Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 14 Januari 2019

WAZIRI UMMY AKABIDHI MAGARI 10,PIKIPIKI 35 KWA LENGO LA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

Baadhi ya Pikipiki kati ya 35 na magari 10 yatayosambazwa katika mikoa mbali mbali, baada ya kukabidhiwa leo jijini Dar es salaam, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, kwa uongozi wa Mikoa kwaajili ya kwenda kusimamia, na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi waandamizi wa Mikoa mbali mbali waliokabidhiwa piki piki 35 na magari 10 leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu moja ya piki piki kati ya 35 zitakazosambazwa katika mikoa mbalimbali kwenye hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata ufunguo wa moja ya gari kati ya 10,yatakayosambazwa katika mikoa 10 ,hafla  ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye moja ya magari hayo kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.






Na WAMJW - DSM
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali nchini huku akisisitiza Serikali ya Awamu ya Tano imejikita kuboresha sekta ya huduma ya afya kwa Watanzania.

Magari na pikipiki amekabidhi leo Januari 14, 2019, Mwalimu amesema tukio hilo la kukabidhi rasmi Magari 10 na Pikipiki 35 kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo ni muhimu . 

"Kama mnavyofahamu bado nchi yetu inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukoma. TB ni hatari kwani inasababisha vifo, na Ukoma husababisha vifo na ulemavu wa kudumu. TB pia inaongoza kusababisha vifo vingi miongoni mwa wananchi wenye VVU," amefafanua Waziri Mwalimu.

Ameongeza kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB wapatao 154,000 ambao kati yao ni 44% (69,818) tu ndio waliogunduliwa. Changamoto kubwa ni jinsi ya kufikishia wananchi wote huduma za kufanya uchunguzi na upimaji pamoja na kuwapatia elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.

Ameongeza Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa inafanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa ugonjwa wa TB na kwamba mojawapo ya juhudi hizo ni pamoja na ununuzi wa mashine za kupima vinasaba vya Kifua Kikuu kitaalamu Gene-Xpert.

Ambapo zimeongezeka kutoka 64 mwaka 2015 hadi 210  Disemba 2018 na kufanya 85% (158/186)  ya Halmashauri zote nchini kuwa na  mashine hizi zinazoweza kupima TB kwa haraka na kwa ufanisi zaidi. 

"Mashine hizo hutoa majibu ndani ya saa 2 tofauti na kipimo cha Hadubini ambazho huto majibu baada ya saa 48. Lengo ni hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wilaya zote ziwe na mashine hizi. Kipimo hiki cha Gene-Xpert hutolewa bure," amesema.

Waziri Mwalimu amesema Serikali hiyo imepeleka huduma ya kifua kikuu sugu karibu kwa wananchi, huduma ambayo wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani ilikuwa inapatikana katika hospitali moja tu ya Kibong’oto lakini kwa sasa inapatikana katika vituo 81 katika mikoa 23. 

"Ni katika kuongeza juhudi hizi, Serikali kupitia Wizara imenunua magari 10 na pikipiki 35 tunazozikabidhi leo kwa lengo la kuhakikisha Waratibu hawa wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.

" Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538. Jumla ni  milioni 778. Mikoa inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa. 

"Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo ," amefafanua.

Pia amesema magari hayo na Pikipiki zinazokabidhiwa kwa uongozi wa mikoa vitasaidia katika usimamizi wa shughuli za Mpango, kuhakiksha wagonjwa wa TB na Ukoma wanapatiwa elimu, wanagunduliwa na kupatiwa matibabu.

 Amesema vyombo hivyo vitatumika kwa shughuli zinginezo za mikoa na wilaya zinazolenga kumfikishia huduma bora za afya mwananchi. Ametoa rai yake kwa uongozi wa Mikoa inayopatiwa vyombo hivyo vya usafirishaji vitumike kwa shughuli iliyokusudiwa kuimarisha huduma za Kifua Kikuu na Ukoma.

