Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 5 Agosti 2019

PREPARING THE HEALTH WORKFORCE TO MAKE THE MOST OF DATA

- Hakuna maoni
DataUseForHealth


Health workers exchange learnings about Tanzania's electronic immunization registry. Photo: PATH/Trevor Snapp. For nearly thirty years as a health worker in Tanzania, Salome has used pen and paper to record patient data. A digital transformation promises to streamline her work and improve patient care. 

Digital health solutions increase data quality and accessibility, but to be effective and improve patient outcomes, health workers must know how to make the most of the information. For many like Salome, Tanzania’s digital transformation will require retraining and developing new digital literacy skills. 



Building the workforce of the future 
The Data Use Partnership—a collaboration between the Government of Tanzania and PATH—aims to equip Tanzania’s health sector and workforce with skills for the country’s changing digital landscape. This includes training existing and future generations of health workers to make better use of digital platforms and data. 

To facilitate trainings, the Data Use Partnership established the Capacity Building Consortium (CBC). Made up of three universities, two health research and training institutes, and zonal health training centers around the country, the CBC fosters a culture of data use and builds the capacity of health workers to identify and solve problems, measure performance, allocate resources, track patients, support clinical decisions, and streamline service delivery. 



Making the most of data 
“In the health sector, a lot of data are collected, but aren’t necessarily put into efficient use when making crucial decisions,” explains Professor Flora Lucas Kessy, Secretariat Chairperson of the CBC and instructor at the Tanzania Training Center for International Health. “The consortium was formed to build the capacity of health workers through both in-service and pre-service training.” 

The consortium is building the health workforce’s capacity by: 
• Developing trainings and innovative platforms: The Data Use Partnership is developing a new series of short-term trainings, using costeffective and innovative platforms. Trainings will be offered in person through zonal health resource centers to ensure greater accessibility, and through eLearning modules that the CBC aims to integrate under a single government-owned National Health eLearning platform.



 • Establishing new delivery methods: eLearning platforms can help deliver trainings to rural health providers, where long distances, limited resources, and poor transportation may otherwise be a barrier to education. “There are lots of current innovations in this country in terms of mobile phone and smartphone use,” explains Professor Kessy. “We can use digital platforms to deliver critical courses even to health providers that are very far away.” 

• Increasing focus on data use and analytics: The CBC will review, develop, and standardize curricula for data analytics training, so that the workforce is operating from a place of common experience. With more than 136 institutions offering certificates and diplomas in health and allied sciences programs, it’s critical that students graduate with a shared skillset, understanding, and appreciation for data use. 



• Fostering government ownership and peer learning: The CBC also recognizes the importance of ensuring that trainings are delivered by their own peers and experts, instead of an outside institution or implementing partner. “Health workers have to feel that they’re being trained by one of their own,” explains Mr. Tumaini Macha, Assistant Director, Monitoring & Evaluation from the Ministry of Health. “This mentorship model is even more efficient and ensures that trainers understand the need in different areas.” 

Achieving digital transformation 
"Having a curriculum that’s strong in data use ensures that whoever graduates from universities and other academic institutions, goes home with knowledge on how to deliver on data use,” explains Professor Kessy. “We've been able to bring together five different prime institutions that have their own different ways of operating. It’s so unique that we can work together, forget our own university boundaries, and build an open consortium that’s focused on data use.” 


The CBC is critical to Tanzania achieving digital transformation. By educating and training the existing workforce and preparing a pipeline of future talent, the health workforce will be able to make optimal use of digital tools, ultimately leading to better patient care and more equitable access to health services.

Jumamosi, 3 Agosti 2019

WAZIRI UMMY AKABIDHI MASHINE YA UPULIZIAJI DAWA ZA KUDHIBITI WADUDU MKOANI TANGA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashine ya kupulizia dawa za kudhibiti wadudu wadhurifu yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa afya wa jiji la Tanga jinsi wanavyowanasa mbu kwa ajili ya kuwafanyia tafiti mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashine ya upuliziaji dawa za kuangamiza wadudu wadhurifu iliyofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akiongelea mkakati wa wizara hiyo wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu ambao utatekelezwa nchi nzima, hapo ni katika makabidhiano ya mashine ya kupulizia dawa za kudhibiti wadudu wadhurifu yakiyofanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.


