Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 20 Januari 2019

SERIKALI YAIONGEZEA UWEZO JKCI





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar es salaam.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu katika Taasisi ya Moyo JKCI wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la watoto wenye magonjwa ya moy.



SERIKALI YAIONGEZEA UWEZO JKCI

Na WAMJW-DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeiongezea uwezo wa kutoa huduma Taasisi ya Moyo ya JKCI kwa kuimarisha jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba vitanda 32 kutoka vitanda 11 hapo mwanzo.

Ameyasema hayo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar es salaam.

“Katika jengo hili kulikuwa na msongamano mkubwa sana wa watoto, sasa hivi jengo hili likikamilika litakuwa na vitanda 32 kutoka vitanda 11, hivyo kulifanya jengo hilo kuwa na vitanda vya watoto tu” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa katika jengo hilo kutakuwa na Vyumba maalumu kwaajili ya Wagonjwa wanaohitaji huduma na uangalizi maalumu 15 (ICU) kwaajili ya watoto tu,  badala ya rika zote kupata huduma hiyo katika chumba kimoja, kama ilivyokuwa hapo mwanzo, jambo litalosaidia kuokoa maisha ya watoto wanaohitaji uangalizi maalum.

“kutakuwa na Vyumba maalumu kwaajili ya Wagonjwa wanaohitaji huduma na uangalizi maalumu 15 kwaajili ya watoto tu,  maana yake tutakuwa tumeokoa maisha ya watoto ambao wanahitaji uangalizi maalumu, kwasababu watoto wanaweza wakawa wanahitaji vyumba vya uangalizi maalumu lakini vyumba hivyo vikawa vimetumiwa na wakubwa” alisema Waziri Ummy.

Waziri ummy aliendelea kusema kuwa kutokana na ufinyu wa nafasi JKCI wanauwezo wa kuafanya upasuaji kwa watoto 20 kwa mwezi, hivyo kwa uwezo huu ambao umejengwa na Serikali kuu kwa kushirikiana na wafadhili Charity Baptism wataweza kufanya upasuaji kwa watoto 40 kwa mwezi kutoka watoto 20.

“Kutokana na ufinyu wa nafasi JKCI ilikuwa na uwezo wa kufanya upasuaji kwa watoto 20,  lakini kwa uwezo huu ambao tumeweza kujengewa na Serikali kuu kwa kushirikiana na wafadhili Charity Baptism wataweza kufanya upasuaji kwa watoto 40 kwa mwezi kutoka watoto 20” alisema Waziri Ummy.


Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhidhinisha kiasi cha Shilingi 500 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo ifikapo Januari 28.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, kitengo hicho kinachotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu, kimegharimu Sh2 bilioni ambazo fedha zingine Sh800 milioni zimetolewa na wafadhili Charity Baptism.

Mbali na hayo Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Hospitali zote na Vituo vya Afya kujiongeza kwa kufanya maendeleo yao wenyewe kwa wadau mbali mbali wa masuala ya Afya badala yakusubili kila kitu kufanyiwa na Serikali.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema mwaka 2018 JKCI ilifanya  oparesheni nyingi zaidi kwa watoto hivyo anategemea mwaka huu zitaongezeka zaidi, “Hii itakuwa wodi ya kwanza kwa ajili ya watoto pekee kwa Afrika Mashariki walio wengi wanachanganya watoto na wakubwa.”

Mkurugenzi Mtendaji JKCI Profesa Mohamed Janabi amesema kitengo hicho kipya kilichoanzishwa pembeni mwa jengo hilo kitakuwa na vitanda 32 kutoka 11 vya awali.

“Watoto walikuwa na vitanda 11 pekee lakini kwa sasa tutakuwa navyo 32 na vitanda vya ICU vitakuwa 15,” amesema Profesa Janabi

MWISHO.