Amesisitiza vyombo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo na wanaamini kwamba Mikoa hiyo itaongeza kwa kasi ugunduzi wa wagonjwa wa Kifua Kikuu na kutokomeza ugonjwa wa Ukoma katika mikoa yenu. 

Ameongeza lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020 tunawaibua na kuwapatia matibabu asilimia 70 ya watu wanaougua TB kutoka asilimia 48 ya hivi sasa.

Waziri Mwalimu amesema kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma ni malengo ya Serikali kutokomeza ugonjwa huo katika Wilaya 20 zilizobakia ambazo ni Liwale, Mkinga, Nkasi, Lindi DC, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga Manispaa, Kilombero, Mafya, Pangani, Mvomero, Masasi, Chato, Mpanda TC, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Ulanga, Morogoro DC na Kilwa DC.

Ametumia nafasi hiyo shukurani kwa  Mfuko wa Dunia (GF – ATM) kwani, fedha hizo ni sehemu ya mfuko huu wa mzunguko wa 2018 – 2020.

Baadhi ya piki piki kati ya 35 na Magari 10 yatakayosambazwa katika mikoa mbalimbali, zilizokabidhiwa leo jijini Dar na Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo. 

Mikoa 10 inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa na Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo.

Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538

Jumapili, 13 Januari 2019

WAZIRI UMMY AWAONYA MADAKTARI...

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) akizungumza na watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati wa ziara yake ya Jimbo la Tanga 





watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya Jimbo la Tanga

Na WAMJW - TANGA

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali. 


Huku akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi. 

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao. 

Wananchi hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari. 

Akiwa kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie. 

“Kwa kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa zake. 

Alisema kwamba hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila wakati na kulazimika kwenda kununua 

“Mh Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na ghamara zinakwenda “Alisema Mussa. 

Alisema wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na hali yake ni mbaya. 

“Unapozungumzia jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema 

Naye kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwao. 

Awali naye mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara. 

Alisema kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa anafariki. 

“Kwa mfano Mh Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi wananchi tunaomba utusaidie “Alisema. 

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia hatua.

TFDA YAJIVUNIA KUIPAISHA TANZANIA KWAKUWA NA MIFUMO BORA YA UDHIBITI

Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bw.Adam Fimbo akizungumza na maofisa habari wa wizara na taasisi(hawako pichani) jinsi mamlaka hiyo ilivyokuwa na mifumo bora ya udhibiti na kuifanya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika katika kampeni ya "Tumeboresha sekta ya Afya"





Kaimu Meneja wa kitengo cha Maabara Micro Biology ya TFDA Catherine Luanda akiwaeleza jambo Maafisa Habari wa Wizara na Taasisi zake namna ya utendaji kazi katika maabara hiyo



Na WAMJW - Dar es Salaam

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema katika kipindi Cha Miaka mitatu imeweza kufanya mambo mbalimbali ya udhibiti wa usalama, ubora na usalama wa bidhaa za ndani na nje ya Nchi ikiwemo kutambulika kimataifa kwa kuzingatia  viwango vya Kimataifa vya ISO 9001: 2015.

Hii ni kutokana na mafanikio ya miaka mitatu ya utekelezaji wa kazi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA,  Bw. Adam Fimbo amebainisha hayo wakati akitoa ripoti ya miaka mitatu ya Mamlaka hiyo  wakati wa ziara maalum ya Maafisa Mawasiliano na habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

"Kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora,  usalama na ufanisi wa dawa, mnamo Mwezi Desemba 2018, TFDA imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vipodozi,  ambapo hatua  hii imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hii

Fimbo ameeleza kuwa, TFDA katika mikakati yake hiyo imeweka mifumo na taratibu za ndani za utoaji huduma na utendaji  bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ISO 9001:2015 kwa huduma za kawaida na ISO 17025:2005 kwa huduma za maabara. 

