Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 19 Agosti 2019

CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

- Hakuna maoni
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Chrisogone Justine German akitoa mafunzo kwa Watoa huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa  wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata  taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC sstandard)

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya, kwa kufuata kanuni za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC standard ).

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akielekeza umuhimu wakufuata taratibu kwa mgonjwa wakati wa kumuudumia (IPC Standard) kwa Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza.


Baadhi ya Watoa  huduma za Afya kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza wakifuatilia Mafunzo kwa makini ya jinsi yakujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata kanuni na taratibu (IPC Standard) wakati wa kumuudumia mgonjwa.

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali jijini Mwanza wakifuatilia kwa makini  Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard)

Picha ya pamoja ikiongozwa na Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa na Watoa huduma kutoka Halmashauri mbali mbali za Mwanza baada ya kumaliza mafunzo ya namna ya kujikinga na kudhibiti  magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa Mkoani hapo.



CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- MWANZA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Mwanza zimeelekezwa kusimamia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi (Magonjwa) wakati wanatoa huduma za Afya kwa Wagonjwa.  

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti  magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande mwingine mafunzo hayo yametumika kama njia ya kusambaza muongozo mpya wa namna ya kujikinga na kudhibiti  maambukizo (IPC Guidline), ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za Afya nchini. 

Katika mafunzo hayo imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Inakadiriwa kuwa watu Bilioni 2.5 Duniani wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, huku kati yao 60% ikiwa ni watu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku nchi za Sudan, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiripoti kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao ulisnza tangu 1976.

Kulingana na Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 1790 wapoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018 Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania tayari imekwisha kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Katika mafunzo hayo, Watoa huduma wameaswa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote wa kutoa huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Akitoa mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo amesema kuwa Watoa Huduma za Afya wapo katika hatari kubwa za kupata maambukizi ya ugonjwa huu, endapo hawatofuata miongozo na taratibu za utoaji huduma kwa kadri ya muongozo huu

“Mara kwa mara ni muhimu kuwa na tahadhari wakati unahudumia Wagonjwa, hususan kunawa mikono kabla na baada ya kutoa huduma kwa wagonjwa na wasio wagonjwa kwani Watoa huduma mpo kwenye hatari kubwa sana yakupata maambukizo” alisema Dkt. Joseph Hokororo.

Ameendelea kusema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Pia alisisitiza kuwa Dunia imekumbwa na tatizo la Usugu wa vimelea vya magonjwa ambukizi dhidi ya dawa (antimicrobial resistance), hivyo amesisitiza juu ya umuhimu mkubwa wa kufuata taratibu za kutoa huduma (IPC Standard) ili kusaidia kutokomeza vimelea hivyo.   

Akitoa mafunzo kwa Watoa Huduma za Afya, juu ya namna ya kukinga maambukizi wakati wa kujifungua, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogone German amesema kuwa ni muhimu kwa Watoa huduma kufuata viwango vya kukinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard) ili kudhibiti ya ugonjwa wakati wa kutoa huduma ikiwemo kuhakikisha kunawa mikono kabla ya kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa.

Aliendelea kusisitiza kuwa, si jambo zuri kwa Watoa huduma za Afya, kufanya mambo kwa mazoea, hali inayopelekea kufanya kazi kwa mazoea na kujikuta kunasambaa maambukizi kutoka kwa mtu anaepokea huduma za Afya au kinyume chake 

Mwisho.

Jumanne, 13 Agosti 2019

WATOA HUDUMA ZA AFYA MWANZA WAFUNDWA

- Hakuna maoni
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akieleza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza.

Afisa Afya ya Mazingira kutoka Taasisi ya JBHN Said Chibwana akitoa Elimu kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya  Watumishi wa Sekta ya Afya  wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akijibu hoja kutoka kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya  Watumishi wa Sekta ya Afya  wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana akisisitiza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Semina hiyo inaendelea Jijini Mwanza.

