Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 12 Septemba 2018

TENDER

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF HEALTH, COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER,
ELDERLY AND CHILDREN



TENDER No. ME/007/2018/HQ/G/113

FOR
PRINTING AND SUPPLY OF
REDESIGNED LOGISTICS SYSTEM FOR PUBLIC HEALTH COMMODITIES IN TANZANIA MAINLAND

Invitation for Tenders

Date: 10th September, 2018
1.      The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children has secured funds from Global Fund towards the cost of Implementation of the Health System Strengthening Program (HSS), and it intends to apply part of the proceeds of the funds to cover payments under the contract for Printing and Supply of Redesigned Logistics System for Public Health Commodities in Tanzania Mainland.

2.      The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children now invites sealed tenders from eligible Suppliers for Printing and Supply of Redesigned Logistics System for Public Health Commodities in Tanzania Mainland as follows:
Item No.
Item Description
Quantity
1
Logistics System – Standard Operating Procedure Manual.
8807
2
Logistics System – Facilitator’s Guide TOT Team.
300
3
Logistics System – TOT Participants Work book.
600
4
Logistics System – Facilitator’s Guide for Health Facilities.
600
5
Logistics System- Participants Work book for health facilities.
7500
6
Logistics Management Services – Standard Operating Procedure Manual.
1000
7
TB Facility Monthly Report Form – Triple carbonated.
5000
8
MDR TB Facility Monthly Report Form - Triple carbonated.
1000


TOTAL
24807

  1. Tendering will be conducted through the National Competitive Bidding procedures specified in the Public Procurement Act 2011 as amended 2016 and related Regulations, 2013 – Government Notice No. 446 as amended in 2016, and is open to all Tenderers as defined in the Regulations.
  2. Interested eligible Tenderers may obtain further information from and inspect the Tendering Documents at the office of the Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, University of Dodoma, Faculty of Social Science in Community Development, P. O Box 743, Dodoma, Building No. 11, 40478 Dodoma, Room 203, from 9.00-3.30 hrs. on Mondays to Fridays inclusive except on public holidays .
5.      Tender Document in English may be purchased by interested Tenderers on the submission of a written application to the address given under paragraph 4 above and upon payment of a non-refundable fee of Tanzania Shillings One Hundred Thousands Shillings Only (TZS. 100,000.00/=). Payment should either be by Cash or Banker’s Draft, or Banker’s Cheque, payable to Principal Secretary, Ministry of Health and Social Welfare, Bank of Tanzania, Account No. 9921145201.

6.      All tenders must be accompanied by a Bid Security or Bid Securing Declaration in the format provided in the Tendering Documents.

  1. All tenders in one original plus two copies, properly filled in, and enclosed in plain envelopes must be delivered to the Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children; University of Dodoma, Faculty of Social Science in Community Development, P. O Box 743, Dodoma, Building No. 11, 40478 Dodoma, Room 203, 1st Floor, before 11:00 hrs. on 24th September, 2018.

  1. Tenders will be opened thereafter in public and in the presence of Tenderers’ representatives who choose to attend in the opening at the Minister’s Conference Hall, Area D, Sengia Street at Ministry of Health, community Development, Gender, elderly and Children Offices, Dodoma.

9.      Late Tenders, Portion of Tenders, Electronic Tenders, Tenders not received, Tenders not opened and not read out in public at the tender opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.




Permanent Secretary,
Ministry of Health, Community Development,
Gender, Elderly and Children,
P.O Box 743, Dodoma,
Tanzania.




Jumanne, 11 Septemba 2018

WABUNGE WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI.

Kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa taarifa juu ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge jijini Dododma.

Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba akitoa Elimu Mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na Jitihada mbali mbali za kudhibiti ugonjwa huo katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Bi. Agatha Chikoti aliewai kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu na kupona kabisa akitoa ushuhuda  mbele ya Wabunge katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Mgeni rasmi ambae ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.


WABUNGE WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI.

Na WAMJW-DODOMA

Wabunge nchini wamehamasishwa kushiriki katika kuongoza juhudi za kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ambao unaonekana kuwa tishio kubwa.