Aidha, ameongeza kuwa  huduma za TFDA hutolewa kwa kuzingatia viwango vya Mkataba wa Huduma Wateja kama ulivyorejewa mwaka 2016. 

"Mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18.

Pia tumesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara." Ameeleza Fimbo.

Aidha, Fimbo ameongeza kuwa TFDA  imekuwa ikifanya tathmini na usajili wa bidhaa kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko.

"Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.

Pia tumeweza kusajili maeneo ya biashara za bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kutambua maeneo ambayo bidhaa hizo zinazalishwa, kuhifadhiwa, kusambazwa na kuuzwa. Mfumo huu husaidia kuhakikisha kuwa maeneo husika yanakidhi vigezo ili kutoathiri usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa". Alieleza Fimbo.

Aidha ameongeza kuwa, TFDA katika kipindi cha miaka mitatu (2015/16 – 2017/18), imeweza kusajili jumla ya maeneo 25,630 ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na maeneo 9,000 yaliyosajiliwa mwaka 2016/17 na maeneo 5,606 mwaka 2015/16, hii ikiwa ni sawa na ongezeko la 60.5%.

 Aidha, katika kipindi hiki, TFDA imeendelea kushuhudia kufikiwa kwa dira yake ya kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja kujifunza mifumo iliyopo  na kwenda kuitekeleza nchini kwao.
 
(mfano nchi za Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh zinekuja kujifunza TFDA).

"Katika kipindi cha mwaka 2015/16 - 2017/18, Mamlaka imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mipango kazi yake.
  
Mamlaka katika kipindi cha 2017/18 itaendelea kutoa kipaumbele katika utekelezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi nane (8) yaliyomo katika Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano (5) yaani 2017/18 – 2021/22, ili kulinda afya ya jamii." Alieleza Fimbo.

Mafanikio mengine ni pamoja na kukamilika kwa jengo la Maabara na kufungwa kwa vifaa vya  kisasa vya uchunguzi  jijini Mwanza jambo ambalo limesaidia kusogeza huduma zaidi kwa jamii.

Jumamosi, 12 Januari 2019

NHIF YAJIVUNIA KUONGEZA WIGO WAKUWAFIKIA WANANCHI





Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi. Angela Mziray akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.  leo 11.1.2019, Makao makuu ya Mfuko huo Jijini Dar es Salaam

 Afisa wa kitengo cha Tehama Charles Madangi Charles akionesha namna ya mfuko wa kisasa unavyofanya kazi katika kitengo cha tehama

Msimamizi wa nyaraka wa NHIF, Erasto Msigwa akieleza namna mfumo huo unavyofanya kazi  wa kutunza kumbukumbu kwa njia ya kisasa

Sabrina Mponda wa kitengo cha CALL CENTER akitoa maelezo namna huduma wanayotoa ikiwemo kupokea simu zaidi ya 200 kwa siku katika kituo hicho ambapo wamefanikiwa kuwafikia watanzania mbalimbali

Kikao cha Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.


 
Na WAMJW, Dar es Salaam.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umejivunia kuongeza wigo wa wanufaika kwa kuwafikia  Wananchi mbalimbali  ikiwemo Wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika kwenye huduma ya Ushirika Afya na watoto kupitia huduma ya Toto Afya Kadi.  Mfuko pia umewezesha upatikanaji wa huduma za Madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa katika Hospitali hapa nchini.

Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Anjela Mziray wakati wa ziara maalum ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Wakiwa Makao Makuu ya NHIF, Maafisa hao waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Mfuko huo kujionea namna huduma zinazotolewa na Mfuko huo sambamba na mafaniko waliyofikia katika sekta ya Afya.

Awali akizungumza mambo mbalimbali Bi. Anjela Mziray aliwaeleza Maafisa hao kuwa Serikali inakusudia kuwafikia wananchi wote na huduma bora za afya. Katika kutekeleza hili Mfuko umewezesha Madaktari Bingwa wa magonjwa ya mbalimbali kama ya Wanawake, watoto, moyo, macho, kinywa na pua na mabingwa wa upasuaji kutoa huduma katika mikoa ya pembezoni kwa kipindi maalum.

