Menu bar
  • Habari
  • Makala
  • Ajira
  • Picha
  • Video
  • Mengineyo
    • Mifumo ya Afya
    • Vipeperushi
    • Kampeni za afya
Wizara ya Afya Tanzania

Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Ripoti Matumizi Mabaya

Kunihusu

Wizara ya Afya
Tazama wasifu wangu kamili

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

  • ▼  2021 ( 19 )
    • ▼  Juni ( 2 )
      • TAALUMA YA FAMASI NI MUHIMU KATIKA VITA YA NCD: Dk...
      • Mganga Mkuu wa Serikali afanya ziara Hospitali ya ...
    • ►  Mei ( 5 )
    • ►  Aprili ( 4 )
    • ►  Machi ( 1 )
    • ►  Februari ( 2 )
    • ►  Januari ( 5 )
  • ►  2020 ( 135 )
    • ►  Desemba ( 15 )
    • ►  Novemba ( 4 )
    • ►  Oktoba ( 5 )
    • ►  Septemba ( 5 )
    • ►  Agosti ( 8 )
    • ►  Julai ( 4 )
    • ►  Juni ( 14 )
    • ►  Mei ( 19 )
    • ►  Aprili ( 13 )
    • ►  Machi ( 15 )
    • ►  Februari ( 17 )
    • ►  Januari ( 16 )
  • ►  2019 ( 206 )
    • ►  Desemba ( 18 )
    • ►  Novemba ( 13 )
    • ►  Oktoba ( 7 )
    • ►  Septemba ( 13 )
    • ►  Agosti ( 22 )
    • ►  Julai ( 22 )
    • ►  Juni ( 11 )
    • ►  Mei ( 8 )
    • ►  Aprili ( 10 )
    • ►  Machi ( 21 )
    • ►  Februari ( 25 )
    • ►  Januari ( 36 )
  • ►  2018 ( 246 )
    • ►  Desemba ( 18 )
    • ►  Novemba ( 20 )
    • ►  Oktoba ( 25 )
    • ►  Septemba ( 14 )
    • ►  Agosti ( 18 )
    • ►  Julai ( 16 )
    • ►  Juni ( 20 )
    • ►  Mei ( 13 )
    • ►  Aprili ( 21 )
    • ►  Machi ( 33 )
    • ►  Februari ( 19 )
    • ►  Januari ( 29 )
  • ►  2017 ( 92 )
    • ►  Desemba ( 22 )
    • ►  Novemba ( 40 )
    • ►  Oktoba ( 30 )

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

  • SERA MPYA YA AFYA KUJIKITA ZAIDI KWENYE KINGA.
    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. @umwalimu akifungua Kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye lengo la kuwal...
  • TAARIFA KWA UMMA
    BARAZA LA WATAALAMU WA MAABARA LINATANGAZA RASMI KUANZA KWA MITIHANI YA USAJILI YA BARAZA KUANZIA MWAKA HUU 2018, HII NI KATIKA KUTE...
  • TRAVEL ADVISORY NO.6 OF 3RD MAY 2021
     

Pages

  • Home

Flickr Images

Jumamosi, 13 Oktoba 2018

UMEZAJI DAWA NDIYO SULUHISHO KAMILI KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE.

Jumamosi, Oktoba 13, 2018 - Hakuna maoni
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Christina Mndeme (aliyesimama) akisema jambo katika Semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyojumuisha Wakuu wa Wilaya pamoja wataalam mbalimbali toka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Ruvuma (hawapo pichani)

Kaimu Meneja wa Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbe Kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Oscar Kaitaba (aliyesimama) akiongea na washiriki wa Semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyojumuisha Wakuu wa Wilaya pamoja wataalam mbalimbali toka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Ruvuma (hawapo pichani)

Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Ruvuma Dkt. Charles Hinju (aliyesimama) akitoa mada katika Semina ya Uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa Viongozi wa Wilaya na Wataalam toka Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi pamoja na wataalam toka Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma wakisikiliza mada katika Semina ya Uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyofanyika katika Ukumbi wa Mipango Mkoani Ruvuma.