Viongozi wa Jiji la Tanga wakifurahia makabidhiano ya Mashine ya upuliziaji dawa za kudhibiti wadudu wadhurifu kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Tangamano jijini humo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Bw. Mustafa Mhina wakiangalia jinsi mashine ya upuliziaji inavyofanya kazi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati), Mkurugenzi wa kinga wa Wizara hiyo Dkt. Leonard  Subi (wa kwanza kushoto) wakiwa pamoja na Mabwana Afya wa Jijini Tanga wanaotekeleza mkakati wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu mkoani humo.

Na Emmanuel Malegi-WAJMW, Tanga

Jiji la Tanga limekua la pili kupata mashine za kupulizia dawa za kuua mbu na wadudu wadhurifu waenezao magonjwa mbalimbali ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI katika kudhibiti wadudu hao.

Akikabidhi mashine hiyo kwa uongozi wa Jiji la Tanga, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema mkakati huo ni wa miaka mitano (2019-2024) na unalenga kuhakikisha mbu na wadudu wadhurifu wanadhibitiwa kwa njia ya utengamano na ameiomba jamii ishiriki kikamilifu katika kupambana na wadudu hao.

“Wizara yangu imeagiza mashine nane za kisasa(foggig mashine) zenye uwezo mkubwa wa kupulizia na zinabebwa na magari na kupuliza eneo kubwa kwa wakati mmoja, hivyo naomba jamii ihakikishe inashiriki kikamilifu katika kupambana na wadudu hawa dhurifu”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa ni vema mikoa ikawekeza katika maeneo ya msingi am bayo ni pamoja na ushiriki wa jamii, sekta binafsi na wadau  kushiriki katika kudhibiti wadudu kwa njia shirikishi zinazolenga kuharibu mazalia ya wadudu. Mikoa kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mbu na wadudu wadhurifu katika ngazi zote na kupanga njia madhubuti za udhibiti wa wadudu hao.

Waziri Ummy amesema katika kuhakikisha mkakati huu unatekelezwa, Wizara ya afya kwa kushirikiana na TAMISEMI imetoa maagizo kwa kila Mkoa, Wilaya na Halmashauri zote ziweze kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango ya utekelezaji wa udhibiti wa mbu na wadudu wadhurifu ambayo itakua mtaa kwa mtaa, Halmashauri kuhakikisha zinaishirikisha jamii katika ngazi zote za mapambano haya ya mbu na wadudu wadhurifu.

Pia Waziri Ummy amezitaka Halmashauri kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkakati huu katika kipindi cha mwaka mmoja na kutoa taarifa ya mafanikio, changamoto na mipango ya Halmashauri katika utekelezaji ikiwa ni pamoja na kununua mashine za upuliziaji (Fogging Machine) angalau moja katika kipindi cha kufikia Januari 2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambae ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw. Thobias Mwilapa amemshukuru Waziri Ummy na Wizara ya Afya kwa ujumla kwa kuupatia mkoa huo mashine hiyo ambayo itasaidia katika utekelezaji wa mkakati wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu ambao wanaeneza magonjwa huku akiitaja Tanga kushika namba mbili kitaifa kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue baada ya Dar Es Salaam.

MWISHO

Ijumaa, 2 Agosti 2019

WAKAZI WA TANGA KUPATA HUDUMA ZA DHARURA NA MAHUTUTI KATIKA HOSPITALI YA BOMBO

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta na Makamu wa Rais wa Taasisi ya ABBOTT Bw. Andy Wilson wakati wa uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea jambo wakati wa uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga mapema leo.
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya ambaye alimuwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Leonard Subi akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi kartika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw. Thobias Mwilapa.




