Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 23 Januari 2018

SERIKALI YASAINI MKATABA WA UJENZI WA KITENGO CHA DHARURA NA MIFUPA.

- Hakuna maoni
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle kulia akisaini mkataba wa ujenzi wa kitengo cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya  Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Naibu Balozi wa Israel nchini Kenya Bw. Michael Baror.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle kulia akibadilishana mkataba wa ujenzi wa kitengo cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya  Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam na Naibu Balozi wa Israel nchini Kenya Bw. Michael Baror.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle akiongea na Waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa kitengo cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya  Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle kulia akimkabidhi zawadi  Naibu Balozi wa Israel nchini Kenya Bw. Michael Baror. Kushoto wakati wa wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa kitengo cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya  Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya.
 Na WAMJW-DAR ES SALAAM

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesaini mkatba wa makubaliano ya ujenzi wa jengo la huduma za dharura na mifupa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani Dodoma kutoka Serikali ya Israel .

Akizungumza baada ya makubliano  hayo eo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle amesema kuwa mkataba huo umefanywa na Serikali ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya ili kuboresha huduma za afya nchini. 

"Licha ya kusaini mkatba wa ujenzi wa vitengo hivyo vya huduma za dharura na Mifupa pia Serikali ya Israel imejitolea na kufundisha wataalam wetu katika vitengo hivyo pindi ujenzi utakavyokamilika" alisema Dkt. Gowelle.

Aidha Dkt. Gowelle amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Israel kwa kuingia mkataba wa ujenzi huo kwani utasaidia Hospitali hiyo kutoa huduma za dharura kwa ubora na kiwango cha juu kulingana na mahitaj ya wananchi.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa Israel nchini Kenya Bw.  Michael Baror amesema kuwa ujenzi huo utakamilika ndani ya  mwaka mmoja na miezi mitatu na kuanza kutoa huduma mara moja.
 

SERIKALI YAENDELEA KUJIZATITI KATIKA KUPAMBANA NA MAGOJWA YASIYO YAKUAMBUKIZA.

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akisikiliza kwa umakini changamoto kutoka kwa mgonjwa, pindi alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake a kukagua Ubora wa huduma za Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akisalimiana na mgonjwa pindi alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, wa kwanza ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Yahya Msuya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi katika Stoo ya Dawa pindi alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake a kukagua Ubora wa huduma za Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wa katikati) akiendelea na ziara yake ya kukagua Ubora wa huduma za Afya, pindi alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Idara ya Maendeleo ya Jamii Dkt. Julius Mbilinyi, Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo.



Na WAMJWW. MBEYA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kujizatiti katika kupambana na magonjwa yasiyo yakuambukiza ili kulilinda kundi kubwa la jamii ya Watanzania.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake Mkoani Mbeya ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kutathimini shughuli za maendeleo ikiwemo upanuzi wa miundombinu kama vile Vituo vya Afya na Shule.

Dkt. Ndugulile alisema kuwa magonjwa yakuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana kutokana na mabadiliko ya mtindo ya Maisha, kutofanya mazoezi na hali ya ulaji usiofaa wa wananchi wengi katika jamii.

“Serikali imezidi kuboresha upatikanaji wa Huduma za magonjwa ya Saratani, mfano kupitia Hospitali ya Ocean Road tulioipatia vifaa vya kisasa sana, sambamba na hilo tumeanza kufanya upandikizaji wa Figo ndani ya Hospitali ya Benjamini Mkapa,” Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kwamba, Serikali imewapeleka madaktari katika nchi za China na India ili kuanza kufanya mafunzo ya upandikizaji wa Ini, hali itakayosaidia kupunguza gharama kubwa kwa wananchi kwenda kutibiwa nje ya nchi. 

Aidha, Dkt. Ndugulile aliupongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Jijini Mbeya kwa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa jamii katika  Hospitali hiyo ikiwemo  upatikanaji wa Dawa ambayo ni zaidi ya Asilimia 90, kuwatambua Wazee na kuwapatia vitambulisha.

“Taarifa niliyoipata katika Mkoa wa Mbeya upatikanaji wa Dawa zote muhimu na za Wazee ni zaidi ya Asilimia 90, na katika Mkoa huu wa Mbeya wamepiga hatua kubwa sana kwa kuweza kuwatambua wazee wengi na kuwapa vitambulisho”, Alisema Dkt. Ndugulile

Alhamisi, 18 Januari 2018

SERIKALI YAJA NA MUONGOZO ILI KUPAMBANA NA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Muongozo wa Matibabu na Orodha ya dawa muhimu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi na kushoto ni Mwakilishi wa WHO.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akionyesha Muongozo wa Matibabu na orodha ya dawa zote muhimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo huo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kuhoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi ,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kinga na Ubora Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed na anayefuata ni mwakilishi wa WHO.