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Seketoure wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini  Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), mafunzo yanaendelea Jijini Mwanza.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya baada ya kumaliza Wiki ya kwanza ya Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Jijini Mwanza.



WATOA HUDUMA ZA AFYA MWANZA WAFUNDWA

Na Rayson Mwaisemba WAMJW-MWANZA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yawafunda Watoa Huduma za Afya Jijini Mwanza  kuwakumbusha namna ya utoaji huduma kwa kufuata misingi na taratibu za utoaji huduma kwa Wagonjwa ili kupunguza maambukizi mapya na vifo visivyo na ulazima.

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na Wizara ya Afya imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Kwa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Aidha, Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Afisa Mkuu Uhakiki Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokololo amesema kuwa zaidi ya watu milioni 1.4 Duniani wanaugua magonjwa yanayosababishwa na kupata maambukizi mapya wakati wakupata huduma ya afya, hii hutokana na Watoa huduma za Afya kutofuata taratibu za namna ya kutoa huduma.

Aliendelea kusema kuwa Asilimia 15 ya Wagonjwa hupata maambukizi ya magonjwa mapya pindi waendapo kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya, kutokana na kutofuatwa kwa taratibu, kanuni za miongozo ya kutoa huduma za Afya (IPC Guideline, SOP).

Kwa Upande wake Afisa kutoka Kitengo Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogane Justine amesema kuwa kufuata taratibu za utoaji huduma kama kanuni za uoshaji sahihi wa mikono kutamsaidia Mtoa huduma kuzuia kusambaza maambukizi ndani ya Kituo cha kutolea huduma za Afya na nje.

Licha ya changamoto za upatikanaji wa huduma za maji safi kwa baadhi ya Vituo vya Afya, Dkt. Chrisogone Justine German amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Mtoa huduma za Afya kuhakikisha ananawa mikono yake vizuri kwa sabuni na maji safi ili kuepuka kusambaza maambukizi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Akitoa Elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi mapya yanayotokea wakati wa matibabu kutokana na baadhi ya Watoa huduma kutofuata taratibu na miongozo Dkt. Radenta Bahegwa amesema kuwa asilimia 40 ya magonjwa yanayopatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya nayosababishwa na kutofuata kwa taratibu za miongozo ya utoaji huduma.

“Asilimia 40 ya ya magonjwa yanayopatikana katika Vituo vya kutolea huduma za Afya husababishwa na kutofuata miongozo (IPC Guidline), ndiomaana asilimia 80 ya UTI zinazoibuka katika Vituo vya Afya zinatokana na kukosea kuweka kifaa cha kupitisha haja ndogo” alisema Dkt. Radenta.

Mtaalamu kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Dkt. Alex Sanga amesema kuwa katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo ametoa wito kwa Watoa huduma kuhakikisha wanafuata miongozo na taratibu wakati wa kutoa huduma ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi mapya katika jamii.

“Tafiti za Shirika la Afya Duniani zinonesha kuwa ndani ya miaka 3 (2015-2018) kati ya watu 33,421, watu 542 walipoteza maisha, huku katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa” alisema Dkt. Sanga.

Naye Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu. 

Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Francisco Chibunda ametoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kufuata miiko na taratibu na miongozo inavyoelekeza jambo litalosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata taratibu na miongozo wakati wakutibu ugonjwa.

“Tunapoteza nguvu kubwa, tunapoteza rasilimali nyingi kwenye dawa na matibabu, mwisho wa siku tunasababisha maambukizi mapya, nah ii hupelekea usugu wa magonjwa , kwa hiyo tubadilike” Alisema Chibunda.

Mwisho.

Jumatatu, 12 Agosti 2019

WAZIRI UMMY ASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA ZOEZI LA KUTAMBUA MAITI NA KUJULIA HALI MAJERUHI

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mmoja wa majeruhi wa moto aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.


Waziri Ummy akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kutambua miili ya ndugu zao.

