Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 12 Machi 2018

MATEMBEZI YA SIKU YA FIGO DUNIANI

- Hakuna maoni

WATANZANIA WATAKIWA KUPIMA UGONJWA WA MACHO ANGALAU MARA MOJA KWA MWAKA.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa uma wakati akitoa tamko katika wiki ya maadhimisho ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho Jijini Dar es salaam. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari wakati akitoa tamko katika wiki ya maadhimisho ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho Jijini Dar es salaam.

Na WAMJW-Dar Es salaam.

WATANZANIA wametakiwa kujua afya zao hususan magonjwa yanayohusu macho angalau mara moja katika mwaka ili kuweza kutambua juu ya mustakabali wa macho yao. 

Hayo yamezengumzwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa   kutoa tamko katika wiki ya maadhimisho ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho Jijini Dar es salaam. 

"Wanaohathirika zaidi na Ugonjwa huu ni Barani Afrika na watu wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea hivyo watanzania tujijengee mazoea ya kwenda kuangalia afya zetu hususani ugonjwa huu angalau mara moja kwa mwaka" alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa ugonjwa huo wa shinikizo la macho huambatana na kushindwa kuona mbali na dalili zake za mwanzo si rahisi kuziona kwa wakati huo. 

Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema kuwa takribani watu  milioni1. 74 wana changamoto ya kutoona vizuri nchini Tanzania na bado haijakadiriwa ni mikoa gani hasa ina athari kubwa kwani ukusanyaji wa takwimu bado unaendelea. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa matibabu ya ugonjwa wa presha ya macho   yanapatikana katika hospitali zote za serikali nchini ikiwemo dawa pamoja na upasuaji kama utawahi mapema. 

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisistiza kuacha utumiaji ovyo wa vilevi, uvutaji sigara na badala yake kujikita kwenye ufanyaji wa mazoezi na kuzingatia lishe bora ili kuepuka magonjwa yasioambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na mengineyo. 

Siku ya Ugonjwa wa presha ya macho itahadhimishwa kwa vituo vya afya kutoa huduma ya upimaji macho kuanzia tarehe 11 mpaka itapofikia kilele 17 machi 2018  na imebeba kauli mbiu   "OKOA UONI WA MACHO YAKO". 

Jumapili, 11 Machi 2018

SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile katika matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria ufunguzi wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo huazimishwa kila machi 8, ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam

Kiongozi wa Lions International Club Sayed Rizwan Qadri akikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.4 kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile ikiwa moja ya juhudi za kuunga mkono kupambana dhidi ya magonjwa ya Figo. Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akifanya mazoezi ya viungo wakati wa kujiandaa kuanza kwa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.




Na WAMJW. Dar Es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeongeza wigo wa kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa figo nchini kwa kuongeza vituo vya usafishaji damu hadi kufikia vituo  zaidi ya 17, na kufanya mafunzo kwa madaktari bingwa ili kuongezea nguvu madaktari bingwa 13 waliopo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika mapema leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.
“Wataalamu tunao 13 kwa upande wa madaktari, tumeiona hiyo changamoto kama Serikali, tumeongeza wigo wakufanya mafunzo kwa madaktari bingwa, na hivi karibuni tutatangaza ufadhili kupitia Serikali, vile vile tumetenga fedha kwaajili ya kuwafundisha madaktari ili kuweza kufanya matibabu ya figo” alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kwamba Serikali imeongeza wigo wa usafishaji damu kwa kuongeza vituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo katika hospitali binafsi na Hospitali za Serikali.
“Tumeongeza wigo wa usafishaji damu hadi tunavyoongea, tunavituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu katika hospitali binafsi pamoja na hospitali zetu za Serikali , Muhimbili kuna vitanda 42, Mloganzira kuna vitanda 12, Bugando vitanda 6, KCMC vitanda 6, Mbeya vitanda 6, bila kusahau Regency, TMJ, Agakhan, Hindumandal,  na tunaendelea kuimarisha huduma”. Alisema Dkt. Ndugulile.
Vile vile Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imeanza upandikizaji wa Figo na imeshafanikisha kwa mgonjwa mmoja mpaka sasa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  na matarajio ni kufanya upasuaji kwa mgonjwa mmoja kila mwezi mmoja.
Aliendelea kusema  mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa shilingi milioni 37 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama ya kusafisha damu. Aidha, anahitaji kusafiri na kufika kwenye huduma kwa wastani wa safari 126 kwa mwaka sawa na wastani wa safari 3 hadi 4 kwa wiki.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliendelea kuwa kukumbusha kuwa Serikali ya awamu ya tano imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 ilipokuwa ikiingia madarakani hadi sasa ni Bilioni 270 kwaajili ya Dawa, vifaa na vifaa tiba kwaajili ya magonjwa yakiwemo magonjwa ya Figo.
“Tumeongeza bajeti kwaajili ya Vifaa, Dawa na Vifaa Tiba kutoka Bilioni 30 wakati Serikali hii inaingia madarakani mbaka Bilioni 270, yaani mara tisa Zaidi, kwahiyo Dawa na Vifaa Tiba kwaajili ya matibabu ya Figo tunazo” alisema Dkt. Ndugulile.
Mwisho Dkt.Ndugulile alitoa wito kwa wananchi kubadili jinsi ya kuandaa vyakula nyumbani, mfano kwa kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula na kiasi cha mafuta kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza magonjwa shinikizo la damu (hypertension), kisukari na unene wa kupindukia, vile vile kuhamasisha familia kufanya mazoezi.
“Watanzania hatujui kula, tunakula bora chakula kuliko chakula bora, Matumizi ya vyakula vya mafuta, matumizi ya chumvi nyingi, matumizi ya vilevi, matumizi ya sigara kama hayana ulazima basi tupunguze, tutumie vyakula vilivyochemshwa na vilivyochomwa, bila kusahau kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi angalau mara 3 kwa wiki kwa lisaa limoja inatosha” alisema Dkt. Ndugulile.

