Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 30 Januari 2018

SERIKALI YA TANZANIA YATIA SAINI MKATABA NA MFUKO WA FEDHA WA PAMOJA WA SHILINGI TILIONI 1.1 KWAAJILI YA KUPAMBANA NA UKIMWI, MALARIA NA KIFUA KIKUU.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kupokea msaada kutoka mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) kilichofanyika jana katika Ofisi za Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.

Meza kuu, Ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (wapili) wakati wa kikao cha kupokea msaada kutoka mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund), kushoto kwake ni Mwakilishi kutoka Global Fund Tatjana Peterson, kulia kwake ni Pro. Faustine Kamuzora, wa mwisho ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. 

Picha ya pamoja ikionesha zoezi la kutia saini baina ya Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Fedha wa pamoja (Global funds).

Picha ya Pamoja ya Makabidhiano ya Mkataba yaliyo sainiwa na Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Fedha wa pamoja (Global funds).




Kikao cha Makubaliano ya kusaini Shilingi Tilioni 1.1 kati ya Serikali na Mfuko wa fedha wa pamoja kilichofanyika jana katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.

 
Na WAMJWW. DSM
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jnsia, Wazee na Watoto imetia saini Shilingi Tilioni 1.1 na mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) kwa ajili ya kupambana na magonjwa ya UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU.
Hayo yamebainishwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa kikao cha Makubaliano ya kusaini fedha hizo kilichofanyika jana katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, napenda kuwashukuru sana Global funds, kwa kuendelea kushirikiana nasi katika kutatua changamoto za rasilimali fedha katika kupambana na UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba utekelezwaji wa makubaliano ya shughuri hii utasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu huku miradi ikitekelezwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Raisi TAMISEMI pia Mashirikayasiyo yakiserikali na Sekta Binafsi.
Pia Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha fedha hizo zilizotolewa na Mfuko wa Fedha wa pamoja kutumika kikamilifu ili kuweza kupata matokeo yaliyotarajiwa ya Asilimia 90 ya wananchi kupima UKIMWI ili kujua hali zao, Asilimia 90 ya Watanzania walio na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waweze kutumia dawa ya kufubaza Virusi hivyo (ARV) na Asilimia 90 ya wanaotumia dawa za ARV, Virusi viwe vimefubazwa (90,90,90).
Mbali na Hayo Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Asilimia 40 ya Watanzania wameweza kufika katika vituo na kupata tiba, huku lengo ni kuhakikisha kwamba itakapofika mwaka 2020, asilimia 70 ya wenye maambukizi ya Kifua kikuu wawe wanajulikana na kuanza kupata huduma za matibabu mara moja.
Kwa upande wa Malaria fedha hizo zitatumika katika kupunguza maambukizi ya Malaria ili kufikia Asilimia 1 ifikapo mwaka 2020.
Akiwawakilisha Makatibu Wakuu wenzake Prof Faustine Kamuzora ameahidi kusimia matumizi sahihi ya fedha zote walizopokea kutoka kwa Mfuko huo katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa maadili ili kufikia malengo waliyojipangia.
“Tutahakikisha kwamba fedha zote zilizopatikana zinatumika vizuri na kuhakikisha kwamba matokeo makubwa yanapatikana, Afya za Watanzania zinahimarika kwa kufanya usimamizi mzuri.” Alisema Prof Kamuzora.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Global Fund Tatjana Peterson ameahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kupambana na magonjwa ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu.
Nae msindika Makohozi Bw. Paskali Mbagala ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusogeza huduma ya kupima na kutibu magonjwa ya Kifua Kikuu kwa wananchi hususani wa vijijini, jambo lililosaidia kupunguza vifo vya watu wengi.
Akiwasilisha Taarifa ya Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Mwenyekiti wake Bw. Justine Bunyoka ameiomba Serikali kuendeleza ushirikiano wa karibu na Mfuko huo ili kurahisisha kufikisha Huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

TAARIFA KWA UMMA.

- Hakuna maoni

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA AFYA NCHINI KATIKA KUBORESHA SEKTA HIYO.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

Watumishi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye Picha) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.

