Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 21 Februari 2018

Usitumie Dawa bila ushauri wa mtoa huduma za Afya

Jumanne, 20 Februari 2018

CHUKUA TAADHARI DHIDI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Alhamisi, 15 Februari 2018

FAHAMU UGONJWA WA KIFAFA










Jumatano, 14 Februari 2018

SERIKALI YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI KWA KUONGEZA VITUO VYA AFYA NCHINI.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi katika ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam, katikati ni Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakisalimiana na Mbunge wa Ilala Mhe. Azan Zungu wakati wa Uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, wa pili ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda na wa mwisho ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda.

Na WAMJW. DSM
SERIKALI yaendelea kuongeza vituo vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali za kuboresha Huduma za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote zitakuwa zimeishia kwenye ngazi ya Kata.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam.
“Kumekuwa na ongezeko kubwa la vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka 2010 hadi vituo vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea, kwaiyo tunaamini  vituo hivi vitaweza kupunguza msongamano katika hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za kuboresha Vituo vya Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo yote nchini.
“Tumeanza kuboresha Vituo vya Afya kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta, wodi za magonjwa yakawaida, maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili kila kituo cha Afya kiwe na miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi” alisema Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu aliendele kusema kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161 katika kuendelea kuboresha Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha ya mama na mtoto jambo ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.
Aidha Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha kundesha shughuli za upasuaji katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.
Wakati akitoa taarifa ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema kwamba wakina mama 126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya, huku wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani wakielekea kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa wa Dar Es salaam.
Idadi ya 2016 inaonesha Zaidi ya akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya kina mama 100,000 waliokuwa wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho yafanyike ni akina mama 57 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua ndio hupoteza Maisha, huku mikakati thabiti yakupunguza vifo hivyo ikiendelea kuwekwa.
Mhe. Makonda aliendelea kusema kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na kuwa salamakatika kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa wakiwa tayari wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .
Pia Mhe. Makonda alimshukuru AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo la Mama na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku akiwataka Wadau wengine kuiga mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la maendeleo katika jamii zetu.
Nae Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni ongezeko la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa Zaidi ya asilimia 80.
“Serikali wakati inaingia madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka unaofuata ikafikia Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni 270, likiwa ni ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mbele na kusema ya kwamba hatuna uhaba wa Dawa muhimu”, alisema Dkt. Ndugulile.

Jumatatu, 12 Februari 2018

TANZANIA INATUMIA DAWA ZILIZO SALAMA KWA UHAKIKA MKUBWA

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika unaofanyika Jijini Dae Es Salaam na kuhudhuliwa nan chi zipatazo 17 za Afrika.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuifungua mkutano huo.
Pichani Naibu Waziri Dkt.Ndugulile akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Bi.Agnes Kijo kwenye mkutano huo utakaofanyika kwa siku tano na kujadili mfumo wa pamoja wa kudhibiti ubora wa dawa barani Afrika.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akifuatilia mada (mwasilishaji hayupo pichani) katika mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi.Agnes Kijo akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa  wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrik.
Msimamizi wa kitengo cha Afya katika Shirika la Maendeleo ya Afrika (NEPAD) yenye makao makuu yake nchini Afrika ya Kusini Bi.Margareth Ndomondo akiongea wakati wa uzinduzi huo.Shirika hilo katika afya linasaidia kupunguza magonjwa yanayoikabili nchi za Afrika.(Picha zote na Wizara ya Afya)

Na.WAMJW-DAR ES SALAAM
TANZANIA ni miongoni mwa nchi inayotumia dawa zilizo salama na ubora wa hali ya juu barani Afrika kutokana na udhibiti na umakini unaofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mamlaka wa Udhibiti  na ubora wa dawa barani afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam.
”Sisi kama Tanzania tunafanya vizuri sana katika udhibiti wa madawa yanayoingia,nataka niwathibitishie  kwamba Tanzania dawa zetu tunazozitumia ni salama na zipo salama kwa uhakika mkubwa” alisema Dkt. Ndugulile