Jumamosi, 19 Januari 2019

MOROGORO WATAKIWA WASIFICHE WAGONJWA WA UKOMA MAJUMBANI


Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro


Baadhi ya wakuu wa idara kutoka mkoa na wilaya wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa(hayupo pichani)ambapo wametakiwa kuhamasisha utekelezaji wa kuwaibua wagonjwa wa ukoma kutoka kila kaya ili kufanikisha malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Ukoma ifikapo mwaka 2020


Picha ya pamoja ya viongozi wa Mkoa, Wilaya,Wizara ya Afya na GLRA mara baada ya ufunguzi

Na.WAMJW,Morogoro

Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na halmashauri zake wametakiwa kutowaficha wagonjwa wenye ukoma majumbani ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa hadi ifikapo mwaka 2020.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari wakati wa ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uongozi  wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya mvomero kuhusu maadhimisho ya miaka sitini (60) ya Ushirikiano kati ya serikali na Shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania(GLRA) pamoja na siku ya ukoma Duniani itakayofanyika Kitaifa wilayani Mvomero mwishoni mwa mwezi huu
“Serikali inawajali sana wananchi wake hivyo  wananchi hampaswi kuwaficha wagonjwa majumbani kwani dawa na vipimo  zinatolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini” Alisema Tandari
Aidha, alisema kuwa mkoa wake utaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza  ugonjwa wa ukoma mkoani hapa  kwani wajibu wao ni kuwasaidia watu hao kupona na kurudi kwenye kazi zao za kila siku watu wagonjwa hao wakishapatiwa dawa wanapona kabisa.
Kwa upande wa ongezeko la wagonjwa wilayani  Mvomero Katibu Tawala huyo alisema sababu kubwa ya kuongezeka kwa wagonjwa hao wilayani hapo ni muingiliano hususan kwenye mashamba hivyo inakua rahisi maambukizi kuwa juu”tutafanya jitihada ili kuweza kufikia viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kutokomeza ugonjwa huu ambapo  malengo ni mgonjwa mmoja kati ya watu elfu kumi.
Naye Mratibu wa Taifa wa ugonjwa wa Ukoma kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Deus Kamara alisema kuwa zipo halmashauri 20 ambazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza ukoma nchini hivyo wizara kupitia mpango wa Taifa wa kutokomeza Kifua kikuu na Ukoma, Mikoa inatakiwa kutengeneza mkakati wa  kuwasaka,kuwafikia, kuwaibua na kuwaweka katika matibabu stahili pamoja na kuzifikia kaya zote zenye wagonjwa wa ukoma kwa kufanyiwa uchunguzi ili wale ambao hawajaugua kuwapatia  tiba kinga ili kutokomeza ukoma katika halmashauri zote ifikapo mwaka 2020.
Wakati huo huo Mwakilishii Mkazi wa Shirika la GLRA Buchard Rwamtoga alisema kuwa shirika hilo mwaka huu linatimiza miaka sitini(60) hapa nchini katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza ugonjwa wa ukoma Tanzania ikiwemo ya kuwajengea makazi bora familia 120 kutoka familia 739 ya watu waliougua ukoma hapa nchini
“Dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba kupitia michango ya wadau mbalimbali,shirika linaweza kusaidia mashirika na taasisi nyingine hasa mpango wa taifa wa kudhitibi ugonjwa wa kifua kikuu na Ukoma kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya”alisisitiza Rwamtoga.
Alitaja mafanikio waliyoyapata kwa miaka 60 Mwakilishi Mkazi huyo alisema shirika lake wameweza kutoa viatu maalum kwa walioathirika na ukoma pea 94,500 kwa watu 47, 250, miguu bandia magongo na baiskeli kwa watu 2, 655, magari 270 kwa Tanzania bara na Zanzibar,kusaidia masuala ya elimu kwa wanafunzi 3,765 pamoja na kuwezesha vikundi vya kusaidiana vipatavyo 50 vyenye wanachama 677 kwa familia za watu wenye kuishi na ugonjwa wa Ukoma nchini.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya ukoma mwaka huu ni “Tutokomeze ubaguzi ,Unyanyapaa na chuki dhidi ya waathirika wa Ukoma” na kitaifa yatafanyika kwenye kitongoji cha Chazi kijiji cha kigugu Wilayani Mvomero tarhe 27 mwezi huu.
-Mwisho-

Ijumaa, 18 Januari 2019

SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUPAA - SERIKALI

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Bw. Macha akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari wakati wa  wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakifuatilia tamko kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018 kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.


SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUPAA - SERIKALI
Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Sekta ya Afya nchini yaendelea kukua kwa kasi, kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Huduma kwa Wananchi zikiwemo upatikanaji wa Dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, huduma za chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto na Huduma za Dharura.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari na baadhi ya viongozi wa Wizara, kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Katika mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086, 930 walihudhuria na kuandikishwa Kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 Mwaka 2017, huku mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza wajawazito kuanza huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa, Katika kipindi cha mwaka 2018 jumla ya watoto 1,568,832 walizaliwa ikilinganishwa na Watoto 1,498,488 mwaka 2017, huku wakipatiwa huduma mbalimbali za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayowaathiri Watoto ikiwemo ugonjwa Kupooza, Kuharisha, Pepopunda, Pneumonia, homa ya ini na Surua.

"Katika kipindi cha mwaka 2018 hali ya chanjo kwa Watoto nchini imeendelea kuwa katika kiwango cha juu zaidi ya asilimia 85 ya kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kama inavyoonyeshaa katik hapa chini" Alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema mwaka 2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693 mwaka 2017, huku Katika kipindi cha miaka yote miwili 2017 na 2018, homa ya mapafu imeongoza kwa kusababisha vifo, ambapo kwa mwaka 2017,  imechangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 imechangia kwa asilimia 12.9 ya vifo vyote. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Mwaka 2018, ugonjwa usio wa kuambukiza (shinikizo la damu) umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo ambapo umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Hali ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini imeendelea kuimarika, hii ni kutokana na Serikali kuongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi milioni 251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka 2018/19.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa hali ya upatikanaji wa Damu Salama ambapo katika kipindi cha mwaka 2018, huku jumla ya chupa za damu salama 307,835 sawa na asilimia 85.5 ya lengo zilikusanywa ikilinganishwa na chupa 233,933 mwaka 2017, huku akiwahasa Wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji.

"Chupa zote 307,835 zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu pamoja na magonjwa makuu manne ambayo ni Ukimwi (HIV,) Homa ya Ini B na C (HBV, HCV) na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa 262,283 sawa na asilimia 85.3 zilikuwa salama na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu." Alisema Waziri Ummy. 

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa, katika mwaka 2018 jumla watu 47,967 waligundulika kuwa na vijidudu vya Kifua kikuu ikilinganishwa na wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka 2017., huku akisisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa Kifua Kikuu limeendelea kuwepo takribani mikoa yote nchini.

kwa upande mwingine, Waziri Ummya amesema kuwa, hadi kufikia Desemba 2018, jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilifikia 7,768 kutoka vituo 7,435 mwaka 2017 sawa na ongezeko la vituo 333 kwa mwaka, amedai kuwa Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma; Mashirika ya dini asilimia 12, Taasisi za Serikali asilimia 3 na vituo binafisi asilimia 15.
Sambamba na hilo, waziri Ummy amesema kuwa, hadi kufikia Desemba mwaka 2018, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na jumla ya wanachama 899,654 na ikihudumia jumla ya wanufaika 4,219,192 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote.
MWISHO.

Alhamisi, 17 Januari 2019

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA UJENZI WA MJI MPYA WA SERIKALI IHUMWA, DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Afya iliyo katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Afya wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, unaoendelea katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma, pembeni yake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa mkandarasi (hayupo kwenye picha) wakati akikagua Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Afya, unaoendelea katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma, katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, wakwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.


Picha ya baadhi ya majengo ya Wizara ya Afya yanayoendelea kujengwa  katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.


WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA UJENZI WA MJI MPYA WA SERIKALI IHUMWA DODOMA.

Na WAMJW - DOM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo amefanya ziara katika mji mpya wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ihumwa jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya shughuli za ujenzi ambazo zinatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Januari 2019,

Katika ziara hiyo Mhe. Majaliwa amemwagiza Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi, na kuongeza idadi ya wafanyakazi ili kuhakikisha anamaliza kazi yake ifikapo Januari 31, 2019 na kukabidhi kwa Wizara ya Afya ili waendelee na majukumu yao ya kuboresha Sekta ya Afya.

Aidha, amemwagiza Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kusimamia kikamilifu ujenzi wa jengo hilo kila siku ili kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika ndani ya muda waliokubaliana, kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.

