![]() |
|
Wadau wa afya kutoka mikoa mbalimbali nchini
wakisikiliza kwa makini mjadala unaoendelea katika kikao kilichoshirikisha
wadau wa afya na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kinachofanyika jijini Dodoma.
|
Jumatatu, 20 Agosti 2018

WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WANAHITAJIKA NCHINI
Jumatatu, Agosti 20, 2018
-
Hakuna maoni

TAARIFA KWA UMMA
Jumatatu, Agosti 20, 2018
-
Hakuna maoni
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VYETI VYA WAHITIMU WA KADA ZA AFYA
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda
kuwajulisha kuwa imepokea vyeti vya wahitimu kutoka Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE).Vyeti hivyo ni kwa wahitimu waliofanya mitihani 2016, mwezi Septemba na Oktoba 2017 kwa Mafunzo ya Astashada na Stashahada ya
Uuguzi na Ukunga, Mafunzo ya Astashahda ya Wahudumu wa Afya ya Jamii na
Mafunzo ya Sayansi Shirikishi za Afya (Utabibu, Wateknolojia wa Maabara,
Famasia, Sayansi ya Afya ya Mazingira, Utunzaji kumbukumbu za Afya,
Mazoezi ya viungo ,Utabibu wa Meno na Wateknolojia Macho).
Wizara
inawajulisha wahitimu wa mafunzo hayo kuwasiliana na Wakuu wa Vyuo
kuanzia tarehe 20/08/2018 ili kuweza kupewa utaratibu wa kwenda kuchukua
vyeti vyao kwenye vyuo walivyopatia mafunzo hayo.
Imetolewa na,
KATIBU MKUU (AFYA)
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
20 Agosti, 2018.
Ijumaa, 17 Agosti 2018

PICHA MBALI MBALI ZA MATUKIO YA KUFUNGA KWA MKUTANO WA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA HALMASHAURI.
Ijumaa, Agosti 17, 2018
-
Hakuna maoni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na
Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakati wa kufunga mkutano wa
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hawapo pichani ,kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula .
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakifuatilia kwa makini maada
mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wawasilishaji mbalimbali hawapo
pichani wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na
Halmashauri uliofanyika jijini Dodoma.

DKT. SUBI AWAHASA WANAWAKE KUWAI KLINIKI PINDI WANAPOHISI WANAUJAUZITO.
Ijumaa, Agosti 17, 2018
-
Hakuna maoni
Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi
Na.WAMJW - Dodoma
Akina
Mama wajawazito wametakiwa kuwahi kliniki mara wanapohisi wana
ujauzito na kufuata ushauri wa wataamu wa afya ili kuwakinga watoto
wanaotarajia kujifungua dhidi ya maabukizi ya Virus vya UKIMWI
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi mjini Dodoma hivyo
kuwataka wananchi kuchukua hatua katika kujikinga na maradhi mbalimbali
ikiwemo Virusi Vya Ukimwa (VVU).
Amesema Utafiti
uliofanywa mwaka 2010 maambukizi ya Virus yalikua asilimia 26 kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto huku utafiti uliofanywa mwaka 2016/2017
unaonesha kuwa maambukizi haya yamepungua na kufikia asilimia 7.6 ambapo
Serikali imesema inatarajia maambukizi haya yapungue mpaka asilimia 2
ifikapo 2020-2021.
“Ni muhimu kwa wajawazito
kuhudhuria kliniki na kupima VVU hii itasaidia kuzuia maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, malezi na makuzi mzuri ya Mtoto
yanategemea wazazi wote wawili yaani baba na mama wazazi wote wanaaswa
kushirikiana hasa katika kupima afya afya ili mtoto atakaezaliwa asiwe
na maambukizi ya VVU”Alisema Dkt.Subi.
Aliongeza
kuwa moja ya changamoto inayokwamisha mpango huu ni wanaume kukumbatia
mila na destuli za kutoandamana na wenzi wao kliniki wakati wa kipindi
cha ujauzito,
“hivyo familia au makabila ambayo bado yanaona kwamba
mwanaume kumsindikiza mwenzi wake kliniki ni kujishushia hadhi waachane
nazo”.
Aidha, Dkt.Subi amewataka vijana kuchukua
hatua za kwenda katika vituo vya afya kupata elimu ya uzazi na kupima
afya zao maana wao ndio mama au baba wanaotarajiwa,mimba za utotoni ni
hatari kwa afya zao na kama kuna tatizo lolote wafike katika vituo vya
afya ili kupata msaada wa kitalaamu.