Afisa Uuguzi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Jane Mazigo akitoa maelezo mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.

Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa akipokea Cheti kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uuguzi na Wakunga, Kulia ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Lena Mfalila
Mwenyekiti aliyeingia kuliongoza Baraza la Uuguzi na Ukunga Abner Mathube akiahidi kuchapa kazi mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Baraza la Uuguzi na Ukunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.


Na WAMJWW.DSM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuendelea kutatua changamoto za zinazowakabili watumishi wa Kada ya Afya nchini ikiwemo kuboresha miundombinu inayowazunguka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akizindua Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
“Asilimia 80% ya Kazi zote za kutoa huduma za Afya, zinafanywa na Wauguzi na Wakunga, kwaiyo wakati tunazungumzia kuboresha huduma za, Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuzifanyika kazi changamoto hizo ikiwemo suala la watumishi” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba, sambamba na changamoto Wauguzi na Wakunga wanazoendelea kukumbana nazo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa kutatua changamoto hizo katika kuboresha Huduma za Afya.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy alimwagiza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Bw. Abner Mathube Kusimamia mabadiliko ya kanuni za maadili ya Baraza hilo ambazo zimeonekana kupitwa na wakati, hivyo kutofanya kazi kwa ufanisi unaostahili na kushindwa kuendana na wakati huu.
“Nimeelekeza zile kanuni za maadili za mwaka 2007 ni lazima zifanyiwe marekebisho, kwani  zimepitwa na wakati, ili tuweze kusimamia taaluma hii vizuri ya Uuguzi na Ukunga.” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Pia Mh. Ummy Mwalimu amelitaka Baraza hilo kujizatiti katika kutoa taarifa za Baraza mbele ya umma katika kueleza shughuli za kila mara za Baraza hilo, jambo litakalosaidia kuwafahamisha wananchi juu ya majukumu ya baraza hilo.
“Jamii haipati taarifa kuhusu utendaji kazi wa Baraza, tunatakiwa kuliona Baraza linakuja mbele, angalau kila robo mwaka katika kila kipindi, kukaa kimya kunafanya wananchi waone Baraza halina meno wala maamuzi” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy amelitaka Baraza hilo kuwachukulia hatua Waauguzi na Wakunga wanaenda kinyume na maadili ya kazi yao, huku akikemea matumizi ya lugha chafu yanayofanywa na baadhi ya wauguzi wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanaitia doa kada hiyo.
Aidha, Mh. Ummy amemshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuliongoza Baraza hilo ikiwemo kusimamia wauguzi na wakunga nchini, kusimamia vyuo na vituo vya kutolea huduma za Afya na kuweza kukamilisha jengo la kuwaendeleza Wauguzi na Wakunga, huku akiwataka waamishe kazi zote za Baraza hilo katika jengo hilo lililopo Kibaha.
Mwisho Waziri Ummy aliahidi kuvifungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havitakidhi vigezo vya kutoa huduma kwa jamii, huku akiwataka Wakurugenzi kujenga tabia ya kuvitembelea vituo hivyo ili kujionea mahitaji ya Vituo hivyo.
“Tutafungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havikidhi vigezo, kwa hili hatutooneana aibu, wala kujali hiki ni kituo cha Afya cha serikali au chabinafsi, wakishindwa kutoa Huduma Bora hatutasita kuvifungia” alimaliza Mh. Ummy Mwalimu.

Jumapili, 28 Januari 2018

SERIKALI YAMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUMALIZIA MAJENGO YA CHUO.





Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara  na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo.

 Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi Mtwara  NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.

Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya jengo la  Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.

 Baadhi ya Majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara na  CoTc yakiwa yamekamilika katika mradi wa ujenzi wa Ujenzi,Upanuzi na ukarabati wa majengo ya chuo hiko na Chuo Cha maafisa Tabibu mtwara yalipokaguliwa na wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya leo mkoani Humo.


Jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa  Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.




NA WAMJW-MTWARA

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi  katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC)  na Chuo cha Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara. 

"Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja" alisema Bw. Simba. 

Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha  Sumbawanga. 