Ijumaa, 9 Machi 2018

DKT. FAUSTINE AKUTANA NA UGENI KUTOKA UBALOZI WA MAREKANI NA WADAU WA AFYA.

- Hakuna maoni



 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akutana na ugeni kutoka ubalozi wa Marekani na wadau wa Afya mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es salaam, lengo ni kujadili namna ya kuimarisha Sekta ya Afya nchini.

ZIARA YA MHE. UMMY MWALIMU WILAYA YA ILEJE, SONGWE

- Hakuna maoni

MAGONJWA YA FIGO YANAATHIRI ZAIDI WANAWAKE

- Hakuna maoni

MAGONJWA YA FIGO YANAATHIRI ZAIDI WANAWAKE

- Hakuna maoni

MAGONJWA YA FIGO YANAATHIRI ZAIDI WANAWAKE.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo mbele ya Watumishi wa Umma na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa ya Siku ya Figo Duniani tukio lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Dkt. Kisanga akifafanua moja ya swali lililoulizwa na mwandishi wa Habari kutoka East Afrika Tv Oliver Nyerige (hayupo kwenye picha) wakati Naibu Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile akitoa tamko la siku ya Figo duniani ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

Watumishi wa Umma na Wataalamu wa magonjwa ya Figo wakifuatilia kwa umakini taarifa ya siku ya Figo duniani iliyosomwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ambapo siku hiyo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.


Na WAMJW. Dar es salaam.
Magonjwa ya figo yanakadiriwa kuwaathiri takribani wanawake milioni 195 duniani kote na yanashika nafasi ya 8 kama chanzo cha vifo vya wanawake duniani na inakadiriwa kuwa wanawake 600,000 hupoteza maisha kutokana na matatizo ya figo duniani kote kila mwaka

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akitoa tamko la siku ya Figo duniani ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

Dkt.Ndugulile alisema tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya figo ukilinganisha na wanaume. Kwa wastani asilimia 14% ya wanawake wanaathiriwa na matatizo ya figo ukilinganisha na asilimia 12% kwa wanaume

Kwa upande wa Tanzania Naibu Waziri huyo alisema ugonjwa huo umekuwa ukiongezeka  na tafiti zilizofanya Kanda ya Kaskazini mwaka 2014, ulionyesha kuwa kati ya 7% – 15% ya Watanzania wana matatizo sugu ya figo na kwa asilimia kubwa yamekuwa yakichangiwa na magonjwa ya Shinikizo la Damu na Kisukari

Hata hivyo aliongeza kuwa kwa utafiti uliofanywa na Hospitali ya Kanda Bugando, umeonesha kuwa 83% ya Wagonjwa wa Kisukari wana matatizo sugu ya figo na kati ya hawa, 25% walikuwa wanahitaji huduma za usafishaji damu.

“Wagonjwa waliokuwa wanapatiwa huduma ya kusafisha damu kutokana na figo kushindwa kufanya kazi, ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) walikuwa 178. Kwa sasa idadi ya Wagonjwa hawa imeongezeka na kufikia 783. 


Aidha, alisema  mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa shilingi milioni 37 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama ya kusafisha damu. Aidha, anahitaji kusafiri na kufika kwenye huduma kwa wastani wa safari 126 kwa mwaka sawa na wastani wa safari 3 hadi 4 kwa wiki.

Alisema Serikali  imekuwa ikipeleka wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo na idadi ya waliokwishapandikizwa figo na ambao wanafuatiliwa matibabu yao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili  ni takribani 204.“Gharama za kupandikiza figo nje ya nchi ni wastani wa fedha za Kitanzania milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja,ikijumuisha upandikizaji,nauli na malazi”Alisema Dkt.Ndugulile

Dkt.Ndugulile alitoa wito kwa wananchi kubadili jinsi ya kuandaa vyakula nyumbani, mfano kwa kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula na kiasi cha mafuta kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza magonjwa shinikizo la damu (hypertension), kisukari na unene wa kupindukia, vile vile kuhamasisha familia kufanya mazoezi.Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya figo ya mwaka huu wa 2018 ni “FIGO NA AFYA YA WANAWAKE: WASHIRIKISHWE, WATHAMINIWE NA WAWEZESHWE”.

