Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 8 Desemba 2017

WATANZANIA WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI YA VYOO BORA

- Hakuna maoni

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo mbele ya wadau na wakazi wa Chang’ombe Mkoa wa Dodoma katika Uzinduzi wa kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba ni Choo iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chang’ombe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa usafi wa mazingira na vyoo bora kutoka halmashauri mbali mbali nchini Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakipiga makofi ishara ya kupongeza uzuri na usafi wa moja ya mfano wa choo bora.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wapili kutoka kushoto wakiwa mbele ya choo bora, tukio lililifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chang’ombe Mkoani Dodoma. Wakwanza ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu, watatu ni Elizabeth Arthur na wa mwisho ni Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wapili kutoka kushoto akiwapungia mkono wakazi wa Chang'ombe na wadau wa masuala ya mazingira na usafi wa vyoo. akwanza ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu, watatu ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Mahenge.

Timu ya viongozi wa serikali ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakiwa tayari kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

Mratibu wa Kampeni ya kitaifa ya Usafi na Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Anyitike Mwakitalima akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuelekeza jambo Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo wakiwa katika banda la maonesho la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mpango wa Simavi Thea Bongertman, wa kwanza ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.

Kikundi cha Burudani kutoka eneo la Chang’ombe Mkoani Dodoma, kikionesha manjonjo mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha akipokea zawadi ya Usafi bora ya gari kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile wakimkabidhi zawadi ya Usafi bora Mwakilishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi Eveline Kibenya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile na Elizabeth Arthur katika bango la kampeni ya “Usichukulie Poa Nyumba ni Choo”

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wa Wizara hiyo Mh. Faustine Ndugulile wakiwa pamoja na Washindi Usafi na vyoo bora kutoka Halmashauri mbali mbali nchini.

NA WAMJW-DODOMA.

WATANZANIA  wanapaswa kuzingatia mambo  ya msingi hususani matumizi ya vyoo bora  ili kuepuka magonjwa  ya kuambukiza na mlipuko kwa ajili ya kujenga Tanzania ya Viwanda pasipokuwa na adui mkubwa wa maradhi nchini.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya taifa ya mazingira uliyofanyika mkoani leo Mkoani Dodoma.

“Watanzania tunapaswa kuzingatia mambo ya msingi ikiwemo kutumia vyoo bora ,kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa mlipuko nchini” alisema Mhe. Samia.

Aidha Mhe. Samia amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuwa kipaumbele kwenye usafi wa mazingira kwa tumepoteza kiasi cha shilingi bilioni 440 kutokana na hali duni ya usafi wa hasa ukosefu wa huduma ya vyoo bora.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu  Hassan amesema kuwa takwimu zinaonyesha watu wapatao elfu thelathini huugua magonjwa ya kuhara kila mwaka na baadhi yao hupoteza maisha hivyo tunatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira  ili kuepuka idadi ya wastani wa watu 83 kwa siku.

“Taifa hatuna kuwekeza nguvu na rasilimali zetu katika suala la usafi wa mazingira ikiwemo matumizi ya maji safi na vyoo bora ili kufikia malengo yetu ya kitaifa pampja nay ale ya kidunia” alisema Mhe. Samia Suluhu.

Mbali na hayo  Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa endapo watoto wataendlea kuishi kwenye  mazingira machafu ni hatarishi kwani kuna uwezekano wa kuwa na watoto waliodumaa kimwili na kiakili.

Kwa upande wake Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Me. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania inaendelea kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ambao ulirejea tena mwaka 2015 baada ya kupotea takribani miaka minne.

“ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameonesha kusikitishwa kwake kutokana na uwepo wa kipindupindu nchini hivyo watanzania hatuna budi kuwa wasafi wa mazingira ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa huo” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewataka watanzania kupambana na adui wa afya kwa kutunza mazingira na kuepuka vishiria vya magonjwa mbalimbali  kuliko kulalamika ukosefu wa dawa kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Kwa upande Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa kupitia ofisi yake atahakikisha anasimamia na kuwaagiza watendaji wake  wa ngazi zote kusimamia  usafi wa mazingira kama alivyoagizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kampeni iliyozinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  jijini Dodoma ni ya awamu ya pili ya usafi wa mazingira ambayo imebeba ujumbe usemao “USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO” imeenda sambamba na ugawaji wa zawadi na vyeti kwa waliofanya vizuri kwenye usafi wa mazingira ambapo Halmashauri ya Mji wa Njombe umeibuka kidedea na kupata zawadi ya Trekta.