Kwa upande wake Mratibu wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Afya  Dkt. Joachim Catherine amesema kuwa  mradi huo  uliofadhiliwa na Global Fund umehusisha ujenzi Wa mabweni matatu yenye vyumba 120, Nyumba za watumishi nane katika chuo cha maafisa tabibu. Katika na Chuo cha uuguzi Mtwara. 

Aidha Dkt. Catherine amesema kuwa Miradi yote imegharimu kiasi cha Shilingi  bilioni 3.3 za kitanzania na kulifanyika ukarabati na upanuzi Wa madarasa, ofisi za wakufunzi, maktaba pamoja na maabara za vitendo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi Mtwara (NTC) Bw.  Frolian Mbungu amesema kuwa amefurahishwa na ukaguzi huo kwani utamfanya apokee majengo kwa kujiamini na kuyatumia kwa ufasaha. 

Aidha wakaguzi hao kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Dkt. Edward Mbanga walitembelea jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa  Hospitali hiyo ni kuweza kutoa huduma za kibingwa.



Jumamosi, 27 Januari 2018

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo.

Waziri ummy Mwalimu akiangalia ramani ya kituo hicho cha afya ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa Viongozi wa Shirika hilo.

Waziri Ummy Mwalimu akiangalia duka la dawa lililopo kwenye hospitali ya Mkoa ya Sekoture ambapo upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa Mwanza ni asilimia 80.

Jengo la Maabara lililojengwa kwenye kituo hicho cha afya katika mpango wa Serikali wa kuboresha huduma za dharura za uzazi kwenye vituo vya afya nchini.(Picha zote na Wizara ya Afya)

Waziri Ummy Mwalimu akiangalia Ramani ya Ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Uzazi linalojengwa hospitali ya Mkoa ya Sekoture jijini Mwanza. 

Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua huduma za afya kwenye kituo cha afya cha kamanga kilichopo Wilaya ya Sengerema.Waziri ummy yupo Mkoani Mwanza katika ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utoaji huduma za afya mkoani hapo.

Waziri Ummy Mwalimu na Naibu Waziri Dkt.Angela Mabula wakikagua ujenzi wa jengo la dharura la uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Igombe Wialayani Ilemela,akiyevaa koti la bluu ni Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Florian Tinuga.

Mawaziri hao wakijadili jambo wakati wa ukaguzi wa jengo la upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni linalojengwa kwenye kituo cha afya cha Karume ,Wilayani Ilemela.


Na.WAMJW,Mwanza
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kusimamia Fedha za kuboresha huduma za dharura zinazotolewa na Serikali zitumike ipasavyo na si kwa matumizi mengine.
 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu jijini hapa wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya pamoja na ujenzi wa huduma za dharura za Uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Igombe Wilayani Ilemela.
 
Waziri Ummy alimpongeza Mkurugenzi wa Ilemela kwa matumizi mazuri ya fedha hizo ambapo alijionea kazi nzuri inayoendelea katika kituo hicho ambapo wametumia wajenzi wa kawaida na ujenzi huo unaenda vizuri na kwa kiwango kinachoridhisha.
 
Aidha,alisema Fedha za kuboresha miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura zitumike kama haya angalau kujengwe chumba cha upasuaji,maabara ya damu na tunamataka wodi ya wazazi na nyumba moja ya mtumishi kuliko kujenga masuala mengine
 
“kama fedha zitabaki unaweza kufikiri kujenga vitu vingine,kuliko kqenda kutumika kwa masuala mengine kama baadhi ya sehemu nyingine wanavyofanya, kama fedha zimebaki nipo tayari kukuruhusu kujenga kitu kingine Mkurugenzi,hongera sana Mkurugenzi na viongozi wengine”.
 
