Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 13 Novemba 2017

WIZARA YA AFYA YAUOMBA UONGOZI WA TIBA ASILI KUTOKA CHINA KUISAIDIA KUJENGA KITUO CHA UENDESHAJI WA TIBA ASILI.



Na WAMJWW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto yauomba ugeni wa Viongozi wa masuala ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka China kuisaidia kujenga kituo cha uendeshaji wa Tiba Asili ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, utafiti wa kina na kuwa na eneo la kumbu kumbu la kutunza miti dawa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya mapema leo wakati apokea ugeni wa Viongozi wa masuala ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka China uliofika nchini tangu Novemba 12, huku ugeni huo ukitarajia kuwepo nchini mpaka Novemba 16.
Pia Dkt. Mpoki ameuomba ugeni huo kuwekeza zaidi katika uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha Dawa, sambamba na kuiruhusu Tanzania kuuza Dawa zake za Asili katika nchi ya China  jambo litalosaidia Tanzania kuwa na mashamba makubwa ya kuzalisha Dawa.
Nae Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohhamad Bakar Kambi ameahidi kushirikiana bega kwa bega na jopo la uongozi huo hususani katika kuboresha huduma za Afya nchini , huku akitia mkazo kuimarisha zaidi ushirikiano katika kufanya tafiti na kubadilishana ujuzi kupitia mafunzo.
Nae kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Peter Mhane amefurahishwa na ujio wa huo huku akiamini kwamba ushirikiano huu ni faida kwa nchi ya Tanzania kwani itasidia kuondokana na umasikini na kuondokana na upungufu wa Dawa.

WIZARA YA AFYA YAPOKEA UGENI KUTOKA CHINA KUHUSU MASUALA YA TIBA ASILI.

Picha ya Ugeni wa viongozi wa Tiba Asili kutoka China wakiwa katika kikao na viongozi wa Wizara ya Afya kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya mapema leo jijini Dar es salaam.








Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza jambo mbele ya jopo la Viongozi wa Tiba Asili kutoka China (hawapo katika picha) waliowasili nchini Novemba 12 lengo likiwa ni kuikuza Sekta ya Afya nchini kulia ni Mkurugenzi msaidizi,idara ya ushirikiano wa kimataifa wa masuala ya Tiba Asili nchini China, Mr Wu Zhendou.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi,Idara ya ushirikiano wa kimataifa wa masuala ya Tiba Asili nchini China Mr Wu Zhendou.







Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akionesha zawadi aliyopokea kutoka kwa Uongozi wa Tiba Asili nchini Chini, wa kwanza kushoto ni Mr. Liu Qunfeng, wa pili ni Mkurugenzi msaidizi,Idara ya ushirikiano wa kimataifa wa masuala ya Tiba Asili nchini China Mr Wu Zhendou na wa mwisho ni Mganga Mkuu wa Serikali  Prof. Bakar Kambi.





Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya muda baada ya kuupokea ugeni kutoka nchi ya China katika masuala ya Tiba Asili, mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Jijini Dar es salaam.

Jumamosi, 11 Novemba 2017

WATANZANIA WAASWA KUFANYA MAZOEZI KUEPUKA UGONJWA WA KISUKARI. NA WAMJW-DA ES SALAAM.N



Na WAMJWW

WATANZANIA waaswakujihusishanatabia ya kupendakufanyamazoeziilikuepukaugonjwawakisukarinaviashiriavyakekatikajamiiyetuinayotuzunguka.

HayoyamesemwanaMkurugenziwaKinga Wizara ya afya Dkt. NeemaRusibamayilaalipomwakilshaWaziriwa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,WazeenaWatotoMhe. UmmyMwalimuwakatiwakuadhimishasiku ya Kisukaridunianileojijini Dar es salaam.

Watanzaniatunatakiwakupendakujijengeatabia ya kufanyamazoezimarakwamarailikuwezakuepukamagonjwayasioambukizaikiwemoKisukarinaviashiriavyakekwaujumla” alisemaDkt. Rusibamayila.