Jumatano, 6 Desemba 2017

WAZIRI UMMY ATAKA UTARATIBU WA UONGOZI KWENYE VITUO VYA AFYA UFATWE


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Mh. Vumilia Nyamonga akiongea na wananchi wake (hawapo kwenye picha) juu ya Usafi wa mazingira na matumizi ya choo, katika ziara ya Waziri wa Afya katika Wilaya hiyo mjini Dodoma, kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles akijibu hoja ya mwananchi wa Kijiji cha Humekwa mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) kuhusu upatikanaji wa kadi za matibabu ya wazee wilayani hapo.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Elizabeth Arthur wakati alipotembelea kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongea na mkazi wa Kijiji cha Humekwa Wilaya ya Chamwino Bi Cesilliah Isaya aliyefanikiwa kujenga choo chenye ubora kwa gharama ndogo ya shiringi 55,000 tu.

 Kikundi cha ngoma kutoka Kijiji cha Humekwa kikitoa Burudani mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Wakazi wa Kijiji cha Humekwa waliojumuika katika kuunga mkono ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) ili kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akifuatilia kwa ukaribu ratiba  katika kituo kidogo cha Afya Kijiji cha Humekwa wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikagua moja ya choo wakati alipofanya ziara katika Kijiji cha Humekwa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma ili kuhamasisha usafi wa mazingira na choo.

 Mwanakijiji wa Kijiji cha Humekwa Bi Evaline Gidore akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati alipofanya ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika kijiji hicho mapema leo.

 Diwani wa kata ya Aneti Mh. Peter Chidawali akitoa mapendekezo mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) kuhusu maboresho katika huduma za Afya kijijini hapo.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles wakati wa ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo, wa katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Mh. Vumilia Nyamonga.


Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongoza  ziara katika kijiji cha Humekwa Wilaya ya Chamwino mapema leo Mkoani Dodoma.






NA WAMJW-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kuhakikisha kuwa kila Kituo cha Afya au Zahanati yoyote inaongozwa na kusimamiwa na mganga na sio mhudumu wa afya au nesi kama inavyofanyika kwenye baadhi ya vituo vya afya .

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira  leo Mkoani Dodoma Wilaya ya Chamwino kata ya aneti Kijiji cha humekwa  kuelekea uzinduzi  wa awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iliyobeba ujumbe wa nipo tayari  ambapo Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi.

"Hatua ya kuimarisha  upatikanaji wa dawa, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba hususani vya dharura na upasuaji sanjari na kuweka mazingira safi ya upatikanaji wa maji na vyoo safi na salama ili kupunguza magonjwa na vifo vitokanavyo na kutokuwepo kwa huduma bora za  maji na afya kwa wakati ndiyo lengo letu" alisema Waziri Ummy.


 Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kabla ya Serikali ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli haijaingia madarakani bajeti ya dawa ya wilaya ya chamwino ilikuwa milioni 113 lakini mwaka jana bajeti ya dawa  ilikuwa milioni 436 ambapo katika mwaka wa pili wametengewa milioni 505 hali inayoonesha jitihada za dhati za serikali ya awamu ya tano kuboresha hali ya  afya ya wananchi hususani waliokuwa Vijijini.

Mbali na hayo Waziri Ummy amewataka wananchi wa kijiji cha Humekwa kukata kadi ya matibabu za CHF kwani zinarahisha upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi na kupunguza gharama .

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wananchi ambao wana ugonjwa kifua kikuu hawana  budi kuwahi hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kupata dawa ili kuokoa maisha yao kwani dawa hizo hazilipiwi gharama yoyote.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Aneti  Peter Chidawali ameiomba Serikali kuwasaidia Wananchi wa Humekwa katika hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa jengo la upasuaji ambalo wananchi wanajitolea michango yao kujenga ili likamilike kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Msomarisala wa Kijiji cha Homekwe Evaline Gidore amebainisha kuwa kampeni ya usafi wa mazingira na ujenzi  wa vyoo bora imeasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa walioathiriwa na magonjwa  yatokanayo na uchafuzi wa mazingira .