Hayo yameelezwa na mbunge wa viti maalumu (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika uzinduzi wa mtandao wa wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Mhe.  Giga amesema kuwa ni wajibuwa kila mbunge nchini kuisimamia serikali ili ishughulikie kikamilifu tatizo la kifua kikuu kwa kutenga rasilimali za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

“Kifua kikuu kinaleta madhara kiafya na huongeza umasikini katika jamii, takribani watu 154,000 uugua kila mwaka na 27,000 ufariki duniani ikiwa ni sawa vifo 74 kwa siku, hii inaonesha ni jinsi gani ugonjwa wa TB ni hatari na hivyo juhudi za ziada zinahitajika ili kuutokomeza”. Amesema Mh. Giga.

Aidha Mh. Giga ameipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuweza kuchunguza na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa kifua kikuu na kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu bure na wanapona kabisa katika hospitali zote nchini.

Mh. Najma amesema kuwepo kwa mtandao wa wabunge wa kupambana na TB nchini (Parliamentary TB Focus) kutawezesha kufikia malengo ya kimataifa na kitaifa ya kutokomeza TB kwa kutambua kuwa ni janga la kitaifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara hiyo inatoa kipaumbele juu ya ugonjwa wa TB kwa kufanya juhudi kubwa ya kuutokomeza ugonjwa huu nchini ikiwemo kuweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209.

“Jambo ambalo tumelifanya kama serikali ni kujaribu kufanya utaratibu tofauti wa jinsi gani ya kufanya upimaji wa ugonjwa huu. Hadi hivi sasa tumeweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209 nchi nzima ambazo utoa majibu ndani ya masaa mawili”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amesema kuwa dawa zote zinazotibu kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu zinapatikana nchini na matibabu yake pamoja na vipimo vyote vinavyohusiana na ugonjwa wa TB yanatolewa bure.

Sambamba na hayo, Shuhuda Bi. Agatha Chikoti aliyewahi kuugua ugonjwa wa kifua kikuu ameiasa jamii kuacha kwenda kutafuta dawa za kienyeji na badala yake kwenda hospitali kupima na kupewa tiba sahihi.

Jumapili, 9 Septemba 2018

WANAUME WASISITIZWA JUU YA KUPIMA VVU.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wakazi wa Naipanga wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi wakati wa kilele cha Kampeni ya Furaha yangu iliyofanyika mkoani humo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipima Virusi vya Ukimwi wakati wa kilele cha kampeni ya Furaha yangu iliyofanyika katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.

Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati ajumjulia hali mkazi wa Nachingwea aliyejifungua wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya utoaji huduma  katika hospitali ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi .

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dawa zilizopo kwenye stoo ya kuhifadhia dawa wakati wa ziara yake ya kujua hali ya utoaji huduma za afya katika hospitali ya Wilaya ya Nachingwea mkoani lindi.

Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia akisikiliza taarifa ya Wilaya ya Nachingwea kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Rukia Mwango aliyesimama kushoto wakati wa ziara yake Wilayani humo Mkoa wa Lindi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akisikiliza maelezo kuhusu upimaji wa VVU kutoka kwa Muuguzi Mkunga Bi. Hidaya Nyenje Hospitali ya Nachingwea wakati wa Kilele cha kampeni ya Furaha yangu Wilayani humo.




Viongozi wa dini zote na Wazee  wa Naipanga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa kilele cha Kampeni ya Furaha yangu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.




WANAUME WASISITIZWA JUU YA KUPIMA VVU. 


Na WAMJW-NACHINGWEA

WANAUME Mkoani Lindi Wilaya ya Nachingwea wamesisitizwa juu ya masuala ya kupima virusi vya Ukimwi ili kujua hali ya maambukizi kwa wakazi wa mkoa huo. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kilele cha kampeni ya Furaha yangu leo katika Tarafa ya Naipanga wilaya ya Nachingwea Mkoani humo. 

