Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 15 Februari 2019

SEKTA YA AFYA ISIWE KIKWAZO KWA WANANCHI KUPATA MATANGAZO YAO MAPEMA

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia daftari la matibabu kutoka kwa moja kati ya wazazi waliopeleka watoto wao kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia moja Kati ya Wazee waliofika kupata huduma za Afya katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi katika chumba cha kuhifadhia Dawa wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na moja kati ya wazazi waliopeleka watoto wao kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
SEKTA YA AFYA ISIWE KIKWAZO KWA WANANCHI KUPATA MATANGAZO YAO MAPEMA.

Na WAMJW - DSM

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameagiza Sekta ya Afya kutokuwa kikwazo kwa wananchi kupata Matangazo ya kuzaliwa kwa watoto kwa ajili ya kupata cheti cha kuzaliwa kwa muda mfupi.

Ameyasema hayo leo, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala jijini Dar ea salaam.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Hospitali hiyo ni lazima ichukue juhudi za makusudi, ikiwemo kuongeza wafanya kazi ili kuhakikisha kwamba Watoto wote wanaweza kupata matangazo yao ndani ya Wiki moja, jambo litaloepusha usumbufu kwa Mwananchi ambao unaweza kuepukika.

" Sisi kama sekta ya Afya, tusiwe kikwazo, vya Mwananchi kupata haya matangazo, na hili nimeliona nimeshatoa maelekezo juu ya hili, na ndani ya wiki moja nategemea kwamba tatizo hili litakuwa limetatuliwa" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile akiongeza kuwa Matangazo haya ni ya muhinu sana katika mchakato wa kupata vyeti vya kuzaliwa, hivyo Mganga Mfawidhi ni lazima aweke mikakati thabiti ikiwemo kuongeza watu ili kuhakikisha kuanzia sasa matangazo yawe yanatoka ndani ya masaa 24. 

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupambana na changamoto ya msongamano wa watu katika Hospitali hiyo, Serikali imeboresha zaidi ya vituo vya Afya 350, huku zikijengwa Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za mikoa 2, ili wananchi waweze kupata huduma katika ngazi ya chini kabla yakufikia katika Hospitali za Rufaa.

"Kama Serikali tunachofanya ni kuboresha vituo vya Afya karibia 350, tunajenga Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za Rufaa za Mikoa 2, hivyo tunatarajia hizi Hospitali zinkianza kufanya kazi na huduma za upasuaji zikianza kupatikana kule, huu msongamano utaamia kule" alisema Dkt. Ndugulile

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza watu wote wenye VVU kujitokeza kupata matibabu, huku lengo la Serikali ni kufikia 909090, yaani 90 watu wote walio na Virusi vya Ukimwi waweze kufikiwa na kupimwa, 90 ya pili ni kuhakikisha waliopimwa waweze kuanzishiwa dawa papo kwa papo, na 90 ya tatu ya walioanzishiwa dawa waweze kufubaza virusi vyao vya Ukimwi, yote ni kuhakikisha ifikapo 2030 pasiwe na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dkt. Mkungu Daniel mesema kuwa Hospitali hiyo inapokea Mwananchi zaidi ya 2000, huku akisisitiza kuwa Hospitali hiyo ipo katika hatua yakujenga jengo ambalo litabeba jumla ya vitanda 150 kwaajili ya mama na mtoto ili kupambana na changamoto hiyo ya msongamano