AidhaDkt. Rusibamayilaamesemakuwawatanzaniawengihawanabudikujikinganaugonjwahuokwaniasilimia 60 wanafarikikwaugonjwahuodunianikilamwaka.

KwamujibuWaDkt. Rusibamayilaamesemakuwaasilimiakubwa ya wanawakenchiniwanauzitomkubwa,mafutamenginahawajihusishinamazoezihivyohupelekeakupatahatharizaugonjwawakisukari.

MbalinahayoDkt. Rusibamayilaamesemakuwalichatu ya kufanyamazoezilakinipiawanatakiwakuepukamatumizi ya vileokama vile uvutajitumbaku,unywajipombenauvutajiwa shisha ilikuepukamagonjwayasioambukizakwaniyamekuwahatarikwawatanzania.

Kwaupande wake KaimuMkurugenziwaKituo cha chakulanaLishe (TFNC) Dkt. VicentAsseyamesemakuwasambambanakufanyamazoeziwatanzaniawanatakiwakuzingatiamloulio bora ilikuepukaugonjwawakisukari.

AidhaDktAsseyamesisitizawalimu , wazazinawatoahudumangazi ya jamaiiwanatakiwakuwakipaumbelekatikakuelimishawatotonajamiinzimakwaujumlajuu ya lishe bora ambayohuletakingazidi ya kisukari.

Siku ya kisukariDunianihuadhimshwaNovemba 14 kilamwakanamwakahuuimeadhimishwasambambanamatembezi ya hiarinamazoezi ya pamojakutokaviwanjavyamuhimbilimpkaMnazimmojanakubebaKaulimbiuisemayo “MWANAMKE NA KISUKARI “ikimaanishawanawakewawemstariwambelekatikakupambananaugonjwahuo.


MATEMBEZI YA SIKU YA UGONJWA WA KISUKARI DUNIANI.

Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya  Dkt. Vicent Assey (aliyevaa tisheti ya bluu) mapema leo katika matembezi ya Siku ya Kisukari Duniani yaliyoanza chuo cha Muhimbili mpaka Viwanja vya Mnazi mmoja.






Watumishi  na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya wakinyoosha viungo baada ya matembezi yaliyo anzia Chuo cha Muhimbili na kukomea viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam katika maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani huku kauli mbiu ikiwa  ni Wanawake na Kisukari.





Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa Umma (HEU) Said Makora (wakushoto) akimsikiliza  Mkurugenzi msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi wakati wa maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.





Mkurugenzi wa kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya  Dkt. Vicent Assey akitoa neon mbele ya wadau wa Afya na Ugonjwa wa Kisukari (Hawapo kwenye picha) wakati wa maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.





Mkurugenzi wa Kinga  Dkt. Neema Rusibamayira ambae alimwakilisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu akisoma taarifa mbele ya wadau wa Afya na Kisukari nchini (hawapo kwenye picha) katika  maazimisho ya Siku ya Kisukari Duniani ambayo kikomo chake ni Novemba 14. Wakwanza  kushoto ni Dkt Waane na wa mwisho ni Mkurugenzi msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi.



Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga  Dkt. Neema Rusibamayira katika  maazimisho ya Siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.







Wadau wa Afya na Kisukari katika matembezi ya Siku ya ugonjwa wa Kisukari Duniani yaliyoanzia Chuo cha Muhimbili na kukomea katika viwanjwa vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam mapema leo.

Ijumaa, 10 Novemba 2017

DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI.

