Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 19 Novemba 2017

WATUMISHI WA AFYA BADO WANAHITAJIKA NCHINI.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya majaribio ya kuchunguza wadudu  kwa kutumia hadumini iliyopo kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wataalam wa chuo cha Afya na Tiba KAM kuhusu vifaa vinavyotumika maabara kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM  hawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM  dkt. Aloyce Musika akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM whawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

 Baadhi Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akipokea na zawadio kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM  dkt. Aloyce Musika kulia wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.


Na WAMJWW
WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM  yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya  imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.
“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba dkt. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.
“Wahitimu waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema Dkt. Musika
Mbali na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.
Naibu Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya fani mbalimbali katika  kada mbalimbali za sekta ya afya.



SIKU YA MATUMIZI YA CHOO DUNIANI, LEO NOVEMBA 19, 201


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAARIFA KWA UMMA
SIKU YA MATUMIZI YA CHOO DUNIANI, LEO NOVEMBA 19, 2017

Tanzania yetu na Vyoo Bora. Bado tunayo kazi kubwa ya kufanya:-
Kaya zenye vyoo bora ni 40% tu. Kaya zenye vifaa maalum (sabuni + maji) vya kunawa mikono ni 34% tu.
Kati ya shule za Msingi (16,088) zenye vyoo bora ni 28% tu. Choo bora kwa kila mtu, kila mahali inawezekana.  
Wilaya ya Njombe, zaidi ya asilimia 95% ya Kaya zina vyoo bora na sehemu maalum za kunawia mikono.
Tujenge na kutumia ChooBora.

Imetolewa na,

Ummy Mwalimu (MB),
Waziri wa Afya,
19 Nov. 2017
Dodoma.

Ijumaa, 17 Novemba 2017

SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI, NOVEMBA 17.

- Hakuna maoni


Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake (Njiti), ni pale ambapo mtoto huzaliwa kabla ya mimba kukamilisha wiki 37 za ujauzito. 

Kumbuka uonapo moja kati ya dalili za mtoto njiti kama zilivyotajwa katika kipeperushi hapo juu  mpeleke mjamzito au mtoto kwenye kituo cha huduma za Afya kwa uchunguzi na matibabu.
OKOA MAISHA.

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA WATOA HUDUMA ZA WATOTO NJITI NA WAMJW-DAR ES SALAAM

- Hakuna maoni
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea vifaa vya kufundishia kutoka kwa Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani  Dr Detlef Wachter katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani inayoazimishwa kila Novemba 17.

 Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani, ambapo shirika la GIZ kutoka Ujerumani lillikabidhi vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dtk. Wedson Sichalwe akiwasilisha taarifa fupi mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Viongozi  na waandishi wa habari(hawapo kwenye picha) katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani.

 Meneja mipango wa Shirika la Giz kutoka Ujerumani  Dkt. Susanne Grimm akielezea baadhi ya mafanikio na mipango ya Shirika hilo wakati wakitoa msaada wa vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.

 Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani  Dr Detlef Wachter akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi na waandishi wa habari wakati  wa utoaji msaada uliofanywa na shirika la Giz katika Taasisi ya Saratani Ocean road jijini Dar es salaam, mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya akimpa mkono wa shukurani  Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani  Dr Detlef Wachter baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya akifungua mkutano katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani, ambapo shirika la GIZ kutoka Ujerumani lillikabidhi vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.



 Na WAMJWW

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa vifaa vya kufundishia watoa huduma kwa watoto njiti vyenye thamani ya shilingi milioni 22. 19 kutoka shirika lisilo la kiserikali GIZ la Ujerumani ili kuweza kutoa huduma bora  katika kuwakuza watoto hao kwa uangalifu wa hali ya juu na kwenye mazingira mazuri.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya mtoto njiti duniani yaliyofanyika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema msaada wa vifaa hivyo utaboresha huduma kwa watoto njiti.
“Kutokana na msaada wa vifaa hivyo naamini rufaa zitapungua kwa kiasi kikubwa na kufanya huduma hizo kutolewa kwenye zahanati zitazopelekewa vifaa hivyo “ alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa watumishi wa afya ambao wamepata mafunzo wanatakiwa kuwaangalia wamama wanaotaka kujifungua ili kuweza kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto nchini.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa wamama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara pindi wanapopata ujauzito ili kuweza kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ili kuepuka kuzaa watoto njiti.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Wedson Sichalwe amesema kuwa anashukuru Shirika la GIZ kwa mafunzo pamoja na vifaa vya kutolea huduma kwa watoto njiti katika mkoa wake ili kutoa huduma bora kwa watoto hao.
“Tumepata msaada mkubwa sana kwa mkoa wetu kwani tulikua tunakabiliwa na changamoto za vifaa vya vya kuhudumia watoto njiti wanaozaliwa katika zahanati na hospitali mkoani kwetu” alisema Dkt. Sichalwe.

TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC

- Hakuna maoni


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC

Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC) kwa kauli moja wamepitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (Pooled Procurement Services (SPPS).

Uteuzi huo wa nchi ya Tanzania umepita bila kipingamizi mwishoni mwa wiki kwenye Mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC uliowakutanisha Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaohusika  na masuala ya UKIMWI uliofanyika mjini Polokwane, Limpopo – Afrika Kusini.

Hatua ya uteuzi wa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara umetokana na juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa MSD ambapo sasa inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa .

Aidha,umahiri na uzoefu wa Bohari ya Dawa (MSD) katika masuala ya ununuzi, utunzaji na usambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara (yaani mnyororo wa ugavi) unaeleweka na kuaminika vizuri hata na nchi nyingine zilizowahi kututembelea kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Kwa hatua hiyo MSD itakuwa na dhamana na majukumu yafuatayo:
·          Kununua Dawa na Vifaa Tiba kwa ajili ya nchi za SADC

·           Usimamizi wa taarifa na takwimu za Dawa na Vifaa Tiba vitakavyohitajika

·          Usimamizi wa kanzidata (Database) ya dawa za nchi wananchama wa SADC na usimamizi wa bei elekezi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara

·           Kusimamia manunuzi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Ukanda wa SADC na kusimamia mnyororo wa ugavi

·          Kutoa huduma za kitaalamu na kupanga bei elekezi na

·          Kutoa huduma za ushauri wa kitaalam katika masuala ya dawa na vifaa tiba.

Hatua hii itapunguza kwa kiasi kikubwa bei ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya nchi wananchama wa SADC. Jambo ambalo limeipatia heshima na sifa kubwa Tanzania, kwani imeaminiwa kufanya ununuzi wa dawa kwa niaba ya nchi nyingine kumi na tano (15) ambazo ni wanachama wa SADC.

Tanzania kupewa jukumu hilo ni jambo la kujivunia sana tena inaonyesha dhahiri tumetambulika tuko vizuri kwenye masuala mazima ya mnyororo wa ugavi kwa nchi wanachama wa SADC.

Faida zitakazopatikana kwa Tanzania kuwa Mwenyeji wa huduma hii ni kama zifuatazo:

·          Heshima kwa nchi yetu kwa kuaminiwa na nchi wanachama wa SADC baada ya kukidhi vigezo vya kitaalam

·          Viwanda vyetu vya ndani vitaweza kuuza dawa zao kwa nchi za SADC, kwani wajumbe wa mkutano tumekubaliana kuwa na kituo kimoja kitakachoshughulikia udhibiti ubora na ukaguzi

·           Bei ya dawa itapungua zaidi maana sasa tutaweza kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji sio kama nchi (Tanzania), lakini kama Ukanda unaoshughulikia nchi 15

·          Itaongeza ajira na kuijengea uwezo Bohari ya dawa(MSD)

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya

16/11/2017

Alhamisi, 16 Novemba 2017

TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC

Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC) kwa kauli moja wamepitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (SADC Pooled Procurement Services (SPPS).

Uteuzi huo wa nchi ya Tanzania umepita bila kipingamizi mwishoni mwa wiki kwenye Mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC uliowakutanisha Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaohusika  na masuala ya UKIMWI uliofanyika mjini Polokwane, Limpopo – Afrika Kusini. 

Hatua ya uteuzi wa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara umetokana na juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa MSD ambapo sasa inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa . 

Aidha,umahiri na uzoefu wa Bohari ya Dawa (MSD) katika masuala ya ununuzi, utunzaji na usambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara (yaani mnyororo wa ugavi) unaeleweka na kuaminika vizuri hata na nchi nyingine zilizowahi kututembelea kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Kwa hatua hiyo MSD itakuwa na dhamana na majukumu yafuatayo:
Kununua Dawa na Vifaa Tiba kwa ajili ya nchi za SADC

Usimamizi wa taarifa na takwimu za Dawa na Vifaa Tiba vitakavyohitajika

Usimamizi wa kanzidata (Database) ya dawa za nchi wananchama wa SADC na usimamizi wa bei elekezi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara

Kusimamia manunuzi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Ukanda wa SADC na kusimamia mnyororo wa ugavi

Kutoa huduma za kitaalamu na kupanga bei elekezi na

Kutoa huduma za ushauri wa kitaalam katika masuala ya dawa na vifaa tiba.

Hatua hii itapunguza kwa kiasi kikubwa bei ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya nchi wananchama wa SADC. Jambo ambalo limeipatia heshima na sifa kubwa Tanzania, kwani imeaminiwa kufanya ununuzi wa dawa kwa niaba ya nchi nyingine kumi na tano (15) ambazo ni wanachama wa SADC.