"Kwa ujumla watu zaidi ya 20,289 wamefikiwa na huduma hii na kati ya hao watu 938 wamefanyiwa upasuaji wa kitalaam na hii ni katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Lindi, Mara, Manyara, Geita, Njombe na Ruvuma huku baadhi ya mikoa tukienda mara mbili” alieleza Bi. Anjela Mziray.

Aidha, katika mafaniko mengine ya kuboresha upatikanaji wa huduma, Mfuko unashiriki juhudi za Serikali za uwekezaji katika viwanda. Mfuko kwa kushirikiana na baadhi ya  taasisi zingine unawekeza katika kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za hospitali zitokanazo na malighafi ya pamba na kiwanda hiko kitajengwa Bariadi Mkoani Simiyu huku kikitarajiwa kuzalisha aina 24 za bidhaa hizo. Wadau wengine wanaoshiriki katika uwekezaji huu ni pamoja na Serikali ya mkoa wa Simiyu, WCF, TFDA, TBS, MSD, TIB, TIRDO na taasisi zingine.

Katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma, alieleza kuwa Mfuko kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani umenawezesha wamama wajawazito kupata bima ya afya ili waweze kupata huduma katika hospitali. Mpaka sasa wajawazito wapatao 1,044,000 wameshafikiwa na mpango huu katika mikoa ya Tanga, Mbeya, Njombe, Lindi na Mtwara.

Mfuko huo pia umeweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya Tehama inayowezesha kutambua wanachama katika vituo, kurahisisha ulipaji wa madai ya watoa huduma kwa wakati, kurahisisha usajili wa wanachama na kuharakisha utoaji wa vitambulisho.

Akizungumzia hili Meneja wa Mifumo ya Tehama Bw. Bakari Yahaya alisema kwa sasa mifumo inamwezesha  mwanachama kupata ujumbe mfupi kwenye simu yake mara tu kadi yake au ya mtegemezi wake inapotumika kwa matibabu. 

Mfuko huu sasa umefanikiwa kuwa na ofisi zake katika mikoa yote ikiwemo Tanzania Bara na Zanzibar huku wakiboresha mfumo wa mawasiliano  kwa kuwa na kituo cha huduma kwa wateja kwa ajili ya kupokea simu za wadau siku zote za juma bila malipo kwa wapigaji. Simu hiyo ni 0800 110063.

Akimalizia maelezo yake alisema, Mfuko umefanikiwa kupata cheti cha ubora wa huduma kwa viwango vya kimataifa ( ISO 9001:2015). "Katika hili tunajivunia kuimarika kwa huduma na ufanisi katika utekelezaji majukumu ya Mfuko kwa manufaa ya wadau wote wa Mfuko" alisema Bi. Mziray.
 
Mwisho.

Alhamisi, 10 Januari 2019

52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU - SERIKALI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wabunge na viongozi wa Wizara wakati wa kikao cha Bunge cha huduma za jamii, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwasilisha taarifa ya Mpango wa taifa wa kudhibiti Ukimwi katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (Wapili kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Mpango wa taiga wa kudhibiti Ukimwi ulofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge  wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Mpango wa taiga wa kudhibiti Ukimwi ulofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini Dodoma.

Wabunge na Viongozi wa wizara na baadhi ya taasisi zake wakiwa katika Kikao cha kamati ya Bunge ya huduma za jamii  kilichofanyika leo jijini Dodoma.


52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU

Na WAMJW-DOM
 
SERIKALI imesema kuwa Watanzania wapatao 2,405,296 hadi kufikia tarehe Oktoba 2018 walipima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya bunge ya huduma za jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma.

“Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2018, jumla ya watanzania 2,405,296 walikuwa wamepima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018” Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Miongoni mwa wote waliopima, wanaume walikuwa ni asilimia 44 huku wanawake wakiwa ni asilimia 56. Kati yao, watu 70,436 (2.9%) walikutwa na maambukizi ya VVU, ambapo wanaume 27,984  (2.6%) na wanawake ni 42,452 (3.2%).
  

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya UKIMWI namba 28 ya mwaka 2008 ili kupendekeza marekebisho yatayoruhusu upimaji Binafsi wa VVU (HIV Self-testing).

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kupunguza umri ya kupima VVU kwa ridhaa ya mzazi au mlezi kutoka miaka 18 hadi 15, hii ni kutokana na kasi ya maambukizi kuongezeka katika umri huo.

Pia, aliendelea kusema kuwa Wizara imeendelea kutoa huduma za Tohara ya Kitabibu kwa Wanaume kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume katika mikoa ya kipaumbele ambayo haina utamaduni wa kutahiri na ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU.  

“Hadi kufikia Septemba, 2018 Mikoa kumi na saba (17) inatoa huduma za Tohara ambayo ni Iringa, Njombe, Tabora, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Kigoma, Mara na Morogoro” Alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa Huduma ya tohara kwa wanaume bila malipo katika vituo vya huduma za afya na kupitia huduma mkoba ngazi ya jamii ambapo hadi kufikia Septemba 2018, jumla ya watu 3,702,387 wamefanyiwa tohara nchini ambao ni wanaume, vijana na watoto wa kiume.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Hadi kufikia mwisho wa Desemba 2018, Wizara iliweza kuwaandikisha katika huduma za tiba na matunzo watu wanaoishi na VVU wapatao 1, 087,382. Watu 68,927 waliandikishwa katika kipindi cha robo ya mwaka cha Juai hadi Septemba 2018 ambapo kati yao, 1,068,282 wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU, ambapo watoto walikuwa ni 58,908.

Idadi ya vituo vinavyotoa huduma na matunzo vimeongezeka hadi kufikia 6,206 Desemba 2018.  Sawa na asilimia 72.7 ya vituo vyote vya huduma za afya nchini. Miongoni mwa vituo hivyo, vituo kamili vinavyotoa huduma za tiba na matunzo ni 2,103 wakati vituo vinavyotoa huduma ya afya mama na mtoto (RCH) ni 4,103. 

MWISHO.

Jumatano, 9 Januari 2019

KARIBU DKT. CHAULA





Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkaribisha Katibu Mkuu Mpya wa Idara Kuu Afya Dkt.Zainab Chaula kwenye ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa

 Aliyekua Katibu Mkuu-Idara Kuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya akimkabidhi baadhi ya vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya Dkt.Zainab Chaula kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara jihini Dar es Salaam.




Waziri wa Afya,Maendekeo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza Katibu Mkuu mpua wa Wizara yake Dkt.Zainab Chaula(picha na Wizara ya Afy)

Picha ya pamoja ya Viongozi wa Wizara na baadhi ya watumishi waliopo ofisi ndogo ya wizara hiyo

Jumanne, 8 Januari 2019

WALIOHUJUMU UJENZI WA KITUO CHA AFYA MKILI WACHUKULIWE HATUA-DKT.NDUGULILE

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wakwanza kushoto) akikagua ramani ya jengo la kituo cha Afya Mkili, ikiwa ni mwendelezo wa Ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na kuhamasisha wananchi katika shughuli za kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua hali ya upatikanaji wa Dawa katika chumba cha Dawa katika kituo cha Afya Mkili kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma, pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Esabela Chilumba.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wakushoto) akikagua  uhifadhi wa Chanjo katika jokofu la kuhifadhia, katika kituo cha Afya Mkili, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na wanakijiji wa Mhagawa kwa pamoja wakishiriki katika zoezi la kuhamasisha ujenzi wa zahanati ya Mhagawa Asili iliyo katika Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile(wakwanza kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 50 ya sement ikiwa ni zoezi la kuhamasisha ujenzi wa zahanati ya Mhagawa Asili iliyo katika Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma.