 

Picha mbalimbali zikionesha Waziri Ummy akishiriki katika kuhakikisha wananchi wanatoka salama katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro kwa kuweka dawa ili wananchi wakanyage wakati wa kutoka mara baada ya kuaga kuondoa madhara wanayoweza toka nayo katika chumba hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi pamoja viongozi wengine wakiwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hopitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro katika kuhakikisha zoezi la kutambua maiti linaenda vizuri.

Na.WAMJW - Morogoro

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Mb), leo ameshiriki katika zoezi la utambuzi na uhifadhi wa miili ya marehemu wa ajali ya lori la mafuta lilioanguka na kuwaka moto katika eneo la Msamvu Itigi mjini Morogoro.

Pamoja na shughuli hizo, Mhe.Waziri Ummy Mwalimu amewatembelea majeruhi na kuwajulia hali, kuwapa pole na kuona mwendelezo wa huduma za matibabu wanazopata na kuwatakia kheri ya kupona haraka na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa majeruhi wote ambao bado wanapata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Aidha, mara baada ya kuwajulia hali alizungumza na ndugu, jamaa na rafiki wa walioathirika na ajali hii iliyopoteza maisha wa wananchi 69 na kusababisha majeruhi 65 ambao maziko ya awamu ya kwanza yanafanyika leo katika makaburi ya Mlima Kolla mjini Morogoro huku majeruhi wakiendelea na tiba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro.

Aidha, amezidi kuwasihi na kuwahimiza wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu katika hali ya kawaida kibinaadamu na kuwahakikishia kuwa Serikali inazidi kuweka nguvu zaidi katika kuokoa maisha ya majeruhi wote katika Hospitali walizopo ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.

"Naomba kuwathibitishia wataalamu wetu kwa pamoja wameunganisha nguvu kutoka Kitengo cha Dharura Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Benjamin Mkapa Dodoma, wote wako hapa ili kuokoa maisha ya ndugu zetu. Na wenzetu wa MSD pamoja na wadau wengine hapa mkoani wamehakikisha kila kinachohitajika kwa waathirika wetu kimepatika na kiko hapa ili huduma muafaka itolewe kwa wakati kulingana na mahitaji ya aina ya janga lenyewe," amesema Waziri Ummy.

Ajali hii ilitokea siku ya Jumamosi Agosti 10, 2019 mida ya saa 2 asubuhi baada ya lori la mafuta lililokua limebeba shehema ya mafuta aina ya petrol na dizeli likielekea Mafinga mkoani Iringa kumkwepa mwendesha pikipiki aliyekatisha ghafla barabarani hivyo gari kupoteza uelekeo na kuanguka kisha kuwaka moto.

Mwisho.

Alhamisi, 8 Agosti 2019

TEKNOLOJIA YA NANO FILTER YAWAVUTIA VIONGOZI WA WIZARA JIJINI ARUSHA

- Hakuna maoni

Dkt. Askwar Hilonga akiwakaribisha Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi na wengineo wakati walipotembelea Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Jijini Arusha.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela Prof. Emmanuel Luoga akiangalia tuzo ya ubunifu wa teknolojia ya maji aliyopewa Dkt. Askwar Hilonga kwenye kikao cha dunia cha masuala ya afya (World Health Assembly) kilichofanyika Jijini Geneva, Uswisi mwezi Mei mwaka huu.

Picha ya pamoja katika ofisi ya Kaimu Mkuu wa chuo cha Nelsona Mandela Jijini Arusha.


Mbunifu wa Teknolojia ya Nano Filter Dkt. Askwar Hilonga akiwaonesha viongozi sehemu ambayo ubunifu huo ulipoanzia katika chuo cha Nelson Mandela.

Mifupa ya wanyama inayotumika katika Teknolojia ya Nano Filter kuchuja na kutibu maji kwa ajili ya matumizi.

Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi akiangalia chengachenga za mifupa inayotumika na teknolojia ya Nano Filter katika kuchuja na kutibu maji ya kunywa.