Aidha ,Dkt. Ndugulile alisema kuwa ongezeko la matumizi ya dawa ambayo hayana kiwango na kutumika katika mfumo wa tiba umeleta changamoto katika kuongeza gharama za matibabu nchini na barani Afrika
Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema changamoto hizo zinasababisha wagonjwa wengi kukaa hospitalini,kuongeza gharama, kuathiri matokeo ya mgonjwa na hatimaye vifo pamoja na kuleta usugu wa dawa kwa kutumia dawa zisizo na kiwango
Hata hivyo Dkt. Ndugulile alisema mkutano huo utajenga utaratibu na mfumo  wa pamoja wa kuona ni jinsi gani wanaweza kudhibiti matumizi ya madawa yasiyo na kiwango barani afrika.
 “Nataka niwathibitishie Watanzania kwamba tuna dawa za kutosha na dawa zote  zinazoingia zina ubora unaotakiwa,Taasisi yetu ya TFDA inatambulika Kimataifa, ina viwango vya Kimataifa na tumeboresha maabara zetu kuwa za kisasa na kutumika katika bara la afrika  katika udhibiti wa madawa”. Alisema Dkt. Ndugulile.
Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi.Agnes Kijo alisema mamalaka hiyo imejidhatiti katika masuala ya udhibiti wa dawa hivyo kupelekea mkutano huo kufanyika Tanzania
“Maabara yetu hivi sasa imewekewa vifaa vya kisasa ambapo mwaka huu wa fedha ilitengewa shilingi  bilioni tano nukta moja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya maabara ya Dar es Salaam na  kanda ya ziwa ambapo itasaidia kufanyiwa uchunguzi wa dawa katika ukanda uliopo na hivyo kutoa majibu kwa wakati na mamlaka kufanya maamuzi sahihi” alisema Bi. Kijo.
Mkutano huo ambao una lengo la kubadilishana uzoefu wa  masuala mbalimbali yanayo uhusiana na udhibiti na ubora wa dawa ambapo kumekuwa na changamoto za matatizo ya madawa yasiyo na kiwango umekutanisha nchi zipatazo  17 na utafanyika kwa siku tano.

TUMEKOSOGEZA KARIBU


Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto.

Inayo furaha kubwa kuwakaribisha wananchi wote ndani na nje ya nchi kutembelea katika mitandao yake ya kijamii ili kupata taarifa mbalimbali za kiafya. Aidha tunakaribisha maoni na ushauri mbalimbali kuhusu sekta ya afya. "Jenga taifa lenye afya bora kwa uchumi imara"
#AFYA_YANGU_MTAJI_WANGU

Jumatano, 7 Februari 2018

SERIKALI YAAZIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.





SERIKALI  imeazimia kukusanya na kutumia takwimu kwa njia ya kielektroniki nchi nzima ili kuweza kumudu na kutoa huduma za afya kwa ubora zaidi nchini.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa kutia Sahihi ya makubaliano ya kuanzisha mfumo wa ukusanyaji takwimu za afya utakaotekelezwa na Wizara ya afya,Wadau wa Maendeleo,Asasi za Kiraia na Shirika la Afya Duniani (WHO) uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
“Takwimu ni muhimu sana amabazo zitazomuwezesha mtoa huduma kujua mgonjwa historia yake ya ugonjwa  na matibabu aliyopewa awali,kuwapa Uwezo utumishi kujua tunahitaji rasilimali watu kwa kiasi gani  katika kituo cha Afya” alisema Dkt. Ulisubsya.

SERIKALI YAAZIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa taarifa mbele ya Wadau wa Sekta ya Afya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini  taarifa ya mgeni rasmi (Hayupo kwenye picha) ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki.

Mwinyekiti wa DPG HEALTH Mhe. Norzin Grigoleit-Dagyab akitutubia mbele ya Wadau wa Sekta ya Afya na Watumishi wa Serikali wa Idara kuu ya Afya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na wa mwisho kulia ni Mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthieu Kamwa.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa na Wadau mbali mbali wa Sekta ya Afya katika Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu wa kielektroniki kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Sekta ya Afya wakiwa wameshika mikataba iliyosainiwa ya makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu wa kielektroniki ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.