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Kushoto) akioneshwa kifaa cha kusaidia mapigo ya moyo na Daktari bingwa wa huduma za dharura Dkt. Juma Ramadhan wakati Waziri alipozindua huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Bombo mkoani Tanga.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa chumba cha wagonjwa mahututi wakati alipotembelea chumba hicho baada ya uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga.


Chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Tanga wakifuatilia Hotuba za uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi Hospitalini hapo.
Na Emmanuel Malegi-WAJMW-Tanga

Wakazi wa Jiji la Tanga sasa wataanza kupata huduma za uhakika za dharura pamoja na huduma za wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo).

Huduma hizo zimefunguliwa rasmi leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati ziara yake ya siku mbili mkoani humo huku akiwahakikishia wananchi wa Tanga kutolazimika kupewa rufaa kwa ajili ya kufuata huduma hizo Muhimbili na KCMC.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kuboresha huduma za afya katika Hospitali za mikoa kwa kujenga jengo la huduma za dharura lililogharimu Tsh. Milioni 211.6 na jingo la kuwahudumia wagonjwa mahututi Tsh. Milioni 350 katika kipindi cha mwaka 2018/19”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameongeza kuwa kuanzishwa kwa huduma hizo za dharura na mahututi zitatatua changamoto zilizokuwepo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/19 Serikali iliipatia Hospitali hiyo ya Mkoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Oksijeni (Oxygen Implantation).

Aidha, Waziri Ummy amesema kuanzishwa kwa huduma za dharura na mahututi zinategemewa kupunguza vifo vitokanavyo na dharura kwa asilimia 50, huku akiongeza kuwa Serikali inatarajia kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kwa asilimia 100 Hospitalini hapo, kutengeneza lifti katika wodi ya Galanos, kujenga kituo cha uchunguzi na vipimo pamoja na kujenga jengo la tiba shufaa kwa wateja walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Pamoja na hayo Waziri Ummy ameishukuru taasisi ya ABBOTT chini ya makamu wake wa Rais Bw. Andy Wilson kwa kusaidia ukarabati wa jengo la huduma za dharura kwa wagonjwa pia Waziri amewashukuru Wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kwa kuchangia kuboresha huduma za afya katika Hospitali hiyo.

Kwa upande Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali  ambaue ni Mkurugenzi huduma za Kinga a Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Leonard Subi amesema uzinduzi huo wa huduma za dharura na chumba cha wagonjwa mahututi ni katika utekelezaji wa mkakati wa Wizara ya Afya kuhakikisha huduma hizo zinapatikana katika Hospitali zote za rufaa nchini.

MWISHO

Alhamisi, 1 Agosti 2019

TANZANIA YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

- Hakuna maoni
Mgeni rasmi wa mkutano huo wa NTD ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Elias Kwesi akifungua mkutano huo ambao unawakilishwa na waratibu wa mpango huo kutoka mikoa mbalimbali,wadau wa ndani na nje ya nchi

Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka wizara ya afya Dkt.Leonard Subi akiongea na vyombo vya habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira akifanya utambulisho wa wageni walioshiriki mkutano wa mwaka wa mapitio na kutengeneza mpango kazi wa mwaka unaofanyika jijini Dar es Salaam

Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt. Christine Musanhu akipeana mkono na Mgeni rasmi wa mkutano huo mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt.Elias Kwesi

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za kitaifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

Kaimu Mwakilishi mkazi wa shirika la afya duniani(WHO)Dkt. Christine Musanhu akiongea kwenye mkutano huo.

Mratibu wa NTD Dkt.Upendo Mwingira akisalimiana na mgeni rasmi Dkt.Elias Kwesi

 Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa mkutano huo.


TANZANIA  YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia wizara ya afya imepiga  hatua katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa wa Wizara hiyo, Dk. Elius Kwesi wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya shuguli wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na mpango kazi wa mwaka.

Dkt.Kwesi alisema mkutano huo ni muhimu kwani watajadiliana na wadau hao kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara hiyo kwa upande wa rasilimali fedha.