Tanzania kupewa jukumu hilo ni jambo la kujivunia sana tena inaonyesha dhahiri tumetambulika tuko vizuri kwenye masuala mazima ya mnyororo wa ugavi kwa nchi wanachama wa SADC.

Faida zitakazopatikana kwa Tanzania kuwa Mwenyeji wa huduma hii ni kama zifuatazo:

Heshima kwa nchi yetu kwa kuaminiwa na nchi wanachama wa SADC baada ya kukidhi vigezo vya kitaalam

Viwanda vyetu vya ndani vitaweza kuuza dawa zao kwa nchi za SADC, kwani wajumbe wa mkutano tumekubaliana kuwa na kituo kimoja kitakachoshughulikia udhibiti ubora na ukaguzi

Bei ya dawa itapungua zaidi maana sasa tutaweza kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji sio kama nchi (Tanzania), lakini kama Ukanda unaoshughulikia nchi 15

Itaongeza ajira na kuijengea uwezo Bohari ya dawa(MSD) 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya

16/11/2017

Jumatano, 15 Novemba 2017

SERIKALI YAPIGA HATUA KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE.


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi akisisitiza jambo wakati wa Semina ya uhamasishaji wa wahariri na wakuu wa Idara ya Afya juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ilofanyika mapema leo katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam, pembeni yake ni  Dkt. Janeth Mgamba.


Mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko Dkt. Janeth Mgamba akitoa taarifa fupi mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya katika semina ya uhamasishaji kuhusu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
 

Watumishi wa Idara ya Afya wakifuatilia kwa makini Semina ya uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi mapema leo katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Blog ya Full Shangwe wa Bahati Bukuku akitoa mchango katika Semina ya uhamasishaji juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya.
 

Meneja mpango wa kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira akiwasilisha mada mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya katika semina ya uhamasishaji wa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele.




Na WAMJWW
 
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto  imefanikiwa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa asilimia 90 kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa hayo hapa nchini NTD.
Hayo yamezungumzwa na Mganga Mkuu wa Serikali  Prof. Bakari Kambi wakati alipofungua semina ya uhamasishaji wa kupambana na magonjwa hayo kwa wahariri wa vyombo vya habari na Wakuu wa idara mbalimbali wa Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam.
“Tumepata mafanikio kwani mpaka kufikia Oktoba  2017  huu  tumefanikiwa kupunguza  ugonjwa wa matende na mabusha katika wilaya 95 sawa na asilimia 77 kati ya wilaya 120 na hivyo tumesitisha kutoa dawa katika wilaya hizo” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa katika mafanikio hayo pia Serikali imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Vikope (Trakoma) katika wilaya 58 sawa na asilimia 82 kati ya wilaya 71 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa kwa maeneo ya nyanda za juu hususan katika maeneo  ya Rungwe,Kyela,ileje na Busekeleo wamefanikiwa kupima wananchi na kuonyesha kuwa maambukizi yamepungua na hivyo kuendelea katika wilaya zilizobaki.
Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa  wa Mpango wa kupambana na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo mwingira amesema kuwa wanajamii wanatakiwa wajitokeze katika kupata dawa za kujikinga na magonjwa hayo  kwani muitikio ni mdogo na inaweza kusababisha madhara makubwa siku za usoni.
Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa Semina hiyo imelenga kuwaelimisha wahariri wa vyombo vya habari ili watoe kipaumbele katika kuhamasisha wananchi juu ya matumizi ya dawa za kukinga magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambayo ni Matende na Mabusha, Usubi,Minyoo na Trakoma ili kuweza kutokomeza kabisa ugonjwa huo hapa nchini.

Jumanne, 14 Novemba 2017

WATANZANIA WATAKIWA KUPATA VIPIMO VYA KITAALAM KABLA YA KUTUMIA DAWA.

- Hakuna maoni
 
Mratibu wa Taifa wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea katika Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) Dkt. Bachana Rubegwa (aliesimama) akieleza maudhui ya semina hiyo niliyofanyika mapema leo katika ofisi za FAO.

 Mwakilishi Mkuu wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea (FAO) Dkt. Raphael Sallu akiwasilisha mchango wake wakati wa seminar na Waandishi wa habari kuhusu matumizi bora ya antibiotic, ilofanyika katika ofisi za FAO jijini Dar es salaam.

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya ugonjwa Bi Rose Shija akiwasilisha mchango mbele ya wadau wa habari, pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Afya Catherine Sungura.

 Mmoja ya wadau wa Habari ambae pia ni mmiliki wa Blog ya Full Shangwe akitoa mchango mbele ya wadau wenzie wa habari na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa  katika Semina ya kuhamasisha matumizi bora ya antibiotic.


NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

WATANZANIA wanatakiwa kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kupata vipimo kutoka kwa wataalam kabla ya kutumia dawa kwa mazoea ili kuepuka usugu wa vimelea vya wagonjwa kwenye miili yao na kusababisha vifo vya mara kwa mara.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mradi wa kupambana na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) Dkt. Raphael Sallu wakati wa semina na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tatizo la kutumia vijiuasumu(Antibiotics) bila ya kupata vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya limekua kubwa ambalo linasababisha madhara ya kiuchumi na uhai kutokana na kuzidiwa na vimelea vya ugonjwa ambavyo vinakua sugu kutokana na  matumizi mabaya ya dawa hapa nchini” alisema Dkt. Sallu.

Aidha, Dkt. Sallu amesema kuwa elimu ya kutumia dawa bila ya kupata ushauri na vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya ianze kutolewa kuanzia ngazi za shule ya msingi na ngazi ya jamii kwa ujumla.

Mbali na hayo Dkt. Sallu amesisitiza kuwa wanahabari wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha umma umuhimu wa kutumia dawa kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam kuhusu ugonjwa unaomsumbua pamoja na matibabu yake.

Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa  Mradi wa kupambana na na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula (FAO) nchini Tanzania Dkt. Bachana Rubegwa amesema kuwa katika kupambana na tatizo hili kunapaswa kuwepo na matumizi ya hali ya juu ya chanjo ili kuweza kuepuka utumiaji hovyo wa dawa bila ya vipimo.

“Katika kupambana na utumiaji wa madawa bila ya utaratibu mzuri ambao hauhusishi vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ni lazima maabara ya kutambua magonjwa sugu ijengwe nchini kwetu” alisema Dkt. Bachana.

Hata hivyo Dkt. Bachana amesema kuwa wazilashaji wa chakula na mifugo wanatakiwa kutumia dawa zinazostahili na sio kutumia antibiotics katika mifugo yao pamoja na shughuli zao za kilimo ili kuepusha watanzania walio wengi kutumia vyakula hivyo vyenye usugu wa vimelea vya magonjwa.

Mbali na hayo Dkt. Bachana ametoa rai kwa watoa huduma za afya nchini kuacha kutoa dawa ambazo ni feki,zilizokwisha muda na kuwashauri wananchi kuepuka matumizi ya dawa yasiyo ya lazima ili kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa kwenye miili ya watanzania.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa Dkt. Rose Shija amesema kuwa watanzania wanatakiwa kutumia dawa sahihi na kwa wakati kadri alivyoelekezwa na mtaalam wa afya ili kuepuka matatizo hayo na kujijengea afya bora.

“Tubadili tabia katika kupunguza maambukizi kupitia chanjo,kuosha mikono kwa maji safi yanayotiririka,kuepuka ngono zembe na utunzaji salama wa chakula na sio kutumia dawa bila ya ushauri kutoka kwa wataalam wa afya ili kuepuka usugu wa vimelea vya magonjwa mwilini” amesema Dkt. Shija.

Jumatatu, 13 Novemba 2017

AFYA YANGU,MTAJI WANGU






 Wiki ya Kampeni ya kuzuia usugu wa vimelea dhidi ya Dawa za Antibiotiki.
 Fuata Ushauri wa mtaalam wa mifugo kabla ya kutumia antibiotiki.

WIZARA YA AFYA YAUOMBA UONGOZI WA TIBA ASILI KUTOKA CHINA KUISAIDIA KUJENGA KITUO CHA UENDESHAJI WA TIBA ASILI.



Na WAMJWW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto yauomba ugeni wa Viongozi wa masuala ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka China kuisaidia kujenga kituo cha uendeshaji wa Tiba Asili ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, utafiti wa kina na kuwa na eneo la kumbu kumbu la kutunza miti dawa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya mapema leo wakati apokea ugeni wa Viongozi wa masuala ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka China uliofika nchini tangu Novemba 12, huku ugeni huo ukitarajia kuwepo nchini mpaka Novemba 16.
Pia Dkt. Mpoki ameuomba ugeni huo kuwekeza zaidi katika uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha Dawa, sambamba na kuiruhusu Tanzania kuuza Dawa zake za Asili katika nchi ya China  jambo litalosaidia Tanzania kuwa na mashamba makubwa ya kuzalisha Dawa.
Nae Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohhamad Bakar Kambi ameahidi kushirikiana bega kwa bega na jopo la uongozi huo hususani katika kuboresha huduma za Afya nchini , huku akitia mkazo kuimarisha zaidi ushirikiano katika kufanya tafiti na kubadilishana ujuzi kupitia mafunzo.
Nae kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Peter Mhane amefurahishwa na ujio wa huo huku akiamini kwamba ushirikiano huu ni faida kwa nchi ya Tanzania kwani itasidia kuondokana na umasikini na kuondokana na upungufu wa Dawa.