Alisisitiza
kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini hivi sasa vinatoa
huduma ya elimu bure kuhusiana na afya ya uzazi na endapo mama mjamzito
atagundulika ana maambukizi ya VVU ataanzishiwa dawa ambazo zitamkinga
mtoto asizaliwe na maambukizi ya Virus vya UKIMWI.
Jumatatu, 13 Agosti 2018
WAZIRI UMMY AMSHUKURU BALOZI WA CANADA NCHINI TANZANIA KWA KUBORESHA SEKTA YA ÁFYA.
Jumatatu, Agosti 13, 2018
-
Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiagana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam baada ya mazungumzo juu ya Maboresho katika Sekta ya Afya.
Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles (Wapili kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo wakati alipotembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam. Wakwanza kushoto ni ofisa wa Ubalozi wa Canada Susan Steffen.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa makini Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles (Hayupo kwenye picha)
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian Myles baada ya kikao cha kumuaga Balozi huyo kilichofanyika mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
WAZIRI UMMY AMSHUKURU BALOZI WA CANADA NCHINI TANZANIA KWA KUBORESHA SEKTA YA ÁFYA.
Na WAMJW - DSM
Waziri
wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameishukuru Serikali ya Canada kupitia Balozi wake nchini Tanzania kwa
ushirikiano walioonesha katika kuboresha sekta ya Áfya hususani katika
Kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Ameyasema
hayo mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Áfya jijini Dar es
salaam wakati akiagana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Ian
Myles anayetarajia kuondoka hivi karibuni hapa nchini.
Nae Balozi wa
Canada nchini Tanzania Mhe Ian Myles ameishukuru Serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Áfya kwa kuendelea kutatua changamoto za sekta ya Áfya
nchini.
Ijumaa, 10 Agosti 2018

TAMKO KUHUSU UGONJWA WA EBOLA ULIOTOKEA KATIKA NCHI JIRANI YA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Ijumaa, Agosti 10, 2018
-
Hakuna maoni
TAMKO KUHUSU UGONJWA WA EBOLA ULIOTOKEA KATIKA NCHI JIRANI YA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Utangulizi
Ndugu wanahabari,
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kutoa
taarifa kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Nchi hiyo ya DRC imetangaza tena kuwa
na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mnamo tarehe 1 mwezi Agosti, 2018, ambapo
jumla ya wagonjwa 26 na vifo 10 vilitolewa taarifa na wagonjwa 4 kati
yao walithibitishwa kimaabara kuwa na ugonjwa wa Ebola. Wagonjwa hawa
wametokea katika vijiji/Maeneo ya Mangina ikiwa ni kama km 30 tu
magharibi mwa mji wa Beni kwenye jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na
nchi ya Uganda ikiwa ni kama km 100 tu, na pia likiwa karibu sana na
nchi ya Rwanda.
Huu ni mlipuko wa 10 wa ugonjwa wa
Ebola kutokea nchini DRC, na umetokea wiki moja baada ya nchi hiyo
kutangaza kuisha kwa mlipuko mwingine uliotokea mwezi Mei mwaka huu
ambao ulikuwa katika jimbo la Equator, Magharibi mwa DRC, umbali wa
zaidi ya km 2,000 kutoka eneo la huu mlipuko mpya uliotokea.
Ndugu wanahabari,
HADI
SASA HAPA NCHINI TANZANIA HAKUNA MGONJWA YOYOTE ALIYEHISIWA AU
KUTHIBITISHWA KUWA NA VIRUSI VYA EBOLA. Hata hivyo, kugunduliwa kwa
ugonjwa huu kwenye jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na nchi za
Uganda na Rwanda ni jambo la kutuweka kwenye wasi wasi kwani eneo hili
liko karibu sana na nchi yetu kuliko eneo lingine lolote ambako ugonjwa
huu umeshawahi kutokea kwenye nchi ya DRC. Hivyo nchi yetu ipo hatarini
kuambukizwa ugonjwa huu kutokana na ukaribu na muingiliano wa watu, hasa
kuhusiana na wasafiri wanaotoka na kuingia hapa nchini.