- Hakuna maoni


Na WAMJWW
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto amewataka watoa huduma na mafunzo kuhusu lishe bora yaanzie ngazi za shule ya msingi ili kuwajenga watoto kuzingatia mlo bora katika kukuza afya za watanzania.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini  inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
“Walimu wawe sehemu ya afua za kufundishia wanafunzi juu ya lishe bora hasa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili kuwajengea mazoea watoto kupenda kula mlo ulio bora hata wanapokuwa majumbani mwao” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa baadhi ya watoto walio vijini na mijini wana utapia mlo kwa kukosa chakula kilicho bora hivyo jamii inatakiwa izingatie lishe bora ili kuimarisha afya za watoto nchini.
Mbali na hayo Dkt. Mpoki amesema kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawe kipaumbele katika kutoa elimu ya lishe bora ili kuweza kujikinga na Unyafuzi, Kwashakoo na magonjwa yasiombukiza kama vile Kisukari,shinikizo la damu ,magonjwa ya moyo yanayotokana na ulaji kupita kiasi.
Kwa upande wake Meneja wa  Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe ECSA Bi. Rosemary Mwaisaka amesema kuwa wameamua kuandaa  vitini na vitita vya kufundishia lishe bora ili kuweza kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kufikisha elimu hiyo kwa walengwa.
“Tumeamua kuandaa vitini hivi ili viweze kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kuweza kuwafundisha wanajamii juu ya umuhimu wa kula mlo bora na vitatumika Kenya,Uganda na Tanzania” alisema Bi. Mwaisaka.
Mbali na hayo Mshiriki wa Mafunzo ya Lishe bora kutoka ECSA  ambae pia ni Mtoa huduma Bi. Evelyne Minja amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutoa huduma katika jamii kuhusu mlo bora hasa kwa watoto vijijini na mijini.
“Mafunzo haya yametufanya tujue jinsi ya kuwahudumia na kutoa ushauri juu ya mlo bora hasa kwa watoto wenye viashiria vya utapia mlo kwa kuwapima na kuwapangia vyakula vinavyostahili” alisema Bi. Minja.

DKT. MPOKI AZINDUA VITINI VYA MAFUNZO YA JUU YA LISHE BORA KATIKA JAMII.

- Hakuna maoni
Katibu  Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wadau mbalimbali wa maswala ya lishe hawapo pichani wakati wa uzinduzi  wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini  inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).





Katibu  Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya kushoto akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vincent Assey wa kwanza kulia wakati wa uzinduzi  wa hivyo vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini  inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).









 Katibu  Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akikata keki kuashiria kuzindua  vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini  inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Afisa msaidizi wa ECSA Bi. Dorin Marandu.






Meneja wa  Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe na Kanda ya mashariki ya kati na kusini  inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA)  Bi. Rosemary Mwaisaka  akiongea wadau mbalimbali wa maswala ya lishe hawapo pichani wakati wa uzinduzi  wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Taasisi hiyo.




Katibu  Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akimlisha keki mmoja wa washiriki na mtoa huduma wa lishe ngazi ya jamii Bi. Evelyne Minja wa pili kushoto wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Alhamisi, 9 Novemba 2017

UFAFANUZI KUHUSU WANAOPASWA KURIPOTI WIZARA YA AFYA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

UFAFANUZI KUHUSU WANAOPASWA KURIPOTI WIZARA YA AFYA


WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO INAPENDA KUTOA UFAFANUZI KUHUSU WALE WANAOPASWA KURIPOTI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA AFYA DODOMA NI WALE WAOMBAJI 30 TU WALIOPANGIWA WIZARA YA AFYA.
WENGINE WALIOPANGWA KWENYE MIKOA NA HALMASHAURI WANAPASWA KURIPOTI KWENYE VITUO WALIVYOPANGIWA NDANI YA SIKU 14 KAMA ILIVYOTANGAZWA KWENYE TOVUTI YA OR TAMISEMI.


Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

09/11/2017.

Jumatano, 8 Novemba 2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TANGAZO LA KUITWA KAZINI.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilipokea kibali cha kuajiri watumishi 3,152 wa kada mbalimbali za Afya nchini. Kibali hiki kilikuwa  kwa ajili ya Wizara, Hospitali za Mikoa, Halmashauri  na Taasisi mbalimbali. Maombi yalipokelewa kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi 31/08/2017.