"Tuna pengo la rasilimali  mbalimbali  na tumewaita hapa Wadau kujadiliana nao Mpango kazi wetu  na kuangalia namna gani watatusaidia kuziba pengo na kutakavyosaidiana kutekeleza," alisema Dkt.Kwesi

Alisema tangu utekelezaji wa Mpango huo ulipoanza nchini umefanikiwa kupunguza magonjwa hayo kwa kiwango cha asilimia 80.

Awali Mkurugenzi wa huduma za Kinga wizarani hapo Dkt.Leonard Subi alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yasipodhibitiwa yatapelekea watu wengi kuugua siku zijazo kwani yana athari kubwa na kusababisha upofu na ulemavu kwa jamii.

“mfano ugonjwa wa kichocho kwa watoto huathiri ukuaji na wengine wanaweza kupata saratani katika maisha yao".Alisema Dkt.Subi

Alisema wizara kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya jitihada kubwa na hivyo kufanikiwa kudhibiti magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa

"Wilaya ambazo zilikua zimeathirika sana na matende na mabusha miaka kumi iliyopita zilikua takribani 120 lakini hivi sasa zimebaki wilaya 24 ambazo bado tunaendelea na ugawaji kingatiba na trakoma kulikuwa na wilaya 71 na sasa zimebaki wilaya sita tu".

Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira amesema kwa upande wa kichocho na minyoo ya tumbo bado inahitajika   kuendelea kuwakinga watoto na baadhi ya wilaya wanaendelea kugawa kingatiba za matende na mabusha pamoja na usubi.

Mwisho

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAAJIRI WANAOWANYIMA HAKI WANAWAKE LIKIZO YA UZAZI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Sekta ya Afya(hawapo kwenye picha), wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akieleza jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Sekta ya Afya (hawapo kwenye picha), wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna, na wa mwisho kulia ni Kaimu Katibu mkuu Wizara ya Afya, ambae pia ni Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice Mutayoba.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Sekta ya Afya   yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna wa mwisho Kulia ni Mwakilishi kutoka UNICEF James Gitau.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia maelezo kuhusu huduma ya unyonyeshaji katika maeneo ya kazi kutoka Afisa kutoka Wizara  ya Afya Bi Tufingene Malambugi wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma.


SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAAJIRI WANAOWANYIMA HAKI  WANAWAKE  LIKIZO YA UZAZI. 

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetangaza kuanza kuwachukulia hatua Waajiri wote ambao wanavunja Sheria kwa kugandamiza haki ya kupata likizo ya uzazi kwa wanawake pindi anapojifungua. 

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu ya “Wawezeshe wazazi kufanikisha unyonyeshaji”.

"Haki ya Mwanamke Kuzaa na kupata likizo ya uzazi ni haki yake ya asili, haitakiwi kuwekewa vikwazo au changamoto yoyote, kwahiyo nitoe wito kwa wanawake ambao wanafanya kazi, ni haki yako kupata likizo, asije mtu anakwambia anaijaza kazi yako kwakuwa umetoka likizo ya kujifungua, tuambie sisi, tutachukua hatua, na huyo Mwajiri  tutamtangaza kuwa ni adui wa Wanawake na Watoto wa Tanzania ".Amesema Waziri Ummy. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuanzisha dawati la kutoa malalamiko litaloshughulikia kupigania na kutetea haki za wanawake kupata likizo ya uzazi, jambo litalosaidia kudhibiti tabia za baadhi ya Waajiri kukandamiza haki za wanawake baada ya kujifungua.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wananyonyeshwa maziwa ya mama, hii inaonesha kuwa hali ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama imepungua ikilinganishwa na takwimu ya mwaka 2015/2016 ambayo ilikuwa ni asilimia 98.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi (ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa) ni asilimia 53 ikilinganishwa na asilimia 51 ya mwaka 2015/2016

Aliendelea kusema kuwa, idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58 ikilinganishwa na asilimia 59 ya mwaka 2015/2016.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni 35%, huku kiwango kikionekana kuongezeka ikilinganishwa na asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, takwimu za utafiti wa hali ya lishe nchini za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa asilimia 31 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa ikilinganishwa na asilimia 34 ya mwaka 2015/2016, huku sababu kubwa ya ikiwa ni ulishaji usio sahihi ambao huchangiwa na majukumu mengi yanayomkabili mama na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto.