WAZIRI UMMY ATAKA WATOTO WA KIKE KUPATA HAKI ZAO ZA MSINGI

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akihutubia Wajumbe (Hawapo Pichani) wanaoshiriki Mkutano wa Mradi wa Elimu kwa Wasichana unaondelea katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na Msichana Agatha Kipeta mkazi wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa aliyekumbana na changamoto ya ukatili wa kijinsia, wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Mradi wa Elimu kwa Wasichana unaofanyika Jijini Dar Es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akihutubia Wajumbe (Hawapo Pichani) wanaoshiriki Mkutano wa Mradi wa Elimu kwa Wasichana unaondelea katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es Salaam.
Wajumbe wa Mkutano wa Mradi wa Elimu kwa Wasichana akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakifuatilia wasilisho lililokua linatolewa na mmoja wa wawasilishaji katika Mkutano wa Mradi wa Elimu kwa Wasichana unaondelea katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es Salaam.
Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi. Pamela O’Donnell akitoa neno kwa wajumbe (Hawapo Pichani) waliohudhuria Mkutano wa Mradi wa Elimu kwa Wasichana unaondelea katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es Salaam.

Na WAMJW- DSM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwakandamiza watoto wa kike na kuwanyima haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kupata elimu.

Waziri Ummy amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa mradi wa Elimu kwa Wasichana inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia uliofanyika unaoendelea katika Hotel ya Hyatt Jijini Dar Es Salaam.

“Serikali ya awamu ya tano imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha Wasichana wanapata elimu bila vikwazo vya kuolewa mapema ama mimba za utotoni, kubwa ni uamuzi wa Rais John Pombe Magufuli kufuta ada kwa wanafunzi wa msingi na sekondari lengo ni kuhakikisha kila mtoto wa kike anapata haki sawa ya elimu kama mtoto wa kiume”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Serikali imeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ambapo katika kipindi cha mwaka 2018 mabweni zaidi ya 530 yamejengwa katika shule mbalimbali za sekondari na kwa kiasi kikubwa wanakaa watoto wa kike ili kujiepusha na vishawishi na hatimaye kupata mimba za utotoni.

Aidha, Waziri Ummy amesema ili kupambana na mimba za utotoni Serikali imefanya mabadiliko ya Sheria ya Elimu ambapo hivi sasa mtu yeyote akioa au kuolewa na mwanafunzi wa Shule ya msingi anakua ametenda kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 30 jela.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema ndoa za utotoni zinamfanya mtoto wa kike kupoteza uelekeo wa maisha yake hivyo Serikali katika kupambana na hilo inahakikisha watoto wa kike wanabaki mashuleni na kuwekewa mazingira wezeshi lakini pia kutoa ushauri ili waweze kujua afya zao na kuepuka mimba za utotoni.

Alhamisi, 14 Februari 2019

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe, ishara ya ufunguzi rasmi wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa NIMRI Prof. Yunus Mgaya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwajulia hali wagonjwa waliokwisha fanyiwa upasuaji wa Mabusha baada ya kufanya uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.

Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (jayupo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza kumsikiliza (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.

Mratibu wa Mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Upendo Mwingira akitabasamu, baada yakupata pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile, kwa  kazi nzuri anayoifanya ya kutokomeza Matende na Mabusha.

Madaktari kutoka Hospitali ya Vijibweni Kigamboni wakifanya upasua wa kutoa busha leo, katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (Hayupo kwenye Picha)



HALMASHAURI ZATAKIWA KUWEKA MIKAKATI THABITI  ILI KUTOKOMEZA UGONJWA WA MABUSHA.


Na WAMJW – DSM

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameziagiza Halmashsuri zote nchini kuhakikisha zinaweka mikakati thabiti ili kutokomeza Magonjwa ya Matende na Mabusha nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye tatizo la ugonjwa wa Mabusha na kuangalia hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Vijibweni Manispaa ya Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Halmashsuri zote nchini wakati zinaandaa Vipaumbele ni lazima watenge bajeti kwaajili ya mipango endelevu ili kuhakikisha kwamba zinaweza kupambana na Magonjwa haya yaliyokuwa hayapewi kipaumbele bila kuwategemea Wafadhili.

“Niwaombe sana, Wakati mnaandaa Mipango hii, tusiweke masuala mengi ya Semina, tuelekeze nguvu katika intervention, tuweke vitu ambavyo vitaleta mabadiliko, tutenge fedha kwaajili ya mipango endelevu, kwaajili yakuhakikisha kwamba tunaanza kujisimamia katika Magonjwa haya, haipendezi kama nchi kwenda kulia kwa Wafadhili kwa mambo ambayo tunaweza kuyafanya” Alisema Dkt. Ndugulile.

Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa, kati ya Wilaya 120 ambazo zilikuwa na uambukizo wa magonjwa haya, Wilaya  96 zimeweza kupunguza maambukizi kwa asilimia 80, hivyo kufikia kiwango cha kusimamisha ugawaji wa Kingatiba kwa jamii katika Wilaya hizo.

Dkt ndugulile aliendelea kuwahasa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki kikamilifu pindi yanapotokea mazoezi kama haya ili tuweze kutokomeza ugonjwa wa Matende na Mabusha, kwani bado Mkoa wa Dar es Salaam, maambukizi yapo juu kwa kiwango cha asilimia 10. 

Aidha, Dkt ndugulile amesema kuwa Watu wapatao 206,708 sawa na asilimia 87.47 katika Manispaa ya Kigamboni walipatiwa Kingatiba, na kwa Manispaa ya Ubungo Watu wapatao 997,632 sawa na asilimia 87.36 walipatiwa Kingatiba, huku manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, jumla ya watu wapatao 5,127, 596 sawa na asilimia 87.63 walipatiwa Kingatiba hiyo. 

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali kupitia uhisani wa CNTD, inatarajia kuwafanyia upasuaji watu 400 wakazi wa Manispaa za Kigamboni na Ubungo huku akiwaomba Wananchi wa Manispaa hizo kujitokeza ili kutumia vizuri fursa hii adimu.

Nae Mratibu Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa Serikali kupitia Mpango huu kwa kushirikiana na Wadau  inatoa huduma hii ya upasuaji kwa wagonjwa hawa bila malipo, hivyo kuwahasa watu wenye ugonjwa huu kujitokeza ili kupata huduma hii.

Nae Shuhuda aliyepata huduma hii ya upasuaji Bw. Ahmed Abrahaman amewahasa Watu wengine walio na ugonjwa huu kujitokeza kupata huduma hii ya upasuaji ili kuondokana na aibu hii kwa jamii, huku akisisitiza kuwa upasuaji huu unafanyiwa kwa njia za kisasa na wa muda mfupi sana.

SERIKALI YAAHIDI KUANZA KUJENGA VITUO VYA UTENGAMAO KWA AJILI YA WATOTO WENYE ULEMAVU NCHINI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akihutubia wananchi, wadau, wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifungua jiwe la msingi lililowekwa katika ujenzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni na katikati ni Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisikiliza jambo alilokua akielezwa na Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha Utengamao wa Watoto wenye ulemavu kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo Bw. Michelangelo Chiurchiu na Kulia ni Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiwa na mmoja wa watoto wenye ulemavu wakati alipotembelea maeneo wanapofundishwa utengamao katika kituo cha utengamao cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

Baadhi ya wadau, wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa katika ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

SERIKALI YAAHIDI KUANZA KUJENGA VITUO VYA UTENGAMAO KWA AJILI YA WATOTO WENYE ULEMAVU NCHINI

Na WAMJW-DAR

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza nia ya kuanza kujenga vituo vya utengamao kwa watoto wenye ulemavu nchini (Rehabilitation Centers).

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha utengamano wa watoto wenye ulemavu cha Kila Siku( Community Based Rehabilitation Centre) kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam.

“Ninaahidi kwenye kila kituo cha afya cha serikali ni lazima tuanze kujenga majengo ya utengamao kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, tuna takribani vituo vya afya 510 nchini tunaweza tusijenge kwenye vituo vyote kwa wakati mmoja lakini naamini tunaweza tukaanza na vituo vya afya 50”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuna changamoto za kupata takwimu sahihi za watu wenye ulemavu ambapo kupitia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha watu wenye ulemavu nchini ni asilimia 5.8 na kati ya hao asilimia 60 ni watoto chini ya miaka 18.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy ameomba wadau mbalimbali wa Afya waweze kusaidiana na Serikali katika kutekeleza azma ya kujenga vituo hivyo, lengo likiwa ni kuwafikia wanawake na walezi wengi wenye watoto wenye ulemavu nchini. 