"Kwa sasa Serikali imejipanga kutomomeza maambukizi ya Ukimwi kwani kila takayepima na kugundulika ana maambukizi ataanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi mara moja ili kufikia lengo la 909090 ifikapo mwaka 2020" alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa bado idadi ya wanaume wanaojitokeza kupima VVU ni ndogo hivyo kuwataka wanawake wawahimize waume na vijana wao wa kiume kujitokeza kutambu afya zao.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile aliutaka uongozi w Hospitali ya Wilaya ya Nchingwea kuboresha mazingira ya kutunzia dawa,  chanjo , damu na vitendanishi kwani bado havipo kwenye mpangilio mzuri wa kuhifadhi. 

"Kiukweli mazingira ya Hospitali sijayapenda hivyo nawapa onyo kwa mara ya mwisho na mchukue hatua haraka ya kuboresha mazingira yenu na hali ya utoaji huduma na kuhakikisha kila mtumishi awe Daktari au Muuguzi kujaza taarifa za mgonjwa kila anapomuhudumia kabla ya Serikali kuchukua hatua stahiki dhidi yenu" alisisitiza Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile alibainisha kuwa Serikali imeipatia Wilaya hiyo kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya hiyo ili kuweza kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Rukia Mwango amesema kuwa anayo furaha kusikia hali ya  maambukizi katika mkoa wao umepungua kutoka asilimia 3. 7 mpaka kufikia asilimia 0. 3. 
Aidha Bi. Mwango amesema kuwa wananachingwea hawana budi kujitokeza kupima VVU kwani maendeleo yao yataletwa na wananchi wenye afya njema na kujitambua kwa uchumi wa Nachingwea. 

Ijumaa, 7 Septemba 2018

DKT. NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA.

- Hakuna maoni
Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wagonjwa waliokua wanasubiri huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua maboksi ya sindano katika stoo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto akikagua kitabu cha taarifa mbalimbali za hospitali wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, kulia kwake ni katibu wa afya wa hospitali hiyo Mwanaisha Hassan
 
Naibu Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto akitoa maelekezo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mashine ya X Ray.

DKT. NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA. 

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kuhakikisha mashine ya kutolea huduma za X-ray  inafanya kazi ndani ya siku 14. 

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kuangalia na kujiridhisha na hali ya utoaji huduma za afya  katika Hospitali hiyo leo jijini Dodoma. 

"Ifikapo Septemba 21 nataka kuona mashine ya kutolea huduma za X-ray na vifaa vingne viwe tayari kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na maeneo yanayoizunguka kwani Hospitali hii ni tegemezi kwa wakazi wa mkoa huu la sivyo hatua stahiki zitachukuliwa bila ya kumuonea mtu haya" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha,Dkt. Ndugulile ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali hiyo kukarabati jengo la bima ya afya baada ya kukagua na kutoridhishwa na muonekano wake kwani linaleta kero kwa wateja wanaokwenda kupata huduma Hospitalini hapo. 

Mbali na hayo Dkt.  Ndugulile ameonekana kukerwa na uzembe  wa watendaji wa Hospitali  hiyo na kusababisha kuwakemea vikali na kuhaidi maagizo aliyoyatoa yasipotekelezwa kwa wakati hatua za kinidhamu zitakuchululiwa kwa vitendo.

Wakati huo huo dkt.Ndugulile ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwarudishia fedha wagonjwa walizotumia kununua dawa pamoja na sindano kwenye maduka yaliopo nje ya hospitali hiyo ilihali wana vifaa hivyo  takribani ya kutosha miezi sita kwenye stoo yao


Jumatano, 5 Septemba 2018

TAARIFA KWA UMMA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO






TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO TUMBO NCHINI

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Napenda kuwataarifu kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na OR -TAMISEMI imekuwa ikitekeleza zoezi la umezeshaji wa dawa za kingatiba dhidi ya magonjwa ya Kichocho na Minyoo ya tumbo kwa watoto walio na umri wa kwenda shule. Zoezi hili lilianza tangu mwaka 2005 kwa baadhi ya Halmashauri zenye maambukizi mengi na makubwa Zaidi ya magonjwa haya na baadae mwaka 2015, Serikali iliweza kuzifikia Halmashauri zote 184 nchini baada ya tafiti kuonyesha kuwa maambukizi yapo kila Halmashauri.