Na WAMJW - NYASA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametoa wiki mbili na kuwaagiza Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwachukulia hatua Kali wabadhilifu wote waliohusika katika kuhujumu ujenzi wa kituo cha Afya Mkili kilichopo katika Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma.

Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo wakati alipokuwa katika ziara  ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya, uboreshaji wa miundombinu na uhamasishaji  kwa wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo yao wenyewe mkoani Ruvuma.

Dkt. Ndugulile alisema hatua Kali za haraka zitachukuliwa kwa yeyote aliyehusika kwa namna yoyote ile katika kukihujumu kituo hicho na kusisitiza kwamba  hatobaki salama," kituo ambacho kilikuwa moja kati ya vituo vya Afya vilivyopewa Fedha za ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa baadhi ya majengo ya Afya".Alisisitiza Dkt.Ndugulile.

"Ofisi ya Rais TAMISEMI wafuatilie hili na ndani ya wiki mbili kuanzia sasa ili Wizara ya Afya ipate taarifa hiyo ya nini kinachojiri, walichokibaini ni nini, hatua ambazo wanachukua na muendelezo wa ujenzi huu" alisema Dkt. Faustine ndugulile.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali hii haitomvumilia mtu yeyote anayecheza na Fedha za dawa, hivyo kumwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Majura Magafu kupitia vyanzo vyote vya mapato ambavyo Serikali inapata kupitia CHF, BIMA YA AFYA, na vyanzo vyote vya papo kwa papo kisha kuangalia matumizi yake ya Fedha.

"Matumizi mabaya ya Fedha za dawa, sasa hilo nalo linahitaji lichunguzwe, Rmo naomba hili lifanyiwe kazi haraka, mkapitie vyanzo vyote vya mapato ambavyo tunapata kupitia CHF, BIMA YA AFYA, na vyanzo vyote vya papo kwa papo na tuangalie matumizi ya Fedha yakoje" alisema Skt Ndugulile.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, huku akitoa maelekezo ujenzi Wa Hospitali hiyo uanze mara moja, huku akisisitiza kuwa utaratibu utaotumika ni wa Forced Account (mafundi wakawaida na wananchi kushiriki katika ujenzi ) jambo litakalosaidia kuokoa Fedha nyingi, zitazosaidia kuboresha sekta ya Afya.

"Tumeleta milioni 400, na tumeleta Bilioni 1.5, hizi fedha zipo, mkurugenzi wa halmashauri yuko hapa, na natoa maelekezo ndani ya muda mfupi ujenzi uanze, utaratibu ni kutumia mafundi, nyie wenyewe wa Nyasa mtajenga Hospitali yenu." Alisema Dkt. Ndugulile

Naye Mjumbe wa kamati ya ujenzi katika kituo cha Afya Mkili Bw.John Ngamanyika amemshutuma mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa Bw.Dkt Oscar Mbyuzi kwa upigaji wa pesa hizo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kumalizika kwa kituo hicho ambacho kilipewa na Serikali jumla ya shilingi Milioni 400 kwa ajili ya kuboresha kituo hicho.

"Mheshimiwa Naibu Waziri fedha zilizotengwa katika kituo cha Afya Mkili shilingi milioni 400, mimi nakuhakikishia zingetosha kabisa kumalizia majengo haya, , hapa kilichotawala ni wizi, na anayeongoza ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya" alisema Bw. John Ngamanyika.

Bw. John Ngamanyika aliendelea kusema kuwa  Mwenyekiti wa bodi ya kituo cha Afya pamoja na Katibu wake wameshikiliwa na polisi kwa wizi wa sementi na kwa sasa wanasubiri jarada lao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa uhujumu huo.

Mwisho.