Pix 4,5 &6
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto mwenye kilemba akiwakabidhi baadhi ya wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Afya nchini Muongozo wa Matibabu na orodha ya dawa wakati wa uzinduzi wa Muongozo huo leo jijini Dar es salaam.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeandaa Muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa zote muhimu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya dawa. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu uliofanyika leo jijini Dar es salaam. 

"Ni muhimu kila kituo cha afya kuwa na dawa za kutosha, vifaa na vifaa tiba lakini ni lazima tuzingatie muongozo wa matibabu na orodha ya dawa kulingana na ugonjwa fulani ili kuepuka tatizo hili" alisema Waziri  Ummy 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Muongozo huo umezingatia vigezo vyote vya kuweka dawa ambazo zilikuwa hazipo katika ngazi ya  zahanati na  vituo vya afya ambazo zimepata uthibitisho kutoka Shirika la Afya la Dunia (WHO). 

Aidha Waziri Ummy amewapiga marufuku Bohari Kuu ya dawa ya Taifa MSD na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) kuagiza na kuandika dawa zilizo nje ya muongozo uliozinduliwa leo ili kuondoa matumizi ya dawa yasiyo sahihi. 

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kila kituo cha afya ni lazima kiongozwe na Tabibu na sio vinginevyo ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika kituo cha afya husika. 

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa itafika kipindi vituo vya afya ambavyo havikizi vigezo vitafungiwa ili kuepuka usababishwaji wa vifo visivyo vya lazima kwa watanzania. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa muongozo wa kutibu magonjwa mbambali 
umezingatia Orodha ya dawa ambazo zitakuwa zinatumika nchini kwetu kama dawa muhimu za kutibu magonjwa hayo. 

UZINDUZI WA MPANGO MKAKATI WA MIAKA 3 WA TAASISI YA TAALUMA YA AFYA YA JAMII AFRIKA KATIKA PICHA .

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa tatu kushoto akionesha kitabu cha mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika pamoja na Mwasisi wa Taasisi hiyo Dkt. Mary Sando wa kwanza kushoto wakati wa uzinduzi wa mpango huo leo jijini Dar es salaam.

Mwasisi wa Taasisi  ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika  Dkt. Mary Sando leo akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Dhima ya Taasisi  ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika (AAPH) ni kushirikiana na Seikali  na wadau wengine wa afya kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu afya ya mama na mtoto,masuala ya afya na lishe,magonjwa yasioambukizwa na yale yanayoambukiza.

WAZIRI UMMY ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA KUHAMISHA WAGONJWA MNH


Pix 1&2
Baadhi ya vitanda vilivyohamishwa wagonjwa katika wodi mbalimbali kwenye jingo la Mwaisela Hospitalini Muhimbili kwenda Hospitali ya Tiba na Taaluma Mloganzila kufuatia utekelezaji wa agizo la Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto la kuhamisha wagojwa katika jingo hilo hivi karibuni.



Pix 3 & 5
Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea baadhi ya wodi zilizohamishwa wagonjwa kwenye jingo la Mwaisela kufuatia agizo alilolitoa la kuhamisha wagonjwa kwenye jingo hilo kuhamia Mloganzila wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa muhimbili kuangalia utekelezaji wa agizo lake.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kulia akimjulia hali mtoto Maria (17) mkazi wa Mtwara aliyetangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ana uvimbe mkubwa wakati alipokwenda kumtembelea kwenye Taasisi ya Mifupa MOI jijini Dar es salaam.


NA WAMJW DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na utekelezaji wa agizo la kuhamisha wagonjwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda Hospitali ya Tiba na Taaluma Mloganzila.

Hayo ameyasema wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuangalia hali ya utoaji wa huduma pamoja na utekelezaji wa agizo hilo alilolitoa wakati alipotembelea Hospitali ya Tiba na taaluma Mloganzila mapema mwezi huu.

“Niliwaagiza MNH kuhamisha wagonjwa waliopo kwenye jingo la Mwaisela kuaznia wodi namaba 3,4,5,6,7 na 8 isipokuwa wagonjwa mahututi na wenye kesi maalumu ila nawapongeza wametekeleza agizo hilo mara moja” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewapongeza MNH kwa  kuwahamisha madaktari bingwa 15  15 na wauguzi zaidi ya 30 kwenda katika Hospitali ya Mloganzila ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma sawa na inayotolewa Muhimbili.