Dkt. Hilonga akitoa maelezo kwa viongozi wa Wizara wakati walipotembelea maonesho ya Sabasaba kwenye banda la Nano Filter.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akiwa na Dkt. Khalid Massa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe, mbunifu wa Teknolojia ya Nano Filter Dkt. Askwar Hilonga na wajumbe wengine wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda la Nano Filter katika maonesho ya Nanenane Jijini Arusha.


Teknolojia ya Nano Filter iliyofungwa katika moja ya Shule Jijini Arusha.

Baadhi ya Wananchi waliofika katika ofisi hiyo kwa ajili ya kujaziwa maji.

Picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara wakiwa na Baadhi ya Wafanyakazi wa Nano Filter nje ya ofisi zao.
Teknolojia ya Nano Filter ikiwa imefungwa katika Maonesho ya Nanenane Jijini Arusha.
Na Emmanuel Malegi-Arusha


Viongozi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wamemtembelea mbunifu wa teknolojia ya kusafisha maji ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichoko Arusha Dkt. Askwar Hilonga.

Katika ziara hiyo Dkt. Hilonga amewaonesha viongozi hao Teknolojia iitwayo Nano Filter yenye uwezo wa kusafisha maji, kuondoa bacteria na virusi, huondoa fluoride na madini yote ambayo hayatakiwi kwa binadamu na kuyafanya maji kuwa safi na salama kwa watumiaji na kwa gharama nafuu zaidi.

Dkt. Hilonga ana tuzo 17 kutoka taasisi na mashirika mbalimbali kutokana na ubunifu huo huku tuzo yake kubwa ikiwa ni ile aliyoipata kwenye kikao cha dunia cha masuala ya afya (World Health Assembly) kilichofanyika Jijini Geneva, Uswisi mwezi Mei mwaka huu.

Jumatano, 7 Agosti 2019

HABARI PICHA : ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA KATIKA WILAYA YA BUHIGWE MKOANI KIGOMA.

- Hakuna maoni
Na Englibert Kayombo, Kigoma


Watoa huduma za afya kutoka Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakiwa wamembeba mgonjwa anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa ebola tayari kumpatia huduma ya kwanza katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo usiingie nchini.

Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa iliyomo hatarini kuathiriwa na ugonjwa huo.

Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo; WHO, FAO, USAID, HRH2030, Shirika la Msalaba Mwekundu (RED CROSS), na USAID Global Health Supply Chain Programu, inaendelea na zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma.

Zoezi hilo linalenga kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo atagundulika, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kigoma.


Mwezeshaji wa zoezi la upimaji wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Christopher Mnzava akifafanua umuhimu wa kuzingatia muda wakati wa maandalizi ya kumhudumia mgonjwa anaehisiwa kuwa na ugonwja wa ebola kwa watoa huduma za afya Katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Watoa huduma za afya mara baada ya kumhudia mgonjwa wa ebola wakiwa wamebeba mifuko maalum kwa ajili ya utunzaji wa mavazi na vifaa vilivyovyotumika kuhumdumia mgonjwa kabla ya kuyateketeza.

Dkt. Refaya Ndyamuba kutoka Shirika la Afya Duniani akielekea kukagua kituo kitachokutumika kuhudumia wagonjwa wa ebola katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola usiingie nchini linaloendelea Mkoani Kigoma.

Bi. Consolata Felix Muuguzi kutoka Wizara ya Afya(aliyesimama kulia) akikagua watoa huduma za afya katika Kituo cha hudumia wagonjwa wa ebola katika Wilaya ya Buhigwe namna wanavyosafisha kitanda kilichotumika kumbeba mgonjwa wa ebola katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola usiingie nchini linaloendelea kufanyika mkoani humo.

"Mahema ya kuhudumia wagonjwa wa ebola yanatakiwa kuwa na hewa safi muda wote" Dkt. Refaya Ndyamuba kutoka Shirika la Afya Duniani akifungua sehemu ya kuingiza hewa kwenye hema linalotumika kuhudumia wagonjwa wa ebola wakati wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma. 