Na WAMJW - RUVUMA

Pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali na wadau mbalimbali katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, mwamko wa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kutumia kingatiba bado upo chini hivyo kukwamisha malengo yaliyokusudiwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme alipokuwa akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa Wakuu wa Wilaya pamoja na wataalam wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika katika ukumbi wa mipango Oktoba 13, 2018.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyataja magonjwa ambayo bado yanaendelea kusumbua wananchi mkoani humo kuwa ni; Usubi, Minyoo ya tumbo pamoja na kichocho huku akiwapongeza wataalam kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti magonjwa ya Vikope (trakoma), Matende pamoja na Mabusha.
Bi. Mndeme amesema kuwa sehemu kubwa ya jamii bado haijahamasika kumeza dawa kutokana na uelewa mdogo wa athari za magonjwa hayo huku wananchi wengi bado wakiwa na imani potofu juu ya dawa hizo.
“Magonjwa haya yamekuwa yakiathiri rika zote katika jamii, tumeona Watoto wakishindwa kwenda shuleni na kusababisha taaluma kushuka huku kwa watu wazima wakipata ulemavu wa kudumu hivyo kushusha nguvu kazi ya Taifa” alisema Bi Mndeme.
Naye Meneja wa Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Oscar Kaitaba, amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa magonjwa hayo yanadhibitiwa kikamilifu hivyo kuwaomba wataalam walioshiriki semina hiyo kusaidia Serikali katika kuelimisha na kuhamasiha jamii kutumia kingatiba ili kudhibiti magonjwa hayo.
“Njia bora ya kudhibiti magonjwa haya ni kuhakikisha wananchi katika maeneo tunayotoka wanakunywa dawa zinazopatikana katika hospitali zetu” Alisema Bwana Kaitaba.
Kwa upande wake Mratibu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Ruvuma Dkt. Charles Hinju amesema shughuli ya kuhamasisha wananchi kumeza kingatiba bado inaendelea kutolewa licha ya changamoto wanazokutana nazo.
“Kwa mwaka 2016 jumla ya watu 1,052,907 kati ya 1,420,317 walipata kingatiba sawa na asilimia 74 huku kwa mwaka 2017 watu 1,192,390 kati ya 1,413,751 walipata kingatiba sawa na asilimia 84.3” alisema DKt. Hinju.
Dkt. Hinju amezitaja changamoto za kuchelewa kwa dawa na rasilimali fedha kuwa zinaathiri ufanisi wa kazi huku pia Halmashauri nyingi hazitengi fedha ili kufanikisha kazi ya kukabiliana na magonjwa hayo.
Akifunga semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme ameishukuru Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuandaa Mpango huo wa kudhibiti magonjwa hayo na kuishauri Wizara kuandaa vipindi maalum kwenye vyombo vya habari ili kuhamasisha jamii kumeza dawa za kutibu magonjwa hayo huku akiwataka wataalam katika maeneo wanayotoka kuelimisha jamii kuachana na imani potofu juu ya dawa hizo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Waganga Wakuu wa Wilaya kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu wanaofika katika vituo vya afya na hospitali ili kusaidia katika maombi ya dawa toka bohari kuu ya dawa.

MWISHO

Alhamisi, 11 Oktoba 2018

TAARIFA KWA UMMA

Habari
Alhamisi, Oktoba 11, 2018 - Hakuna maoni
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TANGAZO KWA UMMA
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) anawatangazia watumishi wote waliopata udahili wa kusoma masomo ya Shahada ya Uzamili (Masters Degree) katika fani za Afya kwa mwaka 2018/2019, kwamba Wizara inaanza kupokea maombi ya Ufadhili kwa mwaka 2018/2019. Maombi haya yatawasilishwa kwa njia ya kielektroniki kwa kujisajili kupitia fomu zilizopo kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz (https://sponsorship.moh.go.tz).Maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yaliyowasilishwa kwa njia ya mfumo huu tu, hivyo waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya tangazo hili wanapaswa kurudia kuomba kupitia  utaratibu huu.

Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada ya mafunzo (Tuition fee), pamoja na posho ya utafiti  (Dissertation allowance). 

Vigezo vitakavyotumika kuchagua ni hivi vifuatavyo :

Kuwasilishwa kwa maombi rasmi ya ufadhili kwa njia ya mfumo (online application)
Mwombaji kuwa Raia wa Tanzania.
Awe amedahiliwa Chuoni kuanza masomo kwa mwaka wa kwanza 2018/2019
Kipaumbele kitatolewa kwa:
Watumishi wa Serikali waliomo kwenye sekta ya Afya wanaofanya kazi katika vituo vilivyoko Wilayani/Mikoani hususani katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambao baada ya mafunzo watarudi kuendelea kufanya kazi katika vituo vyao vya awali, au watapangiwa vituo vya kazi sehemu nyingine yeyote nchini
Waombaji waliodahiliwa katika fani ambazo ni za msingi katika utoaji wa huduma za rufaa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa. Nyanja hizo ni Anaesthisiology, Surgery, Neurosurgery, Obstetrics and Gynaecology, Orthopaedics Surgery, Emergency Medicine, Paediatrics, Internal Medicine, Critical Care in Nursing na Midwifery and Womens Health, Radio-pharmacy,Epidemiology and Lab.Management
Waombaji waliodahiliwa katika nyanja za Ubingwa/Ubingwa wa Juu (Specialities na Super-specialities) zenye umuhimu mkubwa katika Hospitali za Kitaifa (kama Cardiology, Nephrology,Opthalmology,Radiography na Oncology) ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi.


Aidha, mwombaji atatakiwa aambatanishe nyaraka zifuatazo wakati wa kufanya maombi:
Barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake
Barua ya udahili kutoka chuoni
Cheti cha taaluma
Cheti cha kuzaliwa



Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe  10/11/2018.  

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Chuo Kikuu Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii
S.L.P 743
DODOMA
11/10/20




WAGONJWA WA MACHO 300 NCHINI WAFANYIWA UPASUAJI NDANI YA SIKU TANO

Habari
Alhamisi, Oktoba 11, 2018 - Hakuna maoni
Mtaalam kutoka Taasisi inayojishugulisha na afya ya macho ONA  Bi. Haika Urasa kulia akitoa miwani ya kusomea kwa mmoja wa wakazi wa Dodoma aliyefika kupata huduma ya afya ya macho katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.

Mtaalamu wa magonjya yasiyoyakuambukiza Dkt. Nleminyanda Hezron katikati akitoa huduma za kupima sukari kwa baadhi ya wakazi wa Dodoma kupata huduma hizo katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.

MMoja ya Wataalam  wa Afya ya macho akitoa elimu juu ya afya ya macho kwa baadhi ya wakazi wa Dodoma waliofika  katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.


Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliofika  katika viwanja vya Nyerere Square  wakisubiri kupata huduma ya afya ya macho na magonjwa yasiyoyakuambukiza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.

NA WAMJW-DODOMA

Wagonjwa 300 waliobainika kuwa na matatizo ya macho wamefanyiwa upasuaji na kurejeshewa hali ya kuona vizuri ndani ya siku 5 ambapo watu wenye matatizo ya macho takribani 700 wamefanyiwa uchunguzi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mpango wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Bernadetha Shilio wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya siku ya afya ya macho duniani kilichofanyika mapema leo katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.

“Siku ya afya ya macho duniani ina lengo kuu la kuhamasisha utekelezaji wa dira ya kimataifa ya kutokomeza upofu unaozuilika ifikapo mwaka 2020, na kutathmini haki ya kuona kwa wote ambapo mwaka 2003 serikali ya Tanzania iliungana na mataifa mengine duniani katika kutekeleza azimio hilo”. Alisema Dkt. Shilio.