Jumatano, 7 Machi 2018

WAZIRI UMMY AWAAHIDI AMBULANCE WAKAZI WA LUBANDA- ILEJE,

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akitoa udongo wakati wa  uchimbaji wa msingi katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mtura kilicho katika kata ya Lubanda Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akielekea eneo la gari lililokwama kutokana na changamoto ya Barabara, wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi, Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Kheri Kagya.
.
Wananchi wa kata ya Lubanda katika kijiji cha Mtura wilaya ya Ileje wakimsalimia Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.

 
Na WAMJW. Songwe
 
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaahidi wananchi wa kata ya Lubanda Wilayani Ileje kuwapatia gari ya kubebea wagonjwa mapema mwaka huu.

Ahadi hiyo ameitoa jana wakati alipotembelea kijij i hicho kujionea ujenzi wa kituo cha afya cha Lubanda kinachojengwa kupitia mpango wa kuboresha vituo vya afya nchini kwa kujenga chumba cha upasuaji wa dharura.

Waziri Ummy alitoa ahadi hiyo baada ya kujionea umbali wa Zahanati ya Lubanda hadi kufika hospitali ya Isoko, pia hali ya barabara kijijini hapo.

"kwakuwa nategenea kununua magari ya kubebea wagonjwa yapatayo 60,Tanzania ni kubwa, nyie mtakuwa namba moja, kwani hali ya barabara nimeiona"alisema Waziri Ummy.

Aidha, alisema anataka kushuhudia  mwanamke mjamzito wa kijiji hicho anaokolewa maisha yake kwa kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya ili huduma zote za upasuaji ukiwemo wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni kwa mama mjamzito zinatolewa katika kituo hicho mapema iwezekanavyo

"Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumuokoa mama mjamzito pale anapopata uzazi pingamizi, hivyo Serikali kuu imetoa shilingi milioni 500 kwa ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya vipatavyo 174 nchini.
Hata hivyo Waziri huyo wa Afya amewataka wananchi hao kujenga utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kupata tiba haraka pale wanapogundulika na matatizo.
 
"hivi sasa wanawake wengi wamegundulika na saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 80 ya wanawake wanaofika hospitalini wapo hatua za mwisho hivyo badala ya kutibiwa wanapunguziwa maumivu" aliendelea Mhe.Ummy
 
Wilaya ya Ileje ina vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 33 ikiwemo hospitali mbili, kituo cha afya kimoja na zahanati 30 zinazomilikiwa na serikali, dini pamoja na watu binafsi.

Jumatatu, 5 Machi 2018

TAARIFA KWA UMMA

- Hakuna maoni



BARAZA LA WATAALAMU WA MAABARA LINATANGAZA RASMI KUANZA KWA MITIHANI YA USAJILI YA BARAZA KUANZIA MWAKA HUU 2018, HII NI KATIKA KUTEKELEZA SHERIA NAMBA 22 YA MWAKA 2007 INAYOSIMAMIA TAALUMA NA HUDUMA ZA MAABARA NCHINI TANZANIA.
 
MITIHANI YA BARAZA NI MATAKWA YA KISHERIA YA KUPIMA UWEZO WA MTAALAMU WA MAABARA KABLA YA KUPEWA USAJILI WA KUDUMU KATIKA KUTOA HUDUMA ZA MAABARA NCHINI.
 
MITIHANI HII ITAFANYIKA TAREHE 12 HADI 15 JUNI 2018 KWA NGAZI YA ASTASHAHADA, (NGAZI ZINGINE WATATANGAZIWA TAREHE YA KUANZA).
 
VITUO VYA KUFANYIA MITIHANI, MALIPO NA JINSI YA KUJISAJILI VIMEAINISHWA KATIKA FOMU YA KUJISAJILI NA MAELEKEZO YANAYOPATIKANA KATIKA TOVUTI YA WIZARA ( www.moh.go.tz)
 
BARAZA LINASISITIZA KURUDISHA FOMU MAPEMA KUPITIA EMAIL ILIYOANDIKWA KWENYE FOMU YA KUJISAJILI AU OFISI YA MSAJILI(hlpc2018@yahoo.com)
 
MWISHO WA KURUDISHA FOMU NI TAREHE 30 APRILI, 2018. TAARIFA YA KITUO ULICHOCHAGULIWA KUFANYIA MTIHANI UTAJULISHWA KABLA YA TAREHE 30 MEI, 2018 
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA OFISI YA MSAJILI KWA NAMBA ZIFUATAZO; 076820091 NA 0716020159
 
Imetolewa na,
OFISI YA MSAJILI;
BARAZA LA WATAALAMU WA MAABARA
03 FEBRUARI, 2018