Mtoa huduma za afya katika Wilaya ya Buhigwe akinawa kwa maji safi yaliyochanganywa na kemikali ya "Chroline" mara baada ya kutoka kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati wa zoezi la tayari wa kukabiliana na ugonjwa huo


Jumatatu, 5 Agosti 2019

WATOA HUDUMA ZA AFYA KIGOMA KUPIMWA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

- Hakuna maoni
Consolata Felix kutoka Wizara ya Afya (aliyesimama kushoto) akifuatilia zoezi la vitendo la utayari wa kukabiliana ugonjwa wa ebola kwa watoa huduma za afya katika jamii.
Washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola Mkoa wa Kigoma wakiwa kwenye mazoezi ya mezani kujadili mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini mapema leo Mjini Kigoma.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Bw  Daniel Machunda akisema jambo kwa washiriki wa kikao kazi katika zoezi la upimaji wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa ebola (hawapo pichani) mapema leo Mjini Kigoma.

Picha ya pamoja ya mgenu rasmi Bw . Daniel Machunda (aliyeketi kati kati) wadau wa maendeleo na washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola nchini katika Mkoa wa Kigoma


Na Englibert Kayombo, Kigoma.

SEREKALI ya Tanzania kupitia uratibu wa wa ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  zitafanya zoezi la kupima utayari kwa watoa huduma za afya katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Mkoa wa Kigoma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Bashiru Taratibu wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau kutoka ndani nan je ya nchi kujadili mikakati iliyopo kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.

Amesema kuwa zoezi hilo litazingatia dhana ya afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya mifugo,binadamu,mifugo,wanyamapori na mazingira katika kujiandaa,kufuatilia na kukabili magonjwa ambayo huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda binaadamu.

"Zoezi hili litapima uelewa wa jamii kuhusu namna ambavyo wanapaswa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola, hivyo wakati wa zoezi watoa huduma za afya na sekta zingine watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo"alisema

Bw. Taratibu amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Agosti katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka ya Mkoa wa Kigoma. Aliendelea kwa kusema kuwa katika zoezi hilo watoa huduma wa afya watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo namna ya kumuhudumia mgonjwa wa ebola atakapogundulika.

Mgeni rasmi katika kikao hicho Daniel Machunda Kaimu katibu Tawala Msaidizi rasilimali watu kwaniaba ya katibu wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchata alisema Mkoa wa Kigoma una njia nyingi zisizo za halali za mipakani(panya road)ambazo zinachangia hatari ya ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa wale wanaovuka mipaka kwenda nchi za jirani."Ikumbukwe kuwa zoezi linahusu upimaji wa utayari kwa Mkoa wa Kigoma na hakuna mgonjwa yeyote wa ebola aliyeripotiwa hadi sasa nchini"alisema Machunda

Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alisema kuwa nchi ya jirani ya DRC(Congo)imeendelea kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu kulipotiwa mlipuko wa ugonjwa huo mnamo mwezi Agosti mwaka 2018.

Dkt Chawote amesema kuwa idadi ya vifo vilikuwa 1823 ikiwa ni sawa na asilimia 67 ya idadi watu walioathiriwa na ugonjwa huo huku nchi ya Uganda ambayo inapakana na DRC na Tanzania imekuwa na wagonjwa 3 wa Ebola kwa mujibu wa taarifa maambukizi hayo yametoka DRC.

"Kwenye mipaka yetu ya DRC na Burundi kuna mwingiliano mkubwa wa watu unaochangiwa na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi hivyo vinachangia hatari zaidi ya ugonjwa wa Ebol kuingia nchini"alisema Dkt Chawote

Remidius Kakulu Afida Afya mwandamizi toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema mpaka sasa mipaka iliyorasmi yote imedhibitiwa na tayati Serikali imefunga vipima joto vya kisasa katika mipaka yote iliyo rasmi.