Dkt. Shilio amesema Serikali ya Tanzania inashirikiana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya afya ya macho ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii, kutoa huduma za uchunguzi wa macho pamoja na kufanya upasuaji kwa wagonjwa ambao watabainika kuwa na matatizo.

Pia Dkt. Shilio ameiasa jamii ya kitanzania kuzingatia kanuni sahihi za utunzaji wa macho ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza na kusababisha uono hafifu na kupelekea upofu.

“Matumizi ya rangi na kope bandia kwenye ukingo wa macho, kuvaa miwani bila kupima, kutumia dawa za mgonjwa mwingine wa macho bila ushauri wa daktari, kutokula vyakula bora vyenye virutubisho na kutokua na tabia ya kupima macho angalau mara moja kwa mwaka vimetajwa kuwa visababishi vikubwa vya kuathiri afya ya macho” alisema Dkt. Shilio.

Aidha, Dkt. Shilio amesema sambamba na huduma za macho pia kumekua na huduma za uchunguzi na ushauri kwa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dodoma, jumla ya watu 400 walifanyiwa vipimo vya sukari, shinikizo la damu na kiwango cha unene. Ambapo asilimia 3 wamekutwa na kiwango cha juu cha sukari, asilimia 47 wamekutwa na shinikizo la juu la damu na asilimia 50 wamekutwa na unene uliopitiliza kiwango.

Kwa upande wake Mgonjwa aliyepata huduma za macho Jijini Dodoma Bi.Veronica Maganga ameishauri serikali kuendelea kutoa elimu, kusogeza na kutoa huduma za macho na uchunguzi wa magonjwa mengine karibu na wananchi ili kuzuia magonjwa yanayoweza kuleta madhara iwapo hayatachunguzwa mapema na kutoa matibabu sahihi.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea huduma hii kwani wengi tumepata matumaini ya kuona tena kwa uono mkubwa ila wangefanya huduma hii iwe endelevu mpaka vijijini ili kuwanusuru wenye matatizo ya macho” alisema Bi. Veronica.


Jumatano, 10 Oktoba 2018

VIJANA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA ILI KUEPUKA ATHARI ZA AFYA YA AKILI

Jumatano, Oktoba 10, 2018 - Hakuna maoni
Mganga Mkuu wa Serikali  Prof. Mohamed Bakari Kambi  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati akitoa tamko la kuadhimisha siku ya afya ya akili ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Oktoba 10.

Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka hospitali ya Milembe Dodoma Dkt. Mwombeki akifafanua jambo juu ya magonjwa ya afya akili mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa tamko la kuadhimisha siku ya afya ya akili ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Oktoba 10.