"Mhe. Waziri hawa wanatakiwa kusimamiwa kila siku, hili ndio jengo lililochini, ukiondoa lile la Waziri Mkuu ambalo wameanza kazi jana, hili ndio lipo chini na ndio la wale wale Mzinga, Kamanda lisije lilakuahibisha hili" alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 

Mbali na hayo, Mhe. Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula na Wakurugenzi wa kuanza kufanya usafi katika maeneo yate ili kupendezesha mazingira ili wanapomaliza ujenzi wa jengo hilo na usafi uwe tayari ili shughuli ziendelee ndani ya muda.

JUMLA YA WAGONJWA 19 WAPANDIKIZWA FIGO NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati akiwasilisha  taarifa ya Wizara ya Afya, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya, uliofanywa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya, uliofanywa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Laurence Museru akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface akielezea jambo mbele ya kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, na baadhi kutoka Taasisi za Wizara wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Afya, uliofanywa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Wajumbe wa ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, Wakurugenzi wa Wizara, na  baadhi ya Taasisi zake,  wakijadili taarifa ya utendaji ya Wizara ya Afya katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

JUMLA YA WAGONJWA 19 WAPANDIKIZWA FIGO NDANI YA MIEZI 5

Na WAMJW - DODOMA
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi Desemba 2018 jumla ya wagonjwa 19 walipata huduma ya upandikizwaji wa figo, hivyo  kufikisha jumla ya wagonjwa 28 waliopata huduma hii toka Hospitali ilivyoanza kutoa huduma za kupandikiza figo mwezi Novemba 2017. 

Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Wizara ya Afya mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 2.24, ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa 28 nje ya nchi kupata matibabu yakupandikizwa figo.

"Gharama ya huduma hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kati ya shilingi milioni 20 mpaka 30 kwa mgonjwa mmoja wakati nje ya nchi gharama hii ni kati ya shilingi milioni 100 mpaka 120. Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 2.24 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu hayo nje ya nchi" Alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili iliona jumla ya wagonjwa 30,189, Idara ya Utengamano ilihudumia wagonjwa 22,379, huku Idara ya Madawa ilihudumia maombi ya dawa 519,216 na  Kitengo cha Figo kilitoa huduma za kusafisha damu kwa mizunguko 13,248, huku Jumla ya wagonjwa mahututi 960 walihudumiwa katika ICU za Hospitali. 

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Katika kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi Disemba 2018 Hospitali imetoa huduma za kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 11 na kufikisha jumla ya watoto 21 waliopata huduma hii toka ilipoanza mwezi Juni, 2017, jambo lililosaidia kuokoa  zaidi ya shilingi milioni  840 ambazo zingetibu watoto 21.

"Kabla ya hapo huduma hii ilikuwa inapatikana nje ya nchi kwa gharama kati ya shilingi milioni 80 mpaka 100 kwa mtoto mmoja, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili gharama nishilingi milioni 35 mpaka 40" alisema Waziri Ummy.

Wakati akijibu maswali ya Wabunge wa kamati hiyo  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Taasisi ya Moyo (JKCI) imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 211, kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watu wazima walikuwa 89 na watoto walikuwa 60, huku watu wazima 62 wenye matatizo kwenye mishipa ya damu walifanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu.

Aidha, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa, wagonjwa 521 walipatiwa matibabu ya upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa upande wa mtambo maalum (catheterization laboratory).

Mwisho.

Jumatano, 16 Januari 2019

SERIKALI YABAINISHA VIPAUMBELE MUHIMU KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI






Picha Mbalimbali zikionesha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile, Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula, Wabunge na Wajumbe mbalimbali wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakiwa katika kikao cha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Desemba, 2018 katika ukumbi wa bunge wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imebainisha maeneo muhimu yaliyowekewa kipaumbele katika bajeti  ili kuboresha miundombinu na hali ya upatikanaji wa Huduma za afya nchini.

Akieleza taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba 2018 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jana jijini Dodoma. Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Mh. Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo iliidhinishiwa na Bunge kupokea na kutumia bajeti ya jumla ya shilingi 866,233,475,000 ambapo Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 304,473,476,000 ilikua ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo shilingi 88,465,756,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 216,007,720,000 kwa ajili ya Mishahara ya watumishi walio makao makuu ya Wizara pamoja na Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Waziri Ummy amesema fedha zilizopokelewa katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2018 zimeainishwa katika utekelezaji wa majukumu ya wizara katika kipindi hicho ambapo maeneo muhimu kama Chanjo, afya ya mzazi na mtoto, mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, upatikanaji wa damu salama, uimarishaji wa huduma za kibingwa, Utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali za Kanda, Maalum, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na uhakiki ubora wa huduma za afya yalipewa kipaumbele.


Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu shughuli zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa na Taasisi zilizopo chini yake. Taasisi hizo ni pamoja na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Mabaraza ya Kitaaluma.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika utekelezaji wa Majukumu ya Wizara (Idara Kuu ya Afya), Waziri Ummy amebainisha changamoto mbalimbali zikiwemo Vituo vya kutolea huduma za Afya kutowasilisha mahitaji ya dawa, Vifaa, Vifaa tiba na Vitendanishi kwa wakati, Upatikanaji wa Huduma Bora na za Uhakika za Uzazi, Mama na Mtoto, Upungufu wa watumishi wenye taaluma ya kutoa huduma za afya ikilinganishwa na mahitaji, Wigo mdogo wa wananchi walio katika mifumo ya Bima za Afya pamoja na Kuongezeka kwa watu wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza.


 







Jumatatu, 14 Januari 2019

DKT. ZAINAB ATINGA OFISI KUU, WIZARA YA AFYA JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akipokea nyaraka za makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ulisubisya Mpoki leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akiteta jambo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma, katika kikao na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya.

Kikao chaWakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya kikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakimpokea Katibu Mkuu mpya Dkt. Zainab Chaula leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma,

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi baada ya Kikao cha kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakwanza Kushoto) akibadilishana mawazo na  Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Watatu kulia) pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya, Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi, pamoja na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya baada ya kikao kifupi cha ukaribisho wa Dkt. Chaula.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, akiwaonesha namna ya ufuatiliaji ili kuboresha Ujenzi wa Mji mpya wa Serikali Ihumwa wakati alipotembelea ujenzi wa TAMISEMI ili kujifunza, Wakwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima, anaefuata ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi na Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi pamoja na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Mbanga.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula pindi walipokutana kwenye ziara ya kutembelea ujenzi wa Wizara ya Afya katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.

Ujenzi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ukiendelea kwa kasi katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.

DKT. ZAINAB ATINGA OFISI KUU, WIZARA YA AFYA JIJINI DODOMA.

Na WAMJW - DODOMA
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na Wakurugenzi wa idara na  Wakuu wa Vitengo wa wizara hiyo tangu alipoapishwa siku chache kushika nafasi hiyo, akitokea TAMISEMI.

Katika kikao hicho Dkt. Chaula amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi hiyo, huku akihimiza kila mmoja kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa weledi ili kulinda taaluma zao. "Tujiandae kufanya kazi kama timu moja katika kutekeleza sera na miongozo ya sekta ya afya na kuhakikisha dhamana tuliyopewa tunaitumikia kadri inavyowezekana".Alisisitiza Dkt.Chaula

Hata hivyo Dkt.Chaula alimshukuru Katibu Mkuu aliyeondoka Dkt.Mpoki Ulisubisya kwa mifumo mizuri aliyoiweka na kuahidi kuendeleza kwa kuanza na changamoto zilizopo.

Aidha,aliwataka wakurugenzi hao kutimiza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa kujituma, huku akiwatoa hofu kuwa ofisi yake iko wazi muda wote na yeyote mwenye wazo zuri la kujenga asisite kumuona, kwani lengo ni kuboresha Sekta ya Afya

"uwezo wa kufanya kazi tunao hivyo.mabadiliko ni vitendo, tufanye kazi kwa matokeo". Alisema Dkt. Chaula 

Wakati huo huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ametembelea ujenzi wa mji mpya wa Serikali Ihumwa na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Afya.