Ni vyema tukakumbuka kwamba nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania ikiwa ni mojawapo zimeridhia azimio Namba 66.12 la mwaka 2013 ambalo utekelezaji wake ni pamoja na udhibiti wa magonjwa ya kichocho na minyoo.



Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Waathirika wakuu wa ugonjwa wa Kichocho na Minyoo ya tumbo ni watoto wenye umri wa kwenda shule, yaani watoto wenye umri kati ya miaka 5 na 14, ambao wanakuwa katika shule za msingi.
Hivyo, kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Afya, inayohimiza kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali, Serikali hutoa dawa hizi za kingatiba ya kichocho na minyoo ya tumbo (Vidonge) walau mara moja kwa kila mwaka katika Halmashauri zote zilizoathirika. Kwa vile magonjwa haya yapo katika jamii na mazingira yetu, zoezi hili limekuwa ni endelevu kwa takribani miaka 13 sasa. Kwa mwaka 2018, Halmashauri zote nchini zimetekeleza zoezi hili kwa mafanikio makubwa, na kwa Mkoa wa Dar es salaam ndio unahitimisha zoezi hili kwa mwaka huu. (Jedwali la zoezi la ugawaji dawa shuleni 2018)

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazosambaa kupitia vyombo vya habari kama magazeti na mitandao ya kijamii inayozungumzia zoezi hilo la umezeshaji wa dawa hizi za kingatiba shuleni. Napenda kutoa ufafanuzi kwamba tunachotoa ni KINGATIBA na sio  CHANJO. Aidha dawa hizi  za kingatiba ni salama na zimethibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania( TFDA) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO). Aidha, dawa hizi (Praziquantel na Albendazole) pia zimesajiliwa kulingana na taratibu za nchi na mamlaka husika. Vile vile, dawa hizi zinazotumika katika zoezi hili zinatumika katika Hospitali na vituo mbali mbali nchini na hupatikana katika maduka ya dawa nchi nzima kwa maelekezo ya Madaktari.



Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Napenda kutoa maelezo kuhusu magojwa ya Kichocho na Minyoo ya tumbo kama ifuatavyo:
Minyoo ya Tumbo: Ipo ya aina tatu (3); Minyoo Mviringo (Round worms), Minyoo Mjeledi (Flat worms) na Minyoo safura (Hookworms). Maambukizi ya minyoo hii hutokea pale mtu anapokula mayai ya minyoo hiyo kutoka katika udongo (kupitia mbogamboga, matunda, au vyakula vingine vibichi ambavyo havijaandiliwa vizuri kwa kufuata kanuni za afya) au kwa mtu kuambukizwa minyoo hii kwa kupenya kwenye ngozi. Dalili za ugonjwa wa minyoo ya tumbo ni pamoja na tumbo kuuma, upungufu wa damu, udumavu, utumbo kujifunga, kukosa hamu ya kula, mwili kuchoka na hivyo kupelekea mahudhurio hafifu shuleni na mtoto kuwa na uelewa mdogo wa masomo.
Ugonjwa wa Kichocho: Husababishwa na minyoo jamii ya Schistosoma. Kuna aina mbili (2) za kichocho; kichocho cha kibofu cha mkojo (husababishwa na minyoo ya Schistosoma haematobium) na kichocho cha tumbo (husababishwa na minyoo ya Schistosoma mansoni). Maambukizi ya vimelea hivi hutokana na mtu kugusa maji yaliyotuama yenye vimelea hivyo. Vimelea hivi hujificha na kukua katika mwili wa konokono waishio katika maji yaliyotuama. Baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni damu kutoka kwenye mkojo na choo, kuvimba tumbo, na baadae inaweza kusababisha saratani ya kibofu cha mkojo, shinikizo la damu kwenye ini, kutapika damu, n.k.