Na WAMJW-DODOMA
Vijana wametakiwa kujiepusha na matumizi  ya madawa ya kulevya , makosa ya kimtandao, kucheza kamali na kukaa katika magenge ambayo yanaweza kupelekea kupata fikra mbaya zinazoweza kusababisha kuathirika kwa afya ya akili.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali  Prof. Mohamed Bakari Kambi  Jijini Dodoma wakati akitoa tamko la kuadhimisha siku ya afya ya akili ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Oktoba 10.
“Utumiaji wa mihadarati kuwa ni changamoto kubwa inayowakabili vijana katika mataifa yote pia utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe vimehusishwa kwa kiasi kikubwa na tabia hatarishi ya ngono zembe na ajali za barabarani” alisema Prof. Kambi.
Prof Kambi amesema kuwa  sambamba na elimu kwa Umma  Wizara itaendelea kutoa matibabu ya afya ya akili katika hospitali zote za Umma nchini pamoja na kuendelea kutoa dawa za Methadone kwa watumiaji wa madawa ya kulevya katika mikoa ya Dar es salaam,Mbeya,Mwanza na Dodoma  hivi karibuni.
Aidha Prof. Kambi amesema kutokana na tafiti za shirika la afya duniani (WHO) zinaonesha vijana wanaoathirika na kupata matatizo ya akili ni wale walio katika umri wa kuanzia miaka 14, lakini wengi wao hawapati nafasi ya kutambulika na kupata matibabu katika wakati muafaka.
“Tafiti za shirika la afya duniani (WHO) zinaonesha takribani nusu ya magonjwa yote ya akili huanzia katika umri wa miaka 14 ambapo magonjwa ya akili na matumizi ya vilevi ni miongoni mwa changamoto kubwa sana za kiafya na kiusalama zinazoathiri rika hili la binadamu”. Amesema Prof. Kambi.
Prof. Kambi amesema kuwa  kujiua kunaaminika kuwa ni chanzo kikuu cha pili cha vifo vyote vinavyowakabili vijana wengi duniani ambapo Ugonjwa wa Sonona (Depression) umetajwa kushika nafasi ya tatu duniani katika magonjwa yote yanayoathiri vijana duniani.
Kwa mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa Takwimu za mwaka 2015 hapa nchini zinaonesha  vijana kuanzia miaka  13 hadi 17 walioko katika shule za misingi na sekondari zinaonesha kuwepo na dalili za Sonona, ambapo vijana zaidi ya asilimia 7 walionyesha kuwa na dalili hizo
Kwa upande wake mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Milembe Dkt. Damas Andrew  kuwa  matatizo ya unywaji pombe na uvutaji wa sigara yalitaarifiwa kwa kiwango sawa cha asilimia 5, huku asilimia 3.1 wakiripotiwa  kuvuta bangi katika maisha yao huku utafiti huo ulionesha kuwa robo ya vijana wote waliohojiwa waliripoti kufanyiwa uonevu na wenzao.
“Vijana wote waliohojiwa waliripoti kufanyiwa uonevu na wenzao ama kwa kupigwa, kusukumwa au kufungiwa madarasani kunakopelekea kupata athari ya akili”. Amesema Dkt. Damas
Dkt. Damas amesema utafiti umeripoti kuwepo kwa matukio mbalimbali ya ukatili kwa vijana kutoka kwa wazazi na walezi yanayosababisha kuzorotesha ya akili kwa watoto na vijana wanaowalea. Vilevile kiwango kikubwa cha unyanyasaji kimeripotiwa kufanyika katika mitandao ya kijamii dhidi ya watoto na vijana na kufanya changamoto hizi kuathiri kwa kiasi kikubwa afya ya akili.

DKT. NDUGULILE AAGIZA KUBORESHWA KWA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKWIMU NCHINI

Picha
Jumatano, Oktoba 10, 2018 - Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya baada ya kufungua mkutano wa masuala mbali mbali ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifungua Mkutano wa Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.

Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula akiongea na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya katika mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam.

Kiongozi Mkuu wa Mkutano wa Masuala ya Afya, hususani katika mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi Bw. Mavelle Tukai akiwakaribisha Wadau wa masuala ya Afya waliofika katika Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea jambo na Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa nchini Bw. Laurean Bwanakunu, katikati ni Afisa mfamasia kutoka Wizara ya Afya Siana Mapunjo.

Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya wakifuatilia kwa makini mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha)


DKT. NDUGULILE AAGIZA KUBORESHWA KWA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKWIMU NCHINI.

Na WAMJW - Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameagiza kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa Takwimu nchini utaosaidia upatikanaji wa takwimu sahihi na zinazifanana katika taasisi zote.

Ameyasema hayo mapema wakati akifungua Mkutano wa masuala ya Afya, hususani katika mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi leo jijini Dar es salaam.

Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inataka kuona mifumo yote ya ukisanyaji Takwimu inaboreshwa mara moja huku akisisitiza kuwa mifumo hiyo ni lazima iweze kuwasiliana jambo litalosaidia kupata Takwimu sahihi na zinazofanana kwa mifumo yote.

