Jumatano, 10 Oktoba 2018
DKT. NDUGULILE AAGIZA KUBORESHWA KWA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKWIMU NCHINI
Jumatano, Oktoba 10, 2018
-
Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wadau mbali mbali wa
masuala ya Afya baada ya kufungua mkutano wa masuala mbali mbali ya Afya
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akifungua Mkutano wa Wadau mbali mbali wa
masuala ya Afya
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainabu
Chaula akiongea na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya katika mkutano
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Mkutano wa Masuala ya Afya, hususani
katika mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa Dawa, Vifaa tiba na
Vitendanishi Bw. Mavelle Tukai akiwakaribisha Wadau wa masuala ya Afya waliofika katika Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea jambo na Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa
nchini Bw. Laurean Bwanakunu, katikati ni Afisa mfamasia kutoka Wizara
ya Afya Siana Mapunjo.
Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya wakifuatilia kwa makini mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.
Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha)
DKT. NDUGULILE AAGIZA KUBORESHWA KWA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKWIMU NCHINI.
Na WAMJW - Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ameagiza kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa
Takwimu nchini utaosaidia upatikanaji wa takwimu sahihi na zinazifanana
katika taasisi zote.
Ameyasema
hayo mapema wakati akifungua Mkutano wa masuala ya Afya, hususani
katika mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa Dawa, Vifaa tiba na
Vitendanishi leo jijini Dar es salaam.
Dkt.
Ndugulile alisema kuwa Serikali inataka kuona mifumo yote ya ukisanyaji
Takwimu inaboreshwa mara moja huku akisisitiza kuwa mifumo hiyo ni
lazima iweze kuwasiliana jambo litalosaidia kupata Takwimu sahihi na
zinazofanana kwa mifumo yote.
"Tunataka
kuona mnaboresha mfumo wa ukusanyaji Takwimu, Takwimu bado ni
changamoto kubwa sana katika utoaji wa huduma za Afya na katika mfumo
mzima wa usambazaji, na ni lazima kuhakikisha kuwa mifumo hii
inawasiliana na inakuwa endelevu" Alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile amewaonya watumishi wa Serikali hususani
kutoka Wizara ya Afya wanaokwamisha mawazo endelevu yanayopelekea
kupiga hatua kwa Sekta ya Afya, na kuahidi kuwachukulia hatua endapo
yeyote atabainika kufanya hivo.
"
Muda wowote, mtu yeyote mwenye Mawazo mazuri na Endelevu kwaajili ya
Maendeleo ya Sekta yetu ya Afya, njoo unione Mimi au Waziri wangu,
milango yetu ipo wazi, wengine sisi hatuna urasimu, Serikali hii ya
awamu ya tano haitaki ubabaishaji" Alisema Dkt Ndugulile.
Aidha,
amewaagiza Waganga Wafawidhi wote nchini kuhakikisha wanaandaa orodha
ya Dawa zilizopo kila mwanzo wa wiki ili kusaidia kufahamu orodha ya
Dawa zilizopo na zinazohitajika kwa kipindi hicho, huku akisisitiza
kumchukulia hatua yeyote ataebainika.
"Tumepata
taarifa baadhi ya makampuni ya Dawa yanapita katika Hospitali zetu,
hususani Hospitali kubwa na wanawarubuni Madaktari wetu kuandika kwa MSD orodha ya Dawa ambazo hazipo katika mwongozo wetu wa Serikali,
tutachukua hatua Kali" Alisema Dkt Ndugulile.
Mbali
na hayo Dkt Ndugulile amepiga marufuku Madaktari wote nchini kuandika
Dawa kwa kutumia majina ya bishara na kuwataka kutumia majina ya asili
ya Dawa hizo.
"Jukumu la
Serikali sio kufanya Bishara ya kumtangazia mtu, mfano Panaldo sio jina
lake kitaalamu, ukienda baadhi ya nchi unaweza usikute Panaldo jina lake
halisi ni Parasetamo na ndio linatakiwa litumike" Alisema Dkt
Ndugulile.