"Kampeni hii imechangia kuepuka magonjwa hatari kama vile kuhara damu, typhoid na minyoo kutoka wagonjwa138 mwezi  disemba 2015 hadi kufikia wagonjwa 26 Novemba Mwaka huu kwa vile tumejitahidi kuzingatia usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora"Alisema Bi Eveline.


Jumanne, 5 Desemba 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEWA NA BALOZI WA JAMHURI YA UJERUMANI

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Detlef Waechter kwenye ofisi yake ndogo Jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yamelenga kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya Afya



Waziri  Ummy Mwalimu (kushoto) akimuelezea jambo Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Detlef Waechter kwenye ofisi yake ndogo Jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akiagana na  Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Detlef Waechter kwenye ofisi yake ndogo Jijini Dar es Salaam mapema leo .



SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA HUDUMA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

- Hakuna maoni
 Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika Mjini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usafi wa Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Stephen Kiberiti akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Andrew Komba wa pili kutoka kushoto katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya.

 Wadau wa masuala ya Afya na Usafi wa mazingira wakifuatilia kwa ukaribu taarifa kutoka kwa mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika mapema leo Mjini Dodoma.

 Mkurugenzi wa Mipango WATERAN Tanzania Abel Dugango akisoma taarifa fupi kuhusu huduma za maji na usafi wa mazingira mbele ya Viongozi wa Wizara na Wadau wa Sekta ya Afya, shughuli inayoendelea Mjini Dodoma.

 Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi na Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Anyitike Mwakitalima akitoa taarifa fupi mbele ya wadau wa Afya katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika  Dodoma.

  Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Mkutano wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya kulia ni mmoja wa waratibu wa kampeni ya Usafi wa Mazingira.

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Bumi Mwamasage akipokea mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambae pia alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.

 Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akipokea vipeperushi vilivyoandaliwa kwaajili ya kutoa elimu kutoka kwa Salome Mtenga.

 Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akiwa na Wadau wa masuala ya Afya katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika  Dodoma.



NA WAMJW-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba ikiwemo zahanati, vituo vya afya na hospitali ikiwa ni katika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya  kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iitwayo NIPO TAYARI.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt. Andrew Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni katika kueleka awamu ya pili ya kampeni ya NIPO TAYARI itakayozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais,Mhe.  Samia Suluhu Hassan ifikapo Desemba 7 mjini Dodoma.

“Mwongozo huo utasimamia na kutekeleza shughuli zinazohusiana na mazingira na umelenga katika kutoa maelezo stahiki namna ambavyo vituo vya afya, ikiwemo ngazi za chini mpaka juu ili maelekezo hayo yaweze kutumika katika upangaji wa mipango na uandaaji wa bajeti zitakazotumika,” amesema Dkt. Komba.

Aidha,Dkt. Komba amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira pamoja kutumia vyoo bora ili kuweza kudumisha afya njema kwa maendeleo ya Tanzania.

Kwa upande wake  Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi ya Mazingira, Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kuwahamisha wananchi kuweza kutumia vyoo bora na mpaka kufikia Juni  2021 kaya zote nchini  ziwe zinatumia vyoo.

“Kutokana  na kulegalega  katika baadhi ya maeneo, waligundua kwamba kisababishi kimojawapo ilikuwa ni ukosefu wa mwongozo wa taifa ambao wadau na serikali ingeutumia kusimamia usafi wa mazingira kwahyo kampeni hii itahakikisha mpaka kufikia 2025 kaya zote zinatumia vyoo vilivyo bora” alisema Bw. Anyitike.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango kutoka Shirika la Water Aid, Abel Duganga amesema kutokana na kukosekana kwa mwongozo huo unaopima hali ya maji nchini utendaji wa serikali na wadau ulikuwa ukisuasua,  lakini sasa utawezesha kuwa na vigezo vinavyofanana katika kupima na kuwa na takwimu sahihi.

TANZANIA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KINGA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Leo ametembelewa na ujumbe wa  pamoja wa umoja wa Mataifa wa Mpango wa Kinga ya Saratani ya shingo ya Kizazi Duniani.