Kwa
sababu hizi, watanzania hatuna budi kuchukua tahadhari ya hali ya juu
ili kujikinga na kudhibiti na ugonjwa wa Ebola. Hivyo Wizara inapenda
kutoa tahadhari ya ugonjwa huu kwa wananchi wote katika Mikoa yote ya
Tanzania, lakini hasa ile inayopakana na nchi jirani za DRC, Uganda na
Rwanda. Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa na
Songwe. Aidha tahadhari na hatua stahiki zichukuliwe katika maeneo yote
ya mipakani ambapo abiria wanaingia nchini kutoka nchi jirani.
Ugonjwa wa Ebola
Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola ambavyo huambukiza kwa njia zifuatazo;
Kugusa Damu au majimaji kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo,
Kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huo,
Kugusa wanyama (Mizoga na wanyama wazima) walioambukizwa kama vile Sokwe na Swala wa msituni.
Dalili za Ugonjwa
Dalili
za Ugonjwa huanza kuonekana kwa mtu aliyeambukizwa baada ya siku 2 hadi
21 tangu kupata maambukizi. Dalili hizo ni pamoja na;
Homa kali ya ghafla,
Kulegea kwa mwili,
Maumivu ya misuli,
Kuumwa kichwa na vidonda kooni.
Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi na pia figo na Ini kushindwa kufanya kazi.
Kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa na damu ndani na nje ya mwili.
Namna ya Kujikinga na ugonjwa wa Ebola:
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:-
Kuepuka
kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na
majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa
wa Ebola
Kuepuka kushughulikia maiti ya mtu
aliyefariki akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa
uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
Kuepuka kula nyama za Wanyama wa porini kama sokwe, swala na popo na pia kugusa mizoga ya Wanyama hao
Kuepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola.
Kuzingatia usafi wa mwili
Kutoa
taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika
ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola.
Kuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.
Hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara kufuatia kupatikana kwa taarifa ya Ugonjwa huu huko DRC
Kufuatia
kuwepo kwa taarifa hizi tangu mwezi Mei 2018, hatua zifuatazo
zinaendelea/zimechukuliwa na Wizara ili kujiandaa kukabiliana na mlipuko
huo:
Kufanya tathmini ya utayari wa kukabiliana na
ugonjwa wa Ebola nchini (Operational readiness assessment) kwa nchi
nzima kwa kushirikiana na WHO na kuainisha mapungufu ambayo yanapaswa
kufanyiwa kazi. Mapungufu hayo yanaendelea kuyafanyiwa kazi ili kujenga
uwezo na utayari katika nchi yetu.
Tumetengeneza
mpango mkakati wa kujiandaa na kupambana na mlipuko wa Ebola endapo
utatokea nchini (Costed Ebola Contingency Plan). Mpango huu umeandaliwa
kwa kushirikiana na WHO. Mpango umeainisha maeneo ya kujenga uwezo kwa
wakati huu wa kujiandaa, pamoja na hatua za kuchukua endapo ugonjwa
utaingia ikiwa ni pamoja na gharama zake.
Tumefanya
mafunzo ya Timu za dharura (Rapid Response Teams) ngazi ya Taifa na
katika Mikoa ya Dar es Salaam, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma na Kagera
Tumeimarisha
ufuatiliaji wa wasafiri mipakani (travellers entry screening) kwa
kutumia vifaa vya kupima joto la mwili (thermo scanners) na fomu maalum
za wasafiri
Wizara imepokea vifaa vya kukabiliana
na Ebola kutoka WHO vikiwemo; Thermo scanners, Vifaa Kinga, au PPE, kama
vile gloves, body bags, vifaa vya ufungashaji wa sampuli nk. Vifaa
hivyo vimeanza kusambazwa mikoani kupitia MSD
Uelimishaji
wa umma umefanyika na unaendelea kufanyika kwa kupitia vyombo vya
habari vya kitaifa na kijamii, na mitandao ya kijamii. Vile vile
vipeperushi na mabango vinaendelea kuandaliwa
Vikao
vya uratibu vimefanyika katika ngazi ya taifa na mikoa ambayo ipo
katika hatari zaidi. Pia ufuatiliaji wa karibu unaendelea kupitia Kituo
cha ufuatiliaji wa magonjwa ya dharura cha Wizara (Public Health
Emergency Operation Centre is on High Alert)
Wataalam
kutoka ngazi ya Taifa kwa sasa wako katika mikoa ya Kigoma Katavi Rukwa
Kagera Kilimanjaro Mwanza Songwe na Mbeya kufanya tathmini ya utayari
katika ngazi ya mikoa na Wilaya (Readiness Assessment)
Maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kutekeleza kazi nyingine kama ifuatavyo:
Kufanya
mafunzo katika mikoa iliyo salia ikiwemo Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya
ambayo imesalia katika ile mikoa nane iliyo katika hatari zaidi
Mafunzo ya waandishi wa habari 30 (media orientation)
Zoezi la udhibiti wa matukio ya dharura (simulation exercise) katika ngazi ya Taifa
Mafunzo kwa wasfirishaji wa sampuli kwenda katika maabara
Hitimisho
Nawaomba
Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wote nchini
kuchukua Tahadhari na kuendelea kuelimisha wananchi wote juu ya ugonjwa
huu na kuwataka kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua tahadhari za
kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa
kuugua ugonjwa huu hapa nchini.