Naye Mwakilishi kutoka UNICEF Bw. James Gitau amesema kuwa, unyonyeshaji ni moja ya njia muhimu kuhakikisha Afya Bora kwa maisha ya mtoto, hivyo kutoa wito kwa wanahabari kuhakikisha wanapeleka Elimu kwa wananchi hususan wanawake kuhakikisha wanafahamu umuhimu wa kunyonyesha Watoto mfululizo miezi sita ya mwanzo,

Pia, Bw. James Gitau ametoa wito kwa Serikali kuongeza nguvu katika uhamasishaji juu ya umuhimu na haki ya Watoto kunyonyeshwa, amesema jambo hili litasaidia kuokoa watoto kupata magonjwa yanayotokana na kukosa virutubisho kutoka kwa maziwa ya mama.

Mwisho.

Jumatano, 31 Julai 2019

SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

- Hakuna maoni
Mkuu wa kitengo cha afya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere George Ndaki akimuonesha ufanyaji kazi wa  mashine za kupima joto(thermo scanner) Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipotembelea eneo la wasafiri wanaoenda nje ya nchi  zilizofungwa kwenye uwanja mpya wa ndege terminal three

Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akionesha kadi za homa ya manjano"Yelow Fever" ambazo zinatolewa na wizara ambapo wizara imefunga kifaa maalum cha kubaini kadi feki ambazo wasafiri huzinunua bila kuchanjwa chanjo hiyo

Dkt.Ndugulile akioneshwa utofauti wa kadi halisi na kadi feki za homa ya manjano.Dkt.Ndugulile amewasihi wananchi wanaotarajia kusafiri nje ya nchi kuacha kununua kadi feki bali kuhakikisha wanapata chanjo hiyo kwenye vituo rasmi vilivyoelekezwa na wizara  ya Afya

Naibu Waziri akikagua vifaa vingine vilivyofungwa terminal three kwa ajili ya kubaini wahisiwa wa Ebola

Katika kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa SADC wizara ya afya imejipanga kukabiliana na dharura kwa wageni watakaoshiriki mkutano huo.Pichani.Dkt.Ndugulile akikagua magari ya wagonjwa wa dharura yaliyopo ofisi za Toyota

 Naibu Waziri akikagua kifaa cha huduma ya dharura kilichopo kwenye magari hayo

Naibu Waziri akikagua moja ya chumba cha dharura kilichoandaliwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya washiriki wa mkutano wa SADC

Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.Juma Mfinanga (kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wakati alipotembelea kujionea hali ya utayari ya kuwahudumia washiriki wa mkutano wa SADC ambao watapata dharura na hivyo kupatiwa huduma za afya kwenye hospitali hiyo



SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

NA.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini hapa.

Dkt.Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa  zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.

"Magari na Mabasi hayo yatatumika kwenye mkutano wa SADC na baadae yatasambazwa katika vituo vya dharura nje ya hospitali ambapo yatatumika kusafirishia majeruhi pindi ajali inapokuwa imetoka.

"Tutayatumia katika mkutano wa SADC, pamoja na ambulance hizo 12 kuna mabasi makubwa mawili ambayo yana huduma zote za msingi ndani ambapo watu wapatao 20 wanaweza kubebwa na kupatiwa msaada wa ajali," alisema.

Alisema serikali imejipanga  pia katika njia ya anga kwa kutumia  ndege  pindi mtu anapohitaji huduma ya dharura kupelekwa haraka katika eneo jingine hususani hospitali ya Taifa Muhimbili.

"Ni utaratibu ambao Serikali inauweka kuhakikisha waathirika wa ajali wanapata huduma za dharura na ajali, mapema iwezekano na tunasema ndani ya masaa yaliyowekwa ya kuwahudumia majeruhi," alisema Dkt.Ndugulile

Naibu Waziri huyo alisema wameagiza magari ya zimamoto na uokozi kwamba si tu liwe na uwezo wa kuzima moto bali linakuwa na vifaa vya kisasa, kwa mfano ikiwa gari limepata ajali, milango inashindwa kufunguka, iweze kukatwa ili kuokoa majeruhi, iwezekane.