Waziri Ummy amesema kuna uhaba mkubwa wa vituo vya Utengamao nchini huku akitoa mfano wa Jiji la Dar Es Salaam lenye vituo visivyozidi 6 lakini idadi ya watu ikiwa ni zaidi ya Milioni 5. Hata hivyo Waziri Ummy ameupongeza uongozi wa Kituo hicho cha Kila Siku Community Based Rehabilitation kwa kuanzisha huduma za utengamao kwa watoto wenye ulemavu na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wenye ulemavu kwenye vituo hivyo kuliko kuwafungia ndani.

Aidha, Waziri Ummy ameagiza Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatoa elimu kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kwenye maeneo yao ili kuondoa dhana potofu ya kufungia ndani watoto na kuwanyima haki zao za msingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Comunita Solidali nel Mondo kutoka nchini Italia Bw. Michelangelo Chiurchiu amesema lengo la kuanzishwa kituo hicho ni ujumuishwaji kwa wote wenye lengo la kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu kupitia uboreshaji wa huduma za utengamao kijamii, kujenga uwezo wa kiuchumi kwa watu wenye ulemavu pamoja na ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu katika elimu ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam.

Jumatano, 13 Februari 2019

SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua idadi ya Wananchi waliofika kupata huduma wakati alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua jokofu la kuhifadhia sampuli ya Damu pindi alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mashine yakupima Sampuli za Damu, Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akiongea na Watumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu katika taasisi hiyo.

Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo, akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha)  wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kumaliza ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.


SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU


Na WAMJW - DSM

Mpango wa Taifa wa Damu salama imetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huyo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu yake.

"Ni lazima kupunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali kwa kuanzisha mfumo wa uchangiaji gharama za huduma za Afya wakati Sera inaelekea kukamilika, Mpango unapendekeza kurudisha gharama kutoka Hospitali binafsi kupitia njia ya Bima" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile alisema kuwa Idadi kubwa ya wanaokuja kuchukua Damu katika Taasisi hiyo ni Hospitali Binafsi ukilinganisha na Hospitali za Umma, ambapo mfumo wake ni wakutoza huduma kwa Wananchi (Biashara)

"Wanaokuja kuchukua Damu nyingi hapa, wengi ni Hospitali Binafsi, kuliko hata za kwetu za umma, Damu nyingi tunawapa, lakini hawa tukiwapa Damu hizi, wao wanaenda wanatoza pesa, kwahiyo sisi tunawatengenezea bidhaa bure halafu wao wanaenda kutoza pesa, hata senti tano sisi hatupati, sio sahihi" alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amewaagiza viongozi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuangalia ni namna gani Damu iwe ni moja ya vitu vitakavyo gharamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

"Muwahusishe Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kuangalia jinsi gani damu itakuwa inagharamiwa na Bima ya Afya, mtuletee mapendekezo na sisi tutafanya maamuzi" Alisema Dkt. Ndugulile.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameagiza kufanya maboresho ya mfumo wa Takwimu kuanzia kwenye ukusanyaji wa mapato  mpaka hatua ambayo mgonjwa anapata damu hiyo jambo litakalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameagiza  kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawabakishia wachangiaji Damu ambao wanakuja kuchangia, hii inatokana na takwimu kuonesha Wachangiaji wa Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63%  mwaka 2017-2018.

"Taarifa yenu ya Mwaka 2017-2018 inaonesha kwamba, wachangiaji Damu wa hiari wanapungua kutoka  67% mpaka 63% , maana yake bado kuna changamoto, na kuna kazi tunatakiwa kufanya ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaowapata Mara ya kwanza kuendelea kuwa nao" Alisema Dkt. Ndugulile

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo amesema kuwa Mpango una mkakati wa kuboresha mfumo wa ukusanyaji taarifa na Takwimu za kielektroniki unaunganishwa nchi nzima ili kuleta tija na ubora wa huduma za damu salama nchini.