"Tunataka kuona mnaboresha mfumo wa ukusanyaji Takwimu, Takwimu bado ni changamoto kubwa sana katika utoaji wa huduma za Afya na katika mfumo mzima wa usambazaji, na ni lazima kuhakikisha kuwa mifumo hii inawasiliana na inakuwa endelevu" Alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amewaonya watumishi wa Serikali hususani kutoka Wizara ya Afya wanaokwamisha mawazo endelevu yanayopelekea kupiga hatua kwa Sekta ya Afya, na kuahidi kuwachukulia hatua endapo yeyote atabainika kufanya hivo.

" Muda wowote, mtu yeyote mwenye Mawazo mazuri na Endelevu kwaajili ya Maendeleo ya Sekta yetu ya Afya, njoo unione Mimi au Waziri wangu, milango yetu ipo wazi, wengine sisi hatuna urasimu, Serikali hii ya awamu ya tano haitaki ubabaishaji" Alisema Dkt Ndugulile.

Aidha, amewaagiza Waganga Wafawidhi wote nchini kuhakikisha wanaandaa orodha ya Dawa zilizopo kila mwanzo wa wiki ili kusaidia kufahamu orodha ya Dawa zilizopo na zinazohitajika kwa kipindi hicho, huku akisisitiza kumchukulia hatua yeyote ataebainika.

"Tumepata taarifa baadhi ya makampuni ya Dawa yanapita katika Hospitali zetu, hususani Hospitali kubwa na wanawarubuni Madaktari wetu kuandika kwa MSD orodha ya Dawa ambazo hazipo katika mwongozo wetu wa Serikali, tutachukua hatua Kali" Alisema Dkt Ndugulile.

Mbali na hayo Dkt Ndugulile amepiga marufuku Madaktari wote nchini kuandika Dawa kwa kutumia majina ya bishara na kuwataka kutumia majina ya asili ya Dawa hizo.

"Jukumu la Serikali sio kufanya Bishara ya kumtangazia mtu, mfano Panaldo sio jina lake kitaalamu, ukienda baadhi ya nchi unaweza usikute Panaldo jina lake halisi ni Parasetamo na ndio linatakiwa litumike" Alisema Dkt Ndugulile.







Jumanne, 9 Oktoba 2018

MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE YANALETA ULEMAVU

Jumanne, Oktoba 09, 2018 - Hakuna maoni
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa Jijini Mbeya.Kulia ni Ofisa mpango toka Wizara ya Afya Osca Kaitaba na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta.
 Ofisa Mpango toka Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Osca Kaitaba akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Wataalam mbalimbali kutoka Sekratariet ya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya  uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi na wataalam wa Sekretariet na Mamlaka za Serikali wa Mkoa wa Mbeya.

Na WAMJW - Mbeya

Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yamekuwa yakusumbua na kuleta athari kwa wananchi wa Mkoa wa mbeya hadi kusababisha ulemavu.

Hayo yamesemwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila katika ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa  iliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Oktoba 9, 2018.

Alisema Magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri zaidi wananchi kwa kiasi kikubwa na kupunguza uwezo wa wananchi katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa taifa.

"Magonjwa haya, pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika pia yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili "alisema Mkuu huyo mkoa.

Aidha Chalamila alisema kwamba uwepo wa magonjwa hayo umefanya watoto kutokuwa na mahudhurio mazuri mashuleni kutokana na muda mwingi kutumika kwenye matibabu.

Hata hivyo alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa kingatiba za kukinga magonjwa hayo katika mkoa wa Mbeya.