DKT. NDUGULILE AITAKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA KUANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitembelea eneo la kuchoma taka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya alipoitembelea kuona hali ya utoaji wa huduma za afya. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Ibenzi Ernest.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dripu aliyowekewa mgonjwa (hayupo pichani) wakati alipotembelea Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua daftari la kutunza kumbukumbu za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipotembelea Hospitali hiyo kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya. Kulia ni muuguzi wa zamu Mary Shayo akitoa ufafanuzi.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua jalada aliloandikiwa mgonjwa kwenda kununua dawa nje ya Hospitali.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kupata huduma mbalimbali za afya.
Na. WAMJW DODOMA

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuhakikisha inaanza kutoa huduma za kibingwa ili iendane na hadhi ya kuwa hospitali ya rufaa.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo katika kikao cha majumusho ya ziara aliyoifanya hospitalini hapo mbele ya viongozi na watumishi wa Hospitali hiyo baada ya kuona maagizo aliyoyatoa katika ziara ya kushtukiza aliyoifanya mwezi Septemba mwaka jana yametekelezwa.

“Tunataka huduma nyingine zisizohitaji rufaa zianze kutolewa katika vituo vingine badala ya kuleta kesi zote katika Hospitali ya rufaa ya mkoa, kesi zinazotakiwa kufika hapa ni zile zilizoshindikana katika hospitali za wilaya zote”. Amesema Dkt. Ndugulile.
 
Kufuatia hatua hiyo ameitaka hospitali hiyo kuacha kutibu kesi za magonjwa madogo madogo kama Malaria, kuharisha na mengineyo badala yake yakatibiwe katika hospitali za wilaya na vituo vya afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema mfumo wa rufaa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo bado haujakaa vizuri kutokana na wingi wa wagonjwa walioko wodini hususani jengo la mama na mtoto ambao wengi wao hawahitaji huduma za kibingwa.

“ Nilikua nasikiliza takwimu tulipopita jengo la mama na mtoto naona bado mfumo wa rufaa haujakaa vizuri, ilitakiwa sehemu ya mzigo huu ianze kubebwa na vituo vingine vya afya ikiwepo kituo cha afya cha Makole, hapa zije kesi ambazo ujauzito wa mama umeshindikana au kuhatarisha maisha ndiyo waje hapa”.

Ili kuepuka hali hiyo, Naibu waziri huyo amesema serikali imeanza kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo ambapo hospitali za wilaya 67 zinatarajiwa kujengwa nchini kote, katika mkoa wa Dodoma itajengwa Hospitali ya wilaya ili iweze kusaidia kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa ya kawaida.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest amempongeza Naibu Waziri kwa kuitembelea hospitali hiyo mara kwa mara na kumuhakikisha huduma za afya zinatolewa katika ubora unaohitajika kukidhi vigezo vilivyowekwa na serikali ili kuwaridhisha wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

WAZIRI UMMY AKABIDHI MAGARI 10,PIKIPIKI 35 KWA LENGO LA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

Baadhi ya Pikipiki kati ya 35 na magari 10 yatayosambazwa katika mikoa mbali mbali, baada ya kukabidhiwa leo jijini Dar es salaam, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, kwa uongozi wa Mikoa kwaajili ya kwenda kusimamia, na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi waandamizi wa Mikoa mbali mbali waliokabidhiwa piki piki 35 na magari 10 leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu moja ya piki piki kati ya 35 zitakazosambazwa katika mikoa mbalimbali kwenye hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata ufunguo wa moja ya gari kati ya 10,yatakayosambazwa katika mikoa 10 ,hafla  ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye moja ya magari hayo kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.






Na WAMJW - DSM
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali nchini huku akisisitiza Serikali ya Awamu ya Tano imejikita kuboresha sekta ya huduma ya afya kwa Watanzania.

Magari na pikipiki amekabidhi leo Januari 14, 2019, Mwalimu amesema tukio hilo la kukabidhi rasmi Magari 10 na Pikipiki 35 kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo ni muhimu . 

"Kama mnavyofahamu bado nchi yetu inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukoma. TB ni hatari kwani inasababisha vifo, na Ukoma husababisha vifo na ulemavu wa kudumu. TB pia inaongoza kusababisha vifo vingi miongoni mwa wananchi wenye VVU," amefafanua Waziri Mwalimu.

Ameongeza kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB wapatao 154,000 ambao kati yao ni 44% (69,818) tu ndio waliogunduliwa. Changamoto kubwa ni jinsi ya kufikishia wananchi wote huduma za kufanya uchunguzi na upimaji pamoja na kuwapatia elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.