"Haya ni maendeleo makubwa kwa Serikali katika kuhakikisha majeruhi wanapata huduma za dharura za awali mapema inavyowezekana, kwani wengi hufariki dunia kwa sababu hukosa zile huduma za awali za dharura katika lile li-saa limoja la kwanza," alisema.

Dk. Ndugulile aliongeza "Inawezekana anavuja damu, anashindwa kupumua vizuri, tuna imani magari, mabasi na mafunzo tuliyowapa wataalamu huduma hizi zitaimarika.

"Natoa rai kwa wananchi, kwani nao wamekuwa wakichangia madhara kwa majeruhi, wanawamalizia wale majeruhi, wakiamini wanawasaidia kuokoa maisha.

"Wahakikishe tu wanamtoa majeruhi na kumuweka pahala pengine mbali na tukio la ajali, kama gari litaweza kulipuka moto ule usimfikie, tunapowabeba 'mzobe mzobe' tunawasababishia madhara zaidi.

"Muhimu tuhakikishe huduma za msingi zinapatikana pale pale, kikubwa ni kuhakikisha yule Mgonjwa anapumua, havuji Damu kwa wingi na njia yake ya Hewa IPO salama.

"Jambo la msingi si kumkimbiza majeruhi hospitalini kwanza bali 'kum-stablize' pale pale eneo la tukio, kama mfupa umevunjika afunge vizuri usining'ingine, abebwe vizuri kama mshipa wa shingo umevunjika usimalizike, kwani wengi kutokana na ule ubebaji huishia kupooza mwili na hata kufa," alisema.

Sambamba na hilo, mapema asubuhi, Dk. Ndugulile alifanya ziara kwenye kitengo cha afya ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA- terminal III), kujionea hali ya utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola.

MWISHO

WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA EBOLA USIINGIE NCHINI

- Hakuna maoni
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora akisema jambo wakati akifungua zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola kwa Watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana ana Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

Washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa wa Ebola kutoka Mkoa wa Kagera wakiwa kwenye majadiliano kuweka mikakati ya ugonjwa huo usiingie nchini.

Wataalam wa Afya katika Mkoa wa Kagera wakiwa katika zoezi la utayari wanajadiliana mikakati ya kudhibiti Ugonjwa wa Ebola usiingie nchini.

Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. Refeya Ndyamuba (aliyesamama) akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola nchini kwa watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma jana Mjini Bukoba.


Picha ya Pamoja washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola na Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora (aliyeketi katikati).


Na WAMJW – Bukoba, KAGERA

Watoa huduma za afya nchini wametakiwa kuweka juhudi madhubuti kuhakikisha Ugonjwa wa Ebola hauingii nchini Tanzania.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustinely Kamuzora alipokuwa akifungua zoezi la utayari jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa wataalam wa afya mkoani humo.

Akifungua zoezi la utayari, Profesa Kamuzora amesema “Tukifanya juhudi zetu za kukabiliana na ugonjwa wa ebola basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” na kuendelea “Juhudi hizi zina matunda makubwa kuliko tukaruhusu ugonjwa huo kuingia nchini”

“Mpaka sasa hivi Mwenyezi Mungu ametujaalia hakuna mtu aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini, tukifanya yale ambayo tunaelekezwa na wataalam wetu basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” amesema Profesa Kamuzora.

Prof Kamuzola amewataka watoa huduma za afya kufuata taratibu zote zilizowekwa ili endapo ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo, basi aweze kupatiwa huduma na wakati huo huo mtoa huduma akawa salama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu amesema kuwa zoezi ya utayari lina lengo la kuzuia maafa yasitokee kwa kuwaweka tayari watalaam wa sekta ya afya kukabiliana na tishio la ugonjwa wa ebola kuingia nchini.