Jumatatu, 7 Januari 2019

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WAKANDARASI UTEKELEZAJI MIRADI KATIKA SEKTA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII NCHINI.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Afya Afisa tabibu COTC Bw. Geoffrey Mdede wakati wakiwa katika chumba cha darasa chuoni hapo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua vyoo vya wanafunzi wa Chuo cha Afya Afisa tabibu COTC Songea wakati akiwa katika  ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Ruvuma

Wanafunzi wa Chuo cha Afya Afisa tabibu COTC Songea wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea taarifa ya hali ya utendaji katika chuo cha Afisa tabibu COTC Songea wakati akiwa katika  ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Ruvuma.


Kaimu Mkuu wa chuo cha Afisa tabibu COTC Songea akisoma taarifa ya utendaji wa chuo hicho mbele ya Naibu Waziri wa Afya, Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha) wakati  wa  ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Ruvuma.


Mkuu wa Wilaya ya Songea mhe. Pololeti Mgema akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile (hayupo kwenye picha) ili aweze kuzungumza na wanafunzi na uongozi wa chuo cha Afisa tabibu COTC Songea,


Na WAMJW - RUVUMA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Halmshauri zote nchini kutotumia wakandarasi katika kujenga miradi inayohusu Sekta ya Afya na Maendeleo  ya Jamii nchini, bali kutumia mtindo wa 'Forced Account' (kuwahusisha mafundi wa kawaida katika kujenga miradi hiyo)

Agizo hilo limetolewa mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na  kujionea ukarabati na ujenzi katika Chuo cha Wauguzi Songea na Chuo cha Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya  ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani hapo.

Dkt. Ndugulile amefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa baadhi ya majengo na ukuta wa Chuo cha Afisa tabibu (COTC - Songea) mkoani humo ambao unagharimu  zaidi ya Shilingi millioni 900 ambazo fedha hizo zingetumia mtindo wa 'Forced Account' zingejenga majengo mengi zaidi na ukuta.

Aidha, Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa katika zama hizi,  Serikali ya Awamu ya Tano itazingatia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya Maendeleo na Wizara itasimamia kwa karibu Miradi hiyo.

"Niseme tu ni marufuku kutumia wakandarasi katika kutekeleza miradi inayohusu Wizara hii niliyopo labda muyafanye haya wakati mimi sipo" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.Pololeti Mgema amemuahidi Naibu Waziri huyo kusimamia uendeshaji wa vyuo vyote  vilivyopo katika Wilaya yake kwa ukaribu.

Akitoa taarifa ya ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Wauguzi Songea Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Geoffrey  Mdede amesema Chuo kinakabiliwa na changamoto za miundombinu pamoja na  upungufu wa wakufunzi ambapo mpaka sasa kuna wakufunzi saba wanaofundisha jumla ya wanafunzi 105.

MWISHO.

Jumapili, 6 Januari 2019

WAZIRI MKUU AMWAGIZA NAIBU WAZIRI WA AFYA KUFUATILIA UHUJUMU WA JENGO LA MAMA NA MTOTO.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati aliponya ziara ya uzinduzi wa Mashine ya X- Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma wakati aliponya ziara ya uzinduzi wa Mashine ya X- Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma. Pembeni yake ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali mgonjwa  aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua mashine mpya ya X-ray aliyoizindua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile, anaefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mdeme.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashine ya X-ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile, wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe. Christina Mdeme, wapili kushoto ni Mbunge wa Songea Mhe. Damas Ndumbalo.


Na WAMJW - SONGEA

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  amemwagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kufuatilia uhujumu wa Fedha za ukarabati wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Ameyasema hayo jana wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuzindua X-Ray Mashine za kisasa katika Mkoa wa Ruvuma.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa Milioni 500 inajenga kituo kizima cha Afya, ambacho kina chumba cha uoasuaji'thieta', wodi ya mama na mtoto, jengo la wagonjwa wa nje,  nyumba ya Mtumishi, mochwari na kichomea taka, hapa jengo moja linalofanana na thieta ni Milioni 129 kule ni Milioni 70, hii haikubaliki hata kidogo.