Hata hivyo alisema Tanzania ni moja ya nchi yenye vifo vingi vya akina mama wajawazito na watoto”leo hii toka saa sita usiku tuanze siku hadi saa sita usiku wanawake 30 wa kitanzania wanafariki kwa sababu tu ya kutimiza wajibu wao wa kuleta kiumbe duniani”
 
“Kwahiyo Mhe.Rais alichokifanya  kwa kushirikiana na wadau tunaboresha huduma za uzazi zikiwepo za upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni,hivyo tumefurahi kuona hapa zile shilingi milioni mia tano zimetumika ipasavyo,binafsi nimedhirika  na kazi iliyofanywa hapa karume hivyo naahidi kuleta fedha kwa ajili ya   kuboresha miundombinu ya kituo cha afya Buzurugwa”alisema Mh. Ummy.
Wakati huo huo nae naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemele Dkt.Angela Mabula alisema wao kama viongozi watahakikisha fedha zote zitakazoenda kwa ajili ya afya itatumika ipasavyo na wataisimamia ili kuweza kuboresha miundombinu ya sekta ya afya
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amewataka wananchi wa    Igombe kuendeleza mshikamano wanaouonyesha ili kuendelea kufanya makubwa zaaidi kwa kujiletea maendeleo”mchakato wa maendeleo chini ya Jemedari wetu rais Magufunli ndo kwanza umeanza”.

SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 ILI KUIMARAISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika kupata huduma katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti cha mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface.


Na WAMJWW.DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi,
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi hiyo.

 “Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua vifaa vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura jambo litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine  Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo  katika kuhakikisha wanaiwezesha zaidi ili kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo litakalopunguza usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini. 

Aidha, Dkt. Ndugulile aliupongeza uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za Afya kwa wananchi hali iliyosaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu ya mifupa.
“Niupongeze uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika magonjwa yanayohusiana na mifupa jambo lililosaidia kupunguza wagonjwa wengi sana kupata huduma nje ya nchi” alisema Dkt. Ndugulile.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani Zaidi ya Asilimia 95 ya maradhi ya mifupa hutibiwa katika Hospitali hiyo na asilimia zilizobaki huwapeleka nje ya nchi.

Dkt. Respicious Boniface aliendelea kuishukuru Serikali kwa Msaada huo wa Fedha kwaajili ya kununua  Vifaa vya MRI na CT-Scan na kuahidi vifaa hivyo vitafika mapema ndani ya mwezi wa Nne, hivyo kazi ya kuwaudumia wananchi itaanza mapema.

“Sababu kubwa ilikuwa ni vifaa, sasa tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imekwisha toa fedha kwaajili ya vifaa hivyo hivyo ndani ya mwezi wa nne vitakuwa vimekwishafika”, alisema Dkt. Dkt. Respicious Boniface.

Ijumaa, 26 Januari 2018

MH. UMMY MWALIMU AZINDUA MASHINE YA CT-SCAN KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ZIWA BUGANDO YENYE GHARAMA YA SHILINGI BILIONI 1.6

- Hakuna maoni
Waziri Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa  CT-Scan kwenye hospitali ya Bugando,kulia ni Baba Askofu wa Kanisa katoriki jimbo la Geita Flavian Kasala na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.

Waziri Ummy mwalimu akiongea na watumishinwa hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa ya bugando wakati wa uzinduzi wa mashine ya CT-scan.

 Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya bugando dkt.Abel Makubi akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa mashine hiyo.

Mtaalamu wa Mionzi wa hospitali ya Bugando akimpatia maelezo Waziri wa Afya mara baada ya ufunguzi wa mashine hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akiwajulia hali wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu.

Waziri Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa Hospitali hiyo kwenye kitengo cha Saratani hospitalini hapo.

Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mzee Juma Salumu kutoka tabora aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya masikio.Waziri amewahakikishia serikali ipo mbioni kuboresha huduma za kibingwa katika hospitali ya mkoa ya Tabora ili kupunguza gharama kwa wananchi.

Mashine ya CT-scan iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6


Na WAMJWW.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB)  ameahidi kuwaletea mashine ya uchunguzi ya MRI katika hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa Bugando mwaka huu
ameyasema hayo leo wakati akifungua mashine ya  CT-scan ambayo itakua inapima magonjwa mbalimbali iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambazo zinetokana na vyanzo mbalimbali vya mapato vya hospitali hiyo.