Aidha
Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali katika kuimarisha
ufuatiliaji na kuendelea kutekeleza mikakati ya kudhibiti ili ugonjwa
huu usiingie nchini. Vilevile Wizara itaendelea kutoa taarifa pamoja na
Elimu kwa Jamii kadri itakavyohitajika.
Imetolewa na
Ummy A. Mwalimu (Mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto
10/08/2018
IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI.
Ijumaa, Agosti 10, 2018
-
Hakuna maoni
Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt
(katikati) akimsalimia mtoto mchanga aliyebebwa na baba yake katika
jengo la Kliniki ya Baba, Mama Na Mtoto. Kulia ni Waziri wa Áfya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisoma mbao ya matangazo katika Zahanati ya Tabata jijini Dar
es salaam pindi alipofika kupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo kutoka
nchi ya Uingereza.
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa Elimu juu ya
umuhimu wa kukata Bima ya Áfya kwa mtoto (Toto Afya Card) kwa mmoja kati
ya wazazi waliofika katika Zahanati ya Tabata kupata huduma za
matibabu ya mtoto.
Mshauri wa masuala Ya Afya kutoka ubalozi wa Uingereza
DKt. Gloria Ngaiza (wapili Kushoto) akimtafasiria Waziri wa Maendeleo
kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt kilichokuwa kikisemwa na
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tabata (Wakwanza Kushoto).Wa mwisho Kulia ni Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu.
IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI
Na WAMJW - DSM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imesema kuwa idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Afya za Kisasa za
uzazi wa mpango zimeongezeka nchini mpaka kufikia Asilimia 32.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu leo wakati alipoupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo
kutoka nchini Uingereza katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam
ukiwa na lengo la kutatua changamoto za Sekta ya Áfya hususani katika
huduma za Afya ya mama na mtoto.
"Kupitia
Msaada wao tumeweza kuongeza idadi ya wanawake wanaotumia huduma za
Kisasa za uzazi wa mpango, hatupo vizuri, tupo Asilimia 32, tumeweka
lengo itapofika 2020 tufikie Asilimia 45 ya wanawake walioolewa
wanatumia njia hizi" Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa, bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo
na uzazi nchini, takribani wanawake 556,000 katika kila vizazi hai laki
moja wanafariki na kwa mujibu wa Wataalam uzazi wa mpango utaweza
kuchangia Mpaka Asilimia 30 katika Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Pia
Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kwa
kutenga fedha za ndani katika kupambana na changamoto za sekta ya Áfya
ikiwemo kuajiri watumishi wa sekta ya Áfya jambo linalosaidia Kupunguza
changamoto hizo za vifo vya akina mama wajawazito na mtoto wachanga.
"Sisi
kama Serikali tumejiongeza, tumechukua hatua na kutenga rasilimali
fedha za ndani ikiwemo kuajili watoa huduma za afya, kuhakikisha Kwamba
tunatatua changoamoto hiyo " alisema Waziri Ummy.
Hata
hivyo Waziri Ummy aliishukuru Serikali ya Uingereza kupitia kwa Waziri
wa Maendeleo Mhe. Penny Mordaunt kwa kushirikiana na Serikali ya
Tanzania katika kuboresha huduma za afya hasa katika huduma za mama na
mtoto.
Kwa upande wake
Waziri wa Maendeleo kutoka Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameshukuru
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Áfya kwa kazi nzuri wanayoifanya
ya kuhudumia wananchi wa Tanzania na kuahidi kupeleka salamu za Tanzania
nchini Uingereza.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)