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Zipo njia mbalimbali za kudhibiti maambukizi ya minyoo ya tumbo na kichocho ikiwemo utoaji wa elimu ya afya, utoaji wa dawa za kukinga na kutibu magonjwa haya, utumiaji sahihi wa vyoo, kuweka maeneo katika hali ya usafi na kula vyakula vilivyopikwa na kuiva vizuri.
Dawa za vidonge za Praziquantel ambayo ni kingatiba ya ugonjwa wa kichocho, na dawa ya Albendazole hutolewa ili kudhibiti ugonjwa wa Minyoo ya Tumbo. Dawa hizi hutolewa kwa watoto kwa kufuata kipimo cha urefu. Kipimo hiki kimehakikiwa na kinashabihiana na uzito wa mtoto husika na hutoa makadirio sahihi ya dozi inayohitajika. Zipo tafiti nyingi zilizohakiki kipimo hicho na kuonyesha kuwa ni kipimo sahihi kinachofaa kwa zoezi la kingatiba kwa watu wengi (Mass Drug Administration - MDA).
Zipo faida nyingi wanazopata watoto wetu kwa kumeza dawa hizi na baadhi ya faida hizo ni:
·        Kuua kabisa minyoo ya kichocho na minyoo ya tumbo
·        Kuboresha ukuaji wa mtoto
·        Kuongeza uelewa wa mtoto awapo shuleni
·        Kupunguza upungufu wa damu na unyemelezi wa magonjwa kama Malaria
·        Kuepusha athari zote za Minyoo na Kichocho mfano Kansa ya kibofu, presha ya ini n.k

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Napenda kuwafahamisha kwamba, kabla ya kuanza zoezi hili kuanza kutekelezwa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI kupitia kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Halmashauri husika walitoa mafunzo kwa waratibu wa afya na wa elimu wa Halmashauri zote. Aidha, uraghabishi (advocacy) kwa kupitia Kamati za Afya za Mkoa na Wilaya (PHC) pia ulifanyika.
Aidha, Halmashauri zote pia ziliandaa mafunzo rasmi kwa walimu wa shule za msingi na wataalamu wa afya wanaohusika na undeshaji wa zoezi hili.
Wanajamii pia wameendelea kuhamasishwa kushiriki kwa wingi katika zoezi hili kwa kupitia njia mbalimbali zinazofaa kwa sehemu husika. Masuala makuu ya hamasa yanahusisha kuandaa chakula ili watoto wapewe mlo kabla ya kumeza dawa na kushiba na kumeza dawa hizo ndani ya masaa 2 baada ya kupata chakula.

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Kama ilivyo kawaida kwa dawa nyingine yapo maudhi madogo madogo yanayoweza kujitokeza pale mtoto atakapomeza dawa hizo, hasa iwapo atameza bila ya kuwa na kitu chochote tumboni. Maudhi hayo ni kama yafuatayo:
·        kutapika,
·        kupata kizunguzungu,
·        kuharisha,
·        mwili kukosa nguvu.
Maudhi haya yatokanayo na dawa hizi yanaisha kwa muda mfupi na yanakabiliwa kwa kumpumzisha mtu sehemu tulivu na kumpatia maji. Maudhi haya yakiendelea baada ya masaa 24 tunashauri mtoto apelekwe kituo cha afya cha karibu yake.

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Napenda kuwathibitishia Watanzania kwamba tangu afua hii ianze kutumika hapa nchini kuanzia mwaka 2005 tumekuwa na mafanikio makubwa, ambayo ni pamoja na kushuka kwa kiwango cha maambukizi (Prevalence) ya ugonjwa wa kichocho na minyoo tumbo kutoka wastani wa asilimia 80 % (2005) hadi 30% (2018) katika maeneo mengi nchini, pia wingi wa maambukizi ya minyoo kwa mtoto mmoja mmoja umepungua sana ambapo hivi sasa ni chini ya asilimia 10 ya watoto walio na umri wa kwenda shule nchini ndio wanamaambuki makubwa ya kichocho na minyoo ya tumbo (High intensity).
Aidha, nia yetu ni kuendelea na afua hii ili hatimaye tuweze kuyatokemeza kabisa magonjwa haya nchini kwetu.