Mbali na hilo Waziri Ummy amesema kuwa zoezi hilo limetoa nafasi ya kuwahamisha baadhi ya wagonjwa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) hususani watoto angalau vitanda 50 kupeleka kwenye jingo la Mwaisela hospitali ya MNH.

“JKCI ni moja wapo ya Taasisi zinazotoa matibabu ya upasuaji hasa ya moyo na ina upungufu wa majengo  hivyo kutokana na uhamishwaji wa wagonjwa jengo la Mwaisela tunawapa nafasi ya kupeleka vitanda 50 kwa ajili ya wagonjwa wao waliofanyiwa upasuaji hususan watoto” aliongeza Waziri ummy.

Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata muda wa kwenda kumtembelea Mgonjwa alikuwa analalamika kwenye baadhi ya vyombo vya habari ajulikanaye kwa jina la Maria (17) mkazi wa Masasi Mkoani Lindi kuwa ana uvimbe mkubwa na akalizimika kuletwa katika Hospitali ya Taifa yMuhimbili.

“ Niliposikia habari ya Binti huyo kwenye baadhi ya vyombo vya habari niliomba namba za wahusika na kuwaelekeza waende Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hivi sasa anapata matibabu kwenye taasisi ya Mifupa (MOI) na wanaendelea na juhudi za kumtibia ili kumrudsha katika hali yake ya zamani” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy alitoa rai kwa Watanzania kuwa wanatakiwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa madaktari bingwa na kuacha imani potofu kwa kwenda kwa waganga wa kishirikina kwa kuamini mgonjwa atakuwa amerogwa ili kuepuka tatizo kuwa kubwa zaidi.

“Kwa mujibu wa madaktari wamesema kuwa Maria alihudhuria hospitali hapo mara mbili na hakurudi tena kama ilitakiwa afanye na badala yake akajikita zaidi kwenye tiba asili mpaka imesababisha tatizo kuwa kubwa zaidi hivyo watanzania tunatakiwa kuwaamini zaidi madaktari na kufuata maelekezo” alisema Waziri Ummy.


Jumanne, 16 Januari 2018

WAZIRI UMMY AWAAGIZA MSD KUWEKA NEMBO YA GoT KWENYE DAWA ZOTE ZINAZONUNU...

- Hakuna maoni

WAZIRI UMMY AWAAGIZA MSD KUWEKA NEMBO YA GoT KWENYE DAWA ZOTE ZINAZONUNULIWA NA SERIKALI

- Hakuna maoni



Pix 1&2
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na wagonjwa na kuuliza changamoto wanazokutana nazo hospitalini hapo wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala Amana ili kujua hali ya utolewaji huduma za afya leo jijini Dar es salaam.




Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwajulia hali wamama waliolazwa na watoto wao katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala Amana wakati wa ziara yake katika Hospitalini hapo ili kujua hali ya utolewaji huduma za afya leo jijini Dar es salaam





Pix 5 &6
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa  zilizopo katika stoo ya dawa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala Amana wakati wa ziara yake Hospitalini hapo ili kujua hali ya utolewaji huduma za afya leo jijini Dar es salaam.



Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua dawa kama ina nembo ya GoT (Government of Tanzania) inayopigwa chapa na Bohari Kuu ya Madawa ( ili kuepuka uchepushwaji wa dawa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala Amana ili kujua hali ya utolewaji huduma za afya leo jijini Dar es salaam.
PICHA NA WIZARA YA AFYA.


TANGAZO LA UFADHILI-MARUDIO

- Hakuna maoni
 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Tanzania Emblem RGB                             

         




TANGAZO LA UFADHILI-MARUDIO

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anawatangazia wanafunzi wote walioko vyuoni na wale wote waliopata udahili wa masomo ya Uzamili katika fani za Afya kwa mwaka wa masomo 2017/2018, kuwa muda wa kuwasilisha maombi umeongezwa hadi tarehe 19/01/2018. Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada pamoja na posho ya utafiti pindi mwanafunzi anapokuwa kwenye kipindi cha kufanya utafiti kama sehemu ya mafunzo yake. Kwa wanafunzi waliokwisha wasilisha maombi yao, hawatakiwi kuomba upya.