Aidha,Waziri Ummy ameahidi ndani ya miaka mitatu kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kupunguza gharama kwa wananchi wa kanda ya ziwa na magharibi wanaopata matatizo ya moyo kwenda kupata vipimo na matibabu kwenye taasisi ya moyo ya  JKCI ya jijini Dar es Salaam.

TAMKO KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKOMA DUNIANI TAREHE 28/01/2018

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari (Hawapo kwenye pich) pindi akitoa taarifa ya siku ya Ukoma Duniani, tukio lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile(Hayupo kwenye picha) katika siku ya Ukoma Duniani, tukio lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.


TAMKO LILILOSOMWA NA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. FAUSTINE NDUGULILE  (MB) KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA UKOMA DUNIANI TAREHE 28/01/2018

Ndugu wanahabari,
Siku ya Ukoma Duniani huadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari. Kwa mwaka huu, siku hii itaadhimishwa tarehe 28 Januari, 2018. Mwaka huu imetimia  miaka 64 tangu siku hii ilipoasisiwa mnamo mwaka 1954 na mwandishi wa habari mfaransa Raoul Follereau kama njia ya kuelimisha na kuongeza uelewa duniani kuhusu ugonjwa huu wa kale ambao una kinga, unatibika  na mgonjwa kupona kabisa. 

Ndugu wanahabari,
Katika siku hii, Tanzania inaungana na mataifa mengine ulimwenguni kufanya maadhimisho hayo ili kuukumbusha umma na kuuelimisha juu ya uwepo wa ugonjwa huu hatari, athari mbaya za vidonda na ulemavu vinavyotokana na ukoma. Ni dhahiri kuwa ugonjwa wa ukoma umekuwa ukiogopwa sana na kusababisha unyanyapaa mkubwa katika jamii zetu hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kudumu  na kwa kiasi kikubwa waathirika hujikuta wakitengwa na kubaguliwa.

Pamoja na kwamba nchi yetu ilifikia viwango vya utokomezaji wa Ukoma kitaifa mnamo mwaka 2006 kwa kiwango cha chini ya mgonjwa 1 kati ya watu 10,000, Ukoma bado unaendelea kuwa tatizo la kiafya miongoni mwa jamii nchini kwetu. Kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma za mwaka 2016, jumla ya wagonjwa  wapya 2,047 waligunduliwa na hivyo kufanya kiwango cha ugunduzi kuwa watu 4 kwa kila watu 100,000. Takwimu hizi zinaifanya Tanzania kuendelea kuwa miongoni mwa nchi  22 zenye wagonjwa wengi wa ukoma duniani.




Takribani mikoa yote nchini mwetu inagundua na kutibu wagonjwa wa ukoma japo kwa viwango tofauti. Hivi sasa bado kuna mikoa kumi ambayo inagundua wagonjwa wapya kila mwaka. Mikoa hiyo ni pamoja na: Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro, Pwani; Tanga, Geita, Dodoma, Tabora and Kigoma. 
Aidha, bado zipo wilaya 20 ambazo kiwango cha ukubwa wa tatizo la ukoma kipo juu sana na bado hazijafikia lengo la utokomezaji, nazo ni Liwale, Nkasi, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga manispaa, Kilombero, Mafia, Pangani, Mvomero, Masasi mjini, Lindi vijijini, Kilwa, Mpanda, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Mkinga, Ulanga, Morogoro vijijini na Chato. 

Ndugu wanahabari,
Takwimu za miaka kumi iliyopita, tangu 2007 hadi 2016, zinaonyesha hapa nchini mwetu watoto wapatao 1,456 waligunduliwa na kutibiwa ukoma. Ugonjwa wa Ukoma miongoni mwa watoto ni dalili ya kuwa bado kuna maambikizi mapya katika baadhi ya maeneo nchini mwetu.  Miongoni mwa hawa, watoto 73  waligunduliwa wakiwa tayari wamepata ulemavu wa kudumu; yaani wakiwa tayari wamekatika baadhi ya viungo vyao na wengine kuhitaji kutumia viungo bandia na kiasi kikubwa kuwa tegemezi maisha yao yote. 