Kwa upande mwingine Dkt. Lyimo amesema kuwa Mpango umefanikiwa katika kipindi cha Mwaka 2018  kwa kushirikiana na timu za Mikoa na Halmashauri ulikusanya jumla ya chupa 307,835 ambayo ni sawa na Chupa 6 kwa kila watu 1000, huku Shirika la Afya Duniani linapendekeza kukusanya chupa 10 kwa kila watu 1000, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la chupa 73,882 sawa na 32% ikilinganishwa na Takwimu za 2017.

Dkt. Magdalena Lyimo aliendelea kusema kuwa kwa Mwaka 2018, Wastani wa chupa 25,653 zilikusanywa kila mwezi na damu zote zilipimwa magonjwa ya HIV,Kaswende pamoja na makundi ya damu, huku matarajio ni kuongeza damu hadi kufikia chupa 375,000 kwa Mwaka 2019.

Mwisho.


WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya wadau wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi katika mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali uliofanyika leo Jijini Dar Es Salaam.

Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa (NHIF) Bi. Anna Makinda akiongea mbele ya wadau wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi katika mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Wabunge wa Bunge la Tanzania katika kikao cha Wadau wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi katika mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali uliofanyika leo Jijini Dar Es Salaam.


Wadau mbalimbali wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi wakisikiliza kwa makini mjadala uliokua ukiendelea katika mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Jijini Dar Es Salaam.

Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely akizungumza mbele ya wadau wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi katika mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi waliohudhuria katika mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Jijini Dar Es Salaam.



Na WAMJW-DAR ES SALAAM

Wananchi wametakiwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kuondokana na adha wanayoipata pale wanapopata maradhi kwa kushindwa kugharamia matibabu na kusababisha madeni , umaskini na pengine kifo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo wakati alipohudhuria mkutano wa wadau wa Bima ya Afya kwa wananchi walio katika Sekta zisizo Rasmi uliojumuisha wadau kutoka nchi mbalimbali uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam.

“Tukiangalia hivi sasa asilimia 67 ya Watanzania wanalipa huduma za matibabu kwa kutoa hela mfukoni, maana yake ni kwamba Watanzania hawa wanapata changamoto pale ambapo wanapata maradhi kwa kutopata huduma nzuri kwa sababu hawana fedha lakini pia wanapata changamoto ya kuingia katika umaskini kwa sababu ya kugharamia matibabu”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imefanya tathmini mbalimbali na kugundua watu wengi hawana uelewa wa masuala ya Bima ya Afya lakini wana uwezo wa kulipa. Kufuatia hali hiyo Serikali imeamua kuboresha mfuko wa afya wa jamii “CHF Iliyoboreshwa” kwa gharama nafuu kwa watu watano kwa mwaka ili kuwawezesha wananchi wengi kujiunga na mfuko huo.

“Hivi sasa asilimia 67 ya wananchi hawana Bima ya Afya, hivyo wanatumia fedha taslimu kupata huduma. Hii ni changamoto kwa wengi kwa kuwa matibabu yana gharama kubwa na ugonjwa huja bila taarifa”. Amesema Waziri Ummy.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Ummy ameeleza dhamira ya Serikali kukamilisha mchakato wa kupitisha Sheria ya Bima ya Afya kuwa ni lazima kwa kila mtu kabla ya mwisho wa mwaka huu 2019. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kupitia utaratibu huu wananchi wengi hasa wa kipato cha chini wanapata huduma nzuri za matibabu na pia kuepuka kuingia kwenye umaskini kwa sababu ya ugonjwa.

Kikao hicho cha siku mbili kimejumuisha wajumbe kutoka nchi za Kenya, Congo, Ghana, Cameroon, Ethiopia, Ujerumani, Ufilipino, Chad, Zambia, Afrika Kusini, Uswisi pamoja na wenyeji Tanzania.