Waombaji  thelathini  (30) wamechaguliwa na kupangiwa ajira Wizara ya Afya kama jedwali linavyoonesha kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya, ili kuona majina ya waliochaguliwa ingia  www.moh.go.tz

Waombaji  2,058  waliochaguliwa katika Hospitali za Mikoa na Halmashauri wametangazwa kwenye Tovuti ya OR TAMISEMI. Waombaji wote wanajulishwa kutembelea Tovuti hiyo www.tamisemi.go.tz. Aidha, Sekretarieti ya Ajira inaendelea kushughulikia ajira kwa Taasisi nyingine.

 Waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia kwa ukamilifu maelekezo yafuatayo:-
i)             Kuripoti  Ofisi za Wizara ya Afya Dodoma katika  muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ajira Serikalini.  Ofisi za Wizara ya Afya zipo  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii, Jengo namba 11.
ii)           Ambao hawataripoti  ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa.
iii)          Wakati wa kuripoti kila aliyechaguliwa atapaswa kuwasilisha vyeti halisi (original Certificates) ambavyo nakala zake zilitumiwa wakati wa  kuombea ajira zao. Hii ni pamoja na Vyeti  halisi vya Elimu, vyeti vya Taaluma,  Leseni   kulingana na sifa za kada zao. 
iv)          Awe na Cheti halisi cha Kuzaliwa  (Original Birth Certificate) ambacho nakala yake aliambatisha kwenye maombi aliyowasilisha.
v)           Mwombaji anatakiwa kuwa  na picha mbili ndogo (passport size). Picha ziwe na muonekano kamili wa sura na ziwe zimepigwa si zaidi ya miezi mitatu.


Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

08/11/2017

Jumanne, 7 Novemba 2017

WIZARA YA AFYA YAWAAGA MADAKTARI 25 KUTOKA CHINA WALIODUMU NCHINI KWA MIAKA 2.

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Dorothy Gwajima akieleza jambo mbele ya jopo la Madaktari kutoka China na watumishi kutoka Idara kuu ya Afya (Hawapo katiaka picha) wakati wa kikao cha cha kuwaaga madaktari 25 kutoka China waliotumikia nchini Tanzania katika sekta hiyo.







Barozi wa PRC Mh. Ms Wang Ke akisisitiza jambo mbele ya jopo la madaktari kutoka China (Hawapo katiaka picha) wa kikao cha cha kuwaaga madaktari 25 kutoka China waliotumikia nchini Tanzania katika Sekta ya  Afya  kwa miaka 2, wakwanza  kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Mohamed na  wa mwisho ni kiongozi wa madaktari kutoka China Dkt. Zhu Jian.


Jopo la madaktari kutoka China wakifuatilia taarifa fupi kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Mohamed wakati wa kikao cha cha kuwaaga madaktari 25 kutoka China waliotumikia nchini Tanzania katika Sekta ya Afya  kwa miaka 2.






 Baadhi ya Watumishi wa Serikali Idara kuu ya Afya wakiwa katika kikao cha kuwaaga madaktari 25 kutoka China waliotumikia nchini Tanzania katika Sekta ya Afya  kwa miaka 2, kilichoongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Mohamed mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.




Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Mohamed, akimkabidhi  zawadi kiongozi wa madaktari kutoka China Dkt. Zhu Jian kama ishara ya shukurani kwa mchango waliouonesha katika Sekta ya Afya nchini Tanzania,  Upande  wa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Dorothy Gwajima.





Picha ya pamoja ikiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Mohamed, wakati wa kikao cha cha kuwaaga madaktari 25 kutoka China waliotumikia nchini Tanzania katika sekta ya Afya  kwa miaka 2, kikao icho kimefanyika mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.

Jumatatu, 6 Novemba 2017

AFYA YANGU MTAJI WANGU.



Kampeni ya mazoezi inaendelea, na kwa mwezi huu itafanyika 11/11, kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 4 asubuhi.
Afya yangu,Mtaji wangu.

Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Leo ametembelewa na ujumbe wa  pamoja wa umoja wa Mataifa wa Mpango wa Kinga ya Saratani ya shingo ya Kizazi Duniani. Waziri Ummy  ameushukuru..