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Kwa kuhitimisha napenda kutoa wito kwa Wazazi na Wananchi kwa ujumla kushiriki katika mazoezi haya ya utoaji wa dawa za kingatiba. Mazoezi haya ni muhimu na endelelevu kwani magonjwa haya yanaathiri sana jamii yetu.
Nanyi wanahabari tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu magonjwa haya na umuhimu wa kingatiba. Dawa hizi huimarisha afya ya mtoto na hivyo kujenga taifa lenye afya bora na lenye nguvu ya kutosha ili kuleta maendeleo.

Aidha Ratiba ya Ugawaji dawa shuleni Mwaka 2018 ilikuwa kama ifuatavyo
Namba
Tarehe
Mikoa husika
1
APRIL, 2018
Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Geita, Rukwa, Katavi, Manyara, Singida, Pwani, Lindi, Mtwara, Tabora, Njombe, Iringa (14)
2
JULAI, 2018
Tanga, Ruvuma, Morogoro, Mbeya, Songwe (5)
3
AGOSTI 2018
Shinyanga, Mwanza, Mara, Kigoma, Simiyu, Kagera na Dar Es Salaam (7)

Ndugu Wananchi na Wanahabari,
Aidha, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inawataka wananchi kuzipuuza taarifa za upotoshaji zinazolenga kuharibu huduma za chanjo zilizotolewa hivi karibuni kwa njia ya Mitandao ya Kijamii kuwa chanjo zinazotolewa zina lengo la kuleta ugumba na kutozaa, na kwamba ni mpango mahususi wa nchi za Ulaya katika kupunguza idadi ya Waafrika duniani. Tunapenda kueleza kuwa taarifa kama hizi zilishawahi kutolewa tena huko nyuma na watu wasio na utaalamu wa masuala ya chanjo na wenye lengo chafu dhidi ya mafanikio ya chanjo nchini na duniani. Aidha ufafanuzi umekuwa ukitolewa mara kwa mara kuhusu upotofu wa dhana hii mbaya.
Wizara inawahakikishia wananchi kuwa Chanjo zinazotolewa nchini ni salama na zinathibitishwa na mamlaka zetu hapa nchini na Shirika la Afya Duniani na zina lengo la kuwakinga binadamu dhidi ya magonjwa hatari ya kuambukiza na si kuzuia mimba au kuleta ugumba.

Ndugu Wanahabari na Wananchi,
Faida za chanjo zinafahamika na mafanikio yake sote tumeyaona. Tunayo mifano mingi sana. Mmojawapo ni kwamba kwa kupitia afua ya utoaji chanjo Tanzania imefanikiwa kutokomeza na kuondoa magonjwa kama vile ndui, ugonjwa wa kupooza (Polio), Surua, na Ugonjwa wa pepopunda wa watoto wachanga. Sote tumeshuhudia kufungwa kwa wodi za wagonjwa wa Surua katika Hospitali zote; kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ugonjwa wa Kuhara kwa watoto n.k. Lengo la kutoa chanjo ni kuundaa mwili kupambana na magonjwa kwa kuuamushia kinga na ni mojawapo ya kinga mahususi dhidi ya magonjwa husika inayoaminika Duniani kote. Aidha, wote tumeshuhudia kupungua sana kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano hadi kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1000 na hivyo kufikia lengo la Maendeleo ya Milenia Namba 4 mwaka 2015.



Ndugu Wanahabari na Ndugu Wananchi,
Wizara inawataka wananchi kupata Taarifa sahihi kutoka Wizara ya Afya, na kuacha mara moja kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kupotosha jamii. Aidha, niwaombe Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kote nchini kuendelea kuelimisha wananchi juu ya faida za chanjo.  Pia Wizara inaviomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua dhidi ya watu wanaopotosha jamii na kuhatarisha usalama na afya za watanzania.

Imetolewa na:

Ummy A. Mwalimu (Mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto
04/09/2018