Waziri Ummy  ameushukuru ujumbe huko kwa kufika nchini na kwa kuichagua Tanzania kuwa Moja ya nchi sita duniani zitakazo nufaika na Mpango huu

Tanzania ni mojawapo wa nchi duniani zenye Tatizo ya saratani ya shingo ya kizazi.katika wanawake 100,000  kuna wanawake 54 wenye tatizo hilo na Vifo 32 katika wanawake 100,000 hiki ni kiwango kikubwa kwa nchi za afrika mashariki(Globocan,2014)

Katika hatua za  kujikinga na hali hii Wizara ya afya inafanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo Tanzania Youth Alliance (TAYOA),Medical Women Association of Tanzania, Wanawake na Maendeleo (WAMA) ,Tanzania Network for women living with HIV(TWN), Mbeya HIV network, T-Marc Tanzania na vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii katika kuhamasisha kuishirikisha Jamii katika suala hili.

Wizara inafanya kila jitihada kuhakikisha Mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na kansa anapata matibabu ya kibingwa maalum ya mionzi katika Hosipiali za Ocean Road na Bugando

Jumatatu, 4 Desemba 2017

MKUTANO WA 18 WA MWAKA WA MAPITIO YA UTEKEKELEZAJI NA UTENDAJI KATIKA SEKTA YA AFYA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya (kulia) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa  Muhammad Bakari kambi wakati wa Mkutano wa 18 wa mwaka wa mapitio ya utekelezaji na utendaji katika sekta ya afya nchini.

Watumishi wa Idara ya Sera na Mipango wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa mwaka wa mapitio ya utekelezaji na utendaji katika sekta ya afya nchini.


Baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa vitengo toka Idara za Wizara ya Afya na Tamisemi wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya mgeni rasmi(hayupo puchani), wakati wa Mkutano wa 18 wa mwaka wa mapitio ya utekelezaji na utendaji katika sekta ya afya nchini.


Na WAMJWW. Dsm

Watumishi na wadau wa sekta ya afya nchini wamekumbushwa kuboresha utendaji wao ili nchi kuwa ya uchumi ifakapo mwaka 2025
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa mwaka wa mapitio ya utendaji wa sekta ya afya.
"wakati Serikali ya awamu ya tano ikisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi ifikapo 2025 ni lazima kila mmoja wetu akubali kwamba Afya inabaki kuwa  muhimu, katika kufanikisha hili ni vyema kuweka mfumo wa utoaji huduma wenye Maendeleo kuendana na lengo la serikali kutilia mkazo wa uboreshaji wa Afya na kinga iliyosawia ili kila mmoja wetu aweze kushiriki katika shughuli za kijamii na kiuchumi" Alisema Dkt. Mpoki Ulisubisya

Mkutano huu  unawashirikisha watalaam Mbali Mbali,wadau wa Maendeleo, Sekta binafsi,Taasisi za utafiti na vyama vya kijamii.

kauli mbiu ya mkutano huo ni "kwa pamoja tunaweza,vifo vya Akina mama wajawazito havikubaliki"

