%), Saeatani ya Damu (4%), Saratani ya Kibofu cha mkojo (3%),Saratani ya ngozi (3%), Saratani ya Macho (2%), na saratani ya tezi dume (2%).  Mbaya zaidi, asilimia 80 ya  wagonjwa wote hao wanafika Ocean Road wakiwa katika hatua za mwisho za  ugonjwa na kufanya matokeo ya matibabu kutokuwa mazuri.


Ndugu wanahabari,
Kupitia takwimu hizi ni dhahiri kuwa Saratani ya Mlango wa Kizazi husababisha vifo vingi kwa wanawake, ikifuatiwa na saratani ya matiti. Na kama ilivyo kwa saratani nyingine, asilimia 80 ya wanawake wanaougua saratani hiiwanafika katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya tiba wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa, ambapo hufanya  matibabu kutokuwa na matokeo mazuri. Aidha Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutibu wagonjwa  hawa.  Saratani ya Mlango wa kizazi inatibika endapo itagundulika mapema sambamba na kusaidia kupunguza gharama za matibabu ambazo Serikali, familia na mgonjwa wamekuwa wakikabiliana nazo.

Tangu mwaka 2008, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilianza kutoahuduma ya uchunguzi kwa kutumia siki(acetic acid) na matibabu ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kutumia tiba mgando (cryotherapy).Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, Wizara imeshaanzisha vituo 459 (vituo 343 vya serikali na 116 vya mashirika na watu binafsi) vinavyotoa huduma ya uchunguzi na matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani ya Mlango wa Kizazi. Wizara inawapongeza na kuwashukuru wadauwote wanaoshiriki katika kuimarisha upatikanaji wa huduma hizi. Kipekee tungependa kutambau mchango wa Jhpiego, ICAP, EGPAF, THPS, Marie Stope, PSI, Umati, MEWATA, T Marc na WAMA.  Tunawashukuru sana!

Ndugu  wanahabari,
Katika kuhakikisha tunaongeza upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ya Saratani ya Mlango wa Kizazi, Wizara ya Afya imekuja na mkakati wa kuboresha huduma hizi kwakununuamashine 100  za tiba mgando  (cryotherapy) na mashine  9 za upasuaji mdogo (LEEP) ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake watakaofanyiwa uchunguzi na kukutwa na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi. Pia tumenunua mitungi 173 ya gesi ya ‘’carbon dioxide‘’ itakayowezesha mashine hizo kufanya kazi. Vilevile, tumeshatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa huduma ili kuweza kutoa huduma hizi bila vikwazo. Vifaa hivi vimekwishawasili nchini na vinaanza kusambazwa katika vituo vya Tiba 100 nchini kuanzia kesho. Vifaa hivyo vitasambazwa katika mikoa 10, halmashauri 31 ambazo tumebaini zina vituo vichache vya kutolea huduma  hizi ukilinganisha na Mikoa mingine. Mikoa hii ni Mara, Singida, Geita, Dodoma, Tanga, Arusha, Manyara, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Ndugu  wanahabari,
Kupitia hatua hii, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Mhe Dr. John Pombe Magufuli inaongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani kutoka vituo 343 (2015) hadi vituo 443 (2017). Huduma hizi zinapatikana katika Hospitali zote za Rufaa za Kanda na Mikoa, Hospitali zote za Wilaya, na baadhi ya Vituo vya Afya na Zahanati.


Ndugu wanahabari,
Kupitia kwenu, napenda kuwahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ya Saratani ya Mlango wa Kizazi katika vituo hivi. Huduma hizi zinatolewa katika kliniki ya afya ya mama na mtoto kila siku na bila malipo yoyote. Aidha ninavielekeza vituo vyote vya umma nchinikutenga siku maalumu katika kila mwezi ambayo kituo kitahamasisha wanawake kuja kwa wingi kupata huduma hizi. Na kwa kuwa mwezi wa Octoba kila mwaka ni mwezi wa uhamasishaji wa upimaji wa saratani ya matiti duniani kote,  nitumie fursa hii kutoa rai kwa wananchi hasa wanawake wenzangu kuhudhuria vituoni kupata huduma za uchunguzi mapema. Wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha aidha kwa kutofahamu au uelewa mdogo kuhusu saratani.

Ndugu wananchi,
Aidha, katika kuhakikisha huduma hizi zinakuwa endelevu, nazielekeza halmashauri zote kutenga fedha za kutosha kuhakikisha huduma hizi zinaingizwa kwenye mipango yao ya bajeti ya vituo na halmashauri. Pia ni lazima wahakikishe mashine hizi zinatunzwa na kufanyiwa ukarabati inapobidi.Kwa upande wetu Wizara ya Afya, tutaendelea kusimamia ubora wa huduma zinazotolewa kulingana na miongozi, kujenga uwezo wa watoa huduma. Vilevile, tutahakikisha mafundi sanifu tiba wanapatiwa uelewa na nyezo za kufanya matengenezo madogo na ukarabati wa mashine hizi kwa kushirikiana na Halmashauri husika.

Kwa ujumla, Serikali  itaendelea kuhakikisha vituo zaidi vinaanzishiwa huduma hii ili ipatikane karibu zaidi na wananchi hasa wa vijijini. Vilevile, tutahakikisha tunapanua huduma za Rufaa za Matibabu ya saratani  nchini kwa kuhakikisha huduma za Tiba kwa kutumia dawa (Chemotherapy ) na Mionzi (Radiotherapy) zinapatikana katika  Hospitali za Rufaa za Kanda- Mbeya, Bugando na KCMC ili kupunguza msongano wa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es salaam.

ASANTENI  KWA KUNISIKILIZA

MH. UMMY MWALIMU (MB) AKABIDHI MASHINE ZA UCHUNGUZI SARATANI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari (hawapo kwenye picha) wakati wakati akikabidhi  vifaa vya uchunguzi wa Saratani kwa Bohari ya Dawa (MSD), tukio lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam, pembeni yake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu  pamoja na Naibu Waziri wake Dkt. Faustine Ndugulile wakipokea vifaa vya uchunguzi wa magonjwa ya Saratani kutoka kwa Mkurugenzi  wa ugavi na ununuzi Wizara ya Afya Casto Simba katika tukio lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.








Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu kuhusu Saratani wakati akikabidhi  vifaa vya uchunguzi wa Saratani kwa Bohari ya Dawa (MSD) mapema leo jijini Dar es salaam.
 







Waandishi wa habari kutoka vituo mbali mbali hapa nchini wakifanya kazi yao kwenye  tukio la kukabidhi  vifaa vya uchunguzi wa magonjwa ya Saratani kwa Bohari (MSD),tukio  lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam










Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akitete jambo na Naibu wake Mh. Faustine Ndugulile wakati wa tukio la kukabidhi  vifaa vya uchunguzi wa magonjwa ya Saratani lililofanyika mapema leo