“Tuhakikishe tunazuia ugonjwa wa ebola usiingie nchini, na endapo ikitokea umeingia basi tuhakikishe tunapunguza athari zitokanazo na ugonjwa huo” amesema Bw. Taratibu.

Naye Mtaalam wa Afya ya Jamii na Masuala ya Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Faraja Msemwa amesema kuwa kupitia mazoezi hayo ya utayari wanapata fursa ya kubaini fursa  na changamoto zilizopo katika kudhibiti ugonjwa huo wa ebola usiingie nchini.
“Katika zoezi hili tunaangalia hawa watumishi wetu wa afya tuliowandaa wana uwezo wa kiasi cha kuweza kufuata miongozo iliyoandaliwa” amesema Dkt. Msemwa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) toka kuripitiwa kuibuka kwa ugonjwa wa ebola nchini Uganda mnamo mwezi Agosti mwaka 2018 jumla ya kesi 2612 za watu kuathiriwa na ugonjwa huo zimeripotiwa huku ukisababisha vifo 1756 (sawa na asilimia 67). Zoezi la utayari limepangwa kufanyika kuanzia leo JULAI 30 mpaka AGOSTI 8 mwaka 2019 ambapo vituo vya kutolea huduma za afya katika Mikoa ya Kagera na Kigoma vitapimwa utayari wao katika kukabiliana na Ugonjwa huo hatari.

Kupitia mazoezi ya utayari, watoa huduma za afya kuanzia ngazi ya jamii wanapata fursa ya kushiriki kwa vitendo namna ya kutambua, kutoa huduma kwa mtu anayehisiwa au kuwa na ugonjwa wa ebola na kuwaondolea woga pindi ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo.

MWISHO.

Jumapili, 28 Julai 2019

4% YA WANANCHI WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akitembelea moja ya banda la kufanyia uchunguzi  wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto  kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiwajulia hali baadhi ya watu waliojitokeza kufanya  uchunguzi homa ya ini, katika  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba.

Wadau mbali mbali wa Afya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiteta jambo na mwakilishi wa WHO Dkt. Christine Chakanyuka Musanhu  wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba, na Kulia ni mwakilishi wa WHO anaitwa Dr. Christine Chakanyuka Musanhu

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika katika picha ya pamoja na Wadau pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.


4% YA WANANCHI WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI

Na WAMJW-DOM

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa miongoni mwa Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wameabukizwa Virusi vya Homa ya Ini aina ya B, hii ni kutokana na Takwimu za Ofisi ya Taifa wa Takwimu 206-2017.

Dkt. Alphonce Chandika amesema hayo leo wakati wa Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo, yenye kauli mbiu ya “Wekeza katika mapambano ya Homa ya Ini “ maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamini Mkapa.

“kati ya wachangiaji damu 307,835 takribani watu 13,613 sawa na asilimia 4.4 walikuwa na maambukizi ya homa ya ini kwa mujibu wa takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)” alisema Dkt. Alphonce Chandika.

Dkt. Alphonce Chandika  aliendelea kusema kuwa Mwaka 2017, kati ya wachangiaji damu 233,953 takribani watu 11,417 sawa na asilimia 4.9 walikuwa na maambukizi, aidha asilimia 0.5 ya wachangiaji damu walikuwa na maambukizi ya homa ya ini aina ya C kwa mwaka 2017 na asilimia 0.3 kwa mwaka 2018.

Aidha, Dkt. Alphonce Chandika alisisitiza juu ya kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya athari za ugonjwa wa  Homa ya Ini katika jamii na kwa nchi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa Serikali itaokoa kiasi kikubwa  cha fedha kama  itawekeza nguvu kwenye kinga, ambacho kinachotumika kwenye matibabu dhidi ya ugonjwa huu wa homa ya ini.

Nae, Mkurugenzi msaidizi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba amesema kuwa huduma  hii ya chanjo ya homa ya Ini imeanza kutolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa za Sokoture Mwanza,Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi Kilimanjaro, Hospitali ya Rufaa ya Geita, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Hospitali ya Muimbili, Moi, Ocean Road  na vituo vyote vya mipakani.

Mwisho.