Ijumaa, 1 Desemba 2017

UFAFANUZI KUHUSU USAMBAZAJI WA KONDOM KWA UMMA

- Hakuna maoni

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU USAMBAZAJI WA KONDOM KWA UMMA.
Kumekuwa na taarifa mbalimbali, hamaki na kejeli zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na taarifa iliyotolewa tarehe 27 Novemba 2017, Mnazi Mmoja kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Kondom kuhusu mpango wa Serikali kununua na kusambaza kondom 500,000,000 katika kipindi cha miaka mitatu 2018 hadi 2020.
Tunapenda kuukumbusha umma wa Watanzania kwamba maambukizi ya VVU na UKIMWI bado ni tatizo katika nchi yetu. Takriban watu 1,400,000 wanakadiriwa kuwa na VVU. Hivyo katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI Serikali inaendeleza afua mbalimbali ili kuzuia maambukizi mapya. Asilimia 40% ya maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa vijana wenye umiri wa miaka 15-24. Aidha makundi maalum kama vile wanaojidunga madawa ya kulevya, wanaofanya biashara ya ngono na wale wanaoamiiana wa jinsia moja wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi.  Makundi mengine ya walio katika hatari ni waendesha magari ya masafa marefu, wavuvi na wananchi wa kwenye migodi.
Wizara inatekeleza afua mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha na kupima uwepo wa VVU, na kisha kuanza tiba na matunzo, pamoja na kutoa dawa za kufubaza kwa watakao kuwa na maambuzi ya VVU. Kuna afua pia za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto, kutoa elimu ya VVU/UKIMWI na afya uzazi kwa vijana, elimu kuhusu VVU/UKIMWI kwa jamii na tohara kwa wanaume. Matumizi ya kondom ni moja wapo ya afua katika kuzuia maambukizi mapya. Hata hivyo utafiti wa viashiria vya Malaria na UKIMWI wa mwaka 2011/12 umebaini kuwa kuna matumizi duni ya kondom, kwani ni asilimia 27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja waliokiri kutumia kondom mara ya mwisho walipofanya ngono. Hivyo Serikali itaendelea kununua na kusambaza kondom kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU, magonjwa ya ngono na mimba zisizo tarajiwa ikiwa ni mojawapo ya afua hizo za kudhibiti maambukizi ya VVU.
Tunasisitiza kuwa Wizara na wadau wake inaendelea kutoa elimu ya kondom sambamba na elimu ya kusubiri kufanya ngono kwa wale ambao hawajaanza na wale ambao wameanza lakini wanapaswa kusubiri (Abstinence) na elimu ya kuwa waaminifu kwa mwenza mmoja aliye mwaminifu na anaejua hali yake ya maambukizi ya VVU (Be faithfull). .
Hivi sasa nchini kuna vyanzo vya upatikanaji wa kondom vya aina tatu. Kwanza ni kondom zinazopatikana kupitia sekta ya umma  ambazo husambazwa na Serikali kwa wananchi bila malipo. Pili, kuna kondom zinazosambazwa na wadau ambazo zinauzwa kwa bei ya chini kwa kuwa wadau wamechangia. Mfano kondom za Salama na Dume, na chanzo cha tatu ni kondom za kibiashara ambazo zinauzwa kwa bei ya kati na ya juu.
Kondom za sekta ya umma husambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na huduma za mkoba ngazi ya jamii, Kondom za wadau na zile za biashara husambazwa katika maduka ya dawa, maduka ya bidhaa mbambali, baa na nyumba za wageni.
Kwa mwaka 2016/17 Serikali iliboresha kondom zinazopatikana kupitia ya sekta ya umma kwa kuipa kifungashio kipya na jina la ZANA, ambapo kondom 36,916,911 zilisambazwa. Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018 hadi 2020 Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Dunia wa kudhibiti malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu inatarajia kununua kondom za kiume takribani 500,000,000. Kondom hizi zitasambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na katika maeneo hatarishi yanayoaminika kuwa na watumiaji wengi. Aidha, kwa vile imebainika kuwa watu ambao hawaumwi hawaendi vituo vya afya kwa  ajili  ya kuchukua kondom tu na hivyo kupelekea kutofikia walengwa, usambazaji na ugawaji huu utalenga maeneo ambayo
Kunamatukio ambayo yanaendana na ngono na yana walengwa wa afua za kondom. Maeneo haya ni kama baa, nyumba za kulala wageni, maeneo yenye mikusanyiko ya magari ya masafa marefu, maeneo ya uvuvi na migodini.
Aidha ikumbukwe kwamba nchi yetu ina sera sheria, mila, desturi na maadili yetu kama watanzania,  Hivyo kondom zote haziruhusiwi kusambazwa bila kufuata miongozo ya Wizara, ili kulinda zisifike kwa wasiolengwa.
Hivyo basi, iwapo tunataka kuzuia na kumaliza maambukizi ya VVU na UKIMWI ifikapo 2030 tunapaswa kama nchi kuwekeza katika kuzuia maambukizi mapya. Matumizi ya kondom, ununuzi wa vifaa tiba, vitendanishi, dawa za ARV na za magonjwa nyemelezi ni afua muhimu. Tunaomba wanahabari na wananchi waunge mkono juhudi hizi kwa kuwa tunahitaji watanzania wenye afya bora na uwezo wa kuzalisha ili kuijenga Tanzania ya Viwanda.

Imetolewa  na:
KATIBU MKUU  - AFYA
30 Novemba, 2017