"Kuna ile mipaka ambayo siyo rasmi ambayo ipo kwenye vijiji na maeneo mengine tunawaomba Viongozi wa Vijiji pamoja na wananchi kutoa taarifa pale mgeni anapoingia au kumpeleka kituo cha afya ili aweze kupimwa"alisema

Mwisho

WIZARA YA AFYA KUDHIBITI KIFUA KIKUU MAGAREZA 15 NCHINI

- Hakuna maoni
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt.Beatrice Mutayoba akiongea na washiriki wa mafunzo hayo(hawapo pichani) kwenye bwalo la Magereza Ukonga

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza Owesu Ngalama akifungua mafunzo ya tathimini ya udhibiti wa TB katika Magereza 15 nchini

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo


Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo hayo ambayo yana lengo la kuyafikia magereza kumi na tano hapa nchini katika kutathimini hali ya huduma ya TB kwenye magereza nchini

Na. Catherine Sungura, WAMJW-DSM
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na Ukoma kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini wanaanza afua ya ufuatiliaji wa kutathimini hali ya huduma za kutokomeza kifua kikuu katika magereza nchini.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza (CP) Owesu Ngalama wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa maofisa wa jeshi hilo yanayofanyika kwenye bwalo la magereza ukonga jijini hapa.
CP Ngalama alisema kuwa afua hiyo itasaidia jeshi la magereza kuweza kubaini hali ya TB kwenye magereza kwani wanaoingia kwenye magereza ni wana jamii hivyo itasaidia kubaini ugonjwa huo kwa wafungwa na kwa jamii kwa ujumla
“Ugonjwa huu unaambukizwa kwa hewa hivyo kwa tathimini hii itasaidia kuleta utaalam mkubwa kwa wataalam wetu wa tiba waliopo kwenye jeshi kwani hali ya TB sio kubwa kwenye magereza  ila lengo ni kuhakikisha hakuna maambukizi makubwa kwani wafungwa wanaingia na kutoka”.Alisema CP Ngalama
Aidha,ameishukuru wizara ya afya kwa kuendelea kushirikiana nao kwa muda mrefu hususan kwenye utoaji huduma za afya ikiwemo utoaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba pamoja na masuala ya lishe kwenye vituo vya afya vilivyopo kwenye magereza nchini.
Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) kutoka Wizara ya Afya Dkt. Beatrice Mutayoba alisema ugonjwa wa Kifua Kikuu bado ni jangwa kwani bado kuna takribani watu laki moja na elfu hamsini na nne wanakadiriwa kuugua kifua kikuu kila mwaka na inakadiriwa vifo elfu ishirini na saba  kila mwaka nchini.
Dkt. Mutayoba alisema kifua kikuu kinaweza kumpata mtu yeyote kwani maambukizi yake ni ya njia ya hewa hivyo yapo makundi hatarishi zaidi ikiwemo magereza hivyo wanaweka jitihada zaidi kuyafikia makundi hayo ili kutokomeza kifua kikuu ifikapo 2030.
“kama nchi tumepiga hatua kubwa sana kutokomeza ugonjwa huu hivyo tunaongeza juhudi zaidi kwenye makundi hatarishi ikiwemo magereza,migodini,wavuvi ili kuwafikia kwa karibu na kuhakikisha tunapunguza maambukizi ndani ya magereza na maeneo haya”.Alisisitiza
Hata hivyo alisema mkakati wa kudhibiti kifua kikuu upo kwa wananchi wote hivyo  kama mpango wanaendelea kutoa elimu kwa watanzania wote mara waonapo dalili waende kwenye vituo vya afya kwani wizara ya afya inatoa dawa,vipimo  na huduma za kifua kikuu bila malipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya “Magerezani tunaweza utaratibu kwa wanaoingia kuwe na taratibu za uchunguzi ili anapokutwa na kifua kikuu waanze matibabu kwani unapoanza matibabu ndani ya wiki mbili huwezi kuambukiza wengine”.Alisema Dkt. Mutayoba
Mikoa kumi na tano itakayoanza na utekelezaji  huo ni pamoja na Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Singida, Tabora na Tanga.
Mwisho