Vigezo vilivyowekwa ni kama ilivyoainishwa kwenye Tangazo la awali ambavyo ni :

1.    Raia wa Tanzania.
2.    Awe amedahiliwa chuoni kuanza masomo kwa mwaka wa kwanza 2017/2018
3.    Watumishi wa Afya wanaofanya kazi katika vituo vilivyo wilayani/mikoani ambao baada ya mafunzo, aidha wanaweza kupangiwa vituo vya kazi (hospitali za mikoa) au kurudi na kuendelea kufanya kazi katika vituo vyao vya awali ambao utaalamu wao utakuwa unahitajika na awe ameruhusiwa na mwajiri wake kwenda masomoni.
4.    Nyanja za Tiba ambazo ni za msingi katika utoaji wa huduma za rufaa katika hospitali za Rufaa za mikoa kama Anaesthisiology, Surgery, Neurosurgery, Obstetric and Gynaecology, Orthopaedic Surgery, Emergency Medicine, Paediatric, Internal Medicine, Critical Care in Nursing na Midwifery and Womens Health
5.    Nyanja za ubingwa (Specialities na Super-specialities) katika hospitali za kitaifa (magonjwa ya moyo, figo, saratani n.k.) ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi.
6.    Awe na barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake (ambatanisha)
7.    Awe tayari kuingia mkataba wa kuitumikia Serikali kwa muda usiopungua miaka 5 baada ya kuhitimu mafunzo.
8.    Mtumishi asiwe na ufadhili mwingine.

Aidha, kwa kuwa wanafunzi wamesharipoti vyuoni, barua za maombi zipitishwe kwa Wakuu wa Vyuo kuthibitisha kuwa mwanafunzi yuko chuoni, na kwa wale ambao bado wapitishe barua kwa Mwajiri wao. Tangazo hili linahusu watumishi wa mwaka wa kwanza wa masomo 2017/2018 tu. Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe  19/01/2018. Waombaji wote watume maombi hayo kwa anuani ifuatayo ;


Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Chuo Kikuu Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii
Jengo Namba 11,
S.L.P 743
40478, DODOMA


Imetolewa na;

Katibu Mkuu - Afya

16/01/2018


Jumatatu, 15 Januari 2018

SERIKALI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA NYOTA KATIKA KUVIPIMA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI NCHINI

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye tisheti ya mistari) akipokea maelekezo ya ramani ya jingo jipya la Mama na Mtoto katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuatia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu na wa mwisho ni Mhandisi Mwakyembe.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua jokofu la Chanjo wakati alipotembelea katika Kituo cha Afya cha Nkomolo kilichopo Nkasi Mkoani Rukwa wakati wa Ziara yake ya kukagua Huduma za Afya Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa zilizoingia na zilizobaki katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Idadi ya watu waliohudhuria Kituoni hapo kupitia mfumo wa Kompyuta katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Majengo Mhandisi Mwakyembe kutoka Ofisi ya Mkoa wa Rukwa.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na ziara yake katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuata ni Mhandisi Mwakyembe na Mbunge wa Nkasi kaskazini Mh.Kessy Ally.


Na WAMJWW. RUKWA-NKASI
Serikali yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
 
“Tumeanza utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt. Ndugulile.
 
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika vituo vyote vya Afya nchini.

“Dawa zote za msingi tunazo zakutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa kutibiwa kisha aambiwe akanunue katika vituo binafsi, Hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri katika kituo hiki na ni asilimia 85 ” aliendelea Dkt. Ndugulile.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy aliupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimia vizuri ujenzi wa kituo hicho, uliojumuisha Thieta, Wodi ya mama na mtoto mochwari na maabara mpaka hatua ya kupaua kwa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 290 kwa kutumia nguvu kubwa ya wananchi (fixed akaunti). 

Akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu amesema kuwa Mkoa wa Rukwa umeendelea kuboresha huduma za Afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini kama juhudi za kupunguza tatizo la vifo vya wanawake na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi.

Dkt. Boniface aliendelea kusema kwamba, Zaidi ya vituo 214 kati ya 223 vilivyopo, vinatoa huduma muhimu za mzazi na mtoto jambo linalosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga licha ya upungufu mkubwa wa vituo hivyo.

Kwa upande mwingine Dkt. Boniface Kasululu alisema kwamba Mkoa unaendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo, Hadi kufikia Mwezi Novembe 2017 jumla ya Watoto 48,494 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja walipewa chanjo, kati ya watoto 50,245 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 jambo lililoufanya mkoa kuvuka lengo la kitaifa la asilimia 90.