Ndugu wanahabari,
Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu inasema “TOKOMEZA ULEMAVU MIONGONI MWA VIJANA WETU”.  ‘ZERO DISABILITIES IN GIRLS AND BOYS” Kila mmoja wetu anahitajika kushiriki kikamilifu kupambana na ukoma, hususani katika halmashauri ambazo zina wagonjwa wengi na hazijafikia viwango vya utokomezaji. Juhudi zetu tuzielekeze katika kuwagundua wagonjwa mapema wakiwa bado wapo katika hatua za awali za ugonjwa, ili kuzuia maabukizi katika jamii hususan miongoni mwa watoto na vijana wetu kabla ugonjwa haujawa mkubwa na kusababisha ulemavu. 





Ndugu wanahabari,
Dalili ya awali kabisa za ugonjwa wa Ukoma ni baka au mabaka kwenye ngozi yasiyo na hisia na yenye rangi ya shaba. Kwa kawaida hayawashi wala hayaumi. Mabaka haya hukosa hisia ya joto, mguso au maumivu. Dalili nyingine za ukoma ni pamoja na vijinundu (vijifundo) kwenye ngozi hasa usoni na masikioni, uvimbe na maumivu kwenye mishipa ya fahamu, ganzi kwenye mikono na miguu, vidonda au kuungua moto katika mikono na miguu bila kusikia maumivu yoyote,  
Athari za Ukoma ambazo pia watu hufikiri ni dalili ni pamoja na kukatika vidole vya mikono na miguu na upofu; athari hizi ni matokeo ya kuchelewa kuanza matibabu. 


Ndugu wanahabari,
Zipo hatua zinazochukuliwa na serikali yetu ya awamu ya tano kudhibiti ukoma nchini. Hatua hizo ni pamoja na:
Kuendesha   kampeni za uibuaji wa wagonjwa wapya ngazi ya  jamii kwa kuwashirikisha watoa huduma ngazi ya jamii ( Leprosy Elimination Campaigns) hasa katika wilaya zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Ukoma,
Utekelezaji wa mpango wa majaribio wa utoaji wa dawa kinga ngazi ya kaya kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ukoma (Leprosy Post-Exposure Prophylaxis). Mpango huu unafanyika katika wilaya za Nanyumbu, Liwale na Kilombero ambapo umeonesha mafanikio makubwa katika kuzuia kuenea kwa ukoma katika jamii,
Utekelezaji wa maazimio ya Bangkok (the Bangkok Declaration Special Fund (BDSF) kwa ajili ya kuhamasisha uibuaji wa wagonjwa wa ukoma mapema na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo watu walioathirika na ukoma.  Zoezi hili linatekelezwa kwenye wilaya za Mkinga, Muheza – Tanga na Chato mkoani Geita,
Utekelezaji wa shughuli za kuzuia ulemavu unaotokana na ukoma ikiwemo kutathmini wagonjwa wenye vidonda, kufanya upasuaji maalumu, huduma za kitaalamu za macho, utoaji wa viungo bandia pamoja na viatu maalum,
Kuagiza na kusambaza dawa za kutosha za ugonjwa wa ukoma nchi nzima.
Kutoa elimu kwa umma kuhusu dalili na tiba ya ukoma.


Ndugu wanahabari,
Pamoja na hatua zanazochukuliwa na serikali na mafanikio zipo changamoto.  Miongoni mwa changamoto zinazotukabili ni pamoja na jamii kuendelea kushikilia imani potofu juu ya ukoma kuwa ni ugonjwa wa kurithi au kulogwa na wagonjwa kuchelewa kujitokeza kupata matibabu hadi wanapopata ulemavu. Ukoma ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na vimelea vinavyoshambulia mishipa ya fahamu na huambukizwa kwa njia ya hewa pekee.