"Hii ni kutokana na lengo la Serikali ya awamu ya tano ambalo ni kudhibiti magonjwa haya na hivyo kupunguza gharama kwa wananchi kwa kugawa kingatiba hizo"Alisisitiza Chalamila

Akielezea zaidi Chalamila alisema Mkoa wa Mbeya walikuwa wanakabiliwa na magonjwa yote matano ambayo ni minyoo ya tumbo, kichocho, matende na mabusha katika Wilaya zote ila kutokana na usimamizi na uhamasishaji nzuri Mkoa wake hivi sasa wamepunguza magonjwa hayo na hivyo kuwataka viongozi wa mkoa na Wilaya zake kuzidi kuhamasisha na kuelimisha zaidi wananchi kujitokeza kumeze kingatiba ili kutokomeza magonjwa hayo.

Aliyataja magonjwa yanayoendelea kuwa changamoto kwa Wilaya za Mkoa wa Mbeya ukiwemo ugonjwa wa Trakoma kwa Wilaya za Kyela, Chunya na Mbarali pamoja na ugonjwa wa usubi kwa Wilaya za Rungwe, Kyela na Busokelo.

Kwa upande wake Ofisa Mipango kutoka Mpango wa Kudhibiti  Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana. Oscar Kaitaba alisema semina hiyo imejumuisha wajumbe kutoka Halmashauri tatu za Mkoa wa Mbeya ambazo ni Rungwe, Kyela, Busokelo.

Aidha Bw. Kaitaba alitaja wajumbe hao kuwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Waweka Hazina za Wilaya, Waganga Wakuu  Waratibu  pamoja na Maafisa Usalama wa Wilaya.



Mwisho.

Jumatatu, 8 Oktoba 2018

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Jumatatu, Oktoba 08, 2018 - Hakuna maoni
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA MAJINA.

Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Nyumbani
Jisajili kwenye: Machapisho (Atom)

Facebook

MOHCDGEC

Tweets

Tweets by TwitterDev

Instagram



Matukio ya Nyuma

  • ▼  2021 (19)
    • ▼  Juni (2)
      • TAALUMA YA FAMASI NI MUHIMU KATIKA VITA YA NCD: Dk...
      • Mganga Mkuu wa Serikali afanya ziara Hospitali ya ...
    • ►  Mei (5)
    • ►  Aprili (4)
    • ►  Machi (1)
    • ►  Februari (2)
    • ►  Januari (5)
  • ►  2020 (135)
    • ►  Desemba (15)
    • ►  Novemba (4)
    • ►  Oktoba (5)
    • ►  Septemba (5)
    • ►  Agosti (8)
    • ►  Julai (4)
    • ►  Juni (14)
    • ►  Mei (19)
    • ►  Aprili (13)
    • ►  Machi (15)
    • ►  Februari (17)
    • ►  Januari (16)
  • ►  2019 (206)
    • ►  Desemba (18)
    • ►  Novemba (13)
    • ►  Oktoba (7)
    • ►  Septemba (13)
    • ►  Agosti (22)
    • ►  Julai (22)
    • ►  Juni (11)
    • ►  Mei (8)
    • ►  Aprili (10)
    • ►  Machi (21)
    • ►  Februari (25)
    • ►  Januari (36)
  • ►  2018 (246)
    • ►  Desemba (18)
    • ►  Novemba (20)
    • ►  Oktoba (25)
    • ►  Septemba (14)
    • ►  Agosti (18)
    • ►  Julai (16)
    • ►  Juni (20)
    • ►  Mei (13)
    • ►  Aprili (21)
    • ►  Machi (33)
    • ►  Februari (19)
    • ►  Januari (29)
  • ►  2017 (92)
    • ►  Desemba (22)
    • ►  Novemba (40)
    • ►  Oktoba (30)

Mifumo ya Afya

  • Rejista ya Vituo vya Afya (HFR)
  • Takwimu za MTUHA
  • Vyuo vya Afya

Huduma nyingine

  • Tovuti wizara ya Afya
  • Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
  • Bohari kuu ya Dawa
  • Programu ya kudhibiti UKIMWI kitaifa
  • Medical Council of Tanganyika

Wageni Waliojivinjari

Sparkline
© Hakimiliki 2017 Wizara ya Afya Tanzania. Imewezeshwa na Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Afya.