Jumanne, 9 Oktoba 2018

MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE YANALETA ULEMAVU
Jumanne, Oktoba 09, 2018
-
Hakuna maoni
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa Jijini Mbeya.Kulia ni Ofisa mpango toka Wizara ya Afya Osca Kaitaba na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta.
Ofisa Mpango toka Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Osca Kaitaba akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Wataalam mbalimbali kutoka Sekratariet ya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi na wataalam wa Sekretariet na Mamlaka za Serikali wa Mkoa wa Mbeya.
Ofisa Mpango toka Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Osca Kaitaba akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Wataalam mbalimbali kutoka Sekratariet ya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi na wataalam wa Sekretariet na Mamlaka za Serikali wa Mkoa wa Mbeya.
Na WAMJW - Mbeya
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yamekuwa yakusumbua na kuleta athari kwa wananchi wa Mkoa wa mbeya hadi kusababisha ulemavu.
Hayo yamesemwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila katika ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Oktoba 9, 2018.
Alisema Magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri zaidi wananchi kwa kiasi kikubwa na kupunguza uwezo wa wananchi katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa taifa.
"Magonjwa haya, pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika pia yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili "alisema Mkuu huyo mkoa.
Aidha Chalamila alisema kwamba uwepo wa magonjwa hayo umefanya watoto kutokuwa na mahudhurio mazuri mashuleni kutokana na muda mwingi kutumika kwenye matibabu.
Hata hivyo alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa kingatiba za kukinga magonjwa hayo katika mkoa wa Mbeya.
"Hii ni kutokana na lengo la Serikali ya awamu ya tano ambalo ni kudhibiti magonjwa haya na hivyo kupunguza gharama kwa wananchi kwa kugawa kingatiba hizo"Alisisitiza Chalamila
Akielezea zaidi Chalamila alisema Mkoa wa Mbeya walikuwa wanakabiliwa na magonjwa yote matano ambayo ni minyoo ya tumbo, kichocho, matende na mabusha katika Wilaya zote ila kutokana na usimamizi na uhamasishaji nzuri Mkoa wake hivi sasa wamepunguza magonjwa hayo na hivyo kuwataka viongozi wa mkoa na Wilaya zake kuzidi kuhamasisha na kuelimisha zaidi wananchi kujitokeza kumeze kingatiba ili kutokomeza magonjwa hayo.
Aliyataja magonjwa yanayoendelea kuwa changamoto kwa Wilaya za Mkoa wa Mbeya ukiwemo ugonjwa wa Trakoma kwa Wilaya za Kyela, Chunya na Mbarali pamoja na ugonjwa wa usubi kwa Wilaya za Rungwe, Kyela na Busokelo.
Kwa upande wake Ofisa Mipango kutoka Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana. Oscar Kaitaba alisema semina hiyo imejumuisha wajumbe kutoka Halmashauri tatu za Mkoa wa Mbeya ambazo ni Rungwe, Kyela, Busokelo.
Aidha Bw. Kaitaba alitaja wajumbe hao kuwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Waweka Hazina za Wilaya, Waganga Wakuu Waratibu pamoja na Maafisa Usalama wa Wilaya.
Mwisho.
Jumatatu, 8 Oktoba 2018
Jumapili, 7 Oktoba 2018
WATANZANIA WAASWA KUPIMA MACHO MARA KWA MARA.
Jumapili, Oktoba 07, 2018
-
Hakuna maoni
Washiriki kutoka taasisi
mbalimbali za serikali na sekta binafsi wakiwa katika maandamano kuadhimisha
wiki ya afya ya macho yaliyofanyika jijini Dodoma mapema leo
|
Mganga Mkuu Wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe akisisitiza jambo katika
uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya afya ya macho uliofanyika katika viwanja vya
Nyerere jijini Dodoma mapema leo.
|
Jumamosi, 6 Oktoba 2018

WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUTOWASAHAU WATOTO KATIKA KUWAKINGA NA MAAMBUKIZI YA VVU.
Jumamosi, Oktoba 06, 2018
-
Hakuna maoni
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