Na WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeazimia kukusanya na kutumia takwimu kwa njia ya kielektroniki nchi nzima ili kuweza kumudu na kutoa huduma za afya kwa ubora zaidi nchini.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa kutia Sahihi ya makubaliano ya kuanzisha mfumo wa ukusanyaji takwimu za afya utakaotekelezwa na Wizara ya afya,Wadau wa Maendeleo,Asasi za Kiraia na Shirika la Afya Duniani (WHO) uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
“Takwimu ni muhimu sana amabazo zitazomuwezesha mtoa huduma kujua mgonjwa historia yake ya ugonjwa  na matibabu aliyopewa awali,kuwapa Uwezo utumishi kujua tunahitaji rasilimali watu kwa kiasi gani  katika kituo cha Afya” alisema Dkt. Ulisubsya.
Aidha, Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa kuanzia zoezi hilo litaanza kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara hatimaye kufikia nchi nzima mpaka kufika 2020 ili kuweza kuwa  na takwimu za afya.
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mfumo wa kujaza takwimu kwenye makaratasi umepitwa na wakati kwani kadri makaratasi ya takwimu yanapokuwa mengi na makosa ya utoaji huduma unaweza kutokea  kwani mpaka uanze kutafuta takwimu zilizopita inachukua muda mrefu tofauti na kuhifadhi takwimu kielektroniki.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mpaka hivi sasa hali ya utoaji wa chanjo imefikia asilimia 97 na lengo letu ni kufikia asilimia 100 kupitia mfumo huu wa kukusanya takwimu kwa njia ya kielektroniki.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa amesema kuwa wapo  tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kutekeleza hilo ili kuweza kuboresha mifumo ya afya nchini.
“Unajua Takwimu ni utajiri hasa katika kutekeleza shughuli za kutoa huduma za afya kwa wananchi hivypo hatuna budi kuunga mkono juhudu za Serikali ya Tanzania katika kufanikisha hili jambo kwani litaturahisishia hata sisi katika kutoa miongozo ya afya” alisema Dkt. Kamwa.

Jumanne, 6 Februari 2018

TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI



Na WAMJWW. Dom
Serikali imejipanga kutumia tiba mtandao kuboresha huduma za afya nchini kwenye hospitali zote za ngazi ya taifa, rufaa na wilaya ili kuwawezesha wagonjwa waishio sehemu mbali mbali nchini kupata huduma za afya kwa wakati na kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la LAPF, Dodoma.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha watendaji wakuu wa hospitali za taifa nchini, madaktari bingwa wa sekta ya Afya, wakuu wa taasisi zinazoshughulika na sekta ya Afya, Wizara ya TAMISEMI, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; taasisi nyingine za Serikali; sekta binafsi na wabia wa maendeleo ili kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja wa kufanikisha utekelezaji wa huduma za tiba mtandao ili kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na madawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na yanayotokana na ajali za barabarani.
“Hadi hivi sasa ni asilimia 37 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ndio wanaotambulika na kupatiwa huduma na Wizara ya Afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo, tiba mtandao itawezesha upatikanaji wa wagonjwa na ufikishaji wa huduma kwao kwa wagonjwa wengine asilimia 63”, alifafanua Dkt. Ulisubisya.

Aliongeza kuwa tiba mtandao itapunguza gharama za wagonjwa na wanaowahudumia kusafiri kufuata madaktari. Aidha, amewataka wakuu hao wa taasisi kuwaruhusu wataalamu wao, wa Wizara ya TAMISEMI na wa Wizara ya Afya, kushiriki mafunzo ya tiba mtandao ili kuongeza ufanisi wao katika kuhudumia wagonjwa.

Amewataka wataalamu wa afya na wakuu wa taasisi zinazohusika na masuala ya afya kununua vifaa tiba vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) vyenye viwango na ubora unaohitajika ili kuwezesha tiba mtandao na manunuzi hayo yazingatie na kufuata ununuzi wa pamoja wa huduma na bidhaa za Serikali.
Vifaa vya kisasa vya TEHAMA vinavyohusika na tiba mtandao vitawawezesha wataalamu kufanya uchunguzi kwa mgonjwa, kupata majibu ya uhakika na kumpatia mgonjwa tiba inayostahili na ya uhakika. 
Aidha, amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Ulanga, ambao ndio waanadaji na waratibu wa kongamano hilo, kushirikiana na TTCL kuhakikisha kuwa tiba mtandao inapatikana katika hospitali zote za rufaa na hospitali ambazo zina changamoto ya kijiografia ya kufikika kwa urahisi.

Ijumaa, 2 Februari 2018

DKT MPOKI ASEMA WATOA HUDUMA ZA USINGIZI WANAHITAJIKA ZAIDI NCHINI.

- Hakuna maoni




Watumishi wa wa afya wa kutoa huduma za usingizi wanahitajika zaidi nchini ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa wingi na ukaribu zaidi mara zinapohitajika kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji kwa usalama katika hospitali zetu