'Waziri utabaki hapa, utafuatilia hiyo, tujue nani aliyeweka zabuni hiyo, tushughulike nae, hatuwezi kuruhusu hali hii, na tukiendelea hivi tutaharibu kila kitu, lazima tuelezane ukweli, Serikali tumetaka kuboresha sekta ya Afya, tumetafuta mfumo mzuri, tunafedha, na tunaendelea kujenga, sasa kuna watu wanaingia huko wanataka kutuharibia" alisema Mhe. Kassim Majaliwa.

Mbali na hayo Mhe. Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali huzipatia Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kiasi kisichopungua Milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa Dawa kila mwezi, huku akiwatoa hofu Wananchi kuwa Dawa zipo na zimefikia Asilimia 92.

"Kila mwezi, halmashauri chini kabisa inayopata Fedha za dawa pekee, sio chini ya Milioni 25 kwa mwezi, kwa miezi mitatu ni shilingi Milioni 75, na Fedha hizi zinakuja na wananunua dawa moja kwa moja, dawa  zipo, na zimefikia Asilimia 92℅ na kuendelea" alisema Mhe. Kassim Majaliwa.

Mhe. Kassim Majaliwa aliendelea kuwahasa Wasimamizi wote waliopo katika vituo vya Afya, kuhakikisha kuwa Dawa za matibabu zinatumiwa vizuri, na zitumike kwa kuwapa Wananchi waliopata maradhi 

"Leo nimeingia kwenye wodi ya watoto wadogo, nimekutana na mtu mmoja aliyekuwa na malalamiko ya dawa, inawezekana mtu, mmoja anataka kuwachafua wengi, kwasababu wote mnajua hapa dawa zipo na mgonjwa atapata Dawa' alisema Mhe. Kassim Majaliwa.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alitoa rai kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma juu ya masuala ya lishe, huku akiwahasa viongozi wa Mkoa kuhamasisha Wananchi ili wafahamu juu ya umuhimu wa Lishe bora.

" Nisisitize masuala ya Lishe, iwe ni ajenda ya kudumu, Mkoa wa Ruvuma unazalisha chakula kwa wingi, lakini sasa ndio unaongoza kwa matatizo ya utapiamlo, maana yake ni kwamba, hatujui namna ya kula" alisema Dkt. Ndugulile

Mwisho












Jumamosi, 5 Januari 2019

SERIKALI YAAHIDI KUTOA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA RUVUM

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua hali ya upatikanaji wa Dawa kwenye chumba cha kuhifadhia Dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine akimjulia hali mtoto aliyepelekwa kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua miguu bandia katika chumba cha kuhifadhia vifaa mbali mbali vya Hospitali, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua Dawa alizoandikiwa mgonjwa katika Wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua karatasi ya idadi ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.


Na WAMJW - SONGEA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya bora kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vifaa vyote vilivyoharibika vinatengenezwa na kuanza kufanya kazi mara moja.

Kwa upande mwingine ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatumia Fedha vizuri katika kufanya maboresho ya majengo ya Hospitali hiyo, ikiwemo kutumia Forced account katika ujenzi huo.

Pia, Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha kila mtoa huduma za Afya anaandika muda kwa usahihi aliomuhudumia mgonjwa kuanzia anapopokelewa, anapofanyiwa matibabu mpaka anapoandikiwa dawa jambo litalorahisisha kubaini mtenda kosa endapo mgonjwa atapata tatizo.

Aidha, Serikali imeahidi kuwapa gari la kubebea wagonjwa katika  Hospitali hiyo ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika endapo gari hilo litakuwepo ikiwemo vifo vya mama na mtoto.

Mbali Na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza Watoa Huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiwatia moyo kuwa Serikali inafahamu mchango wao na itaendelea kuboresha mahitaji yao.

#TunaboreshaAfya