SERIKALI YAANZISHA HUDUMA ZA KIBINGWA MATIBABU YA MOYO DODOMA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliye mbele) akizindua rasmi maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo (Cathlab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma walio kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce chandika.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielekezwa namna magonjwa ya moyo yanavyochunguzwa katika maabara ya uchunguzi na tiba ya moyo Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini  Dodoma

Picha ya pamoja Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na wataalam wa uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dsm.

Mashine ya uchunguzi na tiba ya moyo (Cathlab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula akisisitiza jambo kwenye halfa ya uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya Moyo. 

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo kwenye halfa ya uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya Moyo. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye halfa ya uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya Moyo. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na wananchi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma alipoenda kuzindua Maabara ya Uchunguzi na Tiba ya Magonjwa ya Moyo (Cathlab)

Na WAMJW – Dodoma. 

Katika azma ya kuboresha huduma za kibingwa za matibabu, Serikali kupitia Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma imeanzisha huduma za matibabu ya moyo kwenye maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo kwa kutumia mashine maalum (Cathlab).

Maabara hiyo ya tatu nchini na ya pili kwenye taasisi ya serikali inatarajiwa kutoa huduma za uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo ndani ya muda mfupi hivyo kuhudumia wagonjwa wengi ndani ya muda mfupi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara hiyo, mgeni rasmi Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa kufunguliwa kwa maabara hiyo ni mafanikio makubwa kwa serikali katika kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakisafiri kwenda mbali kufuata huduma za matibabu.

“Huduma za kibingwa zimepunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanasafiri au kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kwa asilimia 95 kutokana na uboreshaji wa huduma za afya ndani ya nchi” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imekuwa ikiwajengea uwezo wataalam wa afya nchini ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi jambo ambalo limezaa matunda kwa kuwa wagonjwa wengi hivi sasa wanapata matibabu ndani ya nchi.

Hata hivyo Waziri Ummy ametoa ufafanuzi wa upatikanaji wa rufaa ya matibabu nje ya nchi na kusema kuwa Serikali haijazuia rufaa za matibabu nje ya nchi bali ni lazima kujiridhisha kwanza huduma za matibabu hazipatikani hapa nchini kabla ya kutoa rufaa.

“Hakuna daktari tuliyemkataza kutoa rufaa nje ya nchi, sasa hivi tuna uwezo wa kutoa huduma za matibabu ya kibingwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima daktari awe amejiridhisha na kuthibitisha kwamba matibabu hayo hayapatikani hapa nchini kabla ya kutoa rufaa” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa kuwa wabunifu na kushirikiana kutoa huduma bora za matibabu ya moyo kwa wananchi na kuzitaka hospitali na taasisi nyingine za afya kuiga mfano wao katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya ili waweze kupata bima ya afya ambayo itawasaidia kupata huduma za matibabu kwa uhakika. Waziri Ummy amesema kuwa ni muhimu kwa watanzania kuwa na bima ya afya ambayo itawapunguzia gharama za matibabu huku akiwataka wananchi kujiwekea malengo na kukata bima ya afya ambayo gharama zake ni nafuu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa ipo haja ya kuwathamini madaktari wazalendo ambao wamekuwa wakijitoa kuokoa maisha ya wagonjwa. Dkt Chaula amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika wataalam wa afya nchini ili kuweza kuwa na madaktari bingwa wengi wanaotoa huduma za kibingwa hapa hapa nchini pamoja na kuwekeza kwenye miundombinu na vifaa.

Awali akitoa salamu zake, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi, ametoa rai kwa wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha, kufanya mazoezi na kula chakula bora ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo kisukari, presha na shinikizo la damu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa maabara hiyo imegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 5 na inatarajiwa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo hivyo kupunguza adha ya wagonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu ambapo awali zilikuwa zikipatikana Dar Es Salaam kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na Hospitali nyingine moja isiyo ya kiserikali.