Nitoe rai kwa jamii, wazazi na walezi kuwa sote tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na ya watoto wetu. Endapo utaona mojawapo ya dalili za Ukoma, unashauriwa kwenda kwenye kituo cha tiba kilicho karibu nawe kwa uchunguzi bila kuchelewa. Hii itawawezesha wataalam wa afya kuchunguza na kubainisha kama mgonjwa ana ukoma ili apate tiba sahihi mapema na hivyo kuzuia maambukizi na ulemavu wa kudumu unaoweza kuzuilika.
Tiba ya Ukoma inapatikana nchini kote na hutolewa bila malipo kwa wagonjwa wote. Nirudie tena kuwa, pale tunapoona mabadiliko yoyote yanajitokeza kwemye miili yetu twende mapema katika vituo vyetu vya huduma kuchunguzwa ili tupate matibabu stahili. 

Ndugu wanahabari,
Aidha, napenda kuwashukuru wanahabari,  watoa huduma katika vituo vya afya kwa juhudi wanazofanya kila siku kuhakikisha ugonjwa huu si tatizo la kiafya tena nchini. 

Pia  nachukua nafasi hii kwa niaba ya serikali ya awamu ya tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuyashukuru mashirika mbalimbali ya ndani na nje kama vile Norvatis Foundation ya Uswisi, Germany Leprosy and Tuberculosis Relief Association (GLRA) ya Ujerumani, Nippon Foundation chini ya  Sasakawa Memorial Health Initiative ya Japani na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa michango yao katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukoma hapa nchini Tanzania. 

“TOKOMEZA UKOMA KUZUIA ULEMAVU MIONGONI MWA VIJANA WETU”.  

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Jumatano, 24 Januari 2018

MH. UMMY MWALIMU AONGOZA KIKAO CHA MWAKA CHA WADAU WA SEKTA YA AFYA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akielezea jambo katika kikao cha mwaka cha Wadau wa Sekta ya Afya nchini mapema leo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Faustine Ndugulile akijibu hoja wakati wa kikao hicho cha Wadau wa Sekta ya Afya, kilichofanyika mapema leo jiini Dar Es Salaam.

Kiongozi wa shirika la Maendeleo ya Afya Milma Kettunem(wa mwisho) akiwasilisha mchango wake katika kikao cha Wadau wa Sekta ya Afya. Wa kwanza ni Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu, na katikati ni Barozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Waechter.

Wadau wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu(hayupo kwenye picha) katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Afya wenye lengo la kubainisha vipaumbele vya 2017/2018 katika Sekta ya Afya.


Na WAMJWW. DSM
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) leo ameongoza kikao cha mwaka cha Wadau wa Sekta ya Afya nchini, huku lengo likiwa kujadili na kubainisha vipaumbele vya mwaka 2018/2019 katika sekta ya Afya.

Akifungua Mkutano huo Mh. Ummy Mwalimu(MB) alisema kuwa katika kuelekea Tanzania ya Viwanda ni lazima taifa lielewe kwamba kuna umuhimu wa kuimarisha Sekta ya Afya nchini katika ngazi ya utoaji huduma na miundombinu kwa jamii ili kuwezesha uwepo wa jamii yenye afya njema itakayoweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
“Ni Vigumu kutekeleza Sera ya Viwanda kama hatutaimarisha Sekta ya Afya nchini”, alisema Mh. Ummy Mwalimu.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Wadau mbali mbali wa Maendeleo, Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mashirika ya kidini na Sekta Binafsi huku  kikitawaliwa na masuala ya kuimarisha Afya ya mama na watoto wachanga, rasilimali watu katika Afya, miundombinu ya Huduma za Afya, rasilimali fedha katika Sekta ya Afya, Muendelezo wa Huduma, Utawala na uwajibikaji na Afya ya vijana hasa wasichana.
 
Akiongea kwa niaba ya Wadau wa Maendeleo, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Waechter ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa nia ya dhati katika kuimarisha na kukuza Sekta ya Afya nchini na kuahidi kuendeleza ushirikiano ikiwemo kutoa rasilimali fedha na utawala ili kufanikisha utoaji wa huduma bora za Afya katika jamii.
 
Kwa upande wa Mashirika yasiyo ya kiserikali wameiomba Serikali kuharakisha mpango wa Bima ya Afya kwa wote jambo litalosaidia kupunguza gharama za matibabu kwa kiasi kikubwa kwa wananchi wa kipato cha chini.