Ameongeza Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa inafanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa ugonjwa wa TB na kwamba mojawapo ya juhudi hizo ni pamoja na ununuzi wa mashine za kupima vinasaba vya Kifua Kikuu kitaalamu Gene-Xpert.

Ambapo zimeongezeka kutoka 64 mwaka 2015 hadi 210  Disemba 2018 na kufanya 85% (158/186)  ya Halmashauri zote nchini kuwa na  mashine hizi zinazoweza kupima TB kwa haraka na kwa ufanisi zaidi. 

"Mashine hizo hutoa majibu ndani ya saa 2 tofauti na kipimo cha Hadubini ambazho huto majibu baada ya saa 48. Lengo ni hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wilaya zote ziwe na mashine hizi. Kipimo hiki cha Gene-Xpert hutolewa bure," amesema.

Waziri Mwalimu amesema Serikali hiyo imepeleka huduma ya kifua kikuu sugu karibu kwa wananchi, huduma ambayo wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani ilikuwa inapatikana katika hospitali moja tu ya Kibong’oto lakini kwa sasa inapatikana katika vituo 81 katika mikoa 23. 

"Ni katika kuongeza juhudi hizi, Serikali kupitia Wizara imenunua magari 10 na pikipiki 35 tunazozikabidhi leo kwa lengo la kuhakikisha Waratibu hawa wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.

" Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538. Jumla ni  milioni 778. Mikoa inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa. 

"Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo ," amefafanua.

Pia amesema magari hayo na Pikipiki zinazokabidhiwa kwa uongozi wa mikoa vitasaidia katika usimamizi wa shughuli za Mpango, kuhakiksha wagonjwa wa TB na Ukoma wanapatiwa elimu, wanagunduliwa na kupatiwa matibabu.

 Amesema vyombo hivyo vitatumika kwa shughuli zinginezo za mikoa na wilaya zinazolenga kumfikishia huduma bora za afya mwananchi. Ametoa rai yake kwa uongozi wa Mikoa inayopatiwa vyombo hivyo vya usafirishaji vitumike kwa shughuli iliyokusudiwa kuimarisha huduma za Kifua Kikuu na Ukoma.

Amesisitiza vyombo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo na wanaamini kwamba Mikoa hiyo itaongeza kwa kasi ugunduzi wa wagonjwa wa Kifua Kikuu na kutokomeza ugonjwa wa Ukoma katika mikoa yenu. 

Ameongeza lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020 tunawaibua na kuwapatia matibabu asilimia 70 ya watu wanaougua TB kutoka asilimia 48 ya hivi sasa.

Waziri Mwalimu amesema kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma ni malengo ya Serikali kutokomeza ugonjwa huo katika Wilaya 20 zilizobakia ambazo ni Liwale, Mkinga, Nkasi, Lindi DC, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga Manispaa, Kilombero, Mafya, Pangani, Mvomero, Masasi, Chato, Mpanda TC, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Ulanga, Morogoro DC na Kilwa DC.

Ametumia nafasi hiyo shukurani kwa  Mfuko wa Dunia (GF – ATM) kwani, fedha hizo ni sehemu ya mfuko huu wa mzunguko wa 2018 – 2020.

Baadhi ya piki piki kati ya 35 na Magari 10 yatakayosambazwa katika mikoa mbalimbali, zilizokabidhiwa leo jijini Dar na Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo. 

Mikoa 10 inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa na Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo.

Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538

Jumapili, 13 Januari 2019

WAZIRI UMMY AWAONYA MADAKTARI...

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) akizungumza na watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati wa ziara yake ya Jimbo la Tanga 





watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya Jimbo la Tanga

Na WAMJW - TANGA

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali. 


Huku akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi. 

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao. 

Wananchi hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari. 

Akiwa kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie. 

“Kwa kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa zake. 

Alisema kwamba hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila wakati na kulazimika kwenda kununua 

“Mh Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na ghamara zinakwenda “Alisema Mussa. 

Alisema wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na hali yake ni mbaya. 

“Unapozungumzia jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema 

Naye kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwao. 

Awali naye mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara. 

Alisema kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa anafariki. 

“Kwa mfano Mh Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi wananchi tunaomba utusaidie “Alisema. 

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia hatua.