Dkt. Chandika amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wataalam kutoka Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi huku akiiomba serikali kuongeza wataalam ili kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma za afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa hadi kufikia jioni jumla ya wagonjwa 13 kutoka Dodoma na mikoa ya jirani tayari walishakuwa wamefanyiwa uchunguzi katika maabara hiyo ambapo kati yao  wagonjwa wanne wakitakiwa kwenda JKCI kwa uchunguzi na tiba zaidi.

Aidha Prof. Janabi alitumia nafasi hiyo kuishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuwapa nafasi na heshima kubwa ya kuja kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu kwa wananchi.

Mwisho


Jumanne, 12 Februari 2019

DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi wa chumba kwa chumba ili kujidhisha na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa  katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza Kulia) akipata maelezo ya mradi ulipofika kutoka kwa Meneja Mradi (Wapili kutoka kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Muonekano wa jengo la Maabara ngazi ya tatu lenye  uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, jengo hilo lililokamilika kwa 90%, linajengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa  katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.


DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII.

Na WAMJW - DSM
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekasirishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara  ya Afya ya Jamii ngazi ya tatu, inayoshughurikia magonjwa hatari ya mlipuko kama vile Ebola, Mabag, Kipindupindu hali inayopelekea  kuchelewesha utoaji wa huduma hizo kwa Wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo hilo lililo eneo la Mabibo jijini Dar es salaam  ili kujidhihirishia thamani ya pesa zilizotumika na kiasi cha ujenzi wa jengo hilo ulipofika.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa haoni sababu ya msingi iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa Maabara hiyo kwani fedha zote zipo, hivyo kukasirishwa kwa kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara hiyo ulioanza tangu mwaka 2016.

" Nitoe asikitiko yangu kwamba, kazi hii imechukua muda mrefu sana, tangia 2016, wenzetu waliozipata fedha hizi wengi wamekwisha kamilisha kazi zao, sisi Tanzania bado tunasua sua, kibong'oto, Temeke, Mawenzi na hapa, najambo linalonisikitisha sana fedha tunazo" alisema Dkt. Ndugulile

pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ujenzi wa Maabara hiyo utaisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho inakipeleka nje ya nchi kwaajili yakupima sampuli za magonjwa hayo, hivyo kukamilika kwa Maabara hiyo kutaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache barani Afrika inayotoa huduma hizo.

Aidha, Dkt Ndugulile ameonekana kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa Maabara hiyo, hivyo kutoa onyo katika matumizi ya fedha za ujenzi wa Maabara hiyo, hii ni kutokana na kufanya marekebisho ya mara kwa mara wakati ramani ya jengo hilo ipo.

"Fedha tunazo nyingi kupita maelezo, na ndiomaana mnaishia kuzitumia vibaya, matumizi ya hovyo yanapitishwa kwa haraka sana, lakini matumizi ya msingi yanasuasua, sasa niombe kwa niamba ya Kazi zote, hizi fedha tuliziomba kwa matumizi mahsusi kujenga hizi Maabara na isolation centers, naomba nitakaporudi haya tuliokubaliana mtimize" alisema Dkt Ndugulile

Kwa upande mwingie Dkt. Ndugulile amewata viongozi wa Wizara ya Afya kutokuwa kikwazo katika taratibu za ujenzi wa Maabara hiyo, ili kuepusha lawama kutoka kwa Wakandarasi, jambo litalosaidia katika kasi ya ujenzi wa Maabara hiyo.

"Taratibu za ndani, sisi kama Wizara naomba zisiwe kikwazo kwakweli, kwasababu gharama za mradi mnazijua, uendeshaji tunaujua, na tulikuwa tunazifahamu, fedha tunazo zakutosha, mzipitishe katika taratibu zake zote ili hawa Wakandarasi wasije kutulalamikia" Alisema Dkt. Ndugulile

Mwisho.